Mazungumzo ya usiku
MAMBO AMBAYO TUMEYAZOEA LAKINI HUTULETEA SHIDA
Q/ Starehe
Starehe ni nzuri lkn huwa inatuletea matatizo mengi sana,kwanza ni rahisi kuipata na rahisi kuifurahia
Ila hutuathiri sana wengi wetu,muulize mtumia madawa ya kulevya yoyote je mwisho wa siku alipata nini? Muulize mwanaume au mwanamke malaya je mwisho wa siku alipata faida gani? Wengi wao hutelekeza familia kwa kuendeleza starehe,wengi hukosa kizazi kwa kutoa sana mimba,wengi hupata maradhi kutokana na athari za pombe na vilevi mbali mbali
Na kibaya zaidi ni product ambayo huwa tunatangaziwa na kuhamasishwa masaa 24,na mwisho wa siku tunaingia kwenye mfumo na kupata madhara kibao
b/ Material success
Watu wengi wanapima utajir au uwezo wao kutokana na kiasi gani cha fedha wanachomiliki,au ni mali ngapi anamiliki,au ni gari ngapi za kifahari anazimiliki
Utafiti unaonyesha kwamba pale mtu anapoweza kupata physical basic needs kama chakula,makazi na mavazi na kadhalika,basi uwiano wa furaha na utajiri huwa karibia na zero
Kama una njaa uko India,ongezeko la dola elfu 10 kwa mwaka litakupa furaha lkn kama upo developed countries ongezeko la dola elfu si chochote kwako,hii maana yake nini? Ina maana unajiumiza mwenyewe kwa kufanya kazi overtime,na wikiend for nothing
Ubaya mwingine wa kuweka sana mkazo kwenye material things kunatufanya kutoyapa kipaumbele mambo mengine yenye thamani katika maisha yetu,kama uaminifu,upendo,kujali,huruma
Pale watu wanapokuwa hawapimi thamani yao kutokana na tabia zao ila kwa kutumia vitu vya kushikika na vya kupita wanakuwa kama wajinga
Mlinzi wa zamu!