Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
na Irene Mark

DAVID Kafulila, mwanachama mpya wa NCCR-Mageuzi, ambaye amekuwa akitumia uhusiano wake binafsi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kama kete ya kisiasa katika ugomvi wake na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema Zitto ni mzushi.

Kafulila, ambaye alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA kabla hajavuliwa cheo hicho na kukimbilia NCCR-Mageuzi, alisema hayo jana Dar es Salaam, wakati akijibu taarifa kuwa mbunge huyo amekanusha kumsaidia magari matatu ya kufanyia harakati za kujijenga kisiasa mkoani Kigoma baada ya kujiunga na NCCR-Mageuzi.

Msukumo wa Kafulila kumshutumu Zitto umetokana na tetesi kwamba amekuwa anatumia barua pepe ya mbunge huyo kusambaza taarifa zinazoleta chokochoko katika CHADEMA, kwa kuwa anajua neno siri la anuani ya barua pepe ya mbunge huyo ambaye amekuwa anamtumia kama msaidizi wake katika masuala mengi walipokuwa CHADEMA.

Taarifa hizo zilitokana na mawasiliano ya Zitto na watu walio karibu naye ambao juzi waliliambia gazeti hili wanachokiita ukweli wa madai ya mbunge huyo kumuunga mkono Kafulila katika harakati zake mpya akiwa NCCR-Mageuzi, kiasi cha kumpatia magari matatu kwa ajili ya kuzunguka maeneo kadhaa ya Jimbo la Kigoma Kusini katika siku chache zijazo.

Jana Kafulila aliiambia Tanzania Daima kuwa kama ni hivyo, Zitto ni mzushi, kwani hajawahi kumpa neno la siri la kufungua anuani ya barua pepe yake, wala hafahamu lolote kuhusu anuani hiyo.

Katika toleo la jana, gazeti hili lilkuwa na habari kuwa Zitto alimkana Kafulila, na kwamba mbunge huyo amekiandikia barua chama chake (CHADEMA) kukijulisha msimamo wake binafsi, kwa maelezo kuwa wanaomhusisha na kauli za Kafulila wana nia ya kumchonganisha (Zitto) na uongozi wa CHADEMA.

Kauli kama hii ilitolewa na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto, katika mahojiano yake na gazeti la MwanaHALISI wiki mbili zilizopita, akisema mwanawe anatumiwa na watu wenye lengo la kuvuruga chama na kumgombanisha mwanawe na uongozi wa chama chao.

Katika kauli yake ya juzi, Zitto alinukuliwa akiwaeleza watu walio karibu naye kuwa hata taarifa zinazoandikwa na vyombo vya habari kuhusu yeye ‘kumbeba’ Kafulila zinamnukuu bila kumhoji yeye.

Lakini jana Kafulila alisema: “Huo ni uzushi unaotengenezwa…password (neno siri) ni kitu muhimu, tena ni siri ya mhusika, sasa iweje Zitto anipe password yake? Hayo ni maneno ya uzushi.” Wakati huo huo, aliyevuliwa cheo cha Ofisa Mwandamizi wa Sera na Utafiti wa CHADEMA, Juju Danda, jana alitangaza rasmi kujiunga NCCR-Mageuzi kama Kafulila.

“Nimefukuzwa bila kufuata sheria. Sijaridhishwa kabisa na maamuzi yale, ndiyo maana nikaona nitafute tumaini jingine ambalo ni NCCR-Mageuzi,” alisema.

Am fed up with this debate.Let me stay away and discuss other issues.
 
Jmushi1,
Kafulila ndiye alisema kapewa magari matatu na naibu katibu wa CHADEMA ili akapige kampeni kwa chama cha NCCR dhidi ya vyama vingine CHADEMA kikiwemo
Mkuu unaweza kutuwekea nakala ya maneno haya toka kwa Kafulila au Zitto mwenyewe maanake navyojua mimi ni waandishi wa haya magazeti waliopandikiza mbegu hizi. Sijawahi soma mahala Zitto akipinga maamuzi ya Dr. Slaa isipokuwa ile siku alokuwa Germany akaambiwa kuhusu mkutano wa siri Dodoma.. na majibu yake yalikuwa wazi kabisa kuwa haiwezekani na itakuwa ni makosa kumfukuza Kafulila Uanachama kulingana na katiba ya chama.

