Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Na Mwandishi wetu
7th December 2009

headline_bullet.jpg
Asema zipo njama kuhamisha ajenda ya ufisadi
headline_bullet.jpg
Adai kunasa mawasiliano ya Zitto na mwingine
headline_bullet.jpg
Ajigamba Chadema hakina mgogoro, kipo imara

Slaa%20na%20Zito.jpg

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa (kushoto) na Zitto Kabwe.

Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, amesema kuna vita kali sasa ya baadhi ya watu kufanya njama za kuhamisha ajenda ya vita dhidi ya ufisadi na kuzungumzia masuala ya mbunge wao, Kabwe Zitto.

“Nadhani sasa Watanzania wanatakiwa wakaelewa…naona sasa kuna vita kali ya kuiondoa ajenda ya vita dhidi ya ufisadi, na sasa wanataka kutuelekeza kumjadili mtu, Zitto.

Na mimi nasema hatuhitaji kujadili watu isipokuwa chama,” alisema Dk. Slaa wakati akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana na kuongeza: Chadema hakina mgogoro na kipo imara na hiyo ilithibitika wakati na baada ya Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Septemba, mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu madai ya Zitto kutembea na barua ya kujiuzulu Chadema, Dk. Slaa alisema ofisi yake haijapata barua, maelezo yoyote au ushauri kutoka kwa Zitto unaoelezea suala hilo.

“Hatuwezi kuendelea na mambo haya ya kuhamisha ajenda ya vita dhidi ya ufisadi na kuanza sasa kujadili suala la mtu binafsi, kama ambavyo sasa inaanza kujitokeza,” alisema.

Alisema Chadema ni taasisi itaendelea kuwepo hata kama yeye ama Mbowe (Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho) au Zitto wataondoka katika chama hicho.

Alisisitiza kuwa chama hicho kitaendelea kupiga vita ufisadi kwa nguvu zote licha ya baadhi ya watu kuanza kudhoofisha ajenda hiyo.

Akifafanua kuhusu suala la Zitto, Dk. Slaa alisema siku moja saa 1:00 jioni kabla ya Mkutano Mkuu wa Chadema uliopita, alipata nafasi ya kuzungumza na mama ya Zitto, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Shida Salum, aliyemhakikishia kwamba Zitto hahusiki na mambo hayo.

“Siku moja kabla ya Kamati Kuu, niliongea na mama yake Zitto na akanihakikishia kwamba hahusiki na mambo haya yanayojitokeza ya kukichafua chama,” alisema.

Alisema alielezwa na mama huyo kuwa wapo watu wanaomtumia Zitto kwa maslahi wanayoyajua wenyewe na kwamba mtu mmoja (jina linahifadhiwa) anayo password ya anuani ya barua pepe ya Zitto ambayo anaitumia kuandika taarifa mbalimbali alizoeleza zinaonyesha kama vile zinatoka kwa Zitto.

Lakini alisema baada ya mazungumzo na mama huyo, kesho yake gazeti moja lilikuwa na habari ya Zitto kukanusha kwamba hahusiki na suala la David Kafulila isipokuwa watu wametumia jina lake.

Dk. Slaa aliongeza baada ya mazungumzo hayo, asubuhi yake alipata taarifa za barua pepe kutoka kwa Mtanzania mwema zinazoonyesha mawasiliano kati ya Zitto na mtu mmoja (jina linahifadhiwa).

Bila kueleza kwa undani taarifa mbalimbali zilizokuwemo katika barua hizo pepe, alisema kwa kifupi kwamba zilikuwa zikionyesha mawasiliano ya kichama kati ya mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam na Zitto ambaye kwa sasa yupo masomoni nchini Ujerumani.

Alisema baada ya kuzisoma aliwasiliana na mkazi huyo wa Dar es Salaam akitamka athibitishe iwapo mawasiliano hayo ya barua pepe yalikuwa ya kwake au la.

Alisema alifanya hivyo kwa kumtumia ujumbe na baada ya muda mkazi huyo alimpigia Dk. Slaa, na akathibitisha kwamba anazitambua barua hizo na mawasiliano hayo yalikuwa ni ya kwake.

Lakini baadaye katika mazungumzo yao ya simu, mkazi huyo wa jijini alimweleza Dk. Slaa kwamba ameingilia mawasiliano yao binafsi, jambo ambalo alilipinga.

