Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Imagine ZITTO anahama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Mkuu umeshathibitisha? ukituthibitishia tutajadili kwa lugha zote. Hatuwezi tukajadili hali ya Chadema mpaka tuone nini kinaendelea ndani.
Mkuu nimesoma mambo haya kupitia gazeti la leo mwananchi kama ndio hivi hawa wakina Zitto wanatuhuzunisha sana katika siasa za Tanzania na pia kama ni kweli basi aje yeye mwenyewe Zitto hapa na kusema madai haya.. Maana mambo kama haya Sisi kama wadau tunahuzunishwa sana
 
Habari zenu ndugu zangu wana Jamii mimi ni mpya humu nawaomba mnipokee kwa hali na mali na mniongoze nnapokosea naomba mnirekebishe asanteni sana...
 
Kweli sasa naamini kuwa Politicians are really dumber people and wako kwa ajili ya maslahi yao
 
Natamani Zitto atoe msimamo wake kwanza kabla sijaanza kutoa hoja,maana hili ni pigo kwa upinzani nchini(Sio Zitto bali migongano hasa nyakati karibu na uchaguzi )
 
Tuangalieni sana kwa makini juu ya tarifa hizi. Kwenye gazeti la mwanachi la leo kuna tarifa hizo za zito kujiuzuru. Lakini ukienda kwenye mtandao wao www.mwananchi.co.tz hakuna kitu kama hicho. Hii inaonyesha kuwa ni habari ya kupika. Halafu ukiisoma vizuri utaona kwamba Zitto aliwasiliana na mwananchi kwa barua pepe, lakini mwishoni wanasema zitto aliwapigia simu? Kipi kati ya hivyo ni sahihi? Na kwanini hiyo habari iliondolewa online kama inaukweli wowote?
 
Issue ya Zitto & Kafulila naona Mwananchi wameishikia kidedea, itaishia pabaya endapo itaendelezwa...!
Sasa basi aje yeye mwenyewe aseme hapa na pia kuliko kuacha mambo yaende hivi hali itakuwa mbaya sana
 
Tuangalieni sana kwa makini juu ya tarifa hizi. Kwenye gazeti la mwanachi la leo kuna tarifa hizo za zito kujiuzuru. Lakini ukienda kwenye mtandao wao www.mwananchi.co.tz hakuna kitu kama hicho. Hii inaonyesha kuwa ni habari ya kupika. Halafu ukiisoma vizuri utaona kwamba Zitto aliwasiliana na mwananchi kwa barua pepe, lakini mwishoni wanasema zitto aliwapigia simu? Kipi kati ya hivyo ni sahihi? Na kwanini hiyo habari iliondolewa online kama inaukweli wowote?
Sasa hapa kama na yeye sio makini na kuona kuwa kipindi hiki kuna vitu vingi basi ataingia kwenye mtego huu na pia pengine habari hizi aseme yeye mwenyewe ni kweli au vipi??
 
Ha, mwananchi hawajipendi? Litabadilika kuwa rai mda si mrefu
Kumbuka kuwa Hata Makamba amelisifia sana Gazeti la Mwananchi?? hivyo sisi kama wadau aje Zitto kudhibitisha habari hizi
 
kwa nini SLAA HAJAANDIKWA?
ZITTO ANAVUNA ALICHOPANDA,

MIMI SIONI SABABU YA KUTOANDIKWA HABARI ZAKE AU CHADEMA HUMU JF, wakati alipokuwa kwenye peak kila mtu alikuwa anaona kuandikwa Chadema au Zitto ni sawa tu, lakini sasa inaonekana inauma.
 
Niliona hicho kichwa cha habari katika website ya mwananchi jana,nilipojaribu kufungua ikakataa.Niliporefresh page ikatoweka kabisa.Mwenye access na gazeti la mwananchi pls atupe walau kwa ufupi nini kimeandikwa kwenye gazeti hilo.
 
kwa nini SLAA HAJAANDIKWA?
ZITTO ANAVUNA ALICHOPANDA,

MIMI SIONI SABABU YA KUTOANDIKWA HABARI ZAKE AU CHADEMA HUMU JF, wakati alipokuwa kwenye peak kila mtu alikuwa anaona kuandikwa Chadema au Zitto ni sawa tu, lakini sasa inaonekana inauma.

Hii habari iko kweli kwenye ukurasa wa mbele wa Mwananchi. Hata hivyi hawa jamaa wa Mwananchi hawana kosa lolote kwa maoni yangu, kwa kuwa kazi yao ni kuandika habari na kuuza story zinazovutia wasomaji wengi. Naamini CHADEMA na Zitto wanalijua hilo. Kama wanataka mambo yaishe basi wawanyime hot stories. Ushauri wangu kwa Zitto na wenzake kwa sasa ni kuwa watakuwa na hekima isiyo kifani kama wakiamua kukaa kimya. Kwa sababu kila neno moja watakalotoa litazaa maneno mengine 1000 (exponential amplification of the stories). Vinginevyo mjadala wa ufisadi umepata mbadala na mafisadi sasa wanapumua. Wakati huo wanahesabu siku na kujipanga na EPA nyingine kuelekea Oktoba 2010.
 
Kwenye gazeti la leo wameandika mwananchi na wawe makini sana wanavyosema zitto amelalamika email yake kuchezewa na wanachadema
 
Tatizo letu siasa zetu bado ni changa sana kama ilivyo nchi yenyewe, siasa inayoruhusu pesa za wafanyabiashara kufanya kazi yake ndiyo tabu yake, mwanasiasa anaonekana ana msimamo mzuri akishaanza kuyumba yumba kwa sababu ya ushawishi fulani uwe wa pesa au wa namna nyingine basi hatufai kamwe!! misimamo mibovu ya watu wa aina hii inawachanganya wananchi na kuwaweka gizani kwamba waelekee wapi sasa!! maana hata wale wanaowategemea kuwaonesha njia muafaka wanajikanganya, HIVI KUNA SIRI GANI YA MIGOGORO NDANI YA VYAMA VYA SIASA VYA TANZANIA?
 
Walikuwepo akina mabere marando na wenzake, walitupa matumaini na tukaamini sasa tumepata ukombozi wa kisiasa, wako wapi? Wametuacha juani, sasa akina zitto nao wamekuja na watatuacha hivi hivi na makelele yetu, watanzania tuko pamoja kweli katika vita hii?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom