Kilimo cha Kisasa cha Mahindi: Mbegu bora, Mbolea bora na magonjwa

Habari ya majukumu,

Mimi ni mpya kwenye kilimo, Mwaka huu nna mpango wa kulima Mahindi, hekari 20 maeneo ya KwaKonji Handeni

Mpaka sasa tumeshafanikiwa kung’oa visiki, na kusafisha shamba tayari kupitisha trekta

Nahitaji kuongozwa vizuri, nijue ni wapi pa kuanzia ili niweze kupata mavuno mazuri.

Vile vile kama kuna taasisi ambayo ningeweza kwenda na kupata elimu hii na mtiririko sahihi nitashukuru mkinipa maoni.

Nawatakia majukumu mema
 
Hongera sana rafiki kwa kuamua kujikita katika Kilimo, maana ndio hasa msingi wa maisha kwa mwanadamu.

Kitu cha msingi kabisa ambacho huamua tija ya mkulima huwa ni mbegu, nakushauri utumie mbegu bora ya Mahindi hasa HYBRIDS ambazo kimsingi huzaa sana na wakati mwingine huvumilia sana ukame na Magonjwa.

Waone SEEDCO au MERU AGROTOUR, Hawa ndio kwa maoni yangu mbegu zao huwa ni za uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru kwa ushauri ndugu,

Duh hekari 20 kuzitoa visiki, umetumia sh ngapi kwa eka kutoa visiki na kusafisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habarini za asubuhi. Naomba kujua kilimo cha mahindi mabichi mikoa ya kusini kikoje. Namaanisha ni mkoa gani hasa unaweza kuingiza nguvu zangu,Bei ya shamba la kukodi kwa hekari,mavuno,masoko na mengineyo. Kwa anaefahamu tafadhali naomba anijuze.
 
Kwa mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma ukiomba shamba la kulima unapata bure ila labda wewe tu ushukuru kwa fedha kidogo na mara nyingi haizidi Elfu hamsini (50,000/=) kwa kijijini. Na hiyo fedha sio kwa hekari ila ni kwa eneo lote ulilolima japo kunabaadhi ya maeneo hukodisha kwa elfu thelethini kwa hekari moja.
Kila la kheri Ndg.
 
Vipi kwa mikoa ya iringa na njobe maana ndo naona wanazalisha sana mahindi mabichi kwenda mikoa ya dar na dodoma upatikanaji wa mashamba ukoje
Kwa mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma ukiomba shamba la kulima unapata bure ila labda wewe tu ushukuru kwa fedha kidogo na mara nyingi haizidi Elfu hamsini (50,000/=) kwa kijijini. Na hiyo fedha sio kwa hekari ila ni kwa eneo lote ulilolima japo kunabaadhi ya maeneo hukodisha kwa elfu thelethini kwa hekari moja.
Kila la kheri Ndg.
 
Habari wataalam,

Kwa mara ya kwanza nimefika katika ardhi isemekanayo kutukuka kwa rutba na mvua za kutusha kwa kilimo cha mahindi kiukweli nimeshawishika sana kuingia katika kilimo cha mahindi japo kilimo cha kutegemea mvua ya mungu kupata ni majaliwa ya Mola lakini mimi nitarisk na nimeplan kuanza na heka kumi (10) kulingana na uchumi wangu.

Nilichokipenda zaidi huku kulimo sio gharama sana gharama kubwa ni yakukodi shamba na kulima kwa trekta basi habari za mbolea hamna kabisa inasemekana ardhi hii inarutba ya kutosha kabisa kustawisha mazao bila kutegemea mbolea.

Kwa hesabu zangu za kawaida gharama ya kulima ekta 10 ni sawa mchanganuo huu chini..

Kukodi shamba 1kt = 30,000/- @10 (300,000/-)
Kulima kwa trekta 1kt = 30,000/- @10 (300,000/-)
Kupanda 1kt = 10,000/- @10 (100,000/)
Palizi 1kt =10,000/ @10x2 ( 200,000/-)
mbegu (200,000/-)

JUMLA. 1,100,000/-
Tuweke laki tano ya dharura ikitokea labda wadudu kununua dawa au kubadilika kwa bei ya vitu vingine
Jumla kuu itakuwa 1,600,0000/-

Sasa basi kwa kawaida kabisa kilimo kikitiki kwa ekta moja kupata gunia 7 ni kawaida kabisa sasa tuchukulie kiwango hichi cha chini kwa gunia7 kwa ekta kwaiyo sasa 7x 10 = 70 na kwa kawaida kabisa gunia moja kuuzwa elfu60 ni bei ya chini hivyo basi 70 x 60,000/- =( 4,200,000/)

Ukitoa hela niliowekeza (4,200,000/-1,600,000 =2,600,000/- ) napiga bingo la 2.6M kwa kipindi cha miezi 3 tu.

Naomba kuwasilisha nakaribisha mawazo na ushauri kutoka kwa wadau wa kilimo hasa kama umewai kulima kiteto.
 
Back
Top Bottom