Wanaboidi,
Kilichotokea kimetokea na haya yote mazungumzo ni baada ya habari kwani Kafulila hakufukuzwa bali alivuliwa cheo chake na Zitto hakupinga hatua hiyo.. hakuna mahala Zitto amesema Chadema au Dr. Slaa amefanya makosa kumwengua Kafulila ktk wadhifa isipokuwa ni waandishi wenye chuki binafsi ndani na nje ya Chadema wanaojaribu kukiharibu chama kwa kupitia mgogoro huu. Ajabu ni kwamba wote hawa walikuwa tayari wamezivua nguo zao kuyakoga maji haya machafu, sasa kinachonishinda kuelewa ni kwamba Kafulila kaondoka, bado mnamfuafuta aliko na maneno mengi kuendelea kuhakikisha Zitto pia anaondoka Chadema...
Hii inatisha sana na pengine inanipa sura kamili ya vichwa vya wanachama wa Chadema..
 
hapa mnajadili matumbo ya watu..........otherwise labda kama mnainterest nao hawa wahusika vinginevyo................mtaumiza vichwa hamuwezi kupata jibu................
let us wait the truth
 
Mkuu tafakari kwanza,mimi sina chama lakini napenda fairness regardless,na ukweli ndio pia muhimu.
Kwanza uzingatie Zitto bado ni CHADEMA,na madai yako kwamba Kafulila keshajiendea zake NCCR na bado hawajaridhika hayana mantiki kwasababu Kafulila ndiye alisema kapewa magari matatu na naibu katibu wa CHADEMA ili akapige kampeni kwa chama cha NCCR dhidi ya vyama vingine CHADEMA kikiwemo.Kwahiyo kama habari hizo ni za kweli then CHADEMA lazima watakuwa concerned na pengine kumwuliza naibu katibu mkuu wao if all this is true.Na ndio maana Zitto akakanusha habari hizo,then ikasemekana kuwa Zitto kasema Kafulila ana password yake,huwezi kujua alibanwa ndani ya chama,Kafulila akaibuka akasema Zitto mzushi,sasa nani kamfata nani?Tulia na tumia busara,reasoning na reality vitake over emotions,you will then see where i am coming from.

Punguza jazba mangi, twende taratibu tutafika tu. Tangu lini umejitoa chadema chalii angu!!??au ndo umeanza kuwakana wenzako?
Jitahidi kufanya homework yako vizuri, isome hiyo makala ya huyo mwandishi vizuri, soma katikati ya mistari halafu uje unionyeshe ni wapi tanzania daima wamezungumza na zitto na akawaeleza kwamba kafulila ana password yake kama si majungu ya tanzania daima &co., Na hata kama aliwahi kumpa password yake kutokana na ukaribu wao, bado siamini kwamba zitto ni mzembe kiasi cha kuzungumza jambo kama hilo mbele ya watu.
kwahiyo usiwe na shaka chalii angu ninakuona vizuri sana "where you coming from".
Kafulila kaondoka zake kwenda nccr na ametangaza kuingia kilingeni kupambana na chadema kwahiyo msiweweseke, jipangeni mkakabiliane nae huko huko kwenye battle field, haya makelele mnayoendelea kupiga inaonyesha ni kiasi gani kafulila amewashika pabaya.
 
Kuna mwanadada mmoja kanipigia simu anasema yeye na Kafulila walikuwa darasa moja na yeye wiki hii Jumamosi anapata cheti baada ya kumaliza degree yake na Kafulila alikwua virus hata darasani . Sijajua ukweli wa habari hizi ina hata wa darasani kwake wanasema jamaa ni troublesome.

Umeishiwa hoja mkuu sasa umeanza personal attacks. Wakati alipokuwa anawatumikia kama afisa habari hamkujua kwamba ni kirusi, mlikuwa mnamuona bonge la kipanga.
sasa leo kaamua kuondoka chadema mnaanza talalila, ooh kafulila kirusi, mara ooh kafulila sisimizi!! Yani ghafla sisimizi amegeuka tembo anawapa presha!!
Huu muda mnaotumia kumshambulia kupitia gazeti lenu na majukwaa mbalimbali muutumie kuweka mikakati ya kulichukua jimbo la kigoma kusini, tena muandae helikopta, mnajua kwamba kafulila anawajua inside out kwahiyo msipojipanga vizuri, mtashangaa 2010 kafulila na zitto wanakaa upande mmoja kule mjengoni.
 
Jmushi1,

Mkuu unaweza kutuwekea nakala ya maneno haya toka kwa Kafulila au Zitto mwenyewe maanake navyojua mimi ni waandishi wa haya magazeti waliopandikiza mbegu hizi. Sijawahi soma mahala Zitto akipinga maamuzi ya Dr. Slaa isipokuwa ile siku alokuwa Germany akaambiwa kuhusu mkutano wa siri Dodoma.. na majibu yake yalikuwa wazi kabisa kwamba itakuwa ni makosa kumfukuza Kafulila Uanachama.

Wanaboidi,
Kilichotokea kimetokea na haya yote mazungumzo ni baada ya habari kwani Kafulila hakufukuzwa bali alivuliwa cheo chake na Zitto hakupinga hatua hiyo.. hakuna mahala Zitto amesema Chadema au Dr. Slaa amefanya makosa kumwengua Kafulila ktk wadhifa isipokuwa ni waandishi wenye chuki binafsi ndani na nje ya Chadema wanaojaribu kukiharibu chama kwa kupitia mgogoro huu. Ajabu ni kwamba wote hawa walikuwa tayari wamezivua nguo zao kuyakoga maji haya machafu, sasa kinachonishinda kuelewa ni kwamba Kafulila kaondoka, bado mnamfuafuta aliko na maneno mengi kuendelea kuhakikisha Zitto pia anaondoka Chadema...
Hii inatisha sana na pengine inanipa sura kamili ya vichwa vya wanachama wa Chadema..

Mkandara,

Hata kwenye thread hii Kafulila kasema Zitto akisema kampa password yake atakuwa mzushi. Sisi sasa tunajadili ya kafulila kumwita Zitto mzushi. Hivi kweli hata tunaelewa tunajadili nini? Kweli Zitto na akili zake atampa mtu mwingine password yake? Kama hakutoa password na hajasema popote kwamba kampa mtu password, tunachojadili hapa hakipo.

Watu wanajadili yale yanayowajia vichwani mwao hata kama hawana uhakika nani kasema au nani hakusema.

Kinachotokea hapa ni ndoa imebadilika kuwa chachu. Baada ya kukubali talaka na kusonga mbele, watu wanatumia muda mwingi kuelezea yale ambayo walipokuwa wapenzi yalikuwa hayaongelewi.

Ukiachana na mtu mtakie mema huko aendako na wewe endelea na ya kwako. Vinginevyo unaonekana una donge, umechukia kupewa talaka au kuachwa na mwisho wake ni kuchafuana tu.
 
Jmushi1,

Mkuu unaweza kutuwekea nakala ya maneno haya toka kwa Kafulila au Zitto mwenyewe maanake navyojua mimi ni waandishi wa haya magazeti waliopandikiza mbegu hizi. Sijawahi soma mahala Zitto akipinga maamuzi ya Dr. Slaa isipokuwa ile siku alokuwa Germany akaambiwa kuhusu mkutano wa siri Dodoma.. na majibu yake yalikuwa wazi kabisa kuwa haiwezekani na itakuwa ni makosa kumfukuza Kafulila Uanachama kulingana na katiba ya chama.

Wanaboidi,
Kilichotokea kimetokea na haya yote mazungumzo ni baada ya habari kwani Kafulila hakufukuzwa bali alivuliwa cheo chake na Zitto hakupinga hatua hiyo.. hakuna mahala Zitto amesema Chadema au Dr. Slaa amefanya makosa kumwengua Kafulila ktk wadhifa isipokuwa ni waandishi wenye chuki binafsi ndani na nje ya Chadema wanaojaribu kukiharibu chama kwa kupitia mgogoro huu. Ajabu ni kwamba wote hawa walikuwa tayari wamezivua nguo zao kuyakoga maji haya machafu, sasa kinachonishinda kuelewa ni kwamba Kafulila kaondoka, bado mnamfuafuta aliko na maneno mengi kuendelea kuhakikisha Zitto pia anaondoka Chadema...
Hii inatisha sana na pengine inanipa sura kamili ya vichwa vya wanachama wa Chadema..

Mkuu wangu this is politics, Kafulila ameondoka na anatoa tuhuma ambazo Chadema kama chama wanaziktaa sasa ulitaka Chadema wafanye nini?
 
Journalistic integrity, nitalia kila siku.

Ona hapa muandishi anakubali kabisa kwamba basis nzima ya habari ni tetesi.Tetesi!

Sio kitu alichosema Zitto publicly kwamba kampa Kafulila password, tetesi tu.

Msukumo wa Kafulila kumshutumu Zitto umetokana na tetesi kwamba amekuwa anatumia barua pepe ya mbunge huyo kusambaza taarifa zinazoleta chokochoko katika CHADEMA, kwa kuwa anajua neno siri la anuani ya barua pepe ya mbunge huyo ambaye amekuwa anamtumia kama msaidizi wake katika masuala mengi walipokuwa CHADEMA.

Sasa tuangalie kwenye article, kwa maneno ya Kafulila mwenyewe - direct quote- bila kufuata interpretation ya muandishi ambayo inaweza kupotosha.

Article nzima ina direct quotes mbili tu.

Moja Kafulila anasema hakupewa password na Zitto, na kwamba huo ni uzushi unaotengenezwa tu (hakusema unatengenezwa na nani)

“Huo ni uzushi unaotengenezwa…password (neno siri) ni kitu muhimu, tena ni siri ya mhusika, sasa iweje Zitto anipe password yake? Hayo ni maneno ya uzushi.”

Direct quote ya pili anasema

“Nimefukuzwa bila kufuata sheria. Sijaridhishwa kabisa na maamuzi yale, ndiyo maana nikaona nitafute tumaini jingine ambalo ni NCCR-Mageuzi,”

Kichwa cha habari kinasema "Zitto ni mzushi - Kafulila"

Watuonyeshe katika article hii ni wapi Kafulila kasema Zitto ni mzushi?
 
Inaelekea harakati za kuhakikisha upinzani hautoi changamoto kubwa kwa CCM katika uchaguzi wa 2010 zinaanza kufanikiwa, tena kwa haraka kuliko ilivyotarajiwa.

Baada ya muda mfupi tu, tutaanza kuelewa kuwa CHADEMA, chama kilichoonekana kuwa usumbufu kwa CCM kitaangamia na kuwa kama baadhi ya vyama vingine vya upinzani.

CCM ina uwezo mkubwa kwa kweli. labda na bahati ya ajabu. Kila wapinzani wanachokifanya wakati kama huu ni kuhakikishia CCM ushindi wa nguvu tu.
 
- Tuache uoga jamani hii ni Demokrasia at work, hivi ni vipimo tu ambavyo hutokea naturally chama cha siasa kinapotaka kusogea kutoka low level kwenda to the next level ambayo inakuwa determnined na the results za how chama kinaweza ku-handle the tribulations, hata TANU walipitia hii stage mpaka Makaputula alipokuja na kuinyooosha jahazi.

- Wakiziweza wanakuwa bigger and better, wakishindwa wanashuka to the lower level kuliko mwanzoni, yaani kama Mrema. Kusingizia wengine kutoka nje ni dalili za a weakness of chama ku-deal na hizi waves za vipimo.

- Wa-Tanzania wakati umefika sasa tujifunze kusikiliza sauti tofauti na tunazozitaka tu! na bila kuamini kwamba zinatumwa na maadui, sometimes huwa ni test kutoka kwa the political Gods, ili watuvushe mbele zaidi!

Respect.

FMEs!
 
Punguza jazba mangi, twende taratibu tutafika tu. Tangu lini umejitoa chadema chalii angu!!??au ndo umeanza kuwakana wenzako?
Jitahidi kufanya homework yako vizuri, isome hiyo makala ya huyo mwandishi vizuri, soma katikati ya mistari halafu uje unionyeshe ni wapi tanzania daima wamezungumza na zitto na akawaeleza kwamba kafulila ana password yake kama si majungu ya tanzania daima &co., Na hata kama aliwahi kumpa password yake kutokana na ukaribu wao, bado siamini kwamba zitto ni mzembe kiasi cha kuzungumza jambo kama hilo mbele ya watu.
kwahiyo usiwe na shaka chalii angu ninakuona vizuri sana "where you coming from".
Kafulila kaondoka zake kwenda nccr na ametangaza kuingia kilingeni kupambana na chadema kwahiyo msiweweseke, jipangeni mkakabiliane nae huko huko kwenye battle field, haya makelele mnayoendelea kupiga inaonyesha ni kiasi gani kafulila amewashika pabaya.

Mwita,sifa yetu ya "upole" naona imejidhihirisha,wapi nimeongea kwa jazba?quote maneno yoyote kwenye posting yangu unionyeshe ni maneno yapi yenye jazba.
Pili mimi si mwana CHADEMA na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote kile...Hiyo ni FYI.

