Yaani we mwandishi ni mpuuzi kweli kweli.
Hivi nyie tz daima kwanini hamna hata chembe ya aibu?Kafulila keshajiondokea zake kwenda nccr lakini hamjaridhika tu bado mnaendelea kumfuata fuata. Nadhani mmetumwa kumgombanisha na swahiba wake zitto na hiyo kazi mnaifanya kwa bidii kweli kweli. Lakini hii yote ni kutaka kummaliza kijana wa watu, muacheni kafulila na nccr yake mnamtafutia nini?Chadema mjipange vizuri na huyo mgombea wenu muslim hassanary akapambane na kafulila msianze kuweweseka saa hizi na kumuandama kijana wa watu. Nyie mlimuona sisimizi kaamua kujiondokea zake. Kajiunga nccr ghafla amegeuka kuwa tembo, sasa anawanyima usingizi. mtachonga sana mwaka huu, mtaandika udaku mpaka mkome. Kama bado mnamuhitaji si mkamuombe tu msamaha muyamalize arudi kundini, hizi siasa za chuki mnazoziendesha hazitawasaidia chochote zaidi ya kuzidi kuwashusha hadhi yenu mbele ya watanzania.
Shame on you tz daima!!