Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Mkuu huu mfano haufanani mbona 🤣

Maana yangu unapoanza kuamini ni tayari umeruhusu ubongo wako ukuundie mapicha picha na marue rue
Mwanaume ambaye amekubali kusikiliza maneno ya watu kwamba mkewe anachepuka basi pia anaweza kuona kila wanapokwaza na mkewe akachukulia ni kwa sababu ya yale aliyoambiwa kuwa mkewe ana mwanaume mwengine ndio maana amekuwa jeuri au hivi na vile, kwahiyo kama asingesikiliza yale maneno wala asingechukulia kuwa huko kukwazana na mkewe ni kwa sababu ana mwanaume huko nje hivyo angechukulia ni mikwazamo ya kawaida tu kwa wanandoa.
 
Mkuu

Hapo utaona kumechanganywa kati ya uhalisia wa uwepo wa uchawi na nguvu ama manufaa ya huo uchawi, sidhani kama ni sahihi kuweka vigezo kwamba lazima huo uchawi uweze kufanya hiki na kile ndio tukubali kuwa kweli huo uchawi upo wakati hata hayo mengine yote yaliyokuwepo yenye kuhusishwa na uchawi(iwe kwenye tiba, mali, kesi, mapenzi n.k) yanakataliwa kwa sababu hakuna uthibitisho, sasa huko kuweka vigezo kwamba kama uchawi ungekuwepo kungetakiwa kuwe na hiki na kile sioni kama ni hoja ya msingi naona ni kuchanganya uwepo wa uchawi wenyewe na nguvu ya huo uchawi.
Mkuu kama huwezi kuthibisha nguvu ya uchawi na matokeo yake basi huo uchawi haupo

Sawa basi tuseme uchawi upo hauonekani kwa macho sawa
nimekubali haya sasa mtokeo ya nguvu yake yapo wapi?

Kama unaweza kumloga mtu akapoteza mwelekeo wa maisha kwanini pia tusiutumie kinyume chake?

Au uchawi upo kwa mambo negative yasio na faida?

Nitakubali hiyo dhana uchawi na kuona unatija kama utakua na pande mbili negative na positive
 
Mwanaume ambaye amekubali kusikiliza maneno ya watu kwamba mkewe anachepuka basi pia anaweza kuona kila wanapokwaza na mkewe akachukulia ni kwa sababu ya yale aliyoambiwa kuwa mkewe ana mwanaume mwengine ndio maana amekuwa jeuri au hivi na vile, kwahiyo kama asingesikiliza yale maneno wala asingechukulia kuwa huko kukwazana na mkewe ni kwa sababu ana mwanaume huko nje hivyo angechukulia ni mikwazamo ya kawaida tu kwa wanandoa.
So hapa tuna kubaliana kua ni saikolojia?
Baada ya mwanaume kusikia maneno ya wapambe kila analofanya mke
Mume huona kua ni matokeo ya yale aliyoambiwa
Hata kama uhalisia haupo hivyo?
 
Hello jamii intelligence 👋

Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an

Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:

Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi

Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi

kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana

Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje

Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.

Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla

Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa

Sasa najiuliza...

Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?

Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?

Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?

Kuna hii pia👇

Ooh, wachawi wanapaa usiku...

Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?

Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa

Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?

Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?

Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu

Basi kuna mtu akamwambia mama:

Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔

Heh! 🤔

Nikastuka

Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?

Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine

Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.

Usiku naogopa kulala mwenyewe.

Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja

Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo

Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha

So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo

Mara nione hiki...

Mara nisikie kile...

Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?

Asieee!

Nikakaa nikasema:

Hapana, hizi mbona kama fix?

Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win

Nikaacha kabisa huo upuuzi

Nikaamua ku-clean akili yangu

Kuanzia hapo nikiambiwa

Njoo kwenye visomo

Nawaambia

Mimi sina tatizo lolote

Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu

Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku

Nikatumia zangu dawa nikawa fresh

Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu

Sioni mauza mauza wala nini

Naishi vizuri kabisa

Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu

Wala hakuna cha uchawi wala nini

Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake

Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...

Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?

Mashetani wana migodi yao huko?

Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi

Je, uchawi ni nguvu halisi?

Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?

Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...

Kwanini usitumike kinyume chake?

Au kama wachawi wanaweza kupaa...

Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?

Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?