“Nilimweleza mkazi huyo kwamba sijaingilia mawasiliano binafsi, kwa kuwa taarifa zilizokuwa zikizungumzwa katika barua hizo zilikuwa zikikihusu Chadema na kwa maana hiyo hazikuwa binafsi,” alisema.

Alisema baadaye mkazi huyo alimjibu Dk. Slaa kwamba anafanya kazi katika kampuni kubwa na kwamba Dk. Slaa hataiweza na afadhali aache.

Aliongeza baada ya gazeti moja kuchapisha habari za Zitto jana, alimtumia Zitto ujumbe wa barua pepe akitaka maelezo kuhusu habari hizo zilizodai kuwa anatembea na barua ya kujiuzulu Chadema.

Dk. Slaa alisema tangu alivyomtumia ujumbe huo jana asubuhi, hajapata majibu yoyote hadi alipowasiliana na Nipashe saa 11:00 jana jioni.

CHANZO: NIPASHE 12/07/2009
 
alisema Dk. Slaa wakati akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana na kuongeza: Chadema hakina mgogoro na kipo imara na hiyo ilithibitika wakati na baada ya Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Septemba, mwaka huu.

  1. Inasikitisha kuona jinsi Dr. Slaa anavyoendelea kulaghai umma kwa kukataa the obvious. Kama hakuna mgogoro, anafafanua nini kila siku kwenye vyombo vya habari?
  2. Huku kumuandama Zitto as if hawezi kumpata kwenye simu na kujadili hayo anayojadili kwenye wanahabari sijui nako kuna nia gani.
Dr. Slaa wa leo sio yule tuliyekuwa tunamjua miezi michache iliyopita. Wa sasa anaonekana shallow na mnafiki.

Nafuu ya Mbowe ambaye yeye kakaa kimyaa kimya kabisaa kama vile sio kiongozi wa CHADEMA. Kamuachia Mzee wa wa watu wa kimbulu amfanyie madudu yake na wakati huo huo kujimaliza mwenyewe.
 
Wewe ulitaka asemeje??
 
mBONA NI KAMA UMETUMWA NA MTU AU TAASISI USEME HAYA MANENO?
 
HUO ndio mwisho wa Chadema.

Mchawi wenu ni Dr Slaa. Kwani Elimu yake ni ubabaishaji mtupu na utata kibao sasa analeta kwenye chama.

Poleni sana Chadema. Akiondoka Zitto na chama kimekufa. maana yake majimbo ya Kigoma zero
 
Chadema is a Movement, Movement can not seaze hata hao wanasemekana wataondoka wakiondoka
 
HUO ndio mwisho wa Chadema.

Mchawi wenu ni Dr Slaa. Kwani Elimu yake ni ubabaishaji mtupu na utata kibao sasa analeta kwenye chama.

Poleni sana Chadema. Akiondoka Zitto na chama kimekufa. maana yake majimbo ya Kigoma zero

Mchawi ni huyo anayekutuma, poleni wewe unayetumiwa na mafisadi kwa kipato haramu,

tuambie hao wasomi wako watakaoikomboa Tanzania, unazungumzia kisomo cha Dr Slaa badala ya kuzungumzia ukombozi watanzania?

Elimu yako inakusaidia nini kama unatumiwa tu kuandika mambo ya ovyo. Wengi wanafahamu mchango chanya wa Dr Slaa wewe watafuta kujua elimu yake itakusaidia nini?

Unasemaje mtumwa wa mafisadi
 
chadema wana mgogoro,na hawataki kuutambua huo mgogoro ili waweze kujua jinsi ya kuutatua na kuutuliza. tatizo ni kutokujitambua cc ni kina nani
 
  1. Inasikitisha kuona jinsi Dr. Slaa anavyoendelea kulaghai umma kwa kukataa the obvious. Kama hakuna mgogoro, anafafanua nini kila siku kwenye vyombo vya habari?
  2. Huku kumuandama Zitto as if hawezi kumpata kwenye simu na kujadili hayo anayojadili kwenye wanahabari sijui nako kuna nia gani.
Dr. Slaa wa leo sio yule tuliyekuwa tunamjua miezi michache iliyopita. Wa sasa anaonekana shallow na mnafiki.

Nafuu ya Mbowe ambaye yeye kakaa kimyaa kimya kabisaa kama vile sio kiongozi wa CHADEMA. Kamuachia Mzee wa wa watu wa kimbulu amfanyie madudu yake na wakati huo huo kujimaliza mwenyewe.

