JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Mazungumzo ya usiku

Muendelezo wa mazungumzo ya jana.....


c/ Tabia ya kuwa Sahihi mda wote

Ubongo wetu sio mashine ambayo ipo sahihi,huwa inafanya makosa,ni mara ngapi tunafanya maamuzi kwa kutumia hisia,tunatabia ya kuwajaji watu,tunakuwa na dhana juu ya mambo mbali mbali tofauti na ukweli halisi

Ukweli ni kwamba watu ambao wanapenda kuwa sahihi kwa kila kitu huwa wanajikosesha nafasi ya kujifunza mambo mapya,wanashindwa kuyaona mambo katika mtazamo mwingine tofauti na wanao uamini wao,watu hao vile vile wanashindwa kujifunza kutokana na makosa yao

Ni vizur zaidi kujifanya hujui na mjinga ili ujifunze mambo mengi zaidi.



d/ Kuwa positive muda wote

Kuna watu ambao wanaangalia thamani ya maisha yao kwa kuwa positive mda wote,akikosa kazi anasema walau amepata mda wa kuexplore,mume wake akicheat na dada yake anasema it's okay walau amemjua mumewe ni mtu wa aina gani

Ila kuna wakati maisha yanazingua sana na kitu bora cha kufanya ni kukubaliana na ukweli tu

Kujaribu kuzikwepa negative emotions ni sawa na kuzidi kuleta matatizo zaidi

Wakati mwingine kuwa positive ni njia ya kukwepa ukweli wa mambo na sio suluhisho la kudumu la kutatua matatizo yako


Kuna nyakati watu wanatuuzi,mambo hayaendi sawa na dili zina buma,kwahiyo kuukubali ukweli na kuwa na negative emotions ni kitu cha kawaida kabisa na ndio ubinadamu wetu

Kukataa negative emotions ni kuleta matatizo na hatutopata suluhisho la kudumu

Siri moja nzuri ya negative emotions ni kuiexpress katika namna nzur inayokubalika na jamii na katika namna inayoendana na thamani yako

Kwa mfano value ya Etugrul bey ni kutopenda ugomvi,kwahiyo nitasolve jambo kwa mazungumzo zaidi,na wewe unajua value yako msomaji wangu

Kwa mfano ninapokuwa na hasira naielezea kwa mhusika lkn sichukui hatua ya kurusha ngumi,hasira kama hasira sio tatizo kwakuwa ndio asili tuliyo umbwa nayo,ila kibaya ni kuielekeza hasira katika ugomvi na uharibifu

Kitu cha msingi ni kuwa na maono mazuri ya thamani yetu na furaha itakuja kama matokeo ya kuwa na good value

Mlinzi wa zamu!
 
Huwa nawakubali sana ninapoona walinzi wanao sign in mida ya night kali!


Hii inaonyesha lindo halibaki bila ulinzi
 
Back
Top Bottom