Tuache ushabiki wa kisiasa usiokuwa na maana, the good thing with members kama mimi ni kwamba sina affiliation na chama chochote cha siasa so nina uhuru wa kumchabanga mwanasiasa yoyote regardless ya chama anachotoka.
Its wrong kumuita Mbowe Mwizi kwa kuwa hajaiba, kuna tofauti kati ya kukopa na kuiba na kamwe hatuwezi kumuweka katika kundi moja na mafisadi-wezi wa CCM.
Mapato ya Hard Rock, Billicanas, Much More na Sugar Mama kwa mwezi yangemuwezesha Mbowe na timu yake kulipa milioni 3 kwa mwezi bila matatizo kama kweli walikua na nia ya kulipa kama makubaliano ya mwanzo kabisa yalivyodai (1990- 6 years repayments of 3ml every month).Badala yake amekaa for 3 years (1993) ndio akafanya 1st repayment baada ya kupigwa mkwala then jiii. Akalipa tena 12m (1998) na 50m (2006)baada ya mkwala wa mahakama kumkamata.
Talk about Mbowe ni kwamba unamuongelea potential president hapa.Habari za hili deni sio uzushi kwa kuwa vilelezo vyote vimetolewa kwenye hiyo habari hapo juu na utaona kwamba hili suala ambalo hata mahakama imelitolea maamuzi, tena mara mbili. Zaidi ya yote mkopo huu umetolewa kwa mkataba ambao naamini Mh. Mbowe alichukua muda kuusoma na kulewa kila kipengele.Ndio maana unaona hadi leo hii na yeye amegeuka kuwa kama Mkapa sasa, hajaongea chochote kuhusiana na hili. Hivi ni kweli tunahitaji rais ambaye atakuwa haheshimu hata mikataba midogo midogo? Raisi ambaye anakaidi hata amri za mahakama? Hivi kweli mnadhani bado watanzania ni mbumbumbu kiasi cha kumchagua mtu kama huyu awe Raisi wao?
Wakati mwingine natamani sana nchi yangu iwe na Rais tajiri, mtu ambaye hana njaa kabisa na hatoingia vishawishi vya kijinga kwa kuwa ana kila kitu. Lakini pia kwa upande mwingine ningependa Rais wangu awe ni mtu ambaye amepitia kwenye umaskini, anaujua umaskini inside out, someone who knows how it feels to go a day without food. Nina hofu kama hujawahi kulala njaa maisha yako yote ni vigumu kuamini kwamba kuna watu wanalala njaa, na kama hutembelei barabara ni vigumu kuamini ubovu wa barabara unaolalamikiwa na wananchi, na kama kipindi hiki tu ambacho unausaka Uraisi unatembelea helikopta je ukiupata huo uraisi itakuwaje? Kwanini asitembelee gari tu akapata nafasi ya kusimama na kusalimiana na kusikiliza shida za wananchi wa kila kijiji? Kama mvua ikinyesha gari lake likizama na akakwama mahali na wananchi kwa siku mbili tatu- kura ngapi zaidi hapo atakuwa amejipatia?
Kama una mapenzi ya kweli na Chadema, you must be concerned now, 2010 ndio hiyo inakuja na chama kinaonyesha mwelekeo mzuri lakini kama hii kasumba ya kisisiemu ya kulindana regardless ya utumbo gani mtu amefanya itaendekezwa ndani ya chama hiki basi wana Chadema mjiandae na kilio, tena kwa sababu ya mtu mmoja tu. Kuna watu wengi safi ambao hawana doa kwenye history zao na ni wachapa kazi ndani ya Chadema, sioni ni kwanini wasipewe hiyo nafasi, sio lazima awe Mbowe.