John F. Kennedy, CIA na Lee Oswald: Ujuaji Vs Dola, Kitendawili cha dunia ambacho hakijateguliwa mpaka sasa

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
843
JONH F. KENNEDY, CIA NA LEE OSWALD: UJUAJI Vs DOLA, KITENDAWILI CHA DUNIA AMBACHO AKIJATEGULIWA MPAKA SASA.

Na Comred Mbwana Allyamtu
Thursday-28/05/2020
Marangu, Kilimanjaro- Tanzania.

John Fitzgerald "Jack" Kennedy ndiye rais wa kwanza wa marekani kuzaliwa karne ya 20, na ndiye rais pekee wa Marekani kuwa muumini wa dhehebu la katoliki, raisi Jonh Fitzgerald "Jack" Kennedy aliuwawa tarehe 22,11, 1963 huko Jimbo la Texas katika mji wa Dallas kwa kupigwa risasi na mtu aliyekuja kutambulika kwa jina la Lee Harvey Oswald, japo hakuna ushahidi wowote ulioonesha Oswald kuhusika, ntalieleza hili mbeleni.

Kennedy ndie rais wa pili Marekani kuchaguliwa akiwa na umri mdogo katika orodha ya marais walio wahi kuhudumu kwenye nafasi hiyo, Jonh Fitzgerald Kennedy alichaguliwa kuwa rais akiwa na umri wa miaka 43 na siku 236. Rais alieingia madarakani akiwa na umri mdogo zaidi ni rais wa 26 aliyeitwa Theodore Roosevelt ambae alikuwa raisi baada ya kuuwawa mtagulizi wake William McKinley.

Theodore Roosevelt alikalia kiti cha uraisi akiwa na umri wa miaka 42 na siku 322. Theodore Roosevelt ndie rais mdogo kukalia kiti cha uraisi huku Jonh Fitzgerald Kennedy ndie rais mdogo zaidi kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani....(The youngest person to assume the office was THEODORE ROOSEVELT, who became president following William McKinley's assassination, at the age of 42 years, 322 days. The youngest person elected president was JOHN F. KENNEDY, who was inaugurated into office at the age of 43 years, 236 days.)

John Fitzgerald Kennedy alizaliwa tarehe 29 Mei 1917 huko Brookline, Massachusetts, Marekani, kwenye familia ya kitajiri, ambapo baba yake mzazi aliitwa Joseph P. Kennedy ambae aliwahi kuwa Meya wa Boston na Mama yake Rose Fitzgerald Kennedy, JF. Kennedy mwenyewe alikuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 1961 hadi alipouawa tarehe 22,11, 1963 huko jijini Dallas Jimbo la Texas Marekani, John F. Kennedy alikuwa ni raisi wa 35 wa Marekani huku Makamu wake wa Rais alikuwa akiitwa Lyndon B. Johnson (ndie alie mrithi urais baada ya kifo chake, tutaona huko baadae) Jonh F. Kennedy aliapishwa kuwa raisi wa Marekani rasmi tarehe 20 januari 1961 kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Dwight D. Eisenhower ambae alikuwa ni raisi wa 34 wa Marekani.

Baada ya kifo chake mnamo tarehe 22 Novemba 1963 kwa kupigwa risasi, Kennedy alikuwa na umri wa miaka 46 na mwili wake ulizikiwa kwenye makaburi ya Arlington National Cemetery, huko Washington DC, John Fitzgerald Kennedy alifunga ndoa na mwanamke mrembo alieitwa Jacqueline Bouvier mwaka 1953 na kubahatika kupata watoto wanne ambao ni Arabella Kennedy, Caroline Kennedy, John F. Kennedy Jr. na Patrick Bouvier Kennedy.

J F. Kennedy alijiunga na Chuo Kikuu cha Harvard na kumaliza masomo mwaka 1940 akichukua Shahada ya mahusiano ya Kimataifa, pia aliwahi jiunga na Chuo Kikuu cha Stanford Lakini aliachia njiani na kujiunga na Jeshi la Marekani mwaka 1941. Jeshini alitumikia ngazi mbalimbali na mpaka anaondoka Jeshini alikuwa na cheo cha Luteni (Lieutenant) na pia alipokea tuzo nyingi hasa mara baada ya vita kuu ya pili ya dunia na hapo ndipo hapo alianza safari yake ya kisiasa.

Mnamo 03 Januari 1947 hadi 03 Januari 1953 alikuwa Mbunge/Mwakilishi wa Wilaya 11 zinazounda Jimbo la Massachusetts na kati ya 03 Januari 1953 hadi 22 Disemba 1960 alikuwa Seneta wa Jimbo la Massachusetts, mnamo 02 Januari 1960 JFK alitangaza rasmi nia yake kugombea Urais kupitia chama chake cha Democratics, pia katika mbio hizo, Lyord Johnson (ambaye alikuja kuwa Makamu wa Rais wake) alitangaza nia ya kugombea Urais.

JF.Kennedy alipingwa na baadhi ya wakongwe wa Chama chake wakidai kuwa hakuwa na uzoefu pia umri wake ulikuwa mdogo, mmoja wa waliompinga ni aliyekuwa rais Mstaafu kwa wakati huo Harry Truman (Rais wa 33 wa Marekani) na wengine wenye nguvu, baadhi yao walimpinga kwa kuwa sera zake zilipingana na Wamarekani wengi walimhusisha kuchanganya masuala ya dini/Kanisa lake la Katoliki na ya nchi na yeye alipinga vikali kwa kusema yeye hasimami kama mgombea urais wa Katoliki bali anasimama kama mgombea Urais wa Democratic na kamwe asingechanganya Kanisa na masuala ya Umma.

J F. Kennedy aliahidi kuleta haki sawa baina ya weupe na weusi (Hiki ndiyo kipindi watu weusi walipamba moto kudai haki zao) pia katika kuleta mahusiano mazuri na Umoja wa nchi za Kisovieti (USSR) pamoja na vita ya Vietnam, licha ya kuwekea vikwazo vingi, J F..Kennedy alimshinda mpinzani wake Richard Nixon wa Republican, huku yeye Kennedy akipata kura 49.7% na Richard Nixon alipata kura 49.5%, na kupata kura za wachaguzi wa majimbo (Electral College) 303 na huku mpinzani wake Richard Nixon akipata 219, matokeo hayo yalimuibua J F Kennedy kuwa mshindi kwenye uchaguzi huo.

JF. Kennedy Baada ya kuwa raisi wa Marekani hakuudumu kwa muda mrefu kwani aliuawa mapema tu mwaka 1963, utawala wake Kennedy ulihudumu kwa siku 1,306 tu , kati ya 20 Januari 1961 hadi 22 Novemba 1963 siku ambayo ni siku ya kifo chake alipokuwa Dallas huko Texas. Ukweli kuhusu kifo cha kennedy bado ulikuwa kitendawili juu ya nini haswa waliohusika katika kupanga na kutimiza lengo hilo, Oswald aliuawa siku chache tu baada ya kifo cha kennedy pia kulizima kabisa kupata ukweli juu ya waliohusika na kupanga mauaji hayo.

Miongoni mwa vitu vilivyoshangaza walimwengu ni kuwa kabla ya kutekelezwa kwa mauaji hayo Oswald alipiga simu kitengo cha upelelezi FBI na kuwaatarifu kuw yeye ni mmoja wa waliopanga kumuua rais Kennedy hata hivyo FBI hawakutilia mkazo taarifa hizo mpaka pale lilipotekelezwa shambulizi hilo baya kuwahi kutokea nchini Marekani karne ya 20, baadhi ya watu wanasema kuwa viongozi wa Cuba,Urusi na Vietnam ndio waliopanga mauaji hayo licha warusi walishakiri wao wenyewe kuwa walistushwa sana na kifo cha kiongozi huyo.

Makundi na magenge ya wahalifu wa Kimafia ni miongoni mwa watu walihusihswa na kifo cha rais JF kennedy, pia uhasama baina ya marekani na mataifa ya Cuba,Korea kaskazini, Urusi na Vietnam ulihusishwa kwa kiasi kikubwa kuwa ndio walipanga na kutekeleza mauaji hayo kwa JF Kennedy, taarifa za kichunguzi zaidi ya 3,100 juu ya mauaji ya JF Kennedy zimetolewa hadharani kwa wananchi tangu 2017 ili angalau kuwafungua akili zao juu ya kifo cha rais wao mpendwa, taarifa hizi zilifanywa kuwa siri kubwa za kitaifa kwa mda wote huo wa miiaka 56 mpaka sasa.

Sasa turudi kwenye tukio lenyewe lenye utata juu ya kifo cha JF. Kennedy...

Mwenzi June mwaka 1963 saa 9:45 asubuhi kulimalizika kikao maalum katika ikulu ya White house kikao hiki kiliwakutanisha raisi Kennedy, makamu wa Rais Lyndon B. Johnson na Gavana Connally kujadili mgogoro uliokuwepo baina ya Raph Yarborough na Don Yarborough dhidi ya Gavana wa jimbo la Texas wa Republican Bw. John Connall, hivyo Connall alialikwa ikulu kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wao, makubaliano yalifikiwa kuwa raisi Kennedy angepaswa kwenda Texas mwezi november kuwasuluhisha.

Mwenzi November mjini Dallas City...

Siku hii Rais Kennedy alikuwa amefika jimboni Texas hapa kwa ajili ya ziara fupi maalumu na mahsusi ili kwenda kusuluhisha mvutano uliokuwepo kati ya wanachama wa Democrat Bw. Raph Yarborough na Don Yarborough dhidi ya Gavana wa Republican Bw. John Connally (nitaeleza huu mgogoro ulihusu nini), Safari hii ya Rais Kennedy kutembelea jimbo la Texas ilikuwa imepangwa na kukubaliana tangu mwezi June ambapo Kennedy, makamu wa Rais Lyndon B. Johnson na Gavana Connally walipokutana kwenye kikao mwezi June mwaka huo 1963 kule Washington DC katika ikulu ya White house.

Safari hii ya Kennedy jimboni Texas ilikuwa na malengo makuu matatu.

Mosi, alikuwa anataka kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kuongeza michango katika mfuko wa kampeni.

Pili, alikuwa anaweka mkakati kwa ajili ya uchaguzi uliokuwa unafuata mwaka mmoja baadae, yaani mwezi Novemba mwaka 1964.

Na tatu, Kennedy alikuwa anataka kujiimarisha zaidi katika jimbo la Texas kwa kuwa alipata ushindi mwembamba sana jimboni hapo na alikuwa na ushawishi Mdogo sana kwenye hili jimbo na hata kwenye eneo la Dallas alikuwa amegalagazwa kipindi cha uchaguzi.

Kwa hiyo licha ya nia yake ya kwenda kusuluhisha mgogoro ndani ya chama cha Democrat lakini pia alikuwa na malengo makuu hayo matatu.

Safari ya Kennedy kutembelea Texas ilitangazwa rasmi kwa umma mwezi September mwaka 1963, Mpangilio wa ruti ambayo msafara wake utapita ulikamilika kupangiliwa tarehe 18 Novemba na kutangazwa asububi ya Novemba 22 ili wananchi wajitokeze barabarani kumlaki, Taarifa ya Ikulu ambayo iliwasilishwa kwa Secret Services ilionyesha kwamba ndege ya Rais itaruka kutoka uwanja wa ndege wa kijeshi wa Carswell Airforce Base maeneo ya Fort Worth na kwenda kutua uwanja wa Dallas Love Field.

Baada ya hapo Rais Kennedy alikuwa anatakiwa kusafiri kwa msafara wa gari kutoka uwanja wa Dallas Love Field na kuelekea eneo la Dallas Trade Mart ambako Kennedy alitarajiwa kupata chakula cha mchana na wenyeji wake, Ruti hii ilipangwa na kupendekezwa na rafiki mkubwa wa Kennedy aliyeitwa Kenneth O'Donnell ambaye alikuwa pia ndiye katibu wake aliyehusika na masuala ya teuzi za watumishi wa ngazi za juu serikalini.

Ruti hii iliyokuwa inapendekezwa (kutoka uwanja wa ndege wa Dallas Love Field mpaka Dallas Trade Mart) ambayo ilikuwa na urefu wa kilomita 16 ilikuwa inategemewa kuchukua takribani dakika 45 kwa mwendo wa taratibu ili kumpa nafasi Kennedy kuwasabahi wananchi kwa kuwapungia mkono, Ratiba hii pamoja na ruti inayopendekezwa iliwasilishwa ofisi ya Secret Services ambapo maafisa walioehusika nayo kuipokea na kuiwekea mkakati wa kiusalama walikuwa ni Special Agent Winston G. Lawson ambaye alikuwa ni 'advance Secret Services agent' (afisa ambaye yuko kwenye Whitehouse Detail kwa ajili ya kumlinda Rais moja kwa moja) Pia alikuwa pamoja Agent Forrest V. Sorrels ambaye huyu ni Special Agent ambaye anahusika na ofisi ya Secret Services eneo la Dallas, Maafisa usalama hawa wawili walikutana mara kadhaa kuweka mkakati wa kiulinzi kwa ajili ya safari hii ya Rais ya Novemba 22.

Moja ya vikao vyao hivyo walikifanya tarehe 14 Novemba kwenye uwanja wa ndege wa Dallas Love Field ambapo baada ya kikao waliendesha gari pamoja kupita njia ile ambayo imependekezwa msafara wa Rais uje kupita wiki moja baadae, Siku hii ya tarehe 14, maafisa hawa walipokuwa wanaendesha gari kupita kwenye hii ruti inayopendekezwa kuna jambo waliliona, jambo ambalo liliwashitua kidogo na kuwafanya waingie wasiwasi juu ya hii ruti inayopendekezwa.

Endapo jambo hili lingezingatiwa, basi Kennedy asingeuwawa wiki moja baadae!

Swali kwanini waliingiwa na wasiwasi baada ya kuona hicho walichokiona lakini bado msafara wa Kennedy ukapita ruti hii hii wiki moja baadae??... Au swali la msingi zaidi waliona kitu gani?... (Tutaona kitu hicho ambacho maafisa usalama hao walicho kutilia shaka huko mbeleni...

ALHAMISI YA NOVEMBA 21...

Rais John Kennedy na mkewe Jackie Kennedy wanawasili na Airforce One jimboni Texas katika uwanja wa ndege wa Carswell, katika viunga vya Fort Worth, Rais na mkewe walikuwa wanatokea Santo Antonio, Huston ambako mchana Kennedy alihutubia katika chuo cha matabibu ya Jeshi la Anga kwenye kituo cha Brooks Airforce Base na Jioni yake alitoa hotuba katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika Rice Hotel ambapo kulikuwa na kumbukumbu ya kifo cha Mbunge mashuhuri wa bunge la Congress aliyeitwa Albert Thomas.

Siku hii ya alhamisi Rais Kennedy na mkewe waliwasili Texas majira ya saa 5 na dakika 7 usiku na kupokelewa uwanja wa ndege na Raymond Buck rais wa Fort Worth Chamber of Commerce, Pia katika ndege nyingine iliyombeba makamu wa Rais Lyndon B. Johnson walikuwa amefuatana na Gavana wa Jimbo la Texas, John Connally pamoja na hasimu wake mkubwa Seneta Ralph Yarborough.

Msafara wa Rais uliondoka uwanja wa ndege kupitia West Freeway ambapo licha ya kuwa ni muda wa usiku sana na mvua ilikuwa inanyesha, wananchi wengi walijitokeza na kujipanga barabarani kumpingia mikono, Walifika Hotel Texas majira ya saa 5 na dakika 34 usiku, ambako katika hoteli hii ndipo ambapo Rais Kennedy na mkewe walilala kwa usiku huo.

IJUMAA, NOVEMBA 22...

Siku hii ya Ijumaa ilianza mapema sana kwa Rais Kennedy kwa shughuli muhimu asubuhi na mapema, Saa 2 na dakika 45 asubuhi, Rais Kennedy akiwa amefuatana na Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson, pamoja na Mbunge wa Congress Jim Wright pamoja na Seneta Yarborough alikuwa anaongea na wananchi eneo la Eighth Street na katika hotuba yake hiyo aliimwagia sifa sekta ya usafirishaji wa anga ya jimbo la Texas.

Baadae majira ya saa 3 na dakika 10 Rais Kennedy alikuwa amesharejea hotelini kwake na alikuwa anatoa hotuba kwa wageni maalumu waalikwa katika ukumbi wa Hoteli, Mkewe Jackie alichelewa na kuwasili dakika 15 baadae akipokelewa kwa makofi ya kishindo kutoka kwa wageni waalikwa, Baada ya Rais Kennedy kumaliza hotuba yake fupi, swahiba wake mkubwa Kenny O'Donnell ambaye pia alikuwa ni katibu wa teuzi za Rais, alimfuata Roy Kellerman Afisa kiongozi wa Secret Services juu ya Safari ya Rais (Secret Service In charge).

Maagizo haya ambayo O'Donnell alimpa Agen Kellerman, ni kwamba alikuwa anamtaka awasiliane na Maafisa wenzake walioko Dallas ambako Kennedy alikuwa anaelekea na kuwataarifu kuwa kama hakukuwa na mvua basi anataka gari itakayombeba Rais iondolewe paa juu (liwe wazi) ili kumpa rais fursa ya kuonekana vyema na wananchi na kupungiana mikono, Msafara wa Rais Kennedy uliondoka Hotel Texas majira ya kama saa 5 na dakika 10 asubuhi na majira ya saa 5 na dakika 23 Airforce One iliruka kutoka uwanja wa ndege wa Carswell kwenye viunga vya Fort Worth na kuelekea Dallas.

Airforce One ilitua Dallas kwenye uwanja wa Love Field majira ya saa 5 na dakika 38, Makamu wa Rais Johnson na Gavana Connally wao walikuwa wamewasili kabla ya Rais Kennedy, kwahiyo Airforce One ilipotua na kumshusha Rais na mkewe walilakiwa na Makamu wa Rais na Gavana wa Texas, Msafara wa Rais Kennedy, Mkewe Jackie Kennedy, Makamu wa Rais, Gavana Connally na Seneta Yarborough uliondoka uwanja wa ndege wa Love Field majira ya saa 5 na dakika 55 asubuhi.

Msafara ulikiwa unatarajiwa kupitia katikati ya mji wa Dallas na kuwasili Dallas Business and Trade Mart majira ya saa 6 na dakika 15 mchana, Msafara ulishika njia kuingia kati kati ya mji majira ya saa 5 na dakika 59…. Pasipo kujua, zilikuwa zimebaki dakika 31 tu za maisha ya Rais JF Kennedy.

DOWNTOWN DALLAS...

Msafara wa Rais ulipokamata barabara kuingia katikati ya mji wa Dallas kuelekea Trade Mart ulikuwa kwenye mpangilio ufuatao;

- Gari ya Mbele

Gari ya mbele kabisa iliyokuwa inaongoza msafara ilikuwa ni gari aina ya Frord Mercury sedan, aliyekuwa anaendesha gari hii alikuwa ni mkuu wa Idara ya polisi katika mji wa Dallas ambaye aliitwa, Jesse Curry, Katika siti ya mbele ya mkono wa kulia alikuwa ameketi Afisa wa Secret Services, Special Agent Winston, Siti ya nyuma ya gari hii mkono wa kushoto alikuwa ameketi Bill Decker, Sheriff wa mji wa Dallas na siti ya mkono wake wa kulia alikuwa ameketi afisa mwingine wa Secret Services, SAIC Forrest Sorrels (SAIC - Special Agent In Charge).

- Gari ya Rais

Gari hii ambayo Rais Kennedy alipanda ilikuwa ni aina ya Lincoln Continental Convertible ya mwaka 1961, ambayo imeboreshwa ili kukidhi masuala ya kiusalama ilikuwa inaendeshwa na afisa wa Secret Services, Agent William Greer. Pembeni yake katika siti ya mbele alikuwa ameketi afisa mwingine wa Secret Services, ASAIC Roy Kellerman (ASAIC - Assistant Special Agent In Charge), huyu ndiyo yule afisa ambaye alipewa maagizo na O'Donnel swahiba wa Kennedy na katibu wake anayeshughulika na masuala ya Teuzi, kuwa kama hakutakuwa na mvua mjini Dallas basi ahakikishe kuwa gari atakayopanda Rais inakuwa wazi bila paa la juu ili kuwarahisishia wananchi kumuona Rais kwa uzuri na kupungiana mikono, Siti ya nyuma (kati za kati kati) mkono wa kulia alikuwa amekaa Gavana Connally huku mkono wake wa kushoto akiwa amekaa mkewe Nellie Connally, Siti za nyuma kabisa za gari hii ya wazi, mkono wa kulia alikuwa ameketi Rais Kennedy huku mkono wake wa kushoto akiwa ameketi mkewe Jacqueline Kennedy.

Pembezoni/ubavuni mwa gari ambalo alikuwa amepanda Rais Kennedy, kulikuwa na pikipiki mbili za Polisi kila upande, ambapo mkono wa kushoto kulikuwa na piki piki zilizoendeshwa na Polisi wa kituo cha mji wa Dallas, ofisa Billy Joe Martin na ofisa Bobby Hargis, Upande wa kulia kulikuwa na pikipiki zilizoendeshwa na ofisa James M. Cheney na ofisa Douglas L. Jackson.

- Gari ya nyuma ya Rais (follow up car)

Nyuma ya gari aliyopanda Rais Kennedy kulikuwa na gari aina ya Cadillac Touring Convertible ambayo iliwabeba maafisa wa Secret Services kwa ajili ya ulinzi wa Rais na First Lady, Dereva wa gari hili alikuwa ni Agen Sana Kinney. Pembeni yake siti ya mbele kulia aliketi ATSAIC Emory Roberts (Assistant To Special Agent In Charge), Katika mlango wa mbele mkono wa kushoto, kwenye mlango alikuwa ananing'inia Special Agent Clint Hill, ambaye anahusika na ulinzi wa First Lady, Kwenye mlango mwingine wa mbele kulia alikuwa ananing'inia Special Agent Jack Ready, Mlango wa nyuma kulia alikuwa ananing'inia Special Agent Paul Landis huku mlango wa mkono wa kushoto alikuwa ananing'inia Special Agent William T. McIntyre.

Ndani ya gari siti ya nyuma walikuwa wameketi watu wanne. Kulikuwa na Kenneth O'Donnell msaidi wa rais na katibu wake wa masuala ya teuzi, pia kulikuwa na David Powers ambaye naye ni msaidizi wa Rais na pambeni yao hawa mkono wa kulia aliketi Special Agent Glen Bennet na mkono wa kushoto aliketi Agent George Hickey.

- Gari ya makamu wa Rais

Nyuma ya gari iliyowabeba maafisa usalama wa ulinzi wa Rais ilifuata gari iliyombeba makamu wa Rais Lyndon B. Johnson, Gari hii aina ya Lincoln Convertible ilikuwa inaendeshwa na Hurchel Jacks, afisa wa Polisi wa kituo kikuu cha Dallas. Pembeni yake mkono wa kulia alikuwa ameketi ASAIC Rufus Youngblood (Assistant Special Agent In Charge), Siti ya nyuma walikuwa wamekaa Seneta Ralph Yarborough (kushoto), Lady Bird Johnson (kati kati) na kulia alikuwa ameketi Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson.

Gari iliyombeba makamu wa Rais kulikuwa na gari ya maafisa wa Secret Service maalumu kwa ajili ya ulinzi wa Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson (VP followup car), Nyuma ya VP followup Car kulikuwa na gari ya Mayor wa Dallas, iliyombeba Mayor Earle Cabell na mkewe Elizabeth Cabell.

Nyuma yao kulikuwa na gari iliyowabeba waandishi wa habari kutoka vituo vikuvwa vya kitaifa (National Press Pool), Nyuma ya gari hii zilifuata gari nyingine tatu za watu wa Picha (Camera Cars), ambazo zilibeba wapiga Picha za video, picha za mnato na waandishi wa habari wenyeji wanaofanyia kazi vyombo vya habari jimboni Texas, Nyuma ya gari hii tatu kulikuwa na gari nyingine tatu zilizowabeba wabunge wote wa Congress kutoka jimbo la Texas, Na mwishoni kabisa mwa msafari kulikuwa na magari makubwa mawili (Buses) ambazo zilibeba watumishi wengine wa Rais wa ngazi za chini, Mfano waandishi wa habari wa Ikulu, makatibu wa Idara za Ikulu, Daktari wa Rais na kadhalika.

Kisha nyuma ya mabasi haya mawili msafara ulimaliziwa na gari ya Polisi iliyofuatia nyuma, Hii ndio picha kamili ya msafara wa Rais Kennedy ulipotoka uwanja wa ndege wa Love Field kuelekea Trade Mart kati kati ya mji wa Dallas, Kama nilivyosema awali kwamba, umbali kati ya uwanja wa ndege wa Love Field na alikokuwa anaelekea Kennedy (Trade Mart) ni kilomita 16 tu, lakini zilipangwa msafara usafiri kwa mwendo wa taratibu na kutumia dakika 45 ili kumpa Rais muda wa kutosha kusalimiana na wananchi njiani.

