Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Source : Mwananchi kwenye habari ya DCI Manumba .......

......

"Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa," alisema Zitto katika taarifa yake kwa Mwananchi.

Hapo Zitto kafulia. Hakuna jipya atakoweza kulifanya ambalo halijawahi kufanyika duniani. Yote tuyaonayo leo yalishafanyika zamani na yanafanyika sasa kwingineko ambayo vyombo vya habari ama havijaona au havioni kama ni news.

Yeye aseme tu kwamba anapumzika awaachie wengine wenye moto mpya kuendeleza yale aliyoyafanya katika mchango wake kama kiumbe hai.

Leka
 
Na Mwandishi wetu
7th December 2009

headline_bullet.jpg
Asema zipo njama kuhamisha ajenda ya ufisadi
headline_bullet.jpg
Adai kunasa mawasiliano ya Zitto na mwingine
headline_bullet.jpg
Ajigamba Chadema hakina mgogoro, kipo imara

Slaa%20na%20Zito.jpg

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa (kushoto) na Zitto Kabwe.

Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, amesema kuna vita kali sasa ya baadhi ya watu kufanya njama za kuhamisha ajenda ya vita dhidi ya ufisadi na kuzungumzia masuala ya mbunge wao, Kabwe Zitto.

“Nadhani sasa Watanzania wanatakiwa wakaelewa…naona sasa kuna vita kali ya kuiondoa ajenda ya vita dhidi ya ufisadi, na sasa wanataka kutuelekeza kumjadili mtu, Zitto.

Na mimi nasema hatuhitaji kujadili watu isipokuwa chama,” alisema Dk. Slaa wakati akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana na kuongeza: Chadema hakina mgogoro na kipo imara na hiyo ilithibitika wakati na baada ya Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Septemba, mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu madai ya Zitto kutembea na barua ya kujiuzulu Chadema, Dk. Slaa alisema ofisi yake haijapata barua, maelezo yoyote au ushauri kutoka kwa Zitto unaoelezea suala hilo.

“Hatuwezi kuendelea na mambo haya ya kuhamisha ajenda ya vita dhidi ya ufisadi na kuanza sasa kujadili suala la mtu binafsi, kama ambavyo sasa inaanza kujitokeza,” alisema.

Alisema Chadema ni taasisi itaendelea kuwepo hata kama yeye ama Mbowe (Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho) au Zitto wataondoka katika chama hicho.

Alisisitiza kuwa chama hicho kitaendelea kupiga vita ufisadi kwa nguvu zote licha ya baadhi ya watu kuanza kudhoofisha ajenda hiyo.

Akifafanua kuhusu suala la Zitto, Dk. Slaa alisema siku moja saa 1:00 jioni kabla ya Mkutano Mkuu wa Chadema uliopita, alipata nafasi ya kuzungumza na mama ya Zitto, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Shida Salum, aliyemhakikishia kwamba Zitto hahusiki na mambo hayo.

“Siku moja kabla ya Kamati Kuu, niliongea na mama yake Zitto na akanihakikishia kwamba hahusiki na mambo haya yanayojitokeza ya kukichafua chama,” alisema.

Alisema alielezwa na mama huyo kuwa wapo watu wanaomtumia Zitto kwa maslahi wanayoyajua wenyewe na kwamba mtu mmoja (jina linahifadhiwa) anayo password ya anuani ya barua pepe ya Zitto ambayo anaitumia kuandika taarifa mbalimbali alizoeleza zinaonyesha kama vile zinatoka kwa Zitto.

Lakini alisema baada ya mazungumzo na mama huyo, kesho yake gazeti moja lilikuwa na habari ya Zitto kukanusha kwamba hahusiki na suala la David Kafulila isipokuwa watu wametumia jina lake.

Dk. Slaa aliongeza baada ya mazungumzo hayo, asubuhi yake alipata taarifa za barua pepe kutoka kwa Mtanzania mwema zinazoonyesha mawasiliano kati ya Zitto na mtu mmoja (jina linahifadhiwa).

