JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mazungumzo ya Usiku

KILA MTU ANATAKA KUWA SHUJAA


Tekinolojia imetatua changamoto ya uchumi lakini imeleta shida kubwa sana na mvurugano katika jamii yetu katika zama hizi

Wale ambao hufanya mambo ambayo sio ya kawaida au ambayo yamepita kawaida ndio huwa mashujaa katika television,magazeti na mitandao ya kijamii,hao ndio hutrend na kuwa sehemu ya habar ya mjini


Tekinolojia inatufanya wote sasa tutake kutrend walau nasi tupate majina hapa mjini na hivyo kutuvuruga na kutufanya tupagawe,mfano kuna ambao wanaoga barabarani na kushoot clip zao na kweli wanatrend,kuna ambao huko ughaibuni wanaenda mashuleni na kuwapiga risasi wanafunzi risasi na wanatrend,na mambo kadha wa kadha

Kwahiyo kila mtu anapambana atoke vipi,saa nyingine tunafanya mambo hata ya kututoa utu wetu kwa jina la tekinoloji ili mradi tuwe vioral mitandaoni,na wakati mwengine tunaandika topic au nyuzi ambazo ni kichefu chefu kwakuwa tunajua ndio zinashika akili za watu basi tunaishi nazo,yaani ni kuvurugwa kwa kwenda mbele

Kwahiyo kwa kiasi fulani ingawa tekinolojia imeleta unafuu na wepesi wa mambo mengi lkn inatuvuruga sana,kwasababu tunajali sana baadhi ya mambo ili nasi tutrend

Kibaya zaidi tunajenga jamii ya kutaka kufanya mambo makubwa na ya kipekee kana kwamba maisha ndio yamepangwa kuwa hivyo,yani bila kufanya mambo ambayo sio ya kawaida inakuwa kama hatuiishi vile

Hao ambao wamefanya mambo makubwa na wanaendelea kufanya,walifanya kwa kujiendeleza na kuwa bora zaidi kwakuwa walifanya si kwa kuwa impress watu ila kwa kutaka kupata matokeo bora zaidi

Ila sisi kinyume chake tunataka greatness out of no where,hatuna misingi ya kutufikisha huko ila tunafanya chochote ili mradi nami Etugrul bey nitrend hapa town

Tumekuwa na jamii ambayo haiamini katika average ila katika extraodinary,yani tukiwa wa kawaida bado hatujaishi ila tukiwa zaidi ya kawaida ndio tunaishi,haya ni majanga

Kwa staili hii kwanini tusiwe na stress? Kwanini tusiwe hatuna furaha,kwanini tusiwe na misongo ya mawazo

Unajua kwanini inakuwa hivi?

Kwasababu tunajali sana hata kwa mambo ambayo hayana ulazima

Mlinzi wa zamu!
😅💯💯💯
 
Mazungumzo ya Usiku

THAMANI YA MAUMIVU

Mnamo mwaka 1944 Jeshi la Japan lilikuwa limetawanyika karibia eneo kubwa la Asia,lkn wakati huo huo ndio mambo yalibadilika dhidi yao ,Jeshi la Amerika lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti wajapani,na askari wa Japan walikuwa na machaguzi mawili tu ama wauwawe au wawe mateka

Lakini wakati huo huo aliteuliwa lutenanti Hiroo Onoda,huyu kazi yake au mission yake ilikuwa ni kuhakikisha anapunguza nguvu ya jeshi la marekani kwa gharama yoyote ile,na katu asikubali kujisalimisha

Mnamo mwaka 1945 mwezi wa august wakashushiwa bomu la nyuklia katika mji wa Hiroshima na Nagasaki na hapo Japan ilisalimu amri rasmi

Lakini huko katika uwanja wa vita lutenant Onoda alikuwa katika vita vya msituni nchini philiphine katika kisiwa cha Lubang,akiwa na watu wake kama watatu hivi aliendelea kupambana dhidi ya jeshi la Marekani

