Habari za mida wana JamiiForums.
Naomba nami nitoe kisa changu cha maisha cha kweli.
Kifupi ni nimelelewa na wazee wangu, nimesoma kwa tabu sana, ila kwakuwa nilikuwa vizuri darasani nilitoboa kila nilipopita.
Nimemaliza chuo kikuu nikarudi home, nikaajiriwa na kampuni binafsi kwa mkataba wa miaka mitatu, ndani ya mwaka serikali ikatangaza ajira na nikaajiriwa baada ya kuapply na interview zote nikashika nambari one.
Nikaanza kazi serikalini, nikaperform Kama yote, nikapandisha mapato ya halmashauri fulani Hadi kutikia kupewa cheti cha mkusanyaji mapato mahiri wa halmashauri.
Nikakutana na kijana mmoja, nilimtangulia chuo mwaka mmoja, akiwa kwenye mishe za yeye naye kutoka, nikamsapoti sana, tukawa wapenzi, nikashika ujauzito, Hadi kuzaa, ingawaje yeye alisita kwakuwa alikuwa Hana mbele Wala nyuma, nikamwambia relax, tuzae tutajua ya mbeleni.
Kweli nikazaa salama kwa kudra za Mungu, na nikahudumia mambo mengi kwakuwa hakuwa na kitu enzi hizo. Tukaenda nikiwa namsapot project zake, alipoanza kutoboa akaanza kubadilika, ukimwuliza anakuwa mkali. Nikavumilia Sana then nikaona nimwache tu, kisicho riziki hakiliki.
Nikamwambia tubaki wazazi, mengine fanya yako nami nifanye yangu, akakubali, so nikawa busy najitafutia na mwanangu. Tukakubaliana fifty fifty kwenye mahitaji ya mtoto, lakini akawa hatekelezi, ikafika kipindi nikaacha kumtafuta manake ukimtafuta anageuza story. Anyways ntarudi manake huyu mtu atakachofanywa ukoo wake mzima utajikusanya.🙏👊🏼
Sehemu ya Pili