Bila kueleza kwa undani taarifa mbalimbali zilizokuwemo katika barua hizo pepe, alisema kwa kifupi kwamba zilikuwa zikionyesha mawasiliano ya kichama kati ya mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam na Zitto ambaye kwa sasa yupo masomoni nchini Ujerumani.

Alisema baada ya kuzisoma aliwasiliana na mkazi huyo wa Dar es Salaam akitamka athibitishe iwapo mawasiliano hayo ya barua pepe yalikuwa ya kwake au la.

Alisema alifanya hivyo kwa kumtumia ujumbe na baada ya muda mkazi huyo alimpigia Dk. Slaa, na akathibitisha kwamba anazitambua barua hizo na mawasiliano hayo yalikuwa ni ya kwake.

Lakini baadaye katika mazungumzo yao ya simu, mkazi huyo wa jijini alimweleza Dk. Slaa kwamba ameingilia mawasiliano yao binafsi, jambo ambalo alilipinga.

“Nilimweleza mkazi huyo kwamba sijaingilia mawasiliano binafsi, kwa kuwa taarifa zilizokuwa zikizungumzwa katika barua hizo zilikuwa zikikihusu Chadema na kwa maana hiyo hazikuwa binafsi,” alisema.

Alisema baadaye mkazi huyo alimjibu Dk. Slaa kwamba anafanya kazi katika kampuni kubwa na kwamba Dk. Slaa hataiweza na afadhali aache.

Aliongeza baada ya gazeti moja kuchapisha habari za Zitto jana, alimtumia Zitto ujumbe wa barua pepe akitaka maelezo kuhusu habari hizo zilizodai kuwa anatembea na barua ya kujiuzulu Chadema.

Dk. Slaa alisema tangu alivyomtumia ujumbe huo jana asubuhi, hajapata majibu yoyote hadi alipowasiliana na Nipashe saa 11:00 jana jioni.

CHANZO: NIPASHE 12/07/2009
Chadema ni taasisi..Hivyo hata kama Zitto akitoka na atoke...Hakika Chadema itaendelea kuwepo...na itazidi kupata umaarufu...Whos Zitto By then..Let Him go even 2day..Hell....Alafu wee...Kubwajinga ni Jinga Kweli kweli do u think Chadema ni Zitto only,...Jinga Kabisa wewe.....
 
huyu aondoke bana anatuvuruga tu akili hapa...Kwani ZITTO nani?he is just another sisimizi ..nenda mwana kwenda wafuate wenzio wakina kafulila
Strong point Kigogo,na aende zake!
 
Kwa heshima na Taadhima ya wana jamii Forums!! Tunakuomba mheshimiwa zitto jitokeze uweke mambo wazi!! Tumechoka kusikia ''udaku'' kwenye media. Please come out and speak!!! sincerely we are missing you out here! hope this message gets home. just hit the nail on the head man!!!!
 
Wanasiasa wa Tanzania bwana, yaani mtu anatoa an open ended statement kama hiyo. Mbunge wa kutumainiwa huyu.

Aliyekuwa anajenga suspense kwa kusema "I'm gonna do a song, that you have never heard before" alikuwa James Brown, na ile ilikuwa showbizz, sasa hizi rants za ki showbizz zinatoka wapi katika siasa zetu?

What am I talking about, as if Siasa is not the low end of showbizz.

Sasa hapa kawaachia watu interpretation.Wanaotaka kusema Zitto anataka kunywa vidonge sawa, wanaotaka kusema Zitto anataka kumcharanga mtu risasi sawa, maana kasema anataka kufanya kitu ambacho hakijawahi kufikiriwa bila kukisema specifically, hata kutoa hint tu.

Huyu huyu mtu analalamika waandishi wanavyomuandika, halafu hapo hapo anawapa an open ended quotation, open to any interpretation, ammunition for some more malicious articles.Huyu mtu yuko serious kweli au ana enjoy hii attention (any publicity is good publicity style)?

Emotional instability ikikufanya uwe controlled na story badala ya wewe kui control story unaonyesha jinsi usivyo na uwezo wa kuongoza.

Huyu anaenjoy publicity, hana lolote na atakuwa na mawasiliano na hawa watu wa media
 
tushamchoka na yeye;uamuzi gani utakuwa mpya...kila mtu anamtabiria kuhama,,lipi jipya labda kuhamia ccm!!!!
 