ShesRise_1 ✋️

Kwanza kabisa uchawi ni nini?

Mimi naona uchawi ni jambo la imani tu mpaka sasa hakuna aliyeweza kuthibitisha huu ni uchawi. Mara nyingi imani za uchawi zinaendana na ujinga, kukosa elimu, kutofikiri kisayansi.

Na kwamba upo tangu kale (imani hiyo ipo), ni sawa, kwa sababu hiyo kale ndiyo tuliamini zaidi mambo ya kijinga, hakukuwa na elimu sana.

Na kwamba upo mpaka katika Biblia na Quran ni sawa, hivyo vyote ni vitabu vya kale vyenye ujinga mwingi wa kale.

Mimi "litmus test" yangu kwenye imani za uchawi ni swali hili.

Tuchukue mfano wa kutoka katika historia.

Wazungu walivyokuja Africa na teknolojia zao nyingi zilizotokana na sayansi, Waafrika waliona kama uchawi. Mfano, juzi jua limepatwa (eclipse of the sun). Enzi hizo, mtu aliyeweza kutabiri kupatwa kwa jua, akaweza kueleza mpaka saa na dakika jua litakapopatwa, na litapatwa kwa muda gani, litapatwa sehemu gani, kwa mtu asiyeelewa Jiografia, hiyo ataonekana ni mchawi tu, mtu atajuaje mambo yote hayo?

Lakini kiukweli, ukijua mienendo ya dunia, mwezi na jua, unaweza kutabiri jua litakavyopatwa kwa maelfu ya miaka inayokuja.

Sasa hawa wazungu walivyokuja Afrika walionekana kama wachawi. Ndiyo maana neno "mzungu" ukitoa "z" tu linakuwa "mungu". Neno "mzungu" katika kiswahili ni la kale sana kabla ya kuja hawa watu weupe. Mzungu kwq sisi tunaokijua Kiswahiki kwa ndani ni aina fulani ya demigod, wapo wengi wana nguvu za ajabu supernatural.

Sasa walivyokuja hawa watu weupe kwetu, kwa sababu tulikuwa tunaamini kuna viumbe wana nguvu hizi supernatural, na kwa sababu tuliwaona wao wana nguvu hizo, ndiyo tukajua hawa ni mizungu, which later became wazungu.

Lakini, tulivyokuja kujichanganya nao na kuwasoma vizuri, tukaja kugundua kuwa kumbe hawa hawana supernatural powers, wana sayansi na teknolojia tu, hata sisi tukiisoma hii sayansi na teknolojia tutakuwa na uwezo kama wao. Hawana uchawi na wala si mizungu.

Sasa hapo ndipo litmus test yangu inakuja.

Unaposema hiki kitu ni uchawi, umejiridhisha vipi kuwa hiki kitu ni uchawi kweli na si kitu tu ambacho hujakielewa kama mzungu kutabiri eclipse of the sun, wewe ukaona uchawi kwa sababu huelewi jiografia, wakati yeye anafanya kitu kisayansi tu bila uchawi, tena pengine anakuchezea kwa mazingaombwe kimakusudi tu?

Kwangu mimi uchawi ni imani gu, inayotokana na ujinga, kutofikiri kisayansi, kuamini mazingaombwe ya makusudi ya kuwahadaa watu.

Na kumuhadaa ntu anayekiamini kitu unachomuhadaa nacho ni rahisi sana, kwa sababu unacheza na confirmation bias yake tu. Wachawi na hata waganga wanaotumia uaguzi wa suoernatural powers huwa wanatumia saikolojia tu kuwapeleka watu mulemule.

Ukienda kwa mganga huku unaamini mama mkwe kakuroga ukaumwa, hapo mganga ana kazi rahisi sana ya ku confirm tu anakwambia "namuona mtu wa karibu nawe hapo nyumbani..." na majibu yote unampa mwenyewe bila kujua, unaona huyu mganga wa kweli kajuaje mambo yote haya?

Kumbe kacheza na saikolojia yako tu kakupitisha kwenye confirmation bias kwa majibu uliyompa mwenyewe.
 
Mkuu kama huwezi kuthibisha nguvu ya uchawi na matokeo yake basi huo uchawi haupo

Sawa basi tuseme uchawi upo hauonekani kwa macho sawa
nimekubali haya sasa mtokeo ya nguvu yake yapo wapi?

Kama unaweza kumloga mtu akapoteza mwelekeo wa maisha kwanini pia tusiutumie kinyume chake?

Au uchawi upo kwa mambo negative yasio na faida?

Nitakubali hiyo dhana uchawi na kuona unatija kama utakua na pande mbili negative na positive
Tatizo mkuu lipo kwenye kukubali hayo matokeo ya nguvu ya uchawi hapo ndipo kwenye shida, kwa sababu ukisema kwamba hicho kinachoitwa uchawi hakina kabisa matokeo basi hata hii imani ya uchawi ingekuwa hadi sasa ishapotea kabisa mkuu. Kwa sababu uchawi ni tofauti na maombi ambayo unangojea ujibiwe au hata usijibiwe, ila uchawi ni vitendo ambavyo unafanya na kutaraji kuona matokeo, sasa kama ingekuwa watu wanafanya hicho kinaitwa uchawi kisha hakuna matokeo sidhani kama hadi leo imani ya uchawi ingeendelea kuaminika.

Mkuu ni mengi tu yenye kuhusishwa na nguvu ya uchawi ambayo ni yenye faida kama vile kuhusu mapenzi, mali, ulinzi, kesi,tiba n.k ila ndio shida ileile kwamba hukataliwa kuwa si uchawi kwamba hakuna nguvu ya uchawi kuathiri hayo mambo.
 
So hapa tuna kubaliana kua ni saikolojia?
Baada ya mwanaume kusikia maneno ya wapambe kila analofanya mke
Mume huona kua ni matokeo ya yale aliyoambiwa
Hata kama uhalisia haupo hivyo?
Sasa hapo ndio inawezakuwa yanayosemwa na watu si kweli au ikawa ni kweli, haya kwenye uhalisia wa maisha tunayaona. Watu wanaambiwa maneno kuhusu wapenzi wao wanapuuza ila baadaye wanakuja kugundua kumbe ilikuwa ni kweli, na wengine wanaambiwa maneno wanasikiliza na kusababisha ugomvi kwenye ndoa mwisho wa siku wanagundua ni maneno tu ya watu hayakuwa kweli.

Kwahiyo unaweza ukapuuza kitu na kweli usione tatizo lakini kumbe ratizo lipo kweli.
 
Kwanza kabisa uchawi ni nini?

Mimi naona uchawi ni jambo la imani tu mpaka sasa hakuna aliyeweza kuthibitisha huu ni uchawi. Mara nyingi imani za uchawi zinaendana na ujinga, kukosa elimu, kutofikiri kisayansi.

Na kwamba upo tangu kale (imani hiyo ipo), ni sawa, kwa sababu hiyo kale ndiyo tuliamini zaidi mambo ya kijinga, hakukuwa na elimu sana.

Na kwamba upo mpaka katika Biblia na Quran ni sawa, hivyo vyote ni vitabu vya kale vyenye ujinga mwingi wa kale.

Mimi "litmus test" yangu kwenye imani za uchawi ni swali hili.

Tuchukue mfano wa kutoka katika historia.

Wazungu walivyokuja Africa na teknolojia zao nyingi zilizotokana na sayansi, Waafrika waliona kama uchawi. Mfano, juzi jua limepatwa (eclipse of the sun). Enzi hizo, mtu aliyeweza kutabiri kupatwa kwa jua, akaweza kueleza mpaka saa na dakika jua litakapopatwa, na litapatwa kwa muda gani, litapatwa sehemu gani, kwa mtu asiyeelewa Jiografia, hiyo ataonekana ni mchawi tu, mtu atajuaje mambo yote hayo?

Lakini kiukweli, ukijua mienendo ya dunia, mwezi na jua, unaweza kutabiri jua litakavyopatwa kwa maelfu ya miaka inayokuja.

Sasa hawa wazungu walivyokuja Afrika walionekana kama wachawi. Ndiyo maana neno "mzungu" ukitoa "z" tu linakuwa "mungu". Neno "mzungu" katika kiswahili ni la kale sana kabla ya kuja hawa watu weupe. Mzungu kwq sisi tunaokijua Kiswahiki kwa ndani ni aina fulani ya demigod, wapo wengi wana nguvu za ajabu supernatural.

Sasa walivyokuja hawa watu weupe kwetu, kwa sababu tulikuwa tunaamini kuna viumbe wana nguvu hizi supernatural, na kwa sababu tuliwaona wao wana nguvu hizo, ndiyo tukajua hawa ni mizungu, which later became wazungu.

Lakini, tulivyokuja kujichanganya nao na kuwasoma vizuri, tukaja kugundua kuwa kumbe hawa hawana supernatural powers, wana sayansi na teknolojia tu, hata sisi tukiisoma hii sayansi na teknolojia tutakuwa na uwezo kama wao. Hawana uchawi na wala si mizungu.

Sasa hapo ndipo litmus test yangu inakuja.

Unaposema hiki kitu ni uchawi, umejiridhisha vipi kuwa hiki kitu ni uchawi kweli na si kitu tu ambacho hujakielewa kama mzungu kutabiri eclipse of the sun, wewe ukaona uchawi kwa sababu huelewi jiografia, wakati yeye anafanya kitu kisayansi tu bila uchawi, tena pengine anakuchezea kwa mazingaombwe kimakusudi tu?

Kwangu mimi uchawi ni imani gu, inayotokana na ujinga, kutofikiri kisayansi, kuamini mazingaombwe ya makusudi ya kuwahadaa watu.

Na kumuhadaa ntu anayekiamini kitu unachomuhadaa nacho ni rahisi sana, kwa sababu unacheza na confirmation bias yake tu. Wachawi na hata waganga wanaotumia uaguzi wa suoernatural powers huwa wanatumia saikolojia tu kuwapeleka watu mulemule.

Ukienda kwa mganga huku unaamini mama mkwe kakuroga ukaumwa, hapo mganga ana kazi rahisi sana ya ku confirm tu anakwambia "namuona mtu wa karibu nawe hapo nyumbani..." na majibu yote unampa mwenyewe bila kujua, unaona huyu mganga wa kweli kajuaje mambo yote haya?

Kumbe kacheza na saikolojia yako tu kakupitisha kwenye confirmation bias kwa majibu uliyompa mwenyewe.

Kwanza kabisa uchawi ni nini?

Mimi naona uchawi ni jambo la imani tu mpaka sasa hakuna aliyeweza kuthibitisha huu ni uchawi. Mara nyingi imani za uchawi zinaendana na ujinga, kukosa elimu, kutofikiri kisayansi.

Na kwamba upo tangu kale (imani hiyo ipo), ni sawa, kwa sababu hiyo kale ndiyo tuliamini zaidi mambo ya kijinga, hakukuwa na elimu sana.

Na kwamba upo mpaka katika Biblia na Quran ni sawa, hivyo vyote ni vitabu vya kale vyenye ujinga mwingi wa kale.

Mimi "litmus test" yangu kwenye imani za uchawi ni swali hili.

Tuchukue mfano wa kutoka katika historia.

Wazungu walivyokuja Africa na teknolojia zao nyingi zilizotokana na sayansi, Waafrika waliona kama uchawi. Mfano, juzi jua limepatwa (eclipse of the sun). Enzi hizo, mtu aliyeweza kutabiri kupatwa kwa jua, akaweza kueleza mpaka saa na dakika jua litakapopatwa, na litapatwa kwa muda gani, litapatwa sehemu gani, kwa mtu asiyeelewa Jiografia, hiyo ataonekana ni mchawi tu, mtu atajuaje mambo yote hayo?

Lakini kiukweli, ukijua mienendo ya dunia, mwezi na jua, unaweza kutabiri jua litakavyopatwa kwa maelfu ya miaka inayokuja.

Sasa hawa wazungu walivyokuja Afrika walionekana kama wachawi. Ndiyo maana neno "mzungu" ukitoa "z" tu linakuwa "mungu". Neno "mzungu" katika kiswahili ni la kale sana kabla ya kuja hawa watu weupe. Mzungu kwq sisi tunaokijua Kiswahiki kwa ndani ni aina fulani ya demigod, wapo wengi wana nguvu za ajabu supernatural.

Sasa walivyokuja hawa watu weupe kwetu, kwa sababu tulikuwa tunaamini kuna viumbe wana nguvu hizi supernatural, na kwa sababu tuliwaona wao wana nguvu hizo, ndiyo tukajua hawa ni mizungu, which later became wazungu.

Lakini, tulivyokuja kujichanganya nao na kuwasoma vizuri, tukaja kugundua kuwa kumbe hawa hawana supernatural powers, wana sayansi na teknolojia tu, hata sisi tukiisoma hii sayansi na teknolojia tutakuwa na uwezo kama wao. Hawana uchawi na wala si mizungu.

Sasa hapo ndipo litmus test yangu inakuja.

Unaposema hiki kitu ni uchawi, umejiridhisha vipi kuwa hiki kitu ni uchawi kweli na si kitu tu ambacho hujakielewa kama mzungu kutabiri eclipse of the sun, wewe ukaona uchawi kwa sababu huelewi jiografia, wakati yeye anafanya kitu kisayansi tu bila uchawi, tena pengine anakuchezea kwa mazingaombwe kimakusudi tu?

Kwangu mimi uchawi ni imani gu, inayotokana na ujinga, kutofikiri kisayansi, kuamini mazingaombwe ya makusudi ya kuwahadaa watu.

Na kumuhadaa ntu anayekiamini kitu unachomuhadaa nacho ni rahisi sana, kwa sababu unacheza na confirmation bias yake tu. Wachawi na hata waganga wanaotumia uaguzi wa suoernatural powers huwa wanatumia saikolojia tu kuwapeleka watu mulemule.

Ukienda kwa mganga huku unaamini mama mkwe kakuroga ukaumwa, hapo mganga ana kazi rahisi sana ya ku confirm tu anakwambia "namuona mtu wa karibu nawe hapo nyumbani..." na majibu yote unampa mwenyewe bila kujua, unaona huyu mganga wa kweli kajuaje mambo yote haya?

Kumbe kacheza na saikolojia yako tu kakupitisha kwenye confirmation bias kwa majibu uliyompa mwenyewe.
Naunga mkono hoja mkuu🤝
 
Sasa wewe mimi ndio nitakukaba mimi ni kachawi kadogo mkuu wangu mshana ana majukumu makubwa anawakaba watu wakubwa kama kina mwigulu Nchemba na kina samia
Na uchawi ungekuwepo na kufanya kazi mngeanza na sa100
Haya niroge tuone
 
Tatizo mkuu lipo kwenye kukubali hayo matokeo ya nguvu ya uchawi hapo ndipo kwenye shida, kwa sababu ukisema kwamba hicho kinachoitwa uchawi hakina kabisa matokeo basi hata hii imani ya uchawi ingekuwa hadi sasa ishapotea kabisa mkuu. Kwa sababu uchawi ni tofauti na maombi ambayo unangojea ujibiwe au hata usijibiwe, ila uchawi ni vitendo ambavyo unafanya na kutaraji kuona matokeo, sasa kama ingekuwa watu wanafanya hicho kinaitwa uchawi kisha hakuna matokeo sidhani kama hadi leo imani ya uchawi ingeendelea kuaminika.

Mkuu ni mengi tu yenye kuhusishwa na nguvu ya uchawi ambayo ni yenye faida kama vile kuhusu mapenzi, mali, ulinzi, kesi,tiba n.k ila ndio shida ileile kwamba hukataliwa kuwa si uchawi kwamba hakuna nguvu ya uchawi kuathiri hayo mambo.
Watu wameamua kuukumbatia uchawi ila ki uhalisia hiyo dhana haina tija yoyote!
 
Sasa hapo ndio inawezakuwa yanayosemwa na watu si kweli au ikawa ni kweli, haya kwenye uhalisia wa maisha tunayaona. Watu wanaambiwa maneno kuhusu wapenzi wao wanapuuza ila baadaye wanakuja kugundua kumbe ilikuwa ni kweli, na wengine wanaambiwa maneno wanasikiliza na kusababisha ugomvi kwenye ndoa mwisho wa siku wanagundua ni maneno tu ya watu hayakuwa kweli.

Kwahiyo unaweza ukapuuza kitu na kweli usione tatizo lakini kumbe ratizo lipo kweli.
Mkuu asante kwa maoni acha niendelee kupuuza mpka siku nikijionea
 
Back
Top Bottom