Tatu,watu wa kukanusha ni wao na si wewe,tusubiri tusikie na wao watasema nini,hayo waliyoyasema ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari.Maswala ya kushikwa pabaya certainly hayanihusu,kila mtu ana haki ya kutoa mchango based anavyoona yeye na si vinginevyo,na huo ndio mchango wangu.Wewe ndiyo ume assume kuwa maneno hayo si ya kweli where as mimi nina analyze habari yenyewe,kama kuna ambao wandhani kuwa hawajatendewa haki na habari hiyo then watatoa statement zao either kukanusha ama kukubali,tofauti yangu mimi na wewe ndio hapo ilipo,wewe umeshaconclude kutokana na mtizamo wako kuhusiana na Tanzania Daima na chadema,vile vile kuna watu wana conclude tofauti kutokana na mitizamo yao kuhusiana na magezeti mbali mbali either na vyama vya kisiasa,wanasiasa ama wafanyabiashara na watu mashuhuri,mara zote yeyote anayeandikwa tofauti na anavyotaka ama kama anaona amelishwa maneno basi lazima ajibu mapigo,ndivyo ilivyo kweye issue zinazoihusisha public,la sivyo unaweza ukawa perceived vinginevyo.

Mimi nili analyze habari hiyo kutokana na matokeo kadhaa ambayo yamejitokeza siku za hivi karibuni kiwa ni pamoja na Kafulila kujitoa,ni wazi Zitto hakupendezwa ila alikubaliana na kusimama upande wa maamuzi ya katibu mkuu wa chama chake,na ni wazi kuwa bado urafiki wao hauwezi kwisha kwasababu ya maamuzi ya katibu,na ndio maana habari ikaja kuhusiana na msaada wa magari matatu,sikuona mahali Zitto amekanusha habari hizo,lakini nilijuwa kama ni kweli basi lazima ndani ya cham chake watamwuliza,muda ukapita,ndio habari hii kaja hapa,na kwa ku connect the dots kutokana na mtizamo wangu,ndio nikaona kuwa inawezekana amebanwa ndani ya chama chake na ikabidi akanushe,na Kafulila kuulizwa akasema Zitto ni mzushi,sasa hadi hapo tutakapopata taarifa zaidi ndio tunaweza ku conclude vinginevyo,wewe umetumia style ya kushambulia upande mmoja na kui disregard habari yote jumla jumla,lets wait and see.
 
Mkuu wangu this is politics, Kafulila ameondoka na anatoa tuhuma ambazo Chadema kama chama wanaziktaa sasa ulitaka Chadema wafanye nini?
Mkuu umeuvaa mkenge vizuri...
Kafulila kaulizwa na kajibu kutokana na upuuzi aloulizwa..Kafulila kasema alosema kama ni uongo wewe inakuuma kitu gani wakati unajua fika hakuna kitu kama hicho Chadema. Sasa wakijibu kwa mapigo kama haya watu kama sisi tutawaelewa vipi kama sii utoto mtupu unaotembea..
Jamani Politics hazichezwi hivi, pengine mnahitaji mtu anayejua kuuza majungu na sii upuuzi kama huu. wataamini tu hao mnaoweza kuwaaminisha lakini ukweli utabakia wazi..

Mbona simsikii Mbowe ama Dr. Slaa wakipiga makelele haya? waoa ndio wanashutumiwa na mengi yanawalenga wao. Mbowe na viongozi wengine wote wanaweza kabisa kujihami inapobidi lakini sii kwa upuuzi kama huu kwani majungu yanayotembea hapa JF na hasa kuhusiana na Zitto inakatisha tamaa.
Bianfsi naamini kabisa Kafulila alifanya makosa mengine kabisa tofauti na habari tuloisoma hapa JF..Nimeunganisha story zote na kufahamu wapi kuna pumba iwe toka kwa Kafulila au Waandishi wa habari. Tatizo ni pale napoona watu wengine wakiamini upuuzi kama huu kwa imani za kupigwa mhuri.
 
umegundua kama kanjanja kama alivyo willy edward

huyu mwandishi yupo too biased,kasahau taaluma yake nini,ndo maana tunazidi kuibiwa tu,maana vibaraka wamezidi,kila gazeti kuna vibaraka wameamua kuipumbaza jamii ya kitanzania kwa uandishi wao uchwara tu,uongo mwingi,hizi siasa za Tz bwana ni kweli hata Mungu kazichoka tu.
 
Umuhimu wa Kafulila ni chama alikotoka, lengo la kwenda alikokwenda na walio nyuma ya mission nzima ya kufanya anayofanya.

Hakuna zaidi na hastahili hata kidogo kujadiliwa hapa jamvini
 
iritating....Kafulila (kafulia), Zitto, Makamba, Simba khaaaaa! Masikio yanauma nawish kungekuwa na mahali ambapo sitasikia huu upupu anymore!!

Ni kweli kabisa, kama tunhetumia mda kuangalia namna ya kufufua maendeleo ya jamii na kuboresha miundombinu tungekuwa mbali
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom