Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,445
- 7,813
Leo bunge limetengua kanuni kuruhusu wageni wasioruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa hotuba ya Rais Samia Suluhu, miongoni mwao ni Makamu wa Rais, Philip Mpango na Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi.
Pia spika Ndugai aliwashauri wabunge wasivae tai nyekundu kwasababu ni kwaajili ya mwenye mamlaka, ushauri wa Ndugai baade ukaondoka kwenye hiyari na kusema watakaovaa wataishia geti la nje. Rais Samia Suluhu anatarajiwa kuhutubia bunge leo saa kumi baada ya kuchukua madaraka ya Urais kutoka kwa hayati John Magufuli.
"Ningependa kuwakumbusha wabunge siku anapokuja kiongozi, mkuu wa nchi haishauriwi sana kwa wenzangu na mimi kuvaa tai nyekundu, nadhani tumekubali ile red inabakia na mwenye mamlaka, ni vizuri kuyajua hayo mambo, jioni tutakaporudi tai nyekundu utarudia geti la nje" Alisema spika Spika Job Ndugai.