Chadema ni chama cha kikabila na kikanda tulizungumza zamani toka enzi za mswahili miaka ile ya 2007 na 2006.

sasa true color inaonekana.

kufa kwa chadema ni fahari kwa kila mtanzania asiependa ubaguzi, naamini chama ambacho kingeliipeleka tanzania niipendayo pabaya ni chama hiki ambacho pia kina udini wa kutupwa.

chadema kife ili watanzania watulie.

chama mbadala kitazaliwa lkn sio chadema.
 
May be uamue kujinyonga ndo tutakushangaa, mengine yoyote utakayoamua ni ya kawaida tu kwa binadamu, we hautakuwa wa kwanza kuamua yafuatayo.

Elnino,hata kujinyonga mbona ni kitu cha kawaida tu siku hizi,yeye afanye lolote analotaka,na aone kama watu watashangaa! Pana kitu kigeni hapa Duniani ambacho hakijafanyika kweli?
 
High expectations za wabongo na kuzalisha touchables na untouchables kutaendelea kurudisha maendeleo ya Tanzania na watanzania kwa ujumla kama mijadala yenyewe ndio hivi. Chadema ni chama kama vilivyo vingine kwa hiyo matatizo yaliyo katika vyama vingine pia yako chadema na lazima na wao wapewe vidonge manake hakuna jiwe litakaloachwa bila kugeuzwa.

Hata wale wanaoshambulia CCM na serikali kila kukicha wanashindwa kukubaliana linapofika swala la Chadema na viongozi wake kukoselewa au kuboronga. Manake kama katibu wa chama kama CEO anashindwa kuongea na subordinates wake na kukimbilia kujenda mijadala isiyo na tija katika media za kibongo iliyona na negative tune unategemea nini kama sio kutuchanganya wananchi.

Slaa na Zitto ni viongozi wenye haiba kubwa katika chama wakae wao chini kwanza wajadiliane halafu ndio waende katika media sio kila moja anaenda kivyake na kuongea mambo yasiyoisha yanayomuhusu mwengine zamani Pascal Mayala alikuwa na kipindi cha kiti moto kama vipi kirudiwe manake kilikuwa kinaondoa majungu ya wanasiasa mtu akichonga pembeni anaitwa a flow live na mshindani wake odience na viewers wanaondoka na majibu. Sio sasa kila mtu anafake tuamini anachotaka kutueleza akiwa pekee na kushambulia upande mwingine.
 
- Mkuu Lunyungu, heshima mbele sana toka niingie JF sijawahi kuona ukiwa emotional like this, ninasema hivi kama kuna waliokuelewa hakuna wa kunizidi, na umenikumbusha tulipoongea kwa simu last time ukiwa kwenye uchaguzi Biharamulo, bado sijahau swali moja uliloniuliza kwamba all the games CCM played katika kuidhinisha ugombea wa Oscar, ili iwe nini?

- Maneno yako yote hapo juu ni 100% right, Chadema ikifa then itakuwa nini? Sidhani kama wengi tunajiuliza maswali serious namna hii, nimesema mara kwa mara kwamba kama sio Chadema, leo serikali ya CCM ingekuwa inatuchapa viboko bara barani!

- However: Kuharibika kwa hewa huko Chadema sasa hivi, ninawalaumu sana wazee wa huko kwa kukosa busara nzito za kuendesha siasa za taifa kichama, hakuna modern tactics, hakuna smart political strategies, huko Chadema inaonekana wanachama na viongozi wanajiendea tu na kufanya anything, I mean mwanachama mdogo sana na wa kawaida ana nguvu za ajabu za hata kuweza kuitisha press conf. na kusema siri nyingi za chama, sasa you wonder amezijuaje kama zinatakiwa kuwa siri tena za juu?

