Lala salama Uzini; CHADEMA yaweka mguu chini, Zitto, Dkt. Slaa, Mkiti Mbowe waongeza nguvu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lala salama Uzini; CHADEMA yaweka mguu chini, Zitto, Dkt. Slaa, Mkiti Mbowe waongeza nguvu

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Tumaini Makene, Feb 8, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wakuu mapambano yanaendelea Uzini. CHADEMA inazidi kuchanja mbuga. Makamanda wanafanya kampeni za lala salama sasa. Mikutano ya hadhara na mobile kampeni. Bila kusahau mtu kwa mtu kampeni, hasa kwa kukutana na wananchi waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura. Makamanda wanakutana na wapiga kura wote, bila kujali vyama vyao. Hoja zinaeleweka, sera zinakubalika. Ni wazi Wazanzibar wanaihitaji CHADEMA kuwa sauti yao, mtetezi wao katika kudai haki na uwajibikaji na CHADEMA kinawahitaji Wazanzibar, katika harakati za kusaka ukombozi wa pili wa Watanzania wote, bila kujali tofauti yoyote.

  Kuanzia leo mpaka Jumapili, Februari 12, 2012, ambapo Watanzania wa Uzini, watakwenda kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwa kuchagua chama na mgombea wanayemtaka, zitakuwa zimebaki siku nne kamili za kampeni. Ni wazi kuwa joto la kisiasa Uzini litazidi kupanda na kuongezeka. CHADEMA kimetangulia.

  Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Yusuf Musa, ametoa taarifa kwa umma leo, kupitia kwa wanahabari hapa Zanzibar, aliokutana nao ukumbi wa Habari Maelezo, maeneo ya Raha leo, kuwapatia tathmini ya CHADEMA juu ya uchaguzi huo, kuwa kesho Naibu Katibu Mkuu Bara, Kabwe Zitto atatia timu Uzini kuongeza nguvu kwenye timu ya kampeni inayomnadi mgombea wa CHADEMA, Maalim Ali Mbarouk Mshimba.

  Baada ya Kamanda Zitto, keshokutwa wataingia Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa pamoja na Kamanda wa anga, Mwenyekiti Freeman Mbowe, ambao watapiga mzigo wa mpaka kieleweke, kwa siku zote zilizobaki za kampeni. Wabunge wengine makamanda wanatarajiwa kuongozana nao! Waweza kufikiria hali itakuwaje? I am anxiously waiting to see who could be the counterparts kwa timu kamili ya CHADEMA itakayokuwa Uzini kwa siku zilizobaki.

  Watu wenye uwezo wa kujenga hoja na kuchambua masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, kuhusu mstakabali wa maendeleo ya watu na taifa lao kwa ujumla. Timu ya watu wenye uwezo wa kufanya kampeni usiku na mchana. Wenye uzoefu mkubwa wa kuvumilia na kufanya kazi kwenye uwanja wa mapambano. Wakiweka mbele kutumikia wananchi. Moja ya spirit inayo-drive politics within CHADEMA ni kugawana majukumu, si kugawana vyeo!

  Katika mkutano wake na wanahabari hao, Naibu Katibu Mkuu Zenj, pia amedokeza tathmini ya CHADEMA, kutokana na kikao cha tathmini ya timu za kampeni, kilichofanyika Februari 5. Amesema mpaka sasa tathmini ya kisayansi iliyofanywa kupitia aina za kampeni zilizotajwa aya kwa kwanza hapo juu, zinatoa asilimia kubwa kwa chama hicho kuibuka mshindi, zidi ya CCM, kama uchaguzi ungefanyika hiyo Februari 5.

  Ili kuepuka 'kubweteka' na tathmini hiyo, chama kimeona umuhimu wa kuongeza 'majeshi' katika uwanja wa mapambano, ili ku-mantain status au kuiongeza zaidi kuelekea siku za mwisho za kampeni.

  Lakini pia ametumia nafasi hiyo kulitaka Jeshi la Polisi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kuchukua hatua zinazostahili juu ya vitendo vya hujuma dhidi ya CHADEMA vinavyoanza kufanywa na CCM, akitolea mfano wa tukio lililotokea jana, ambapo vijana wa CCM wakiwa katika gari lao, walilipita gari la CHADEMA kisha wakalirushia mawe na kuvunja kioo cha mbele. Alhamudulillah waliokuwemo ndani ya gari walinusurika.

  Mbali na tukio hilo kuripotiwa polisi, Naibu Katibu Mkuu Yusuf ametoa angalizo kuwa iwapo hatua kali hazitachukuliwa kadri inavyopasa kwa vitendo hivyo na wahusika wake, hali ya vurugu itakayotokea, kutokana na watu kutoona haki ikitendeka na hata kukosa matumaini katika mchakato huu, kwa siku zilizobaki hivyo kusababisha uvunjifu wa amani, lawama zitakuwa mikononi mwa Polisi na ZEC.

  "Uwezo wetu na mbinu zetu za kujilinda ni mkubwa mno. Tunaweza kujilinda. Mathalani jana usiku, walituma mtu wao kuja kufanya ukachero katika kambi yetu kuu iliyopo Uzini, vijana wetu waliweza kumkamata, kumdhibiti na kisha wakampeleka polisi kwa hatua zinazostahili...Iwapo uchaguzi utafanyika katika hali ya haki na uhuru, tutakuwa tayari kupokea maamuzi yatakayofanywa na wananchi katika sanduku la kura," amesema Yusuf.

  Wakuu kampeni za Uzini ndiyo hizo zinayoyoma, ushindani ni baina ya CHADEMA na CCM, Cuf wanakuja kwa mbali. Sababu nimeshazisema mara kadhaa, kwa nini jamaa hali haiwaendei vyema, specifically kwa hapa Uzini. TADEA na AFP nao pia wapo. Wanashiriki huu uchaguzi.

  Mgombea wa CHADEMA ni mzaliwa wa Uzini. Amezaliwa Tunduni, amekulia Tunduni, amesomea Tunduni (na Fidel Castro, Pemba), amechezea Tunduni na sasa anasomesha Uzini, katika skuli ya Mchangani. Mwaka wa juzi, wakati wa uchaguzi mkuu aliwania ubunge. Kura hazikutosha. Akawa mshindi wa pili, nyuma ya mgombea wa CCM.

  Mgombea wa CCM mnamjua. Mohamedraza Hassanali Mohamedali. Mfanyabiashara anayeishi Mtoni, Jimbo la Bububu, ambako pia aliwania uwakilishi, lakini akashindwa kwenye kura za maoni za chama hicho. Kutokana na kuwa si mkaazi wa Uzini (hapa wananchi wanamwita mgeni), na alijiandikisha kupiga kura jimbo jingine, katika uchaguzi huu, hataweza kujipigia kura. Yale ya Ali Mohamed Shein yanajirudia hapa Uzini.

  Mgombea wa CUF ni Salma Hussein Zaral. Ni mfanyabiashara. Mgombea wa AFP anaitwa Rashid Yusuf Mchenga, mfanyabiashara. Wa TADEA ni Khamis Khatib Vuai, yeye ni mkulima.

  Baada ya Uzini, mapambano yanahamia Arumeru Mashariki. Habari Leo, wameweka headline nzuri juu ya hilo. Asanteni.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  PHP:
  Baada ya Uzinimapambano yanahamia Arumeru MsaharikiHabari Leowameweka headline nzuri juu ya hiloAsanteni
  Hakuna kulala mpaka kieleweke!
  Peopleeees Power!
   
 3. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  ccm hawapumui bado kuna majimbo mengi sana yanafuata hapa ni mwanzo tu, sasa nawahi arumeru kufungua bar kule nitauza sana kwa mwezi mmoja tu wa kampeni itanilipa faida ya miaka minne.,,,
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  vipi helcopta inatua lini Uzini?
   
 5. d

  dotto JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ipi hiyo?
   
 6. k

  kwamagombe Senior Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa kutujuza kinachoendelea huko Uzini, uendelee na moyo huo huo
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Jina la hilo Jimbo na vichwa vya habari mnavyotumia si salama. Lala salama Uzini? Ndio nini sasa
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Ahadi yangu ipo pale pale...
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Helkopta ya nini wakati unaweza kulizunguka jimbo lote kwa baiskeli kwa masaa tu.
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Indicator ya kijani hiyooooo imewashwaaaaaaaaa
   
 11. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Ukianza kuvua nguo niite tu ili ukameruniwe
   
 12. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  All the best makamanda wetu....mungu akisema ndiyo akuna awezaye kusema hapana!
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kazi nzuri Makene.Hongereni wana uzini.
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,332
  Trophy Points: 280
  CDM mwendo mdundo, CCM ipo wodi ya Mwaisela hoi na madaktari ndhiyo wamegoma kwa hiyo kupona HAKUNA ....:lol:
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  zanzibar imepata okello wa demokrasia.
   
 16. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,793
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  Awali nikupongeze kwa ripoti yako ambayo imetoa picha halisi huko Uzini na ishallah basi tuombe iwe hivo, ila sahihisho dogo tu ni kuwa jumapili ijayo ni February 12 sio February 2 kama ulivoandika!! otherwise I appreciate your coverage!!
   
 17. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #17
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  tuna hitaji changa moto za kweli
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nafasi ya ushindi wa chadema jimbo la uzini ni sawa na ngamia kupenya katika tundu la sindano.

  Ok jitahidini labda ataweza kupenya.
   
 19. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tunajiandaa kujionea senema ya bure ya watu wazima kutembea wakiwa watupu kutoka Posta hadi Kimara Bonyokwa.
   
 20. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tunajiandaa kujionea senema ya bure ya watu wazima kutembea wakiwa watupu kutoka Posta hadi Kimara Bonyokwa. Au kujinyonga kama mlivyoahidi!
   
Loading...