Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Watu wameamua kuukumbatia uchawi ila ki uhalisia hiyo dhana haina tija yoyote!
Kuna makundi aina tatu ya watu wenye kupinga uchawi. Wapo ambao wao wanapinga na kusema kabisa kuwa hakuna uchawi, wapo ambao wanapinga uchawi kwa sababu hawajawahi kushuhudia hiyo nguvu ya uchawi zaidi ya kusikia tu kuna muda watu hawa hukubali uwepo wa uchawi pale itokeapo kushuhudia hiyo nguvu ya uchawi, lakini pia wapo ambao wanaamini kuwepo uchawi ila si kitu ambacho hukihusisha kwenye maisha yao ya kila siku na pengine huona kuna uwongo mwingi kuliko ukweli.

Sasa shida nyengine humu zile imani potofu za watu ndio hutumika kama kigezo cha kuonyesha kwamba hakuna uchawi bali ni ukosefu wa elimu na uelewa wa watu, kitu ambacho sio sahihi maana imani potofu ziko hadi katika mambo mengine pia.

Kwahiyo mimi bado nasisitiza kama hicho kinachoitwa uchawi ingekuwa hakina matokeo basi imani ya uchawi ingekuwa ishaisha.
 
Sawa mkuu asante kwa maoni
 
Hakuna uchawi bali utapeli.
Mkuu ukitaka kuzungumzia utapeli kwenye imani za kichawi tunaweza kuzungumzia ila pia ukitaka kuzungumzia uchawi pia tunaweza kuzungumzia, tusichanganye mambo mkuu maana utapeli upo kila mahali.
 
Mkuu ukitaka kuzungumzia utapeli kwenye imani za kichawi tunaweza kuzungumzia ila pia ukitaka kuzungumzia uchawi pia tunaweza kuzungumzia, tusichanganye mambo mkuu maana utapeli upo kila mahali.
Kwangu uchawi na utapeli havitenganishwi.
 
Kwangu uchawi na utapeli havitenganishwi.
Ni kwa sababu wengi wenu humu uchawi ni kitu mnachokisikia zaidi kuliko kushuhudia, wengi humu mnazungumzia story za utapeli wa waganga, imani potofu ambazo mnazisikia zenye kuhusishwa na uchawi. Kwahiyo kama uelewa wako kuhusu uchawi ni kupitia hizo story za utapeli basi ni wazi lazima ushindwe kutenganisha.
 
Usibishane nao list yao ninayo hapa inafanyiwa uhakiki ili mgao ufike kila kaya
 
Attachments

  • downloadfile-27.jpg
    downloadfile-27.jpg
    86.9 KB · Views: 3
Nimewekea rejea ya vitabu vya dini kwa kutaka kuonesha kua hii dhana ya uchawi ni ya kale

Ajabu yake huko vitabu vya dini na imani vilipoanzia hawajishughulishi na hii dhana ya uchawi kama huku africa

Kama unaweza kufanya mtu akupende na akakupenda je hakuna namna mzazi anaweza kufanya kutumia huo uchawi mtoto akashika no moja darasani
Yaani kwa faida maana umesema wanafaika wa uchawi ni wachawi wenyewe

Alieunda uchawi alikua hopeless kaunda kitu hakina manufaa zaidi ya uharibifu tu

Mimi binafsi nikitaka kujiunga na wa chawi ili nipate hiyo cheap ya usafiri nawezaje?

Kikundi cha kikuda hiki hakina faida yoyote
Genz mna vituko sana.
Kwa hiyo unataka kuwapanga wachawi wawe wanakupa lift ya usafiri kwenda Town
 
Hello jamii intelligence 👋

Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an

Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:

Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi

Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi

kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana

Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje

Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.

Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla

Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa

Sasa najiuliza...

Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?

Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?

Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?

Kuna hii pia👇

Ooh, wachawi wanapaa usiku...

Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?

Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa

Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?

Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?

Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu

Basi kuna mtu akamwambia mama:

Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔

Heh! 🤔

Nikastuka

Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?

Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine

Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.

Usiku naogopa kulala mwenyewe.

Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja

Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo

Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha

So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo

Mara nione hiki...

Mara nisikie kile...

Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?

Asieee!

Nikakaa nikasema:

Hapana, hizi mbona kama fix?

Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win

Nikaacha kabisa huo upuuzi

Nikaamua ku-clean akili yangu

Kuanzia hapo nikiambiwa

Njoo kwenye visomo

Nawaambia

Mimi sina tatizo lolote

Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu

Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku

Nikatumia zangu dawa nikawa fresh

Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu

Sioni mauza mauza wala nini

Naishi vizuri kabisa

Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu

Wala hakuna cha uchawi wala nini

Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake

Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...

Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?

Mashetani wana migodi yao huko?

Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi

Je, uchawi ni nguvu halisi?

Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?

Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...

Kwanini usitumike kinyume chake?

Au kama wachawi wanaweza kupaa...

Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?

Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?

ShesRise_1 ✋️
Uko sahihi,,,,,
Ila UCHAWI upo.....
 
Uchawi ni saikolojia. Wachawi & waganga hucheza na saikolojia zetu
Eeh ni issue za saikolojia ukiambiwa umerogwa hapo hapo unaanza kuona mauza uza wakati kabla ulikua huyaoni
 
Eeh ni issue za saikolojia ukiambiwa umerogwa hapo hapo unaanza kuona mauza uza wakati kabla ulikua huyaoni
Nendq kaishi Sumbawanga vijijini au Gamboshi halafu uwaambie wazee kwamba"uchawi hakuna ni mambo ya kisaikolojia tu" halafu sikilizia matokeo ndani ya mwezi mmoja utapata majibu
 
Nendq kaishi Sumbawanga vijijini au Gamboshi halafu uwaambie wazee kwamba"uchawi hakuna ni mambo ya kisaikolojia tu" halafu sikilizia matokeo ndani ya mwezi mmoja utapata majibu
Huko ndiyo makao makuu ya uchawi?
Nataka uniroge hapa hapa jeyihefu
 
Back
Top Bottom