- Freeman amejitahidi sana lakini na yeye anafika mahali anahitaji msaada, bado ni mchanga pia kisiasa na hasa busara za siasa za taifa, mnamnyima Zitto uenyekiti, sawa mlitakiwa kutathmini matokeo bila kuwa bias, mlihitaji a devil advocate wa kuweza kuwaambia msiyoyataka, kwamba Zitto ni maarufu na yuko juu sana kisiasa, sasa kwa sababu hamumpi uenyekiti, basi mpeni hata umakamu, au kama hamumutaki kwenye chama, basi mruhusuni agombee mkamchinje kwenye majukwaa na uwe ndio mwisho wake kisiasa, lakini kwa mnayoyafanya sasa hivi, sio siri kwamba mna safari ndefu sana kwa sababu mmeshindwa kutathmini the effect ya Zitto na kukosa uenyekiti, sasa mzimu wenu wenyewe unawala!

- Sijawahi kuona siasa foolish kama hizi mnazozifanya sasa, unamnyima kiongozi maarufu wa chama chako kugombea nafasi kubwa, halafu unaanza kumnyanyasa kwa njia za kijinga jinga ambazo hata ukiulizwa na wenye akili nyingi huwezi kuzi-defend, wala kuzi-define ukaeleweka, hujui kwamba in-the process unazidi kumjenga, huku ukikaribisha unwanted attention ndani ya chama chako, sasa unaona kina Manumba wameshaanza kujisogeza pole pole, the next thing utamsikia Hosea akija huko kunusa nusa halafu mtaishia kulaumu kila mtu isipokuwa nyinyi wenyewe ambao ndio hasa chanzo cha huu upuuuzi!

- Mkuu Lunyungu, hapa niko na wewe kwamba Chadema wanahitaji kuweka sawa nyumba yao, a house divided against itself haiwezi kusimama na kutusaidia taifa, wazee huko Chadema hebu kaeni chini na Zitto, mumsikilize anasema nini na anataka nini, sio lazima mumpe kila kitu anachotaka lakini ikibidi mkutane kati kati basi, na kufanya hivyo kwenye siasa sio kushindwa wala ujinga ndio smart modern politics zinavyotaka, ninarudia tena maneno yangu ya juzi kwamba Chadema, kukua kwenu na kufa kwenu, sasa hivi kunategemea mtakavyo -deal na hii ishu ya Zitto, msim-underestimate huyu mtajimaliza wenyewe, sasa ondoeni hizi habari zenu kwenye media kwanza, waiteni wale wote waliojitoa muone kama mnaweza kuwarudisha chamani un-conditionally, na ndugu yangu Freeman kama haya maji ni mazito mno basi busara hapa ni kuachia ngazi ikibidi kwa manufaa ya chama.

- Hivi Chadema mmeshawahi ku-imagine mkifa mtakuwa mmetufanyia nini wanachi wa Tanzania? I mean inasikitisha sana eti! Dr. Slaa kwa kusema haya uliyoyasema hadharani exactly unategemea ku-accomplish what? Mawasiliano ya siri ya Zitto yanayolindwa na sheria ya jamhuri kama haki zake za kibinadam wewe umeyapataje kama hukuvunja haki zake kisheria? Hivi huko chadema hakuna washauri wa siasa wala sheria?

Respect.

FMEs!

Maneno haya yanaingia mpaka kwenye mifupa....

wanachadema wale vichwa vya panzi hawajui athari za hii migogoro utasikia mwache aende, halafu hawapigi mahesabu chadema/upinzani wanarudi nyuma miaka mingapi!!
 
DCI: Zitto, tuletee tuhuma za chadema
broken-heart.jpg
Na Ramadhan Semtawa

SIKU chache baada ya naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kulalamika kuingiliwa kwenye anuani yake ya barua pepe, Jeshi la Polisi limesema kuingilia mawasiliano ya faragha ya mtu ni jinai na kumtaka mwanasiasa huyo atoe taarifa polisi ili waanze kulishughulikia.

Zitto, ambaye yuko Ujerumani ambako anasoma, alikaririwa na vyombo vya habari wiki iliyopita akidai kuwa anaingiliwa mawasiliano katika anuani yake ya barua pepe (e-mail), kitu alichosema ni aghalabu kufanywa hata na Idara ya Usalama wa Taifa.

Zitto, ambaye juzi alituma barua pepe kwenye gazeti hili kulalamikia kitendo hicho huku akitangaza kutembea na barua ya kujiuzulu uongopzi Chadema, alieleza kusikitishwa na kitendo hicho ambacho alidai kinafanywa na chama chake.

Hata hivyo, DCI Manumba alipoulizwa jijini Dar es Salaama jana kuhusu malalamiko ya Zitto, alijibu: "Sisi hutujapata rasmi malalamiko hayo, lakini akileta tutachunguza kwa kuwa si sahihi kuingilia mawasiliano ya mtu."

Kwa mujibu wa DCI Manumba, mawasiliano ya barua pepe na mengine ni faragha hivyo ni makosa kwa mtu yeyote kuingilia mawasiliano ambayo hayamhusu.

"Kwa kawaida ni makosa kuingilia mawasiliano ya mtu siku zote tukipata taarifa kama hizo tunachoweza kufanya ni kuchunguza kuthibitisha kwanza kwani ni suala kitaalamu zaidi," alifafanua DCI Manumba.

DCI aliongeza kwamba, siku zote wamekuwa wakichunguza malalamiko yote yanayofikishwa kwao kama yanahusiana na uingiliaji wa faragha ya mtu ikiwemo mawasiliano yake.

Alifafanua kuwa iwapo mlalamikaji akifikisha malalamiko yake, wao huwa hawasiti kuchunguza bila kuangalia jambo lenyewe lina mlengo gani.

"Ni sawa na mtu akimpiga mkewe sisi tukiletewa taarifa, kwanza tunachunguza halafu tunachukua hatua za kisheria kwa mhusika baada ya kujiridhisha. Kwa hiyo hata yeye (Zitto) akileta tutachunguza," aliongeza.

"Siku zote tunafanyia kazi taarifa zinazotufikia, kama kuna mtu anazo taarifa akileta kwamba mawasiliano yake yameingiliwa tutafanyia kazi tukio hilo ili kujiridhisha."

Malalamiko ya Zitto yalitokana na taarifa iliyotolewa na chama hicho kilichodai kuwa ofisa habari aliyetimuliwa, David Kafulila anatumia anuani ya barua pepe ya Zitto visivyo halali. Kafulila na Zitto ni marafiki wakubwa.

"Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa," alisema Zitto katika taarifa yake kwa Mwananchi.

Alisisitiza kwamba kamwe hatasukumwa na Chadema na kwamba "wanapaswa waniache nipumzike na kufanya mambo yangu".

"Hakuna mtu ananayeweza kuzungumza kwa niaba yangu hata kama ni rafiki yangu, siasa siyo chaguo langu la pekee katika maisha," alisema.

Katika kuonyesha kuchukizwa na baadhi ya taarifa alizoziita za kizushi zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku (si Mwananchi), Zitto, alisema: "Faragha yangu ni faragha yangu, Zitto ni Zitto kama yeye na siyo mali ya Chadema.

Akizungumzia uhusiano wake na Kafulila aliyehamia NCCR-Mageuzi kutoka Chadema, Zitto alisema: "Siku zote msimamo wangu umekuwa kwa wale wanaokandamizwa... na katika hili David (Kafulila) ndiye anayekandamizwa."

Alisisitiza kwamba kamwe hatasukumwa na Chadema katika kufanya mambo yake.

"Hakuna mtu ananayeweza kuzungumza kwa niaba yangu hata kama ni rafiki yangu, siasa siyo chaguo langu la pekee katika maisha yangu."

"Msimwandame Kafulila. Mumwache mtoto wa watu. Mmeshamwita sisimizi inatosha. Msijaribu kunigombanisha na Kafulila. Sitaki... sitaki... sitaki," aling'aka Zitto

SRC
MWANANCHI
 
Kwa yote yanayomkamkabili Mh. Zito ni sehem ya matunda ya siasa changa ndani ya nchi na vyama vyenyewe. Zito siyo malaika hivyo kuwa na makosa ni moja ya sifa ya kibinadamu lakini ubinadamu wake unakamilika pale anapotambua makosa yake. Nimeuona wasifu huo kwa Zito pekee ndani ya CHADEMA, lakini ninafadhaishwa na utukufu wanaojivika wakuu wengine ndani ya CHADEMA!! Jamani tuwe wakweli kuwa kuna mmomonyoko usiojua nyakati ndani ya CHADEMA, CCM ni chama chenye matatizo makubwa ndani yake hapa nchini ila wao wana sifa mmoja ya kujivumilia katika nyakati maalum. Zito ni kijana mwenzetu, jasiri, mweledi na muungwana, nadhani wasaa umefika sasa kwake kujiweka sawa na kuangalia mbele kwa niaba ya maslahi ya Umma na siyo chama au genge la watu wachache.

