Mazungumzo ya usiku
JITAMBUE WEWE BINAFSI
Tuchukue mfano wa kitunguu,kitunguu kina layer mbali mbali au maganda ambayo yamebebana kutoka juu kwenda chini
Na kadri utakavyo zidi kuyatoa ndio kuna uwezekano mkubwa wa kujikuta unatoa machozi
Jambo la kwanza mtu anatakiwa ajue kuhusu hisia zake,ajifahamu anahisia zipi,kadri anavyozidi kujichunguza atazidi kufahamu je hisia hizi ni za furaha au huzuni
Na baada ya kujua hisia zake,mathalani amejitambua kwamba ana husia za huzuni,basi hatua inayofuata anatakiwa ajiulize je hizi hisia zinasababishwa na nini?
Na hapa ndio kwenye mtihani mkubwa,kwa kutojua nini hasa ni sababu ya kuhisi hivi tunavyo hisi basi inakuwa vigumu kutatua changamoto ambayo iko mbele yetu
Usipopata sababu halisi zinazo sababisha huzuni yako tegemea kutotua tatizo na kuendelea kupata huzuni siku zote
Badala yake utakuwa unajiipoza kwa kujipa furaha ya mda mfupi na baadae tatizo liko pale pale
Mfano unasumbuliwa na tamaa ya kutaka hiki na kile,kila fashion mpya ikiingia unataka uende nayo sawa,kuna simu toleo jipya unataka upate,gari toleo jipya unataka uwe nalo
Matokeo yake ukivikosa unakuwa na huzuni,sasa usipojichunguza kwa makini unawe dhani kwamba tatizo la huzuni yako tatizo la kutokuwa na pesa ya kununua product mpya,matokeo yake hata ukipata pesa na kupata vitu hivyo,utafurahi baada ya mda,ila ikija model mpya utakuwa na huzuni tena
Lkn kumbe lau ungejichunguza kwa makini ungejitambua kwamba tatizo au chanzo cha huzuni yako ni HUTOSHEKI NA ULICHO NACHO
Lau ukijua kumbe shida yangu ni kutotosheka na nilicho nacho ndio chanzo cha huzuni yangu,,,litakuja swali la pili,je nifanye nini ili niepukane na tabia hii
Jibu ambalo ni la kudumu la kuondoa huzuni yangu ni KUJIFUNZA KUTHAMINI NILICHO NACHO PAMOJA NA KURIDHIKA NACHO
Hapo utakuwa na amani pamoja na furaha siku zote
So jichunguze na jitafakari na ujitambue
Mlinzi wa zamu!