Dr. Slaa Vs Lowassa Urais 2015

Dr. Slaa Vs Lowassa Urais 2015

Nani unaona anafaa kuwa Rais kati ya Wawili hawa?

  • Edward Lowassa

    Votes: 103 13.0%
  • Dr. Willibrod Slaa

    Votes: 640 80.6%
  • Wote hawafai/sijaamua

    Votes: 51 6.4%

  • Total voters
    794
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Mkuu, HAMY D, hongera sana kwa uchambuzi wako. Naona misukule imeanza kukushambulia kwa vile umenena ya kweli
 
HAMY-D Bora ugeendelea kuongea na uyo ndugu hapo jilani yako kuhusu kauli za mwenyekiti wenu jana uko Mbeya kuliko kuandika kitu kama hii.
Mkuu, hata hili pia ni hoja ya kujadiliwa. Maana misukule wengi wamelaghaika sana
 
Kwani wanapambanisha upana wa historia zao?
Anyway, msimamo ukoje hadi sasa? Hapa JF na huko kwingine...
 
Dr. Wilbrod Slaa ameshagombea uraisi na kiukweli alishinda kabla manyang'au hayajachakachua. Je Lowasa naye aligombea nafasi gani kubwa zaidi ya ubunge? Wabunge wengi wa CHADEMA wapo Bungeni kutokana na juhudi za Slaa. Je wangapi wapo Bungeni kwa juhudi za Lowasa? Yuko wapi Sioi Sumary? Yuko wapi Batilda Buriani?
 
Jk jana alisema alikuwa wapi siku za nyuma kujipitisha pitisha kutoa michango(Rushwa)iweje karibu na Uchaguzi ndio anatoa takrima,Naichia kamati ya Maadili iwajadili by Baba Riz1
 
Dr slaa ndigo raisi, raisi wa kutogomboa na umaskini katu hawezi toka ccm tena chama chenye makundi, akiingia ndi yale yale kulindana, kuiba pesa ili kulipa fadhila wa wahisan wake wanaomchangia, umasikini utaendelea,ufisadi utaendelea kama kawaida sababu yeye ndiyo muasisi wao.
 
Dr Slaa ametumia asilimia 65 - 70 ya maisha yake yote kama padre

Kweli shule za kata janga. Ina maana Dr amekuwa nje ya Upadre kwa 30% ya maisha yake. Kama Dr akipata Upadre akiwa na miaka 28, na tangu ameacha upadre ni miaka 18, Jumla ni miaka 46.
Kama miaka 46 ni 30% ya maisha ya Slaa, ina maana Slaa ana miaka 153...

Eti nyie ndo mmepewa Unaibu wizara ya Fedha!!!
 
WanaJF,

Kwa ufahamu wangu wa mambo ni kwamba siku zote ukitaka kulinganisha vitu, huwenda kwa kufananisha au kuvipambanisha, ni lazima angalau viwe ama wawe (kama ni watu), vyenye kukalibiana.

Nimeona uzi hapa JF na baadhi ya vyanzo vingine vya mawasiliano vikiweka mashindano ya aina hii, yani kati ya Lowassa na watu aina ya Dr Slaa. Haya ni matusi wanaJF.

Hapa Tanzania, Lowassa ana historia pana na ndefu sana katika siasa zetu, hili halihitaji mjadala. Lowassa amekuwapo enzi na enzi, Lowassa anayajua mawimbi ya kila aina ya mikiki mikiki ya siasa, Lowassa anajua kupwa na kujaa kwa siasa, Lowassa anaijua saikolojia ya Watanzania vizuri. Kweli mtu wa aina hii una mlinganisha na Dr Slaa?!!!

Dr Slaa ametumia asilimia 65 - 70 ya maisha yake yote kama padre (ingawa palimshinda), mbali na hilo, ametumia asilimia 40 - 50 ya maisha yake nje ya mipaka ya Tanzania, Dr Slaa hatujui Watanzania. Iweje leo mtu wa aina hii awe na uhalali wa kupambanishwa na gwiji?

Namaliza kwa kusema kwamba, kama kuna matusi ya kumtukana Lowassa yapo basi yatumike hayo mengine, ila naombeni msimtukane Lowassa kwa kumpambanisha na Dr Slaa. Chonde chonde wana JF.

Ana historia ndefu ya kushindwa kujibu swali la Mwalimu Nyerere tangu mwaka 1995 hadi leo kwamba "Utajiri wake aliupata wapi'!? Wakati alikua mtumishi wa umma siku zote.Hadi leo kashindwa kujibu swali linalohusu maisha yake mwenyewe,atajibu maswali gani yanayohusu watanazania zaidi ya milioni 45?

Saikolojia yake imemshinda ataweza Saijolojia ya watu Milioni 45? Labda kama anaongozwa na falsafa ya waganga wa kienyeji ya kutoa utajiri kwa watu huku yeye mwenyewe hajitambui
 
nenda pale juu kabisa pameandikwa TOUCH bofya hapo, kisha shuka chini kabisa pameandikwa FULL SITE, pabofye hapo na utakuwa tayari kupiga kura yako kwa kwenda kwenye poll moja kwa moja.

Asante mkuu, nshampigia Dr wa ukweli awe rais wangu.
 
Hao wote ni wadini/wakatoriki hawapaswi kuongoza hii ni wabaguzi mno.
 
Jk jana alisema alikuwa wapi siku za nyuma kujipitisha pitisha kutoa michango(Rushwa)iweje karibu na Uchaguzi ndio anatoa takrima,Naichia kamati ya Maadili iwajadili by Baba Riz1

Eti JK naye analalamika!
 
huyu aliyeanzisha thread hii atakuwa na mtindio mkubwa sana wa ubongo. namshauri atembelee uzi unaoratibu kura ya maoni kati ya Lowassa na Dr. Slaa. majibu yako wazi kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom