Mbowe: Kama serikali inayosubiri kuingia madarakani, msimamo wa CHADEMA ni kwamba Mkataba huo ufutwe wote

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Mbowe akiwa kwenye Mkutano na Waandishi wa habari akisoma maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA asema, "kwakuwa hakuna utafiti, ushahidi, wala tathmini ya kina iliyofanywa juu ya jambo hili na kwakua serikali imekosa majibu yenye ushawishi kwa umma, na kwakuwa chama tawala hawasikilizi maoni ya wananchi juu ya rasimili zao sisi CHADEMA kama serikali inayosubiri kuingia madarakani tunatoa msimamo wa mwisho ufuatao;

"Kwasababu hizi zote na sababu nyingine nyingi msimamo wa CHADEMA ni kuwa Mkataba huu ufutwe wote.

Akiendelea kuwa, "CHADEMA itatumia njia mbalimbali ndani na nje ya nchi yetu kuhakikisha kwamba mkataba huu unafutwa na rasimali za nchi yetu na maslahi ya nchi yetu yanalindwa."

Pia soma: Freeman Mbowe: Tunazindua "Operation +255 Katiba Mpya Okoa Bandari Zetu" kuwaambia watanzania ubaya wa Mkataba wa DP World
 
Njia mbalimbali Kutoka NJE YA NCHI zitakazosaidia KUVUNJA mkataba huu BATILI , ni kama zipi hizo mkt Mbowe?
 
Back
Top Bottom