- Hii ni baada ya kusema Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa"
- Chadema yaharisha damu!
- CCM yapiga vigelele kama vile mwana kakutwa bikra kwenye harusi ya ndoa!
Baada ya kusoma maelezo ya Mhe Zitto katika gazeti la Mwananchi la jana, ile network ya watafutaji wa habari za kweli na za kuaminika hapa Tanzania (yaani Wagagagigikoko) waliingia kazini na kuzungumza na Watanzania kadhaa mjini DSM na kwenye vitongoji vyake, ili kujua wanategemea Mhe Zitto atafanya maamuzi gani ambayo hayajawahi kufikiriwa.
Mhe Zitto tayari keshajiunga na CCM na kadi keshapewa, alisema mwananchi mmoja ambae hakutaka jina lake litajwe mpaka mwenyewe Mhe Zitto atamke hadharani. Hizi ndio lugha zao, mwanasiasa akisema nitafanya kitu, basi ujue tayari keshafanya hicho kitu na Mhe Zitto ndio hivyo hivyo, aliendelea mwananchi huyo.
Mwananchi mwengine ambae kajitambulisha kama ni mwanachama asilia wa Chadema alisema huku machozi yakimtoka kuwa, I say, sina hata nguvu. Huyu Mhe Zitto tukimtegemea atuokoe Watanzania katika hili janga la CCM, tukimuona yeye kama Obama wa kitanzania, lakini inaonesha na yeye ndio keshajiunga nao. Anyway, mimi tokea alivyomsifia yule Dr Rashid nilijua kama hapa lipo jungu linapikwa na naona sasa lishawiva. Alipoulizwa kama kweli Mhe Zitto anaweza kujiunga na CCM baada ya shutuma zake zote zile nzito nzito dhidi ya CCM, huyu mwanachama wa Chadema alijibu kuwa, Kwa mwanasiasa chochote kinawezekana, alijibu na huku akikataa kujibu masuala zaidi.
Makachori wa Wagagagigikoko walimpigia simu mwanachama mmoja mashuhuri wa JF na kumuuliza anaona vipi hali ya opposition parties Bara, na yeye akajibu, Mhe Zitto ni mwanachama wa Chadema na madamu bado hajatamka kutoka Chadema, tafadhalini tuwaachieni akina Dr Slaa na Mbowe wayamalize wenyewe, na huku akikata simu kama mtu aliyekasirika kwa kuulizwa suala hilo.
Mwanachama mmoja wa CCM alikutwa akipiga vigelegele na huku akigonga debe bovu kwa nyundo kama vile mwanawe wa kike kakutwa bikra katika harusi yake. Alipoulizwa anafurahia nini alijibu, Mimi ni CCM. CCM ndio baba na ndio mama yetu. Wakirejea CCM tutawalea kama watoto wetu na katu hatutowakataa, kwani mzee hamkatai mwanawe.
Wagagagigikoko, wameendelea kusema kuwa political pundits wa mji wa DSM jana baada ya kusoma maelezo ya Mhe Zitto kwenye gazeti la Mwananchi, wengi walikuwa wakisikika wakisema hadharani kuwa kwa sasa hata kama Mhe Zitto atabakia Chadema, maafa (damage) tayari yashatokea na kutendeka and Chadema will never be the same again.
Chadema itaendelea kuharisha damu mpaka Dr Slaa na Mbowe watakapo yakabili kijitukizima matatizo yaliyojitokeza. Bila ya hivyo, chama ambacho kilikuwa kikitegemewa na wengi to put up a productive opposition in the country will slowly and surely bleed to an ignominious death!, walimalizia Wagagagigikoko.
Sources: Wagagagigikoko News Network (Wanene)