Yaani we mwandishi ni mpuuzi kweli kweli!
Hivi nyie tz daima kwanini hamna hata chembe ya aibu?Kafulila keshajiondokea zake kwenda nccr lakini hamjaridhika tu bado mnaendelea kumfuata fuata. Nadhani mmetumwa kumgombanisha na swahiba wake zitto na hiyo kazi mnaifanya kwa bidii kweli kweli. Lakini hii yote ni kutaka kummaliza kijana wa watu, muacheni kafulila na nccr yake mnamtafutia nini? Chadema mjipange vizuri na huyo mgombea wenu Muslim Hassanary akapambane na Kafulila msianze kuweweseka saa hizi na kumuandama kijana wa watu.
Nyie mlimuona sisimizi kaamua kujiondokea zake. Kajiunga nccr ghafla amegeuka kuwa tembo, sasa anawanyima usingizi. mtachonga sana mwaka huu, mtaandika udaku mpaka mkome. Kama bado mnamuhitaji si mkamuombe tu msamaha muyamalize arudi kundini, hizi siasa za chuki mnazoziendesha hazitawasaidia chochote zaidi ya kuzidi kuwashusha hadhi yenu mbele ya watanzania.
Shame on you Tz Daima!!
All these guys are political dumber guys, hakuna jipya hapa ndugu zangu
ni lazima tuhoji aina ya mwandishi na aina ya makala....
ni nidhamu gani ilyotumika kumshughulikia JOHN HECHE ambaye ni KIBARAKA wa MBOWE aliyetishia kumpiga makofi Zitto na kutukana matusi ya nguoni viongozi Huku akijua ni Naibu katibu mkuu wake na ndiye selling picture ya chama?..
Mbona wewe kinabo ni mwanachama wa CHADEMA, sasa iweje umjadili kiongozi wako mkubwa wa chama Gazetini?..tena katika gazeti la bosi wako?...kama kafulila hana nidhamu kwa kuwasema viongozi wake magazetini, wewe pia vipi?...
Edward Kinabo
basi anayejadiliwa ni mtu ambaye kwa majukumu ya cheo chake, ana dhamana kubwa katika ama kuboresha au kuangamiza mustakabali wa taifa hili maskini.
Iweje kumsaidia mtu ambaye anaamini kuwa ana umuhimu wake katika kuwezesha demokrasia nchini kutofautiane na mustakabali wa Taifa mradi tu ameshindwa kukubaliana na aina ya uongozi wa Mwenyekiti wako ambaye naye hajawahi kuficha chuki zake kwake hadi kushindwa kwenda kumtakia hali hospitalini alipodondoka ghorofa kadhaa akiwa anatekeleza majukumu yake ya CHAMA chenu.....
Nikiri kuwa mimi ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa kijana huyu. Mbali ya kuwa kijana mwezangu na mwanaharakati mwenzangu, nimekuwa nikiguswa na uwezo wake wa kujenga hoja pamoja na misimamo yake katika baadhi ya masuala ya kitaifa, kabla na baada ya kuwa mbunge. Kama Watanzania wengine wengi, nami nilisisimka sana, pale aliposimamia ile hoja ya mgodi wa Buzwagi iliyompatia umaarufu baada ya kusimamishwa ubunge.
Ni wazi ushabiki wako unatokana na kusisimkwa kwako na sio misingi, itikadi, dira na mitizamo ya Zitto hivyo sio ajabu kutomuelewa.
Yaani unaamini kazi ya Zitto ni hii ya vita dhidi ya ufisadi na utawala mbovu wa CCM tu? Again muono wako finyu wa kisiasa kama huu ndio maana huwezi kamwe kumuelewa ZittoKwa nafasi yake kama kiongozi wa juu wa moja ya vyama vikubwa vya upinzani nchini (CHADEMA), nimekuwa nikiitazama karama yake ya kisiasa, kama nyenzo ya kukiimarisha chama chake, ili kuwapatia Watanzania chama imara kabisa cha upinzani, kinachoweza kuwatetea na kuwapigania dhidi ya ufisadi na utawala mbovu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
lakini pia kwa kushiriki kujiandikisha, kupiga kura na kuzilinda kura hizo
No wonder ukashindwa kulinda kura za Mnyika 2005. Ningekuwa mzushi kama ninyi ningedai mliuza ushindi kwa CCM
Hali ya mazingira, wakati na mwenendo mzima wa tukio hilo inafanya iwe vigumuu katofautisha yaliyomtokea Kafulila na "sakata" la Zitto kujaribu kushindana na Mwenyekiti wako katika nafasi ya uongozi wa juu wa chama chenu.....Ni matukio yanayomhusu Kafulila
Kwa hulka hii bado mnaamini kuwa ninyi mnaweza kuwa mbadala wa CCM? Hii lugha haitofautiani kabisa na ya kina Makama..Kinachonifanya nisimwelewe Zitto ni kutoa kauli za moja kwa moja katika vyombo vya habari akipinga na kuonyesha kutoridhishwa na uamuzi wa kuondolewa Kafulila katika nafasi ya uofisa habari. Pengine ingelikuwa ni busara kwake kushauriana na viongozi wenzake kwanza juu ya mawazo yake, badala ya kulipuka kwenye vyombo vya habari akimtetea Kafulila aliyetenda kosa la dhahiri.
Hivi baada ya yale matusi ya nguoni na kutishia kumdhuru Zitto kulikofanywa na mgombea wenu wa uenyekiti wa Baraza la Vijana John Heche, watanzania walimsikia Mbowe ama Slaa akipinga kitendo hicho, Ina maana kunyamaza kwako kulikuwa kubariki utovu wa nidhamu wa aina ile?Kitendo cha Zitto kupinga uamuzi huo, hakina tafsiri nyingine yoyote zaidi ya kubariki au kufumbia macho utovu wa nidhamu, eti kwa sababu tu Kafulila ana akili nyingi, anajua kujenga hoja na huenda akashinda Kigoma Kusini.
Hivi mara ngapi ninyi kama wanachama na hata viongozi wa CHADEMA mmekuja hapa kumtukana Zitto na kumzushia kila aina ya uchafu lakini hatujasikia si chama wala viongiz wake kuwakosoa wakati wote mnajuana huku na majina vivuli mnavyotumia na hata kuazimana password kufanya shunghuli hizo eti kwa umakini...
Ni hatari kuwa na upungufu wa wabunge wa upinzani, lakini ni hatari zaidi kuwa na maofisa wasio na nidhamu kwa chama wala kwa viongozi wa kitaifa wanaoheshimika na waliokijengea chama haiba njema hata kukubalika kwa Watanzania walio wengi.
Tuache kujidanganya. Unaposema watanzania walio wengi wanakubali haiba ya chama inayojengwa na Mbowe ama Slaa utakuwa unaendelea kujidangany na kubweteka. Majibu ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita yalipaswa kuwaamsha kutoka katika usingizi wa pono mnaojilaza nao...
Hivi kuna umuhimu gani kulinda utovu wa nidhamu wa ofisa wa chama, huku chama kizima kikiwa kimechafuliwa na ofisa huyo na kuvunjiwa heshima mbele ya umma wa Watanzania, kwa viongozi wake wakuu kudaiwa kufanya vikao ghetto?
Unajua wazi kuwa hiyo ilikuwa ni sababu tu ya utekelezaji wa mpango ulikarabatiwa siku nyingi na kuhalalishwa na kikao hicho alichokilalamikia Kafulila. Hivi ni tangia wakati gani ambapo mwenyekiti wenu alikuwa akidai kuwa hawezi kufanya kazi na Kafulila. Hayo sio maneno aliyoyatumia wakati akimfanyia kampeni Heche dhidi ya Kafulila?
Watanzania watakiungaje mkono chama ambacho viongozi wake wanafanya vikao vyao ghetto? Simuelewi Zitto Kabwe!
Ni vizuri yakatoka haya mapema ili mbadilike mapema.....
Je, kuna ubaya gani wa hili? Ina maana kwenu ushindi wa upinzani ni lazima utoke CHADEMA na sio kwengine? Hivi kweli unaamini bila ya mahusiano mema kama haya kati ya vyama vya upinzani mnaweza kweli kushindana na CCM? Acheni kujidanganya....Kwa mujibu wa habari hiyo, kiongozi huyo wa CHADEMA ameamua kumuunga mkono Kafulila ili kuhakikisha jimbo hilo linaondoka mikononi mwa CCM na kwenda upinzani.
Masahihisho. Hili neno la ufadhili linatumika kuendeleza propaganda zenu dhidi ya Zitto. Kufadhili kunaonyesha kuwa Zitto amewapa NCCR Mageuzi magari hayo tofauti na ukweli wenyewe. Kwanza magari hayo yasemwayo yote ni mabovu yako yamelala gereji kutokana na kutumika kwa shuguli za CHADEMA mkoani kigoma na zaidi katika operesheni SANGARA ambako tpfauti na wengine, Zitto hajawahi kudai malipo ya matumizi ya vitu vyake na wala fedha zake.Kwamba, Zitto ametoa ufadhili wa magari matatu kwa Kafulila wa NCCR-Mageuzi ili zimsaidie katika ziara ya jimboni kwake anayokusudia kuifanya hivi karibuni kwa lengo la kuwaeleza wanachama wa CHADEMA sababu za kujiondoa CHADEMA na hatima yake kisiasa.
Pia mantiki ya Zitto ni kumuazima magari hayo kama Kafulila ataweza kuyalipia matangenezo yanayohitajika na kuyatumia katika ziara ya ke ya hivi karibuni tu na sio vinginevyo.
Zaidi ya Kafulila, ni kiongozi yupi wa CHADEMA kutoka makao makuu ambaye amekuwa akisota kufanya kampeni na shughuli za chama chenu katika jimbo hilo? Hivi hata fedha za shughuli hizo anazozifanya Kafulila zimewahi kutoka katika mfuko wa CHADEMA? Usipindishe maneno, Zitto alisema Kafulila ndiye aliyejenga CHADEMA huko Kigoma Kusini hadi kufikia kushindana viti na CCM na NCCR mageuzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita tofauti na ilivyokuwa miaka minne kabla.Kwamba, Zitto anaamini Kafulila ndiye aliyejenga CHADEMA kama chama ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano na NCCR-Mageuzi katika maeneo ambayo chama hicho kina nguvu.
Unapodai kuwa "ilikoelezwa" kuwa yuko masomoni kama vile wewe hujui wakati hata katibu mkuu wako alilisemea hilo kwa uwazi una maana gani? Ama tayari mmeshasuka jungu la kitu kingine mtakachodai Zitto anakifanya huko? Apokee simu yako ili iweje wakati ni wazi nia na madhumuni yako ni kuendelea vita yenu dhidi yake.....Habari hiyo sawa na ile iliyomkariri Zitto akipinga kuondolewa kwa Kafulila katika uofisa habari, hadi namaliza kuandika makala hii ilikuwa bado haijakanushwa. Jitihada zangu za kumpata Zitto kuthibitisha ufadhili wake kwa Kafulila na NCCR-Mageuzi hazikufanikiwa, kwani simu yake anayotumia huko Ujerumani ilikoelezwa kuwa yu masomoni, iliita bila kupokewa.
Hivi kweli kwa siasa mnazifanya sasa CHADEMA mnaweza kuwa na uthubutu wa kumnyoshea kidole yeyote anayefanya siasa chafu mnaziita siasa za maji taka dhidi yenu? Kuna siasa za maji taka zinazoendelea sasa kama sio hizi zenu dhidi ya Zitto? Anayoyasema Kafulila sasa hajawahi kuyasema wakati akiwa ndani ya CHADEMA tena ndani ya vikao vya chama? Unategemea yeye angefanya nini kama nanyi mmeshindwa kuwa na uvumilivu wa tofauti za kimitazamo ndani ya chama?Ninamshangaa kwa kumfadhili kada wa chama kingine cha siasa (NCCR-Mageuzi), ambaye tangu ajitoe CHADEMA amekuwa akifanya kazi ya kukichafua chama hicho cha Zitto kwa propaganda za uongo na siasa za maji taka, kwa lengo la kujijengea umaarufu.
Hoja yake ya kumsaidia Kafulila ashinde ubunge ili kuimarisha upinzani inanishangaza. Ni kweli tunahitaji upinzani imara bungeni, lakini hatuwezi kuimarisha upinzani bila kuimarisha kwanza vyama na kuvilinda visiporomoke. Siasa zetu ni siasa za vyama, wabunge wote wa kuchaguliwa hutokana na vyama.
Kwa mtazamo huu ni wazi kuwa kamwe huwezi kumuelewa Zitto na jinsi gani ulivykosea kuwa shabiki wake kwa kuchochewa na hamasa tu. Wakati niny mnafikiria Tanzania ya ndani ya CHADEMA na nje ya CCM na UFISADI, Tanzania anayoiona Zitto ni kubwa na pana zaidi petty Tanzania of urs. Chama kinachodai kupigania demokrasia na uongozi bora hakiwezi kuwa na mtazamo wa kuwa tofauti za ndani za kimitazamo ama uhuru wa kutoa mawazo kwa jinsi alazimikavyo (ndiyo mmemlazimisha Kafulila kutumia style aliyotumia) mwanachama kama dalili ya kuporomoka kwa chama. Chama makini kingelichukulia tofauti hizo kama chachu ya kujirekebisha na kujijenga zaidi na si vinginevyo.
Zitto na hili mmelikubali katika chama kuwa kwa sasa muhimu ni kujitahidi kuondoa ukiritimba wa CCM katika siasa za nchi ikiwemo kuondoa "absolute" majority ya CCM katika bunge. Sasa hivi kweli unataka kujidanganya CHAMDEMA mna uwezo, mbinu na nafasi ya kulifanikisha hilo 2010 bila ya ushirikiano na vyama vingine pale ambapo ni wazi wana nafasi kubwa ya kuishinda CCM zaidi yenu?Hivi Zitto kwa nafasi yake kama Naibu Katibu Mkuu, atakuwa ameimarisha vipi upinzani kwa kumfadhili Kafulila na harakati zake za kujiongezea umaarufu kwa kuichafua CHADEMA?
Yaani huu umaarufu unaochuja kwa haraka mlioupata hivi karibuni tena kwa Kafara ya Zitto tayari mmeshaanza kujidanganya kuwa mnaweza kujenga upinzani imara bila ya kusihirikiana na vyama vingine vya upinzani...
Kafulila ni mtu au kwa maneno ya Dk. Slaa ni sisimizi tu. CHADEMA ni chama.
Hii inaonyesha jinsi gani mnavyojidanganya. Yaani hata baada ya kushindwa kutumia nafasi mliyokuwa nayo kuhakikisha mafanikio makubwa katika uchaguzi uliopita, mmeshakuwa na jeuri ya kuanza kuitana sisimizi. huu ushabiki usio na mashiko endelevu unawafanya tayari nanyi mjione mmekuwa TEMBO kama CCM?
Unabariki Slaa kumwita Kafulila sisimizi halafu unamshutumu Kafulila kuwa ni mtovu wa nidhamu kwa kusema kuwa Slaa aliitisha mkutano wa GHETTO?
Mko tayari "kummaliza" kisiasa kinara wenu katika wabunge mlio nao na bado mnajidanganya watakuja wengine kupata ubunge kupitia chama chenu..Tunapozungumzia ubunge, Kafulila akishinda atakuwa ameshinda yeye tu kama Kafulila lakini tunapozungumzia hadhi na mwelekeo wa CHADEMA kama chama, watu wengi zaidi wanaweza kupata ubunge kupitia chama hicho.
Ufinyu wa mitizamo mwengine huu. Yaani unadhani kuwa UPINZANI ni CHADEMA na CHADEMA ni UPINZANI. Kwa lipi hilo? Wabunge watano wa kuchaguliwa na sita wa kuteuliwa na asilimia saba za kura za watanzania?Kumbe Zitto anaimarisha upinzani kupitia kwa mtu anayebomoa upinzani. Vituko vitupu.
Last time niona sehemu imeainishwa kuwa zitto amejitole magari matatu kwa ajili ya ku facilitate ziara ya kafulila huko kigoma.
Lakini pia nimeshtuka sana kusoma gazeti la jana la Tanzania Daima kuhusu Kafulila na Zitto.
Please naombeni na nyie mcheki below kama ilivyo;
na Irene Mark
DAVID Kafulila, mwanachama mpya wa NCCR-Mageuzi, ambaye amekuwa akitumia uhusiano wake binafsi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kama kete ya kisiasa katika ugomvi wake na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema Zitto ni mzushi.
Kafulila, ambaye alikuwa Ofisa Habari wa CHADEMA kabla hajavuliwa cheo hicho na kukimbilia NCCR-Mageuzi, alisema hayo jana Dar es Salaam, wakati akijibu taarifa kuwa mbunge huyo amekanusha kumsaidia magari matatu ya kufanyia harakati za kujijenga kisiasa mkoani Kigoma baada ya kujiunga na NCCR-Mageuzi.
Msukumo wa Kafulila kumshutumu Zitto umetokana na tetesi kwamba amekuwa anatumia barua pepe ya mbunge huyo kusambaza taarifa zinazoleta chokochoko katika CHADEMA, kwa kuwa anajua neno siri la anuani ya barua pepe ya mbunge huyo ambaye amekuwa anamtumia kama msaidizi wake katika masuala mengi walipokuwa CHADEMA.
Taarifa hizo zilitokana na mawasiliano ya Zitto na watu walio karibu naye ambao juzi waliliambia gazeti hili wanachokiita ukweli wa madai ya mbunge huyo kumuunga mkono Kafulila katika harakati zake mpya akiwa NCCR-Mageuzi, kiasi cha kumpatia magari matatu kwa ajili ya kuzunguka maeneo kadhaa ya Jimbo la Kigoma Kusini katika siku chache zijazo.
Jana Kafulila aliiambia Tanzania Daima kuwa kama ni hivyo, Zitto ni mzushi, kwani hajawahi kumpa neno la siri la kufungua anuani ya barua pepe yake, wala hafahamu lolote kuhusu anuani hiyo.
Katika toleo la jana, gazeti hili lilkuwa na habari kuwa Zitto alimkana Kafulila, na kwamba mbunge huyo amekiandikia barua chama chake (CHADEMA) kukijulisha msimamo wake binafsi, kwa maelezo kuwa wanaomhusisha na kauli za Kafulila wana nia ya kumchonganisha (Zitto) na uongozi wa CHADEMA.
Kauli kama hii ilitolewa na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto, katika mahojiano yake na gazeti la MwanaHALISI wiki mbili zilizopita, akisema mwanawe anatumiwa na watu wenye lengo la kuvuruga chama na kumgombanisha mwanawe na uongozi wa chama chao.
Katika kauli yake ya juzi, Zitto alinukuliwa akiwaeleza watu walio karibu naye kuwa hata taarifa zinazoandikwa na vyombo vya habari kuhusu yeye kumbeba Kafulila zinamnukuu bila kumhoji yeye.
Lakini jana Kafulila alisema: Huo ni uzushi unaotengenezwa password (neno siri) ni kitu muhimu, tena ni siri ya mhusika, sasa iweje Zitto anipe password yake? Hayo ni maneno ya uzushi.
Nimefukuzwa bila kufuata sheria. Sijaridhishwa kabisa na maamuzi yale, ndiyo maana nikaona nitafute tumaini jingine ambalo ni NCCR-Mageuzi, alisema
Sasa tuamini yupi?
Yani mpaka inakera sasa, Nahisi hawa jamaa journalists wa TZ wamekosa habari. Maana za Ufisadi sijui zimechakaa?Guys,why don't you give Zitto a break!!!!!!,this Zitto issue imekuwa too much sasa,kila kukicha Zitto Zitto aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaargh,inaboa sasa!!
Iweje kumsaidia mtu ambaye anaamini kuwa ana umuhimu wake katika kuwezesha demokrasia nchini kutofautiane na mustakabali wa Taifa mradi tu ameshindwa kukubaliana na aina ya uongozi wa Mwenyekiti wako ambaye naye hajawahi kuficha chuki zake kwake hadi kushindwa kwenda kumtakia hali hospitalini alipodondoka ghorofa kadhaa akiwa anatekeleza majukumu yake ya CHAMA chenu.....
Omar;
Usimzushie Mwenyekiti wa CHADEMA kwa kadri ya taarifa ambazo zililetwa hapa JF na hata magazetini huyo Bwana Kafulila alianguka ghorofani mwezi Disemba 2008, wakati huo uchaguzi wa CHADEMA umefanyika Septemba 2009; vipi useme alikuwa na chuki nae? Umekuwa ukisema hapa kwamba Mdee na Mnyika wapo kundi la Mbowe; mbona imeelezwa hapa kwamba hawa ndio wamekwenda kumtibu na kulipia matibabu yake? Kama ingekuwa chuki ya unachokiita kambi ya Mbowe si wangemuacha tu ili apelekwe hospitali na kambi ya Zitto ambayo mama yake alikuwepo eneo la tukio?
Ni wazi ushabiki wako unatokana na kusisimkwa kwako na sio misingi, itikadi, dira na mitizamo ya Zitto hivyo sio ajabu kutomuelewa.
Yaani unaamini kazi ya Zitto ni hii ya vita dhidi ya ufisadi na utawala mbovu wa CCM tu? Again muono wako finyu wa kisiasa kama huu ndio maana huwezi kamwe kumuelewa Zitto
No wonder ukashindwa kulinda kura za Mnyika 2005. Ningekuwa mzushi kama ninyi ningedai mliuza ushindi kwa CCM
Wewe umetajwa humu kuwa ni msaidizi binafsi na rafiki wa karibu wa Zitto. Unaweza kutueleza maono yake? Umemtaja mwandishi wa makala hii Edward Kinabo kuwa alishindwa kulinda kura za Mnyika mwaka 2005, unaweza kutuambia ilikuwaje? Alikuwa ndio mlinzi wake wa kura?
Hali ya mazingira, wakati na mwenendo mzima wa tukio hilo inafanya iwe vigumuu katofautisha yaliyomtokea Kafulila na "sakata" la Zitto kujaribu kushindana na Mwenyekiti wako katika nafasi ya uongozi wa juu wa chama chenu.....
Kwa hulka hii bado mnaamini kuwa ninyi mnaweza kuwa mbadala wa CCM? Hii lugha haitofautiani kabisa na ya kina Makama..
Hivi baada ya yale matusi ya nguoni na kutishia kumdhuru Zitto kulikofanywa na mgombea wenu wa uenyekiti wa Baraza la Vijana John Heche, watanzania walimsikia Mbowe ama Slaa akipinga kitendo hicho, Ina maana kunyamaza kwako kulikuwa kubariki utovu wa nidhamu wa aina ile?
Hivi mara ngapi ninyi kama wanachama na hata viongozi wa CHADEMA mmekuja hapa kumtukana Zitto na kumzushia kila aina ya uchafu lakini hatujasikia si chama wala viongiz wake kuwakosoa wakati wote mnajuana huku na majina vivuli mnavyotumia na hata kuazimana password kufanya shunghuli hizo
Haya ni madai mazito sana umetoa kuhusu mwandishi wa makala hiyo. Unaweza kutuambia ni kwa vipi chaguo la Mbowe kwenye uenyekiti wa vijana alikuwa John Heche Diwani wa Tarime? Hilo tukio la John Heche kutaka kumchoma kisu Zitto Kabwe lilitokea wapi? Ulilishuhudia wewe mwenyewe au umehadithiwa? Maana tukio la Mbunge kuchomwa kisu lilipaswa kuwa tukio kubwa ambalo lingekuwepo vyombo vyote vya habari na hata taarifa zingekuwa polisi? Kama ni Kafulila, unaweza kutuambia ni lini na wapi alitishiwa na walau ukataja mashahidi wawili watatu? Unaweza kujikuta unaeneza uzushi wa gazeti la Mwananchi. Nakumbuka Bwana Heche aliwahi kuhojiwa na magazeti mbalimbali akaeleza uzushi wa habari ile kumchafua, akataka ajitokeze yoyote hata kama ni Kafulila aseme kama ni kweli yeye ametishia yoyote kwa kisu. Kuhusu Zitto kuchafuliwa, unaweza kututajia ni viongozi gani, wamemchafua wapi kuhusu nini? Sana sana mimi nakumbuka Zitto aliwahi kukukanya hapa kwa tabia yako hii ya kuendelea kuzusha mambo ambayo yanamfanya awe na malumbano na viongozi wenzake. Je, amekupa ruhusa urudi tena kuanzisha malumbano?
Tuache kujidanganya. Unaposema watanzania walio wengi wanakubali haiba ya chama inayojengwa na Mbowe ama Slaa utakuwa unaendelea kujidangany na kubweteka. Majibu ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita yalipaswa kuwaamsha kutoka katika usingizi wa pono mnaojilaza nao...
Unaweza kutupa hayo majibu ya serikali za mtaa, mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya pamoja na uchambuzi wako ili tujadili vizuri hapa allegations zako? Maana tumeona humu tamko la Kamati Kuu lilitolewa kuhusu uchaguzi huu. Lina hoja, ukilinganisha na tuhuma zako za ujumla
Umerudia tena kutoa tuhuma kwa Mwenyekiti wa chama ambacho wewe umekuwa ukisema hapa hutaki kujiunga nacho. Halafu unajiita rafiki wa Zitto na mshauri wake wa kisiasa. Unakuwaje mshauri wa Naibu Katibu Mkuu wakati huo huo unasambaza matusi na uasi dhidi ya CHADEMA ambayo yeye anaiongoza? Sasa tueleze hapa kwa hoja, lini mwenyekiti Mbowe alitangaza kumkataa Kafulila na kumuunga mkono Heche. Kwa kuwa tu Zitto alikuja hapa na kutangaza kwamba anakwenda kufanya kampeni Kafulila achaguliwe huku viongozi wenzake wakikaa kimya kuachia vijana wachaguane wenyewe basi ndio unadhani kwamba ni lazima kila kiongozi wa chama awe na makundi na mgombea wake wakati wa uchaguzi wa ndani ya chamaUnajua wazi kuwa hiyo ilikuwa ni sababu tu ya utekelezaji wa mpango ulikarabatiwa siku nyingi na kuhalalishwa na kikao hicho alichokilalamikia Kafulila. Hivi ni tangia wakati gani ambapo mwenyekiti wenu alikuwa akidai kuwa hawezi kufanya kazi na Kafulila. Hayo sio maneno aliyoyatumia wakati akimfanyia kampeni Heche dhidi ya Kafulila?
Ni vizuri yakatoka haya mapema ili mbadilike mapema.....
Je, kuna ubaya gani wa hili? Ina maana kwenu ushindi wa upinzani ni lazima utoke CHADEMA na sio kwengine? Hivi kweli unaamini bila ya mahusiano mema kama haya kati ya vyama vya upinzani mnaweza kweli kushindana na CCM? Acheni kujidanganya....
Masahihisho. Hili neno la ufadhili linatumika kuendeleza propaganda zenu dhidi ya Zitto. Kufadhili kunaonyesha kuwa Zitto amewapa NCCR Mageuzi magari hayo tofauti na ukweli wenyewe. Kwanza magari hayo yasemwayo yote ni mabovu yako yamelala gereji kutokana na kutumika kwa shuguli za CHADEMA mkoani kigoma na zaidi katika operesheni SANGARA ambako tpfauti na wengine, Zitto hajawahi kudai malipo ya matumizi ya vitu vyake na wala fedha zake.
Pia mantiki ya Zitto ni kumuazima magari hayo kama Kafulila ataweza kuyalipia matangenezo yanayohitajika na kuyatumia katika ziara ya ke ya hivi karibuni tu na sio vinginevyo.
Kwa hiyo Omar, tuchukulie kwamba hii ni kauli rasmi ya Zitto kupitia kwako kwamba amefadhili magari matatu kwa NCCR kupitia kwa Kafulila? Maana Mwenyekiti wa NCCR sio ulimuona akitoa tamko kwenye taarifa ya habari ya TBC la kumshukuru Zitto kwa kuichangia NCCR?
Zaidi ya Kafulila, ni kiongozi yupi wa CHADEMA kutoka makao makuu ambaye amekuwa akisota kufanya kampeni na shughuli za chama chenu katika jimbo hilo? Hivi hata fedha za shughuli hizo anazozifanya Kafulila zimewahi kutoka katika mfuko wa CHADEMA? Usipindishe maneno, Zitto alisema Kafulila ndiye aliyejenga CHADEMA huko Kigoma Kusini hadi kufikia kushindana viti na CCM na NCCR mageuzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita tofauti na ilivyokuwa miaka minne kabla.
Omar, tatizo wewe si mwanaCHADEMA kwa hiyo huijui CHADEMA. Kamwambie Zitto akueleze kuhusu CHADEMA. CHADEMA kwa kawaida wanagawana maeneo ya kukijenga chama, ndio maana unaona kuna watu wamepewa kazi ya kujenga maeneo mbalimbali na ruzuku ya chama na michango mingine inatumika kwa ajili hiyo. Zitto Kigoma Kaskazini; Kafulila na Muslim Hassanal Kigoma Kusini, Mama Kiwanga Kilombero, Benson Kibakwe, Msafiri Mtemelwa Urambo Mashariki nk. Kwa hiyo huwezi kuwalaumu viongozi wa chama kutokwenda huko kama ambavyo huwezi kuwalaumu kwa kutokwenda Kilombero. Lakini kukiwa na Operesheni za pamoja si unawasikia wanazunguka wote? Kwa hiyo Sangara ikienda Kigoma viongozi wote hao watakwenda huko Kigoma Kusini.
Halafu sio kweli kwamba Kafulila hakupewa ruzuku ya chama kuhamasisha chama kule. Yeye mwenyewe amekiri katika mahojiano na waandishi wa habari kuwa alipewa fungu la chama kwenda kuhamasisha huko akalitoa kwa uongozi wa mkoa wake.
Umesema hakuna kiongozi wa kitaifa aliyekwenda Kigoma Kusini; Muslim Hassanal ana cheo gani? Si ametangaza kuwa yeye ndio alikuwepo huko wakati wote wa serikali za mitaa na kusaidia ushindi wakati Kafulila alikuwa Dar es saalam na Zitto? Unaweza kumuuliza Zitto Muslim ni nani na yuko wapi kwa sasa, na utueleze hapa kwa kuwa hata mimi ningependa ajitokeze maana naona mko kumsema Kafulila tu wakati chama jimbo lile kilianza kujengwa toka mwaka 2005 wakati Muslim alipogombea ubunge akiwa na miaka 22 na kupata kura 16,000.
Unapodai kuwa "ilikoelezwa" kuwa yuko masomoni kama vile wewe hujui wakati hata katibu mkuu wako alilisemea hilo kwa uwazi una maana gani? Ama tayari mmeshasuka jungu la kitu kingine mtakachodai Zitto anakifanya huko? Apokee simu yako ili iweje wakati ni wazi nia na madhumuni yako ni kuendelea vita yenu dhidi yake.....
Umemtuhumu tena mwandishi wa habari kuwa anagenge laki lenye vita dhidi ya Zitto, unaweza kutupa ushahidi wa tuhuma zako hata kama ni wa kimazingira? Maana mtu mzima kama wewe sio vizuri kuropokaropoka ambaye Zitto amekueleza humu JF kuwa ni mshauri/msaidizi wa karibu wa Salim Ahmed Salim huwezi kuropoka kwa kiwango hiki.
Hivi kweli kwa siasa mnazifanya sasa CHADEMA mnaweza kuwa na uthubutu wa kumnyoshea kidole yeyote anayefanya siasa chafu mnaziita siasa za maji taka dhidi yenu? Kuna siasa za maji taka zinazoendelea sasa kama sio hizi zenu dhidi ya Zitto? Anayoyasema Kafulila sasa hajawahi kuyasema wakati akiwa ndani ya CHADEMA tena ndani ya vikao vya chama? Unategemea yeye angefanya nini kama nanyi mmeshindwa kuwa na uvumilivu wa tofauti za kimitazamo ndani ya chama?
Tuhuma nyingine bila maelezo wala ushahidi. Tufafanulie
Kwa mtazamo huu ni wazi kuwa kamwe huwezi kumuelewa Zitto na jinsi gani ulivykosea kuwa shabiki wake kwa kuchochewa na hamasa tu. Wakati niny mnafikiria Tanzania ya ndani ya CHADEMA na nje ya CCM na UFISADI, Tanzania anayoiona Zitto ni kubwa na pana zaidi petty Tanzania of urs. Chama kinachodai kupigania demokrasia na uongozi bora hakiwezi kuwa na mtazamo wa kuwa tofauti za ndani za kimitazamo ama uhuru wa kutoa mawazo kwa jinsi alazimikavyo (ndiyo mmemlazimisha Kafulila kutumia style aliyotumia) mwanachama kama dalili ya kuporomoka kwa chama. Chama makini kingelichukulia tofauti hizo kama chachu ya kujirekebisha na kujijenga zaidi na si vinginevyo.
Unaweza kuyaeleza hayo maono ya mbali? Pia Kafulila amelazimishwa vipi kutumia staili ya kuita viongozi wenzake kuwa ni wafanyaji wa vikao visivyo rasmi vya Ghetto asivyotambua maamuzi yake na kwamba vikao hivyo viliamua kumvua uanachama, tuhuma ambazo ilibainika hazina ukweli wowote?
Zitto na hili mmelikubali katika chama kuwa kwa sasa muhimu ni kujitahidi kuondoa ukiritimba wa CCM katika siasa za nchi ikiwemo kuondoa "absolute" majority ya CCM katika bunge. Sasa hivi kweli unataka kujidanganya CHAMDEMA mna uwezo, mbinu na nafasi ya kulifanikisha hilo 2010 bila ya ushirikiano na vyama vingine pale ambapo ni wazi wana nafasi kubwa ya kuishinda CCM zaidi yenu?
Unataka kuwaeleza watanzania kuwa Omar Ilyas, ambaye ni mtu wa karibu na Salim Ahmed Salima; wote wawili wakiwa si wanachama wa CHADEMA, anaweza kuwashauri CHADEMA waachie NCCR mageuzi jimbo la Kigoma Kusini na wakiunge mkono chama ambacho Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe ambaye ni mtu wa karibu yake pia; amekitaja hapa JF kuwa kilipewa fedha za EPA mwaka 2005 kwenda kuvuruga majimbo ambayo CHADEMA ilikuwa na nguvu?
Yaani huu umaarufu unaochuja kwa haraka mlioupata hivi karibuni tena kwa Kafara ya Zitto tayari mmeshaanza kujidanganya kuwa mnaweza kujenga upinzani imara bila ya kusihirikiana na vyama vingine vya upinzani...
Tatizo lako wewe una ugonjwa wa kufikiria Zitto tu; huwezi kuzungumzia umaarufu wa CHADEMA bila kutambua mchango wa Mbowe aliyekiongoza chama na kukikuza kwa ziara toka mwaka 2003 na kuongeza hamasa alipogombea urais mwaka 2005 wala huwezi kuacha kutamja Slaa, ambaye wakati hoja ya Zitto ya Buzwagi inawasilishwa bungeni yake ya BOT ikazuiwa. Mapokezi ya Zitto yakafanyika Dar es salaam, ziara zikaanza nchi nzima na kumalizikia tena Dar es salaam Mwembe Yanga ambapo Dr Slaa na Tundu Lissu walisoma Orodha ya Mafisadi(List of Shame). Kama unadhani kwamba Zitto pekee ndio Kafara ya umaarufu wa CHADEMA nitaanza kufikiri kwamba urafiki wenu ni zaidi ya maneno unayoyaandika hapa JF, inawezekana mnaurafiki wa vitendo ambao mimi siwezi kuuingilia. Ila ushauri wangu kwako, usipende sana kumzungumzia mtu mmoja tu, na kuwaona watu wengine hawana maana duniani; hizo ni tabia za wanaume kama mabinti.
Asha
Hii inaonyesha jinsi gani mnavyojidanganya. Yaani hata baada ya kushindwa kutumia nafasi mliyokuwa nayo kuhakikisha mafanikio makubwa katika uchaguzi uliopita, mmeshakuwa na jeuri ya kuanza kuitana sisimizi. huu ushabiki usio na mashiko endelevu unawafanya tayari nanyi mjione mmekuwa TEMBO kama CCM?
Unabariki Slaa kumwita Kafulila sisimizi halafu unamshutumu Kafulila kuwa ni mtovu wa nidhamu kwa kusema kuwa Slaa aliitisha mkutano wa GHETTO?
Mko tayari "kummaliza" kisiasa kinara wenu katika wabunge mlio nao na bado mnajidanganya watakuja wengine kupata ubunge kupitia chama chenu..
Ufinyu wa mitizamo mwengine huu. Yaani unadhani kuwa UPINZANI ni CHADEMA na CHADEMA ni UPINZANI. Kwa lipi hilo? Wabunge watano wa kuchaguliwa na sita wa kuteuliwa na asilimia saba za kura za watanzania?
Kuna Habari kupitia gazeti la Mwananchi kuwa Zitto ameweka bayana kuwa anataka kujivua nafasi zote kupitia Chadema kutokana na hali ya kisiasa kupitia Chadema na kudai kuwa anataka kuendelea na maisha yake ya kawaida na pia amesema kuwa ataendelea kumuunga mkono mgombea wa NCCR MAGEUZI Kigoma Kusini hata kama CHADEMA wakiweka mgombea wao. Je Ndugu zangu wadau wanasemaje huu ya hali ya mambo ndani ya CHADEMA. Hali kama hii inakatisha sana tamaa na kuona badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma.