Nikilala kila movement sauti itakayokua karibu yangu basi hua naisikia.
(Hasa ukitaja jina langu)
Sasa kuna jamaa alikua form 4 mm niko form 2 alikua anakuja tunasoma. Siku moja kaja kunigongea saa4 usiku nimelala nikamfungulie aingie tusome.. Nikamsikia nikawa naamka nikafungue Usingizi ukanipitia tena moja kwa moja sijaenda kufungua.
Cha ajabu nikaota kua nilienda kumfungulia akaingia tukasoma kuna kisehem alikua ananifundisha kipya. After 2 hour tukaenda kulala. Sasa asubuhi naamka nijaandae kwenda shule namuangalia mwenzangu niliyelala nae simuoni kitandani. Ndio nikajua yote usiku nilikua naota.
Keaho yake jamaa akaniambia kua aliniita nikaitika ila sikumfungulia Why? Ikabidi nijieleze!!! Cha ajabu kile nilichofundishwa kipya Kwenye ndoto nikabaki nacho kichwani nakielewa!!!
Hii situation sijawahi kuielewa