Day 03
wale jamaa wamerudi tena ila Leo nashangaa wamewahi siku ile ilikuwa around saa saba ila Leo wako wachache wapo wawili mmoja anachana wavu mwengine anameshika spray ila sio dirisha lilelile la mbele kidogo nawachungulia tu nawachora hii ni kweli wakuu sio utani
Badala ya kurudishia pazia taratibu na kuendelea kuchati humu kama siku ile nilivyowaona Mara ya kwanza niwakaelezea humu nimeona niache ujinga
Hapa nimeamua niache upuuzi nimezima taa ya nyuma ya upande wa kwangu ambayo kamwanga kanaelekea hadi nyumba ya jirani kule kwa mbali ambayo madirisha yake ya nyuma yanatizamana na yangu kwa nyuma kumekua Giza kidogo nimerudishia pazia taratibu nimechukua simu haraka kwa upesi ndo nimeingia jf naperuzi
23:57
Sent using
Jamii Forums mobile app