Nimepanda kwa kutumia mbolea isiyofaa, hatua gani nichukue?

clinician

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
1,631
3,494
Habari zenu wana jukwaa la kilimo.

Nina shamba ninafanya kilimo cha mahindi. Nimenunua mbolea ya kupandia lakini muuzaji alichanganya akawapa vibarua UREA badala ya mbolea ya kupandia.

Naomba kujua hatua za kuchukua baada mkanganyiko huu kwani vibarua wameshapanda kwa kutumia UREA.
 
Wakati wa kupanda mahindi yanahitaji phosphorus kwaajili ya kustawisha mizizi, sasa kama wamepandia Urea fanya hivi mahindi yakiota;
  • tafuta mbolea/booster isiyo na kirutubisho Cha Nitrogen ambayo tayari inapatkana Kwa wingi kwenye urea,
  • Tumia booster ya amcofert(0-30-40), mpaka mahindi yafike wiki sita(kimo Cha magoti)
 
Hiyo ndo booster yenyewe
112714463.jpg
 
Sidhani kama kuna madhara yoyote yataikuta mimea sema mbolea haitafanya kazi iliokusudiwa na mimea haita kuwa na afya uliokusudia
 
Habari zenu wana jukwaa la kilimo.

Nina shamba ninafanya kilimo cha mahindi. Nimenunua mbolea ya kupandia lakini muuzaji alichanganya akawapa vibarua UREA badala ya mbolea ya kupandia.

Naomba kujua hatua za kuchukua baada mkanganyiko huu kwani vibarua wameshapanda kwa kutumia UREA.
Subiria mahindi yatoke kwanza,muda gani umepita toka mmependa na matokeo yakoje katika utokaji.

Haya ya mbolea utapewa abc kutoka katika majibu ya hapo juu,hongera kwa kupambana na pole kwa challenges
 
Back
Top Bottom