Wakulima wa kilimo cha mahindi piteni hapa tafadhali

Kinumbo

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,742
4,931
Wakuu kheri ya mwaka mpya kwenu nyote, natumai mko poa. Hongereni pia kwa mapambano ya kilimo.

Wakuu nahitaji muongozo kadhaa kuhusu kilimo Cha mahindi. Nahitaji kwenda kufanya kilimo cha mahindi mkoani Morogoro. Nina ndugu yangu huko nae anajihusisha na kilimo katika kuwasiliana nae alinieleza kuwa kule hupanda mahindi mara mbili kwa mwaka katika nyakati tofauti. Ile ya kwanza ilinipita sasa nataka niende hii ya pili ambayo katika maelezo yake ni mwezi wa pili baada ya mavuno ya kwanza.

Nondo ninazo taka kujua ni kama ifuatavyo, kwanza kabisa kwa wale wanao fanya kilimo cha mahindi mkoani Morogoro huo muda nimeambiwa ni sahihi? Yaani kwa mwezi huu wa kwanza ni kuandaa shamba kisha mwezi wa pili ni kupanda na vipi kuhusu mvua kwa kipindi hicho huwa zipo kweli?

Nahitaji kwenda kufanya kilimo cha utaalamu zaidi maana kule wanafanya kienyeji tu sasa mimi naenda kivingine. Kwa maana hiyo napenda kujua ni mbegu aina ipi inakubali na kuzaa kwa wingi ukanda huo? Kwenye heka moja nitahitaji kuwa na mbegu kiasi gani kwa kilogram maana nitanunua zile zilizo kwenye pakti. Kwenye shimo niweke mbegu ngapi na kila umbali wa shimo na shimo uwe urefu upi?

Baada ya kupanda nisubili muda kiasi gani mpaka napiga palizi ya kwanza, hapo hapo baada ya kulima nisubili pia muda gani kwa kupiga madawa? Kule hawatumii mbolea ila mimi nataka nikatumie, mbolea kama DAP, CAN na UREA niweke muda gani kwa kila aina ya mbolea na kwa kila heka nitumie kiasi gani kwa kilogram? Madawa nitumie aina zipi kwa kila hatua itapendeza zaidi mkinitajia majina ya hizo dawa. Yapo mengi ya kuuliza nadhani tuta kuwa tunajulishana hapo chini kwenye reply.

Nisiwachoshe wakuu lengo kuu nahitaji kuingia na kufanya kilimo cha mahindi. Mimi sijawahi jihusisha na kilimo hicho ndio maana nimekuja hapa kuomba muongozo sahihi. Natambua kuwa katika jukwaa hili kuna wakulima wakubwa na wataalamu katika kilimo hichi cha mahindi hivyo napenda kupata muongozo sahihi kutoka kwenu.

Karibuni sana, niko hapa.
 
Habari mkuu,kati ya watu ambao nimetokea kujua kwamba wanapenda kilimo wewe ni mmoja wapo.
Hakuna thread ya kilimo itapita hapa bila kuchangia,nakushauri muulize uyo jamaa yako yuko wilaya gani hapo morogoro? maana kilimo tunachofanya sisi cha kujitafuta kinataka mvua za uhakika sio za kukadilia.Nakushauri fanya utafiti wa eneo hilo je kuna mvua za kutosha?
Pia kama una dreams kubwa za kufanya kilimo kizuri tafuta maeneo mazuri ambayo kilimo cha mahindi kinafanyika kwa uzuri na kuna mvua za kutosha E.g Rukwa,Katavi,Ruvuma nk.
Asante mkuu yangu ni hayo.
 
Kwa mtazamo wangu,maeneo mengi yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka,mvua za msimu wa pili si rasmi kwa kilimo kwa maana ya kuwa huwa si za kutosha sana,
Sasa ukiwekeza kwa kiasi kikubwa na mbolea utakozoweka ukikutana na mvua chache hapo itakuwa changamoto,
Kama upo serious sana na kilimo nenda kalime kwanza ule msimu wa mwanzo ili ujue na kupata uzoefu vizuri
 
Shukrani sana mkuu, kiukweli kilimo nakipenda sana.

Asante kwa ushauri mzuri.
Kwa mtazamo wangu,maeneo mengi yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka,mvua za msimu wa pili si rasmi kwa kilimo kwa maana ya kuwa huwa si za kutosha sana,
Sasa ukiwekeza kwa kiasi kikubwa na mbolea utakozoweka ukikutana na mvua chache hapo itakuwa changamoto,
Kama upo serious sana na kilimo nenda kalime kwanza ule msimu wa mwanzo ili ujue na kupata uzoefu vizuri
 
Wakuu kheri ya mwaka mpya kwenu nyote, natumai mko poa. Hongereni pia kwa mapambano ya kilimo.

Wakuu nahitaji muongozo kadhaa kuhusu kilimo Cha mahindi. Nahitaji kwenda kufanya kilimo cha mahindi mkoani Morogoro. Nina ndugu yangu huko nae anajihusisha na kilimo katika kuwasiliana nae alinieleza kuwa kule hupanda mahindi mara mbili kwa mwaka katika nyakati tofauti. Ile ya kwanza ilinipita sasa nataka niende hii ya pili ambayo katika maelezo yake ni mwezi wa pili baada ya mavuno ya kwanza.

Nondo ninazo taka kujua ni kama ifuatavyo, kwanza kabisa kwa wale wanao fanya kilimo cha mahindi mkoani Morogoro huo muda nimeambiwa ni sahihi? Yaani kwa mwezi huu wa kwanza ni kuandaa shamba kisha mwezi wa pili ni kupanda na vipi kuhusu mvua kwa kipindi hicho huwa zipo kweli?

Nahitaji kwenda kufanya kilimo cha utaalamu zaidi maana kule wanafanya kienyeji tu sasa mimi naenda kivingine. Kwa maana hiyo napenda kujua ni mbegu aina ipi inakubali na kuzaa kwa wingi ukanda huo? Kwenye heka moja nitahitaji kuwa na mbegu kiasi gani kwa kilogram maana nitanunua zile zilizo kwenye pakti. Kwenye shimo niweke mbegu ngapi na kila umbali wa shimo na shimo uwe urefu upi?

Baada ya kupanda nisubili muda kiasi gani mpaka napiga palizi ya kwanza, hapo hapo baada ya kulima nisubili pia muda gani kwa kupiga madawa? Kule hawatumii mbolea ila mimi nataka nikatumie, mbolea kama DAP, CAN na UREA niweke muda gani kwa kila aina ya mbolea na kwa kila heka nitumie kiasi gani kwa kilogram? Madawa nitumie aina zipi kwa kila hatua itapendeza zaidi mkinitajia majina ya hizo dawa. Yapo mengi ya kuuliza nadhani tuta kuwa tunajulishana hapo chini kwenye reply.

Nisiwachoshe wakuu lengo kuu nahitaji kuingia na kufanya kilimo cha mahindi. Mimi sijawahi jihusisha na kilimo hicho ndio maana nimekuja hapa kuomba muongozo sahihi. Natambua kuwa katika jukwaa hili kuna wakulima wakubwa na wataalamu katika kilimo hichi cha mahindi hivyo napenda kupata muongozo sahihi kutoka kwenu.

Karibuni sana, niko hapa.
Zao la kila mtu, kwa kifupi Mahindi ndio yanalimwa na kila mtu nchi hii na sio kitu cha kushangaza kwamba mtu analima mahindi,
 
Info za kilimo cha mahindi zimetaoakaa mno, huko huko unako enda kulima waulize, humu utapewa info za mtu yuko Musoma huko. Mahindi ni zao linalimwa hadi na watoto wadogo huko vijijini unakuta wana mashamba yao ya mahindi, binafisi katika zao ambalo sishangai mtu akilima ni Mahindi.
 
Wakuu kheri ya mwaka mpya kwenu nyote, natumai mko poa. Hongereni pia kwa mapambano ya kilimo.

Wakuu nahitaji muongozo kadhaa kuhusu kilimo Cha mahindi. Nahitaji kwenda kufanya kilimo cha mahindi mkoani Morogoro. Nina ndugu yangu huko nae anajihusisha na kilimo katika kuwasiliana nae alinieleza kuwa kule hupanda mahindi mara mbili kwa mwaka katika nyakati tofauti. Ile ya kwanza ilinipita sasa nataka niende hii ya pili ambayo katika maelezo yake ni mwezi wa pili baada ya mavuno ya kwanza.

Nondo ninazo taka kujua ni kama ifuatavyo, kwanza kabisa kwa wale wanao fanya kilimo cha mahindi mkoani Morogoro huo muda nimeambiwa ni sahihi? Yaani kwa mwezi huu wa kwanza ni kuandaa shamba kisha mwezi wa pili ni kupanda na vipi kuhusu mvua kwa kipindi hicho huwa zipo kweli?

Nahitaji kwenda kufanya kilimo cha utaalamu zaidi maana kule wanafanya kienyeji tu sasa mimi naenda kivingine. Kwa maana hiyo napenda kujua ni mbegu aina ipi inakubali na kuzaa kwa wingi ukanda huo? Kwenye heka moja nitahitaji kuwa na mbegu kiasi gani kwa kilogram maana nitanunua zile zilizo kwenye pakti. Kwenye shimo niweke mbegu ngapi na kila umbali wa shimo na shimo uwe urefu upi?

Baada ya kupanda nisubili muda kiasi gani mpaka napiga palizi ya kwanza, hapo hapo baada ya kulima nisubili pia muda gani kwa kupiga madawa? Kule hawatumii mbolea ila mimi nataka nikatumie, mbolea kama DAP, CAN na UREA niweke muda gani kwa kila aina ya mbolea na kwa kila heka nitumie kiasi gani kwa kilogram? Madawa nitumie aina zipi kwa kila hatua itapendeza zaidi mkinitajia majina ya hizo dawa. Yapo mengi ya kuuliza nadhani tuta kuwa tunajulishana hapo chini kwenye reply.

Nisiwachoshe wakuu lengo kuu nahitaji kuingia na kufanya kilimo cha mahindi. Mimi sijawahi jihusisha na kilimo hicho ndio maana nimekuja hapa kuomba muongozo sahihi. Natambua kuwa katika jukwaa hili kuna wakulima wakubwa na wataalamu katika kilimo hichi cha mahindi hivyo napenda kupata muongozo sahihi kutoka kwenu.

Karibuni sana, niko hapa.
Mimi ni Mkulima wa Mahindi ingawa niko mkoa wa Tanga ambapo pia wanapata mvua mara mbili yaani mvua za masika na mvua za vuli
Nikuweke sawa kuanzia mwezi wa pili hizo ni mvua za msimu wa masika ambazo mvua hizo zinakua ni za uhakika tofauti na mvua za vuli
Huku mkoa wa Tanga huwa mvua za kupandia zinaanza mwezi wa tatu na huko morogoro ni kweli wanapanda mwezi wa pili

Hatua muhimu kwa kilimo Cha mahindi

Kama unalima Morogoro ambapo wanatarajia kupanda mwezi wa pili jitahidi mpaka mwisho wa mwezi wa kwanza Shamba liwe safi
Kama Muda unao jitahidi uchimbe mashimo Kipindi cha kiangazi ili yakae wazi ili siku mvua ikinyesha uwe na kazi moja tu ya kufukia mbegu

BAADA YA MAHINDI KUOTA

Baada ya mahindi kuota kuna uwezekano wa kupita Kipindi cha jua kali,
Kipindi hiki kinapelekea mahindi kushambuliwa na wadudu aina ya Sondo siwajui kingereza chake hivyo puliza dawa ya kuua Sondo na ikiwezekana changanya dawa ya Sondo na mbolea ya Maji (Busta)

Baada ya wiki mbili au Tatu jitahidi upalilie palizi ya kwanza kwani hii ndio sehemu muhimu sana kwenye kilimo
Jitahidi mvua za masika zikukute ushapalilia
Baada ya hapo piga tena dawa ya Sondo na busta
Baada ya hapo piga palizi ya pili
Baada ya hapo subiri kuvuna

NB
Aina ya Mbegu
Mimi tokea nianze kilimo natumia Mbegu aina ya DK na haijawahi kuniangusha
Ninapanda Mbegu mbili kwa kila shimo kwa umbali wa cm 60 shimo kwa shimo na cm 75 Mstari kwa Mstari
Na kama shamba limepimwa kitaalam na halina mti wowote ndani ni wastani wa kilo 8 yaani mifuko 4 kilo 2 kwa kila ekari

Nafikiri nimekupa mwangaza japo kidogo
Nimekupa Experience from field kwani maisha yangu kwa zaidi ya Asilimia 80 nayaendesha kupitia kilimo
 
Shukrani sana na nimefurahi sana kupata neno kutoka kwa mkulima halisi. Mkuu hongera sana kwa kufanya kilimo, muongozo wako nitaufanyia kazi. Nitakutafuta kwa mara nyingine tena
Mimi ni Mkulima wa Mahindi ingawa niko mkoa wa Tanga ambapo pia wanapata mvua mara mbili yaani mvua za masika na mvua za vuli
Nikuweke sawa kuanzia mwezi wa pili hizo ni mvua za msimu wa masika ambazo mvua hizo zinakua ni za uhakika tofauti na mvua za vuli
Huku mkoa wa Tanga huwa mvua za kupandia zinaanza mwezi wa tatu na huko morogoro ni kweli wanapanda mwezi wa pili

Hatua muhimu kwa kilimo Cha mahindi

Kama unalima Morogoro ambapo wanatarajia kupanda mwezi wa pili jitahidi mpaka mwisho wa mwezi wa kwanza Shamba liwe safi
Kama Muda unao jitahidi uchimbe mashimo Kipindi cha kiangazi ili yakae wazi ili siku mvua ikinyesha uwe na kazi moja tu ya kufukia mbegu

BAADA YA MAHINDI KUOTA

Baada ya mahindi kuota kuna uwezekano wa kupita Kipindi cha jua kali,
Kipindi hiki kinapelekea mahindi kushambuliwa na wadudu aina ya Sondo siwajui kingereza chake hivyo puliza dawa ya kuua Sondo na ikiwezekana changanya dawa ya Sondo na mbolea ya Maji (Busta)

Baada ya wiki mbili au Tatu jitahidi upalilie palizi ya kwanza kwani hii ndio sehemu muhimu sana kwenye kilimo
Jitahidi mvua za masika zikukute ushapalilia
Baada ya hapo piga tena dawa ya Sondo na busta
Baada ya hapo piga palizi ya pili
Baada ya hapo subiri kuvuna

NB
Aina ya Mbegu
Mimi tokea nianze kilimo natumia Mbegu aina ya DK na haijawahi kuniangusha
Ninapanda Mbegu mbili kwa kila shimo kwa umbali wa cm 60 shimo kwa shimo na cm 75 Mstari kwa Mstari
Na kama shamba limepimwa kitaalam na halina mti wowote ndani ni wastani wa kilo 8 yaani mifuko 4 kilo 2 kwa kila ekari

Nafikiri nimekupa mwangaza japo kidogo
Nimekupa Experience from field kwani maisha yangu kwa zaidi ya Asilimia 80 nayaendesha kupitia kilimo
 
SIJAJUA KM KUNA UHITAJI WA MBOLEA MARA3 KWA MOROGORO.MM NALIMIA HANDENI TANGA KILIMO KWANGU SEHEMU YA MAISHA TUNAPATA MVUA MISIMU MIWILI yani mvua ya vuli na masika.masika ndyo mvua ya hakika.hatutumi mbolea na kipato kiko vizuri.mwak hu ndyo natka kujaribu mbolea.nakushauri kabla hujatumia mbolea uliza wenyeji wanatumia mbolea?km jibu ni hpana tumia mbolea ya yaramila mara moja tu.usilime eneo kubwa
 
Mimi ni Mkulima wa Mahindi ingawa niko mkoa wa Tanga ambapo pia wanapata mvua mara mbili yaani mvua za masika na mvua za vuli
Nikuweke sawa kuanzia mwezi wa pili hizo ni mvua za msimu wa masika ambazo mvua hizo zinakua ni za uhakika tofauti na mvua za vuli
Huku mkoa wa Tanga huwa mvua za kupandia zinaanza mwezi wa tatu na huko morogoro ni kweli wanapanda mwezi wa pili

Hatua muhimu kwa kilimo Cha mahindi

Kama unalima Morogoro ambapo wanatarajia kupanda mwezi wa pili jitahidi mpaka mwisho wa mwezi wa kwanza Shamba liwe safi
Kama Muda unao jitahidi uchimbe mashimo Kipindi cha kiangazi ili yakae wazi ili siku mvua ikinyesha uwe na kazi moja tu ya kufukia mbegu

BAADA YA MAHINDI KUOTA

Baada ya mahindi kuota kuna uwezekano wa kupita Kipindi cha jua kali,
Kipindi hiki kinapelekea mahindi kushambuliwa na wadudu aina ya Sondo siwajui kingereza chake hivyo puliza dawa ya kuua Sondo na ikiwezekana changanya dawa ya Sondo na mbolea ya Maji (Busta)

Baada ya wiki mbili au Tatu jitahidi upalilie palizi ya kwanza kwani hii ndio sehemu muhimu sana kwenye kilimo
Jitahidi mvua za masika zikukute ushapalilia
Baada ya hapo piga tena dawa ya Sondo na busta
Baada ya hapo piga palizi ya pili
Baada ya hapo subiri kuvuna

NB
Aina ya Mbegu
Mimi tokea nianze kilimo natumia Mbegu aina ya DK na haijawahi kuniangusha
Ninapanda Mbegu mbili kwa kila shimo kwa umbali wa cm 60 shimo kwa shimo na cm 75 Mstari kwa Mstari
Na kama shamba limepimwa kitaalam na halina mti wowote ndani ni wastani wa kilo 8 yaani mifuko 4 kilo 2 kwa kila ekari

Nafikiri nimekupa mwangaza japo kidogo
Nimekupa Experience from field kwani maisha yangu kwa zaidi ya Asilimia 80 nayaendesha kupitia kilimo
NAMBA YAKO MKUU. NAHITAJI USHAURI JUU YA KILIMO CHA MAHINDI ENEO KABUKU TANGA
 
Mvua za msimu wa pili zinakuwa sio za uhakika sana, na kwa sababu kilimo chetu watu wa hali ya chini kinategemea asilimia mia mvua pekee sikushauri kulima na kuwekeza kiasi kikubwa hasa msimu wa pili,,

Pia fanya utafiti kwa kuwauliza wenyeji wako na watu wengine wa wilaya husika ambayo unataka kufanya kilimo, kuwa mvua za misimu yote zipoje, aina nzuri ya mbegu inayopatikana huko pia wewe mwenyewe kaangalie ubora wa udongo kwa macho( hapa utahitaji mzoefu wa kilimo cha mahindi) na pia kwa vipimo vya wataalamu ikiwezekana.

Angalia upatikanaji wa viutilifu vinginevyo hasa zile pesticides pia waulize wenyeji kama kunakuwaga na magonjwa mbalimbali ya mazao, pia upatikanaji wa mbolea ( ya ruzuku au hata isiyo ya ruzuku, ulizia vizuri maana kuna mbolea nyingine unaweza pigwa), pia aina ya mbegu nunua katika maduka yaliyothibitishwa na yana vibali kabisa.

Yote kwa yote, pia unaweza fanya research ndogo ya maeneo tofauti na morogoro hasa yale yanayozalisha mahindi kwa wingi kama Rukwa, Ruvuma, Mbeya, n.k
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom