Tumpinge Lissu kwa hoja. Kutumia ulemavu wake kama hoja ya kisiasa ni kumwezesha kupata kura za huruma kwa wananchi

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,221
22,295
Binafsi sikubaliani kabisa na ushenzi aliofanyiwa Lissu na watu ambao hadi leo hawajajulikana. Lile tukio lilikuwa ovu mno kuwahi kutokea. Mimi naamini katika utawala wa sheria. Kama kuna kosa alifanya basi ilipaswa tu kumfikisha mahakamani na sio kumshindilia marisasi.

Kila ninapokumbuka Lissu alikuwa mzima kabisa na leo ni mlemavu kwa kulazimishwa kuwa huwa naumia sana. Alitendewa unyama. Kabla ya uongozi wa awamu ya 5 ilikuwa kawaida wanasiasa kutwangana kwa hoja bungeni na kwenye majukwaa ya kisiasa lakini nje na hapo ni marafiki kabisa hata club utawakuta wote. Siasa sio uadui.

Hata mara baada ya lile tukio la Lissu tuliona wanasiasa wengi wakisikitishwa mno bila kujali vyama. Mama Samia alionyesha mfano kwa kwenda kumtembelea Lissu hospitalini Nairobi kumjulia hali. Wanasiasa waandamizi ndani ya CCM hawajawahi kutamka maneno mabaya kuhusiana na Lissu. Mashetani wachache kama Musiba na Sabaya ndo wamewahi kuongea mbovu kabisa kuhusiana na mkasa uliompata Lissu.

Hapa JF kumetokea mashetani chipukizi wengi wakija na threads za kejeli dhidi ya ulemavu wa Lissu hadi inashangaza. Tukumbuke lile tukio lilibadilisha mwelekeo mzima wa maisha ya Lissu hivyo tunavyomwona anaongea ongea kuhusu hilo basi ndo anazidi kuiponya nafsi yake. AACHWE TU AONGEE. Kama atavuka mipaka vyombo vinavyohusika na sheria vipo. Kumkejeli na kumbeza ni sawa na kumsaidia yeye na chama chake kupata kura za huruma toka kwa wananchi.

Ikumbukwe Lissu kisiasa ni mdogo mno kumlinganisha hata na Hawa Bananga, Nusrat Hanje au Abdul Nondo hivyo kupangua hoja zake ni jambo jepesi mno. Pia ana udhaifu wa kutanguliza hisia (emotions) kwenye mambo yake hivyo hupatwa na hasira kirahisi mno. Mwanasiasa mwenye hisia kali ni rahisi mno kumbomoa kwa hoja. Lissu hajui aongee nini na mahali gani. Pia msimamo wake wa kutetea ushoga kwa hoja ya kuheshimu faragha za watu ni point nzuri sana ya kummaliza kisiasa.

Mwisho tukumbuke kila mtu anaweza kuwa mlemavu muda wowote. Unaweza kujikuta unapoteza hivyo vidole vinavyoandika upuuzi dhidi ya Lissu. Kuwa makini.
 
Akija na hoja za ulemavu atapigwa kwa ulemavu akija na sera za maana atajibiwa

USSR
 
Ikumbukwe Lissu kisiasa ni mdogo mno kumlinganisha hata na Hawa Bananga, Nusrat Hanje au Abdul Nondo hivyo kupangua hoja zake ni jambo jepesi

Hapo juu imebidi nicheke kwanza.
 
Binafsi sikubaliani kabisa na ushenzi aliofanyiwa Lissu na watu ambao hadi leo hawajajulikana. Lile tukio lilikuwa ovu mno kuwahi kutokea. Mimi naamini katika utawala wa sheria. Kama kuna kosa alifanya basi ilipaswa tu kumfikisha mahakamani na sio kumshindilia marisasi.

Kila ninapokumbuka Lissu alikuwa mzima kabisa na leo ni mlemavu kwa kulazimishwa kuwa huwa naumia sana. Alitendewa unyama. Kabla ya uongozi wa awamu ya 5 ilikuwa kawaida wanasiasa kutwangana kwa hoja bungeni na kwenye majukwaa ya kisiasa lakini nje na hapo ni marafiki kabisa hata club utawakuta wote. Siasa sio uadui.

Hata mara baada ya lile tukio la Lissu tuliona wanasiasa wengi wakisikitishwa mno bila kujali vyama. Mama Samia alionyesha mfano kwa kwenda kumtembelea Lissu hospitalini Nairobi kumjulia hali. Wanasiasa waandamizi ndani ya CCM hawajawahi kutamka maneno mabaya kuhusiana na Lissu. Mashetani wachache kama Musiba na Sabaya ndo wamewahi kuongea mbovu kabisa kuhusiana na mkasa uliompata Lissu.

Hapa JF kumetokea mashetani chipukizi wengi wakija na threads za kejeli dhidi ya ulemavu wa Lissu hadi inashangaza. Tukumbuke lile tukio lilibadilisha mwelekeo mzima wa maisha ya Lissu hivyo tunavyomwona anaongea ongea kuhusu hilo basi ndo anazidi kuiponya nafsi yake. AACHWE TU AONGEE. Kama atavuka mipaka vyombo vinavyohusika na sheria vipo. Kumkejeli na kumbeza ni sawa na kumsaidia yeye na chama chake kupata kura za huruma toka kwa wananchi.

Ikumbukwe Lissu kisiasa ni mdogo mno kumlinganisha hata na Hawa Bananga, Nusrat Hanje au Abdul Nondo hivyo kupangua hoja zake ni jambo jepesi mno. Pia ana udhaifu wa kutanguliza hisia (emotions) kwenye mambo yake hivyo hupatwa na hasira kirahisi mno. Mwanasiasa mwenye hisia kali ni rahisi mno kumbomoa kwa hoja. Lissu hajui aongee nini na mahali gani. Pia msimamo wake wa kutetea ushoga kwa hoja ya kuheshimu faragha za watu ni point nzuri sana ya kummaliza kisiasa.

Mwisho tukumbuke kila mtu anaweza kuwa mlemavu muda wowote. Unaweza kujikuta unapoteza hivyo vidole vinavyoandika upuuzi dhidi ya Lissu. Kuwa makini.
Katoa hoja gani huyo msanii?
 
Ukongwe katika siasa nadhani usitazamwetu kwa kigezo cha muda bali tuangalie na matokeo chanya aliyofanya mwana siasa

Nisawa na mtu kujisifia kuanza kutafuta hela zamani mbele ya kijana mdogo mwenye mafanikio lukuki.

Uzoefutu sio kigezo maana hata viongozi wakuu wa nchi kama Rais na Waziri mkuu wapo watu kibao walio wazidi umri na uzoefu wakati wanazaliwa walikua kwenye siasa na hata leo wanaminyana hata udiwani au ubunge hawajapewa

Kisiasa kumlinganisha nusrat na bananga dhidi ya Lissu naona unafanya dhihaka
 
Back
Top Bottom