Kama agenda yake ni KATIBA mpya basi huyo ndiye mwamba tunayetaka kumsikiliza.Maana katiba ndio inayotengeneza mfumo wa utawala na namna ya kuwajibika. Labda Kama hujui nguvu ya katiba katika maisha ya kawaida, ukadhani NI kakijitabu tu basi, ninakupa pole Sana. Na hiyo ndio 95% suruhisho la matatizo yetu
 
Aisee Lissu hana jipya; ni matatizo yake binafsi hana analojua kuhusiana na maisha ya wananchi wala nini.

1. Hoja ni kiinua mgongo chake

2. Kuishi Ulaya kwa tabu kama mgonjwa

3. Kutembelewa na makamu wa rais akiwa hospitali

4. Dereva wake alipo

5. Katiba na mikutano ya siasa

Kama kuna mtu anadhani kuna jipya kwa lisu atasubili sana.

USSR
Wewe una hoja gani zaidi ya Uchawa? Naona Wajinga mnaongezeka kwa Kasi ya kitisha
 
Eti kaenda kijijini kwao kuonyesha makovu yake, duh. Hilo lijamaa limeshageuza makovu kuwa agenda kuu.

:p:p😂😂😂😌
yaani kama namsikia na kumuona vile, akiwa anageugeuka kuonyesha na kusema, '....hapa ndio ya kwanza ilipoingia'....', hapa ndio dereva aliponiambia geuka, alinichuuza nikapewa nyingine!, '....nikajilalia...', wakendelea kumwaga aisee mijamaa mikatili, mmh nyingine imeingia wakati najaribu kuangalia wapi cctv ipo....duh!

Jokes aside aliumia kweli na simwombei kiumbe chochote machungu anayo yapata au aliyoyapata,kwani majeraha aliyopata mhhh manake hata katika mchepuko anaulizwa na '...hapa je? Yaani anatoneshwa kidonda na mchepuko...

Hatahivyo na yeye ajaribu kupata usaidizi wa majeraha yake badala ya kuendelea kuchokonoa kidonda kwa kutoa dukuduku hadharani wakati anajua Hayati magufuli alikuwa na Familia, aidha walikuwa hawajui hulka zake au wameanza kujua baada ya mauti, kwa vyovyote vile inauma.

Wananchi wameumia, hatuwezi kuendeleza kutoneshana vidonda sababu tu ya kutaka dola, sababu ya kutaka huruma.

Tundu Lissu anaweza kupaa bila kinyongo au kisasi.

Amani
 
We we magonjwa mtambuka unacheka unaona haya ya kucheka😁
😁😁😁😜😏😝
 
Aisee Lissu hana jipya; ni matatizo yake binafsi na jamii inayafahamu sana maana taarifa za yeye kushambuliwa na kukimbilia Ulaya sio jambo gani masikioni mwa watanzania kama ni pole tulimpa sana sasa maisha lazima yaendelee tu ,kwa waliosomea mambo ya habari watakubaliana na mimi kuwa kama jambo linajulikana sio habari tena.

Kwa sasa hoja za kitaifa ishu za maisha magumu ,tozo , uzembe kazini, mfumuko wa bei,na n.k ishu ya katiba CCM ya Samia imesha sema watawapa sasa lisu aje na ishu za msingi sio za kujiita chiba hana analojua kuhusiana na maisha ya wananchi wala nini anawaza maisha yake tu.

1. Hoja ni kiinua mgongo chake

2. Kuishi Ulaya kwa tabu kama mgonjwa

3. Kutembelewa na makamu wa rais akiwa hospitali

4. Dereva wake alipo

5. Katiba na mikutano ya siasa( hii walishakubaliana na CCM

Kama kuna mtu anadhani kuna jipya kwa lisu atasubili sana.

Anadai anaiamini zaidi CCM ya kuliko wapinzani wenzake huyu hayuko sawa kwani UKAWA vipi tena

USSR
Jee hayo anayazungumzia kwenye mikutano? Hapana usipotoshe makusudi.
Kwenye mikutano kazungumzia hali ya nchi na ugumu pamoja na utatuzi.
Hayo ya kushambuliwa kayasemea kwenye mahojiano mbalimbali na yameendana na maswali yaliyo andaliwa na walio mwalika.
Mlitaka aulizwe hali ya afya yake yeye ajibu kuhusu kilimo cha umwagiliaji? Msiwaze kijinga namna hiyo!
 