Yeye hakujua kama vita imeisha,lkn baadae Japan kwa kushirikiana na Marekani wakasambaza vipeperushi kutoa ujumbe kwamba vita imeisha,lkn pamoja na Lutenant Onoda kuona ujumbe huo,yeye aliamini hizo ni njama za Marekani katika kutaka kumdhoofisha,aliamini bado vita inaendelea

Alikuwa anavamia wanakijiji na kupora na kuwaua yeye na vijana wake,karibia miaka 30 huyu mwamba anapambana tu msituni,pamoja na jitihada kufanywa tena kwa kurusha vipeperushi kwamba vita imeisha lkn bado mwamba aliamini huo ni uongo tu,alichojua yeye ni kufanya misheni yake

Baadae akabakia yeye mwenyewe baada ya wenzie kufa,msako ulifanywa sana na majeshi kumtafuta lkn hakupatikana,kukawa na maneno mengi sana juu ya legend huyu huko Japan,hivyo ikampa hamasa kijana mdogo Suzuki ambaye aliacha shule na mapenzi yake makubwa ilikuwa ni kufanya adventure

Hivyo akaamua this time akamtafute huyo legend,kwakuwa kulikuwa na imani kwamba huenda bado yupo hai,akaenda huko kisiwa cha Lubang akiwa hana mbinu zozote za kijeshi wala dhana za kivita wala silaha

Alichofanya ni kuita kwa sauti kubwa "Onoda emperor anahuzunika kwa kutopatikana kwako' na cha kustaajabisha ndani ya siku nne tu Suzuki alimpata lutenant Hiroo Onoda

Watu hawa wakawa marafiki huko msituni, Onoda baada ya kugundua kuwa ni kweli vita ilishakwisha alishangaa na kuhuzunika sana,lakini alisema wala hajutii kwa yalitokea kwasababu alikuwa anatimiza mission yake

Hiroo Onoda akamuuliza sababu gani iliyomfanya kijana mdogo kama Suzuki kwenda msituni kumtafuta yeye, Suzuki akajibu kuwa alikuwa na mission tatu,ya kwanza ni kumtafuta Onoda,ya pili ni kumtafuta Panda na tatu ni kwenda kumtafuta Snowman/mtu wa barafu huko Himalayas

Kweli huyu dogo aliendelea na adventure yake ambayo huenda baridi kali huko ilikuwa ndio kifo chake

Baada ya Onoda kurudi Japan mwaka 1975 akawa mtu mashuhuri sana,si televisions wala redio stations zote zilikuwa zikimuarika kwa mahojiano ya hapa na pale,na vile vile akachapisha kitabu,pamoja na hayo yote serikali ikampa hela nzuri sana

Lakini Onoda alikuwa na huzuni juu ya maadili ambayo yamebadilika nchini kwake Japan,sasa haikuwa tena ile Japan aliyoipigania na kuwa tayar kufa kwa ajili ya taifa lake,ilikuwa Japan ya kibepari,wanawake wanavaa nusu uchi kama nchi za magharibi

Hili lilimpa huzuni sana hakufurahia tena maisha ya Japana,kwakuwa sio ile Japan ambayo aliipigania,kwake ni afadhali angeendelea kuishi msituni huko Lubang nchini Philiphine kuliko kuona Taifa lake la Japan lilivyobadilika

Mnamo mwaka 1980 akaamua kuhamia kl Brazil na ndiko alikofia huko

Lutenant Hiroo Onoda alijali sana kuhusu Japan ya zamani ambayo alikuwa tayar kufa kwa ajili yake,na hakuwa tayar kuikubali Japan mpya,na huo ndio ukawa mwanzo wa kukosa furaha na kuwa na msongo wa mawazo

Nasi hivyo hivyo huwa kama Lutenant Onoda,huwa tunashindwa kukubali kwamba kuna mambo fulani fulani katika maisha yetu lazima yabadilike,na hatuwezi kuyazuia,tuna option mbili ama tukatae ukweli tuwe na huzuni pamoja na stress au tuuKubali ukweli na kwenda nao sawa na tuwe na furaha

Mlinzi wa zamu!
 
Back
Top Bottom