Akibaki ndani ya CHADEMA sawa,Akienda CCM sawa, NCCR sawa, akirudi katika uanaharakati vema.

Wana Jf tusimuhukumu Mh.Zitto, tukiangalie CHADEMA kama taasisi dhidi mtu mmoja tu na nguvu wanayoitumia sasa.

All the best Mheshimiwa Zitto, binafsi ninakuunga mkono kwa maono yako kisiasa na kianaharakati. Big up Young Brother
Kati
 
DCI: Zitto, tuletee tuhuma za chadema
broken-heart.jpg
Na Ramadhan Semtawa

SIKU chache baada ya naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kulalamika kuingiliwa kwenye anuani yake ya barua pepe, Jeshi la Polisi limesema kuingilia mawasiliano ya faragha ya mtu ni jinai na kumtaka mwanasiasa huyo atoe taarifa polisi ili waanze kulishughulikia.

Zitto, ambaye yuko Ujerumani ambako anasoma, alikaririwa na vyombo vya habari wiki iliyopita akidai kuwa anaingiliwa mawasiliano katika anuani yake ya barua pepe (e-mail), kitu alichosema ni aghalabu kufanywa hata na Idara ya Usalama wa Taifa.

Zitto, ambaye juzi alituma barua pepe kwenye gazeti hili kulalamikia kitendo hicho huku akitangaza kutembea na barua ya kujiuzulu uongopzi Chadema, alieleza kusikitishwa na kitendo hicho ambacho alidai kinafanywa na chama chake.

Hata hivyo, DCI Manumba alipoulizwa jijini Dar es Salaama jana kuhusu malalamiko ya Zitto, alijibu: "Sisi hutujapata rasmi malalamiko hayo, lakini akileta tutachunguza kwa kuwa si sahihi kuingilia mawasiliano ya mtu."

Kwa mujibu wa DCI Manumba, mawasiliano ya barua pepe na mengine ni faragha hivyo ni makosa kwa mtu yeyote kuingilia mawasiliano ambayo hayamhusu.

"Kwa kawaida ni makosa kuingilia mawasiliano ya mtu siku zote tukipata taarifa kama hizo tunachoweza kufanya ni kuchunguza kuthibitisha kwanza kwani ni suala kitaalamu zaidi," alifafanua DCI Manumba.

DCI aliongeza kwamba, siku zote wamekuwa wakichunguza malalamiko yote yanayofikishwa kwao kama yanahusiana na uingiliaji wa faragha ya mtu ikiwemo mawasiliano yake.

Alifafanua kuwa iwapo mlalamikaji akifikisha malalamiko yake, wao huwa hawasiti kuchunguza bila kuangalia jambo lenyewe lina mlengo gani.

"Ni sawa na mtu akimpiga mkewe sisi tukiletewa taarifa, kwanza tunachunguza halafu tunachukua hatua za kisheria kwa mhusika baada ya kujiridhisha. Kwa hiyo hata yeye (Zitto) akileta tutachunguza," aliongeza.

"Siku zote tunafanyia kazi taarifa zinazotufikia, kama kuna mtu anazo taarifa akileta kwamba mawasiliano yake yameingiliwa tutafanyia kazi tukio hilo ili kujiridhisha."

Malalamiko ya Zitto yalitokana na taarifa iliyotolewa na chama hicho kilichodai kuwa ofisa habari aliyetimuliwa, David Kafulila anatumia anuani ya barua pepe ya Zitto visivyo halali. Kafulila na Zitto ni marafiki wakubwa.

"Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa," alisema Zitto katika taarifa yake kwa Mwananchi.

Alisisitiza kwamba kamwe hatasukumwa na Chadema na kwamba "wanapaswa waniache nipumzike na kufanya mambo yangu".

"Hakuna mtu ananayeweza kuzungumza kwa niaba yangu hata kama ni rafiki yangu, siasa siyo chaguo langu la pekee katika maisha," alisema.

Katika kuonyesha kuchukizwa na baadhi ya taarifa alizoziita za kizushi zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku (si Mwananchi), Zitto, alisema: "Faragha yangu ni faragha yangu, Zitto ni Zitto kama yeye na siyo mali ya Chadema.

Akizungumzia uhusiano wake na Kafulila aliyehamia NCCR-Mageuzi kutoka Chadema, Zitto alisema: "Siku zote msimamo wangu umekuwa kwa wale wanaokandamizwa... na katika hili David (Kafulila) ndiye anayekandamizwa."

Alisisitiza kwamba kamwe hatasukumwa na Chadema katika kufanya mambo yake.

"Hakuna mtu ananayeweza kuzungumza kwa niaba yangu hata kama ni rafiki yangu, siasa siyo chaguo langu la pekee katika maisha yangu."

"Msimwandame Kafulila. Mumwache mtoto wa watu. Mmeshamwita sisimizi inatosha. Msijaribu kunigombanisha na Kafulila. Sitaki... sitaki... sitaki," aling'aka Zitto

SRC
MWANANCHI

JF

Tanzania hatuna sheria juu ya mawasiliano ya Computer kwamba je mtu akitumia vibaya mtandao inakuwaje kwa mfano
Nikitumia mtandao na kuniwezesha kutoa hela kwenye account A kwenda Account B, je mkinikamata mtanifunga kwa sheria ipi? waingeleza na nchi zingine za ulaya wanazo hizo ACT. je jeshi letu la police lina mbinu za kubaini wizi wa namna hii?

La pili na muhimu ni kwamba inategemea email aliyokuwa anatumia bwana Zitto kuwasilana na jamaa zake ni ipi, kama ni ya CHADEMA ukumbuke email za kampuni au za kazini ni mali ya mwajiri na kuna policies zake kwa mfano boss anaweza ku-redirect email zako kwake kama ana suspect yeyote na huwezi mshitaki na pia anaweza kutumia vielelezo alivyoviona katika mawasilano yako either kukushitaki au kukufukuza kazi, onyo etc

Mfano ukikutwa upo kwenye JF, yahoo, msn, etc wakati wa kazi wakati policy yenu hairuhusu unaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Kuna email za binafsi hizi ni Gmail, yahoo, hotmail na zinginezo hizi lazima uwe makini na password yako, ndo maana unashauriwa kutunza na kubadili password yako mara tu unapohisi kuna mtu ana access na inbox yako.

Sasa sijajua kuna nini hapa cha maana, kama zitto alitumia email system ya CHADEMA basi hakuna kesi yoyote na CHADEMA wanaweza kumshitaki sababu anatumia CHADEMA resorces kufanya mawasiliano yake binafsi au hata ya kichama lakini hayana maslahi au tija. na kama alitumia hotmail, yahoo gmail au nyingine ya online basi kosa ni lake kutotunza password yake mwenyewe na hakuna ushahidi wa nani atamkamata sababu password alishatoa kwa watu then akasahau ni nani aliyonayo na ameigawa kwa kina nani.

DCI Manumba pia aelewe kuwa katika sehemu kazi kuna masharti ya mwajiri (User manual policies) wakati unapopewa internet / email access na hata katika vyama vya siasa vivyo hivyo kuna kanuni zake sasa asikurupuke tu- awaulize wana JF ambao ni ma ICT watampa ufafanuzi. Swala la kupiga mkeo hilo lipo wazi huwezi kuringanisha na senario hii.

Mfano ICT - Administrator wa CHADEMA anaweza ku-redirect email za mfanyakazi ziende kwa boss wake kama boss atahitaji - kama ni sehemu ya utaratibu waliojiwekea.

Kifupi Usithubutu kutumie Internet / Email ya kampuni, taasiri, shirika hata chama kwa manufaa yako mwenyewe, ukigundulika unaweza kuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na kupoteza ajira yako.

na ieleweke kuwa ICT Administrator yoyote anaweza kusoma email ya mtu yeyote aliyepo katika organisation hiyo akitaka sababu ameaminiwa na kampuni, taasisi, shirika husika kuweka siri zote za ki electronic za kampuni hiyo.

Kwa hilo zitoo simsaidii hata kidogo na kanumba ajitahidi kuelewa senario hii.
 
cHADEMA WAMECHANGANYIKIWA.CHAIRMAN KIDATO CHA NNE NA KATIBU ANA MZIGO FEKI(PhD).KAZI KUBWA.

Huyu mjinga katoka wapi? Freeman alisoma Kibaha Secondary School na alipata division One halAFU AKAENDA IHUNGO High school kuchukua PGM. Haya nayakumbuka kwa kuwa tulisoma wote
 
MOD unaonaje thread za karibuni za chadema na zitto wao zikaunganishwa ili kuwe na mtiririko mzuri...
 
Mafisadi finally have managed to distract us from the constructive agenda of naming and shaming corruption.

We should understand that the corrupts are always distracting from our main agenda, to keep it confused and inconsistent .We are going to get out of this confusion while the corrupts will be in state house with 10 years mandate to derail this country back. By the way did you no that poverty remains a critical concern for Tanzania, with income levels among the lowest in Africa.

Between 1992 and 2001, the proportion of people living below the national poverty line fell slightly from 39 percent to 36 percent, while the number of people living below the international "dollar a day" poverty line was 58 percent.life expectancy from 44 years in 1978 to 54 years for males and 56 years for females in 2002; infant mortality dropped from 100 to 68 per 1000 between 2000 and 2004, while child mortality dropped from 141 to 112 per 1000 in 2004. The fraction of chronically undernourished or stunted children declined from 44 percent in 1999 to 38 percent in 2004. However, infant and maternal mortality rates remain amongst the highest in the world, literacy rates are low, and more than one third of all children under five are malnourished. The HIV/AIDS prevalence rate is currently estimated at 6% among men, and 8% among women ages 17-35. The proportion of the rural population with access to safe water remains very low (Household budget survey 200. (Economic survey 200.
 
mimi nina wasiwasi na Zitto nahisi kama anatumiwa tu. Aangalie asije akatumiwa then akatupwa kama takataka zinapopelekwa Dampo. Mbona haweki wazi misimamo yake? na hiyo barua ya kujiuzulu kwanini haitoi basi badala ya kutisha watu kuwa anatembea nayo. Tazama mtu mzima hatishiwi nyau😕
 
Date::12/6/2009

DCI: Zitto, tuletee tuhuma za chadema

Na Ramadhan Semtawa

SIKU chache baada ya naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kulalamika kuingiliwa kwenye anuani yake ya barua pepe, Jeshi la Polisi limesema kuingilia mawasiliano ya faragha ya mtu ni jinai na kumtaka mwanasiasa huyo atoe taarifa polisi ili waanze kulishughulikia.

Zitto, ambaye yuko Ujerumani ambako anasoma, alikaririwa na vyombo vya habari wiki iliyopita akidai kuwa anaingiliwa mawasiliano katika anuani yake ya barua pepe (e-mail), kitu alichosema ni aghalabu kufanywa hata na Idara ya Usalama wa Taifa.

Zitto, ambaye juzi alituma barua pepe kwenye gazeti hili kulalamikia kitendo hicho huku akitangaza kutembea na barua ya kujiuzulu uongopzi Chadema, alieleza kusikitishwa na kitendo hicho ambacho alidai kinafanywa na chama chake. Hata hivyo, DCI Manumba alipoulizwa jijini Dar es Salaama jana kuhusu malalamiko ya Zitto, alijibu: "Sisi hutujapata rasmi malalamiko hayo, lakini akileta tutachunguza kwa kuwa si sahihi kuingilia mawasiliano ya mtu."

Najuliza, kwanini DCI anachangamkia kesi za wapinzani?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom