JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Nimefungua uzi huu kutokana na kuwa na janga la kukata usingizi usiku. Kama na wewe ni mmojawapo naomba tuungane pamoja hapa kwa kuandika ulipo na unafanya nini kwa wakati huo baada ya kukosa usingizi.

Muda wa jukwaa ni kuanzia saa 6 usiku mpaka 11 asubuhi. Mimi hapa leo tangu nimeamka nimeamua KUFANYA IBADA Tuuuu!
1746822471017.png
 
Mazungumzo ya usiku

TUJIFUNZE KUKATALIWA

Kalamu ya mlinzi wa zamu inamulika haya yafuatayo

Hakuna kitu kigumu kukipokea kama kukataliwa na Yule unayempenda au unaye tarajia kuwa nae ktk Maisha ya kimapenzi.

Tujue Kwanza kukataliwa ni haki ya yule anayetukataa,ana Uhuru na uamuzi wa kufanya hivyo,kwakuwa naye ana vigezo vyake vinavyo mfanya amchague mtu Fulani,kwahiyo tusipokuwa na vigezo hatuna haki ya kupendwa na mtu huyo,tukubali ukweli na kusonga mbele.

Kukataliwa ni sehemu ya Maisha ya kila siku,wewe sio wa Kwanza kukataliwa,usijione hauna thamani kwakuwa Tu eti umekataliwa,tambua kwamba haujakizi Tu vigezo vya huyo umpendaye lkn haimaanishi kuwa ndiyo hauna thamani laa! Thamani IPO pale pale Ila Tu haujakutana na Yule ambaye anaijua thamani yako,so IPO siku utampata Yule ambaye anaijua thamani yako na mtainjoy mahusiano yenu.

Kukataliwa usikuchukulie upande wa negative Tu bali chukulia upande wa positive pia Kwa faida yako,je unajuaje kama huyo aliye kukataa alikuwa mtu sahihi kwako? Je Una uwakika gani kwamba angekupa furaha ambayo ungeitamani? Kwahiyo kukataliwa wakati mwingine ni faida kwako kuepukana na mtu ambaye angekuwa sababu ya maumivu yako au mateso yako,umekataliwa huenda kuna mtu mwingine ambaye unatakiwa ukutane na ambaye atakuwa ulimwengu wako,atakuwa nuru yako na atakuwa pumziko lako.

Na kitu kingine ambacho watu hawajui ni kuwa,wanaotukataa ndio huenda wamekula hasara! Ndiyo narudia tena wamekula hasara,unajua Kwa nini? Kwasababu wanakosa Yale mazuri ambayo wangepata kutoka kwetu,wanakosa utulivu ambao wangeupata kutoka kwetu na wanakosa MAHABA ambayo wangepata kutoka kwetu,kwahiyo wakati mwingine badala ya kuumia na kukosa Raha inatakiwa tuwaonee huruma Tu.


Mlinzi wa zamu!
 
Back
Top Bottom