Za CCM ni zipi ambazo ni mpya kwa zaidi ya miaka 50? Ujinga
 
Kwani matatizo yenu watanzania yamebadilika?

1.UJINGA.
2.MARADHI.
3.UMASIKINI.
 
Kwani matatizo yenu watanzania yamebadilika?

1.UJINGA.
2.MARADHI.
3.UMASIKINI.
Bora hayo kuliko makovu ya mtu kwani kuna mtu hana kovu makovu yapo kwa watu wengi tu

USSR
 
Hivi hiyo katiba ndo itaitoa CCM madarakani ?

Lissu alituachia nchi leo anakuja na complications kibao

Mwambieni tufanye kazi kwanza, maneno yote tunayajua.

Sijasikia hata akitushukuru tuliompigia kura.
 
:p:p😂😂😂😌
yaani kama namsikia na kumuona vile, akiwa anageugeuka kuonyesha na kusema, '....hapa ndio ya kwanza ilipoingia'....', hapa ndio dereva aliponiambia geuka, alinichuuza nikapewa nyingine!, '....nikajilalia...', wakendelea kumwaga aisee mijamaa mikatili, mmh nyingine imeingia wakati najaribu kuangalia wapi cctv ipo....duh!

Jokes aside aliumia kweli na simwombei kiumbe chochote machungu anayo yapata au aliyoyapata,kwani majeraha aliyopata mhhh manake hata katika mchepuko anaulizwa na '...hapa je? Yaani anatoneshwa kidonda na mchepuko...

Hatahivyo na yeye ajaribu kupata usaidizi wa majeraha yake badala ya kuendelea kuchokonoa kidonda kwa kutoa dukuduku hadharani wakati anajua Hayati magufuli alikuwa na Familia, aidha walikuwa hawajui hulka zake au wameanza kujua baada ya mauti, kwa vyovyote vile inauma.

Wananchi wameumia, hatuwezi kuendeleza kutoneshana vidonda sababu tu ya kutaka dola, sababu ya kutaka huruma.

Tundu Lissu anaweza kupaa bila kinyongo au kisasi.

Amani
Japo umechangia kiutu uzima, nakukosoa kidogo. Tusimchagulie Lisu namna ya kulia. Mwacheni alie kadri atakavyo kwani ndio njia pekee ya kuponya hisia chungu. Hao wanaoumizwa na kulia kwake wavumilie tu kama yeye alivyovumilia maumivu makali kabisa kuwahi kumtokea maishani.
 
Sidhani kama kuna mtu anakataa Tundu Lissu kulia.

Sidhani kama kumtaja taja Hayati Magufuli ni hivi na vile ni kulia-
...binafsi naweza sema anamchafua ili yeye aonekane ni bora yake- kumbe jamaa ni lidikteta hatare.

Maumivu yalioipata nchi hii ni makubwa kwa.namno yeyote ile unayoangalia jambo la Kuumia, kuumizwa. ..Machozi hayakuwa ya mamba wala vilio havikuwa vya fisi tuliyoyaona na vilio tulivyosikia ndii ulikuwa mustakabali wa nchi.... Vidonda bado vibichi, yeye anakuja kutonesha tu. Kuna watu na ndevu za masikioni wanaona hayo

Naamini ana uwezo wa kufikisha ujumbe bila ya kutaka/kulazimisha huruma huruma. Kumbuka alikuwepo 2020 kwenye kinyanga'nyiro hatukusikia haya tunayoyasikia, kulikoni?

Nikupe nayoyaona?

Wamefinywa midomo- gagged-kuzungumzia CCM au Raisi moja kwa moja;amekiri hayo juzi kiaina kwa madai yeye hawezi kuzungumzia mambo ambayo mwenyekiti wake anajadiliana na CCM! kwa hivyo yeye hana issue zaidi ya kuonyesha makovu.
 
Back
Top Bottom