JamiiForums Usiku wa manane
Mazungumzo ya usiku


UKIWA MUELEWA NA MPOLE UTATHAMINIWA

Kalamu ya mlinzi wa zamu inayaangalia yafutayo....


Ilikuwa miaka kadhaa huko nyuma baada ya kumaliza masomo...nilipata kazi moja ya Usimamizi wa hotel flan mkoani Morogoro haikuwa na hadhi kubwa ila ya wastani tu, kuna matukio mawili ambayo yalitokea na ndio msingi wa bandiko langu hili.

Ilikuwa Mda wa kupata chakula cha mchana,na hiyo hotel kwakwel kwenye chakula ilikuwa imejaaliwa na misosi mizur ambayo iliwafanya watu wengi wapendelee kuja kupata huduma pale. Kwakuwa huwa na wateja wengi basi sometime wengine huchelewa kupata oda zao na hii hutokea mara chache sana kama unavyojua wengine hubwatuka na kusema ovyo, lkn kuna mwamba mmoja alikuwa amechill Tu pamoja na kwamba oda yake ilikuwa imechelewa,nilimfuata na kumwomba radhi na akasema ''usiwe na hofu broo ndo ubinadamu''.

Nilivutiwa na hekima aliyoionyesha yule mwamba na nilimpa respect Sana kwakuwa alikuwa muelewa ikawa kila akija Mimi binafsi naenda kumsikiliza na kuhakikisha anapata huduma stahiki alinifundisha Utulivu na Uelewa ndio Jambo kubwa ambalo binadamu yoyote anapaswa awe nalo.

Ebu ongeza pop con kidogo hapo au kahawa huku unaendelea Kula madini. Tukio la pili kipindi kile kuna maji Fulani yalikuwa na hadhi kubwa kidogo sitaki kuwapa promo,najua wajanja mtakuwa mmejua hiyo brand au sio? Basi mteja wangu aliuliza bei za maji nikaanza na hiyo brand nikamtajia bei akaonekana kama kashtuka hivi. Basi nikamwambia kuna mengine bei ni hii. Daah nikayakoroga wakulungwa! Kwake yeye ilionekana kana kwamba nimemuona Hana hela. Basi akaongea shit kuwa kwani yeye nimemuona Hana hela na blah blah kibao. Basi muungwana nikamwomba radhi na kumwambia wala sikuwa na dhamira hiyo ambayo amekuwa nayo. Nikajiuliza kitu cha ajabu lilikuwa ni nini mpaka apaniki vile, lakini nikajua ndo wale watu wasiojiamini ndo huwa hivyo.

Watu kama hawa tupo nao wengi katika jamii, huenda hata wewe msomaji wangu ni mmoja wapo hahahaha. Chill na relux kwani Maisha yenyewe ni mafupi na mambo ni mengi au Sio wadau? Tukiwa waelewa na watulivu mahala popote pale tutathaminiwa na kupata heshima pia, kuwa mtu ambaye wengine watapenda kuiga kutoka kwako.
 
Back
Top Bottom