JamiiForums Usiku wa manane
Mazungumzo ya usiku

TATIZO LA MWANA ROCK STAR

Mwaka 1983 huyu mpiga gita akiwa na band yake ambayo ilikuwa mda si mrefu warekodi album yao ya kwanza,mara ghafla tu bila sababu yoyote anapewa tiketi ya basi na band yake arudi Los Angeles

Akiwa njiani akajiuliza maswali mengi sana kwa nini ameachwa kwenye kikosi,hii ilimuumiza sana,lkn wakati anafika Los Angeles,akawa amemua kitu kimoja,kwamba hakuna huzuni tena ila dawa ni moja tu,kuanzisha band mpya na kuifanya hiyo band iwe kubwa zaidi kuliko hiyo waliyo mtema,na awe maarufu sana,wamuone kwenye tv,na wamsikilize kwenye redio mbali mbali

Kweli alitafuta wapiga wazuri na akaunda band moja inaitwa Legendary Heavy Metal Megadeth,Mungu si Etugrul Bey kweli akafanikiwa kurekodi album yao ya kwanza na wakafanikiwa sana na kushika chat za juu,alipata mpunga wa maana na kuwa mtu famous sana

Mpiga gitaa huyu alijulikana kama Dave Mustaine,aliuza album kama Milioni 25 duniani kote,na ziara mbali mbali duniani


Lakini baadae ikafahamika kwamba kwa miaka mitatu (3) band yake ya zamani ambayo iliuza nakala milioni 180 ambayo inajulikana kama Metalicca ilikuwa imeshika rekodi ya band bora zaidi kwa wakati huo

Hili lilimuumiz sana huyu Dave,kuona band ambayo imefanikiwa zaidi ndiyo iliyo mpiga chini,yani pamoja na mafanikio aliyoyapata na umashuhuri na mpunga mrefu,bado kwake yeye ilikuwa ni failure kubwa

Hapa tunajifunza nini? Je kushindwa unakuchukuliaje?

Je kushindwa kwako ni kwasababu unajifananisha na mtu fulani au hali fulani au kushimdwa kwako kutokana na malengo ambayo umejiwekea na kwa bahati mbaya hujayafikia


No matter what, usijifananishe na mtu yeyote yule hapa duniani kwani utaishiwa kuwa disappointed

Mlinzi wa zamu!
 
Ez4pqemVEAAeXbT.jpg
 
Back
Top Bottom