FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 731
Mkuu FD,
I hope hapo juu una maana unalipa kidogo kidogo kulingana na masharti ya mikopo yako.
Kama una maana tofauti na hiyo, hilo ni jambo la hatari sana. Kukiuka masharti ya mkopo kwa sababu zozote zile si jambo la kujivunia na badala yake ni hatari mno.
Unapokuwa kiongozi wa siasa inakuwa hata hatari zaidi maana ukifilisiwa, kweli wewe unafaa hata kuongoza chama?
Ni kweli nchi haiwezi kuendelea bila wananchi wake kuweza kukopa na kuendesha biashara zao. Lakini inapotokea kwamba viongozi wanakopa sehemu kama NSSF ambako kuna nafuu kubwa na kuwaacha wananchi wanasota na mabank
ambako kuna interest rate zaidi ya 20%, kwa kweli haiwezi kuwa sawa. Matokeo yake viongozi huwa hawachukuia hatua kubadilisha sheria za mabank maana wanakuwa hawalipati hilo joto la jiwe ambalo linawakumba wananchi wa kawaida.
Wanasiasa waache kukimbilia sehemu kama NSSF na badala yake wakakope kwenye hayo mabank sawa na wananchi wengine.
Tupo pamoja mkuu. Deni langu nalipa kidogo kidogo kama tulivyokubaliana.
Ninachopinga ni watu kuongelea vitu visivyo na msingi kama kumiliki Vogue.
Pia rudi nyuma kidogo usome post ya Techmaro. Huu ni mkopo wa kibiashara, mabenki kukosa FOREX pia ni kigezo tosha cha kukaa meza moja kujadiliana na aliyekukopesha. Kuna mambo mengi hasa kama aliyekukopesha alijua nia yako ni nini, It is a business loan sio personal loan.
Mimi pia napinga Mbowe kutorejesha on time hela hizo.