Mbowe: Serikali iwachukulie hatua wote walioliingiza Taifa katika Mkataba wa Bandari

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, amesema Mkataba huo ni Mbovu, haurekebishiki na umelidhalilisha Taifa kwa uamuzi wa Watu wachache ambao wanapaswa kuchukuliwa hatua za Kisheria

Akitaja Maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho amesema Bunge linatakiwa kufuta Azimio lake la kuridhia Mkataba wa Uendeshaji wa Bandari kwasababu hauna Maslahi kwa Nchi

Aidha, Mbowe amesema Kamati Kuu ya CHADEMA inaunga mkono jitihada za Wananchi kupinga Mkataba huo ikiwemo Wanasheria waliofungua Kesi katika Mahakama mbalimbali Nchini.

====

MAAZIMIO YA KAMATI KUU JUU YA MKATABA WA BANDARI.

1) Kamati Kuu inalitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta azimio lake la kuridhia mkataba wa uendeshaji wa Bandari nchini kwa sababu mkataba huo hauna maslahi yoyote kwa nchi yetu.


2) Kamati Kuu inaitaka Serikali kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria wote walioshiriki kuingiza nchi kwenye mkataba huu mbovu ambao haurekebishiki.


3) Kamati Kuu inaunga mkono jitahada mbalimbali zinachochukuliwa na
wananchi mbalimbali nchini kupinga mkataba huo ikiwemo wale waliochukua hatua za kufungua kesi dhidi ya Serikali kwa ajili hiyo katika Mahakaka Kuu ya Tanzania.


4) Kamati Kuu imeazimia pia kwamba itashirikiana na wananchi kupitia makundi mbalimbali bila kujali itikadi zao katika kupinga mkataba huu wa uendeshaji wa Bandari nchini.


5) Kamati Kuu inawahimiza wananchi kwamba Mkataba wa Bandari pamoja na mikataba mingine ya siri ambayo ni mibovu na inayoliingiza taifa
kwenye hasara kubwa ni chachu ya kuona haja ya kuendelea kutaka nchi
yetu kuwa na Katiba Mpya ambayo itaweka utaratibu wa namna ya Bunge na vyombo vingine kupitia mikataba hiyo kwa maslahi ya Taifa.


6) Kamati Kuu imeazimia kwamba ikiwa Bunge na Serikali haitachukua hatua kuhusu malalamiko ya wananchi dhidi ya mkataba wa Bandari; Chama kitaanzishe na kuhamasisha umma kuchukua hatua kali dhidi ya serikali mpaka itakapousitisha mkataba huu .


7) Kamati Kuu imeridhika Mkataba hauna maslahi yoyote kwa nchi yetu na haukubaliki kwa CHADEMA na kwa mtu au taasisi yoyote inayoitakia nchini yetu mema. Kwa maneno ya mtaalamu maarufu wa sheria nchini kwetu, huu ni mkataba wa haki kwa upande mmoja (Dubai), na wajibu kwa upande mwingine (Tanzania);


8) Kamati Kuu imebaini kuwa kwa jinsi mkataba huu ulivyo, na kwa maoni ya CHADEMA na ya wataalamu mbali mbali walio huru, mkataba huu haurekebishiki bila kuubadilisha wote, na bila makubaliano na Dubai. Chama cha Mawakili wa Tanganyika kimeonyesha katika uchambuzi wake kwamba mkataba huu unahitaji marekebisho katika vifingu vyake vyote muhimu.


9) Kamati Kuu imeridhika kuwa Mkataba huu ni kinyume cha Katiba ya nchi; kinyume cha sheria za nchi na kinyume cha sheria za kimataifa. Mkataba umepelekea Serikali hii ya CCM kuwasilisha muswada wa kubadilisha sheria zinazohusu umiliki wa rasilimali asilia za nchi yetu ili kujaribu kuuhalalisha;


10) Kamati Kuu imebaini hakuna utafiti wowote wa kisayansi uliofanywa na
serikali na ukawekwa kwa umma kuthibitisha ufanisi au uduni wa bandari zetu na ubora wa DPW ili kushawishi wananchi juu ya ufanisi
utakaotokana na DPW. Kila jambo lilifanywa kisirisiri, kienyeji na hakuna data zitokanazo na utafiti.


11) Kamati Kuu imejiridhisha kuwa Wananchi hawajui ASILI wala SHABAHA ya mkataba huu wa DPW na wao ndiyo wanaoathirika wakuu kwa
maaamuzi haya ya serikali.


12) Kamati Kuu imetambua hakuna utafiti wowote wa kisayansi kuonyesha njia mbadala za kuboresha ufanisi wa bandari. Utafiti huo ungesaidia wananchi kulinganisha faida na hasara za kila mbadala unaopendekezwa.
Badala yake tumeletewa DPW ikiwa imeshasaini mkataba ili sisi turidhie.


13) Kamati Kuu imebaini hakuna utafiti uliofanywa na serikali kuonyesha "faida" za kifedha wanazozungumza, wala hakuna ushahidi wa utafiti
uliofanyika kuonyesha faida zisizo za kifedha zitokanazo na umiliki na uendeshaji wa bandari. Faida na hasara halisi hazipaswi kuwa za kinadharia bali ndizo zingekuwa sehemu ya vigezo vya kuamua taifa lifuate mbadala upi.


14) Kamati Kuu imebaini huwa hakuna utafiti wowote unaothibitisha kuwa Unyeti wa bandari kwa usalama wa taifa umezingatiwa kabla ya kuingia mkataba huu.

15) Kamati Kuu imejiridhisha kuwa hakuna ushahidi kwamba serikali ilifanya uchambuzi wa kiuchumi, kijamii, kisiasa au kiusalama kabla ya kuamua na kusaini mkataba huu. Kama hayo yangefanyika, na yakawekwa wazi, mjadala juu ya bandari usingekuwa hivi ulivyo.


16) Kamati Kuu imejiridhisha pasipo shaka kuwa Serikali, Bunge na baadaye CCM ilikurupuka na kujaribu kuficha mapungufu ya mkataba kwa
propaganda na taarifa zisizo za kweli. Matokeo yake, sasa inagombana na wananchi, inawagawa wananchi, na inatumia nguvu na ushawishi haramu kuliko ushawishi wenye HOJA, UTAFITI NA USHAWISHI. Badala ya kujibu maswali, serikali inaibua maswali magumu zaidi.


17) Kamati Kuu imebaini mchakato wa kufikia makubaliano na DPW
haukufuata kanuni za kisheria, kisiasa, kisayansi na hata kitaaluma. Na hata mfumo wa serikali kujibu HOJA za wananchi, haufuati kanuni za
kisayansi na kitaaluma. Ndiyo maana unasikia wananchi wengine tayari wameanza kutishwa, makundi yanayotumika kutetea mkataba si makundi yenye dhamana wala utaalamu wa jambo husika.


18) Kamati Kuu imejiridhisha kuwa kwa kuwa hakuna utafiti, ushahidi wala tathmini ya kina iliyofanywa na serikali juu ya jambo hili, na kwa kuwa serikali imekosa majibu yenye ushawishi kwa umma, na kwa kuwa chama tawala na serikali hawasikilizi maoni ya wananchi juu ya raslimali zao hizi, sisi Chadema kama serikali inayosubiri kuingia madarakani, tunatoa msimamo ufuatao:


19) Kwa sababu hizi zote na sababu nyingine nyingi,
msimamo wa CHADEMA ni kwamba mkataba huu ufutwe
wote. Aidha, CHADEMA itatumia njia mbali mbali, ndani na nje ya nchi yetu, kuhakikisha kwamba mkataba huu unafutwa na rasilimali za nchi yetu na maslahi ya taifa letu yanalindwa.

20) Kamati Kuu imekubali kwa kauli moja kuwa mifumo yote
ya Chama nchi nzima iongeze juhudi za kuufahamisha umma
wa Watanzania, ubovu na hatari za Mkataba huu kwa nchi
yetu.


21) Kamati Kuu sasa imeridhia Operation +255 Katiba Mpya
inayoendelea nchi nzima, sasa iongezewe wajibu na kuwa
Operation +255 Katiba Mpya Okoa Bandari zetu.


22) Kamati Kuu na Chama chetu kitaunga mkono uwekezaji wowote Mkubwa unaotokana na utafiti wa kisayansi, usiohatarisha usalama wa nchi yetu ikiwemo Utaifa wetu (sovereignity), wenye uwazi na tija kwa pande zote mbili na utakaolinda Uhuru na Haki zetu kama Taifa.

Pia soma: Freeman Mbowe: Tunazindua "Operation +255 Katiba Mpya Okoa Bandari Zetu" kuwaambia watanzania ubaya wa Mkataba wa DP World
 
Kwamba Serikali ijichukulie Hatua ? As you know kwa hizi nchi hizi so called Taasisi sio Taasisi bali ni watu.....

Kwahio ili haya mambo yasitokee tena kupata kama hili baada ya hili...; inabidi kuwe na uwazi chochote chenye maslahi ya nchi kionekane (usiri waufanye kwenye mambo personal sio ya Taifa)
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, amesema Mkataba huo ni Mbovu, haurekebishiki na umelidhalilisha Taifa kwa uamuzi wa Watu wachache ambao wanapaswa kuchukuliwa hatua za Kisheria

Akitaja Maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho amesema Bunge linatakiwa kufuta Azimio lake la kuridhia Mkataba wa Uendeshaji wa Bandari kwasababu hauna Maslahi kwa Nchi

Aidha, Mbowe amesema Kamati Kuu ya CHADEMA inaunga mkono jitihada za Wananchi kupinga Mkataba huo ikiwemo Wanasheria waliofungua Kesi katika Mahakama mbalimbali Nchini.

Pia soma: Freeman Mbowe: Tunazindua "Oparesheni +255 Katiba Mpya okoa bandari zetu" kuwaambia watanzania ubaya wa Mkataba wa DP World
Ccm janga la kitaifa wanaingiaje mkataba wa kimangungo wa kuuza bandari zetu za Tanganyika kirahic hivyo lazima tuendelee kuzipigania rasilimali zetu na ipo siku wahusika wote watafikishwa mahakamani
 
Huu ujinga hata nami sijauelewa, alitakiwa kusema serikali itupishe, haina dira wala mwelekeo.
Ni alitakiwa aongoze wananchi kuandamana kukataa mkataba.

Bado siamini kama ametoa kauli hiyo!!
 
Back
Top Bottom