Ngoja niweke habari vizuri;huyu budda tulizungumza kitambo hata mtoto hajafikisha miaka miwil,akasuggest nifungue akaunti ya mtoto kwaajili ya matumizi ya mtoto na hata ada.Nikafungua akaunti crdb kwa jina la mtoto,nikawa naweka hela na makubaliano ilikuwa naye awe anaweka ili mtoto asipungukiwe kwenye mahitaji yake.Toka nimefungua hiyo akaunti huu ni mwaka wa 4 hakuwahi kuweka hata senti 5,kila ukimkumbusha anasema ataweka Ila hakuwahi kuweka.
Ikawa sio ishu kwakuwa nami nilikuwa kazini na kipato napata nikawa namuhudumia mwanangu ile kizungu.Nikapata changamoto kazini nikadrop kiasi Fulani,nikaona sio kesi Basi ni muda wa budda naye kuchangia,akagoma kutoa ushirikiano.Napo nikaona nimpotezee nifanye yangu.
Sijakaa vizuri limekaa,ng'ombe hili na limke lake yanahangaika kuniulia mtoto,geez hata Kama ni wewe ndugu msomaji huwezi kaa kimya.Inauma mtu akuulie mtoto uliyembeba miezi 9 na kumgharamia mwenyewe,bila yeye kufanya lolote.Waishi maisha yao,wampotezee mwanangu,Ila kutaka kumdhuru siwezi kaa kimya Kama mama.