The Fixer
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 1,365
- 594
Kwenu Watanzania !
Nimesoma kwa makini kabisa kinachoendelea katika sakata la kibiashara ambalo Mh Mbowe anahusishwa na ukopaji wa kupita kiasi ! Nasema wakupita kiasi kwani Mh Mbowe alikuwa anajua kabisa mwenendo wa hizi benki zetu za nyumbani katika maswala yote ya kubadilisha fedha, hali ya kibenki ilivyokuwa na mahitaji yote ya vifaa vya utengenezaji ama ukarabati wa hizo nyumba zake za kibiashara .
Sitaki kuamini kuwa eti, Ukopaji huo wa Mh Mbowe ulikuwa wa kukurupuka bila kupiga hata mahesabu,Alisoma alama za nyakati na akaamua tena akiwa na Baba Mkwe ambaye alishawahi kuwa hata Gavana wa Benki inamaana alikuwa na kila sababu ya Kufanya Mkopo huo ufikie kilele kwani kama ni ushauri wa kifedha upo nyumbani kwa Mkwe wake kwahiyo vile visingizio alivyotoa huyo Meneja wa Biashara wa Bilicanas ni visingizio vya kitoto tu !
Kilicho mgharimu Mh Mbowe ni Maisha ya ANASA aliyoyaishi.....Anayoyaishi na Yatakayo endelea kumgharimu kama hata fanya mabadiliko katika maisha yake halisi ! Mimi hapa naona swala la Mh Mbowe kiuadilifu hakuna na wala asisimame jukwaani kuhubiri yale ambayo yeye hayafanyi, Kama atahubiri Uzalendo je, yeye ni mzalendo kiasi gani ? Na kama atasema ile ni kampuni ....Sasa anataka kutuambia kuwa kampuni inaundwa na nani kama sio watu tena ni hao hao watu ambao tunawatafuta huku kwa Akina Richard Monduli na EPA na kule BOT NA KWINGINE KWING TU !......Mh Mbowe, anaendesha gari aina ya Range Rover gari yenye thamani kubwa yapata hata Milllino 120, na hiyo nyumba anayoishi ni kufuru kwani mie nimeshawahi kufika yaani kila ukipiga hatua moja kutoka getini kwake kunawaka taa ambazo kila ukiiacha hatua moja nyuma inazimika...acheni wajameni ! Yaani maisha yake ni Anasa....Anasa tupu ! Ndio maana hata shule imemshinda kabisa pale Londoni !
Mh Mbowe anataka kuishi maisha ya watu waliomtangulia mbali kama akina Mengi, Bakhressa, Manji, Hossea yule wa PCB ! Ukiwaauliza hawa wote watakwambia ni Biashara lakini Tanzania Biashara zipo nyingi bwana......Huyu Hossea mimi sisemi yaani anabonge la Nyumba hapa Mbezi utadhani ni mfanya biashara kumbe ni mwajiriwa wa serikali ila kama utamuuliza Hossea ...Sijui atakujibu nini ??
Mh Mbowe ....Acha ...Anasa ! Ulipe hayo madeni manake sisi kama wanachama na wafanyabiashara wenzako...Tumejisikia vibaya sana kwani....Uzalendo huanzia Nyumbani !
EVEN FOOLS WE'RE RIGHT SOMETIMES !