Si bure utakuwa umetumwa tu! Ni kweli wewe ni kubwa jinga kama jina lako linavyosema,umekaliam ushabiki badala ya kujenga hoja.Dk Slaa we always be the same.
 
Zitto rafiki yangu, wewe bado kijana mdogo; pia lilikuwa tumaini letu vijana, sasa mbona unatuangusha? kuna rafiki yangu mwana CCM miezi nane iliyopita aliniambia tusijivunie Zitto wa Chadema kwa sababu soon atakwenda CCM. nilibishana naye sana sana ila sasa ninaambiwa tulikuambia.
Zitto tulia sasa ni mda wetu wa kukupima msimamo wako wa kiongozi. Hivi leo Zitto ungekuwa mwenyekiti wa chama harafu kiongozi mmoja analeta dharau katika utendaji wako ungempongeza? na inapotokea viongozi wenzako wanamtetea mtu anayechafua chama ungechekelea? Kaka Zitto tafakari upywa Msimamo wako.

Jinsi siku zinavyoenda ndivyo tunavyozidi kuwa na mashaka na vijana wetu tulio watumaini.
Kaka Zitto muangalie Mrema, Mrema alisifika Tanzania nzima na mimi nilikuwa nyuma yake lakini leo yuko wapi? Najua sasa unajina kubwa ila harifikii hata nusu ya Mrema wa 1995; Mrema kisha zeeka zake ila wewe na mimi tunasiku nyingi kama Mungu atapenda.
Angalia rafiki, pata ushauli wa Bure kwa Father Dr Slaa.
 
Kujadili Zitto kila siku inachosha, aondoke CHADEMA na tuone outcomes itakuwaje, kila siku kutishia anatoanatoka, kwani Zitto kuondoka CHADEMA atakuwa wa kwanza au wa mwisho mbona kuhama vyama ni kitu cha kawaida na kama kuna watu ataondoka nao na wao waondoke ili kujenga demekrasia
 
chadema wana mgogoro,na hawataki kuutambua huo mgogoro ili waweze kujua jinsi ya kuutatua na kuutuliza. tatizo ni kutokujitambua cc ni kina nani
CHADEMA siku itakapokua haina mgogoro ndo siku itakayo kuwa mfu , maana taasisi itakosaje miogoro, hii ni ishara kua chama hiki ni hai.

Zito amekua na tabia kama ya mtu asiejua nini anataka, na hili ni hatari, na muunga mkono Dr Slaa, kama anataka kwenda aende zake tu, tabia ya kuringa na kunata zinamfanya asiwe mtu makini wala wakuaminika, anatishia sana nyau, anadhani CHADEMA itakufa kisa yeye na wale wahuni wamejiunga NCCR Mageuzi.

CHADEMA imejegwa katika misingi yake,inawanachama makini ambao wamelelewa na kukulia mle hawana papara kama za huyu dogo,kifupi hawadanganyiki. akitaka aweza kwenda kwa kina juju, anatuboa tu.

sasa hawayumbishwi na kelele zake na mafisadi wa new habari co.

DAIMA MBELE-HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.
 
Jamani, mpunguzieni pressure asome shule. Kama mnamtakia mema katika masomo yake, acheni kumjadili apate nafasi ya kusoma vizuri...tafadhali
 
  1. Inasikitisha kuona jinsi Dr. Slaa anavyoendelea kulaghai umma kwa kukataa the obvious. Kama hakuna mgogoro, anafafanua nini kila siku kwenye vyombo vya habari?
  2. Huku kumuandama Zitto as if hawezi kumpata kwenye simu na kujadili hayo anayojadili kwenye wanahabari sijui nako kuna nia gani.
Dr. Slaa wa leo sio yule tuliyekuwa tunamjua miezi michache iliyopita. Wa sasa anaonekana shallow na mnafiki.

Nafuu ya Mbowe ambaye yeye kakaa kimyaa kimya kabisaa kama vile sio kiongozi wa CHADEMA. Kamuachia Mzee wa wa watu wa kimbulu amfanyie madudu yake na wakati huo huo kujimaliza mwenyewe.

Kubwajinga usiwe kama hilo jina lako. Dr. Slaa halaghai umma na wala hamuandami Zitto. Kimsingi Slaa ni yule yule hajabadilika ila hali ya siasa ndani ya chama ndo inamfanya aonekane hivyo. Elewa wazi kuwa kazi ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu anao wajibu wa kulinda na kutetea maslahi ya chama chake. Kwa hali hiyo hawezi kukurupuka na kusema kitu ambacho hakijafanyiwa utafiti na ndo maana amejaribu kueleza kwamba kuna watu wanatumia jina la Zitto kwa mijadala ili kuuwa mjadala wa mafisadi. Hakuna mahali popote alipomwandama Zitto kwani ukiangalia kwa makini utaona kwamba bado anatetea kuwa Zitto bado ni chadema kwa kuwa hajapata barua yoyote kutoka kwake na kuna mtu ana password ya email address ya Zitto ndo anazusha haya mambo. Kama ulisoma JF last week kuna mtu aliandika kuwa Kafulia ndiye mwenye password ya Zitto na ndo maana Zitto alikanusha kutokutoa msaada wa magari kwa Kafulia. Kwanza nilishangaa Zitto aliyapata wapi magari hayo kwani mimi nafahamu anakaa karibu na gate la UDSM na usafri alio nao unafahamika? Kimsingi simtetei Slaa ila naangalia nafasi yake kama katibu mkuu angefanyaje kukilinda Chama kisimeguke. Je ungekuwa wewe KUBWAJINGA ungefanyaje.
Try to put your feet in his shoes.CHEERS.
 
Miezi michache iliyopita tulimshambulia Kibanda hapa kwa makala yake kuhusu misimamo ya huyu Zitto na vision yake, now it gets clear that the guy was right!! This is so frustrating.
Hatuhitaji kuwekeza kwenye watu ambao wanaweza kununuliwa au chochote kutokea, tuwekeze kwenye ukweli na misingi sahihi ya kuokoa nchi hii kutoka kwenye mikono ya wanyang'anyi. forget about Zitto and co.
 
HUO ndio mwisho wa Chadema.
You are very wrong

Mchawi wenu ni Dr Slaa. Kwani Elimu yake ni ubabaishaji mtupu na utata kibao sasa analeta kwenye chama.
Wewe ndie mchawi na aliyekutuma. Elimu yako haitoshi kufahamu elimu ya Dr. Slaa, rudi darasani.

Poleni sana Chadema. Akiondoka Zitto na chama kimekufa. maana yake majimbo ya Kigoma zero
Wameondoka kina Kabouru na wengine wengi na hakikufa kife leo!!!. Mlipiga propaganda baada ya kifo cha Wangwe lakini mbona CHADEMA walichukua jimbo. Hata kigoma msishanga kafulila akaafulia huko kusini na CHADEMA wakachukua.

Habari ndio hiyo.
 
Swala si migogoro ndani ya CHADEMA. Zitto alitumwa na mafisadi kuuwa CHADEMA. Ndio maana alianza kufagilia ununuzi wa DOWANS.

Sasa tujiulize, je huyo ndie Zitto alietaka kuwa mwenyekiti? Angeupata huyo uenyekiti, si angeuwa chama?

Zitto si CHADEMA, CHADEMA itaendelea kuwepo bila Zitto au Dr. Slaa.

Kumbukeni CHADEMA na Dr. Dlaa ndie walitufundisha kuhusu mafisadi, EPA, Kagoda etc.
 
Mchawi ni huyo anayekutuma, poleni wewe unayetumiwa na mafisadi kwa kipato haramu,

tuambie hao wasomi wako watakaoikomboa Tanzania, unazungumzia kisomo cha Dr Slaa badala ya kuzungumzia ukombozi watanzania?

Elimu yako inakusaidia nini kama unatumiwa tu kuandika mambo ya ovyo. Wengi wanafahamu mchango chanya wa Dr Slaa wewe watafuta kujua elimu yake itakusaidia nini?

Unasemaje mtumwa wa mafisadi
usishangae kaka yangu kwamba kuna watu wenye fikra finyu. Ngurumo aliwahi sema M2 ANAPOWASILISHA HOJA YA KUJADILI UTAONA MWENYE FIKRA MBOVU. BADALA YAKUJADILI HOJA, WATAISALITI NA KUMJADILI MTOA HOJA. hawa niwapumbavu. tuwaache.

tujadili hoja. ma hoja ni Zitto nimsaliti. katumwa kuzima hoja ya ufisadi. kwakuwa tumeshashtuka, tutaendelea kumpuuza zitto na mafisadi waliemtuma.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom