Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,354
- 18,628
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu, amesema kwamba ingawa katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho alimuunga mkono Freeman Mbowe, katika maisha yake binafsi alikuwa rafiki zaidi wa Tundu Lissu tangu walipokuwa pamoja bungeni.
Katika uchaguzi huo, Joseph Mbilinyi (Sugu) amekiri alimuunga mkono Mbowe, ingawa katika maisha yake binafsi yeye ni rafiki zaidi wa Lissu tangu walipokuwa pamoja bungeni.
“Of course (bila shaka), mimi nilikuwa kambi ya Mbowe, lakini sikuvuka mipaka yangu, nikijua kwamba hawa ni viongozi wetu. Sawa, mimi nilikuwa namuunga mkono Mbowe, lakini Lissu ni mwanangu zaidi kuliko Mbowe. Hata tukiwa Dodoma, wakati ule mchana, unamuuliza bwana uko wapi twende nyumbani tukale ugali? Uko wapi twende tukale pizza? Ni kaka yangu,” amesema.
Kwa sababu hiyo, amesema hata Mbowe aliposhindwa haikumsumbua wala kumkatisha tamaa kama ilivyokuwa kwa makada wengine waliokihama chama hicho, kwa kile anachoeleza kuwa aliamini ushindi wa Lissu ni wa Chadema.
Baada ya uchaguzi huo, amesema aliamini kuwa, kwa nafasi yake, anapaswa kufanya jambo kuhakikisha chama kinasonga mbele, ndiyo maana ziara ya “No Reforms, No Election” ilianzia katika kanda anayoiongoza.
“Chadema ipo imara kuliko kipindi chochote. Tunawaambia kila siku, hasa hawa wanaojaribu kuiua. Chadema ilishavuka kuwa chama cha viongozi, kwamba kwa sababu ya kiongozi fulani chama kinasimama. Chadema kipo kwenye mioyo ya Watanzania,” amesema.