Wananchi walikuwa wamejitokeza wengi haswa na kujipanga barabarani kumlaki Rais, Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu laki moja na nusu mpaka laki mbili walikuwa wamejitokeza, Msafara ulizidi kuchelewa zaidi baada ya Rais Kennedy kuamuru msafara kusimama mara mbili barabarani nje ya ratiba iligopangwa ili aweze kuwapa mikono wananchi, Mara ya kwanza aliamuru msafara usimame ili kuwapa mikono watawa wa kikatoliki waliokuwa wanampungia mikono barabarani. Mara ya pili walikuwa ni wanafunzi wa shule ambao nao walikuwa wamejipanga barabarani kumshangilia.

Majira ya saa 6 na dakika 29 msafara wa Rais uliingia katika eneo kubwa (mtaa) ujulikanao kama Dealey Plaza ambao zamani ulikuwa na bustani na maeneo ya watu kupumzika, mbele ya macho lilikuwa linaonekana "jengo lililobeba kifo" cha Rais Kennedy, Jengo la Texas School Books Depository, Wakiwa bado eneo hili hili la Dealey Plaza, msafara wa Rais ukakata tena kona ndogo kutoka mtaa mdogo wa Houston Street na kuingia mtaa wa Elm Street, Bado jengo la Texas School Book Depository, "jengo lililobeba kifo" cha Kennedy lilikuwa katika upeo wa macho yao japokuwa walikuwa wanaelekea kulipita.

Kennedy na Mkewe Jackie walikuwa wanapungia mikono mamia ya wananchi waliojipnga barabarani kumshangilia, Kwa kuzingatia kuwa Kennedy alipata kura kiduchu eneo hili la Dallas wakati wa uchaguzi mkuu, hivyo mkewe Jackie akamgeukia na kumtania,"…kwa hizi shamra shamra, huwezi kusema eti wananchi wa Dallas wanakuchukia…" Jackie akaongea huku anatabasamu kumuangalia mumewe, "…hakika! Siwezi kusema wananichukia.!!" Kennedy akamjibu kwa kifupi mkewe huku anatabasamu na kuwapungia mikono wananchi.

Na hii ndio ilikuwa kauli ya mwisho ya Rais JF Kennedy… tayari ilikuwa ni saa 6 na 30. Na mbele yake alikuwa amebakiza chini ya sekunde 15 za uhai wake.

Mlio wa kwanza wa risasi wengine wanadai kwamba hawakuusikia, na hata baadhi ya maafisa wa Secret Services baadhi yao nao wanadai kwamba hawakuusikia. Na hata wale waliosikia walidai kwamba walidhani labda ilikuwa ni pancha ya tairi la gari au kitu kingine, hii ndio sababu ukiangalia katika kipande cha video ya tukio lile baada ya kupigwa kwa risasi ya kwanza hakukuwa na taharuki yoyote kutoka kwa wanausalama wa kumlinda rais na msafara uliendelea kama kawaida.

Risasi hii ilipigwa katika muda ambao Rais Kennedy, mkewe Jackie na Gavana Connally wote walikuwa wameguukia mkono wa kushoto kupungia wananchi na ghafla wote wakageuka mkono wa kulia kupungia wananchi walio upande huo, Ni muhimu kukumbuka kwamba katika muda huu walikuwa wekwisha lipita Jengo la Texas School Book depository, na wamelipa mgongo kwa kuliacha umbali wa takribani mita 81.

Risasi ya pili kupigwa (risasi ya kwanza nitaiongelea baadae) ilifyatuliwa sekunde ambayo Kennedy ameinua mkono mmoja juu aliwapungia wananchi, risasi hii ilimpenya nyuma yake katikati kabisa ya shingo na nyama ya juu ya bega na kusababisha uharibu Mdogo kwenye uti wa mgongo, na kisha kupenya ndani na kuharibu sehemu ya juu kabisa ya pafu la kulia na kutokea kooni ikiharibu sehemu kubwa ya koromeo, baada ya kupigwa na risasi hii, katika kipande cha video unaweza kumuona Rais Kennedy akiwa amekunja ngumi na kuelekeza mkono mbele ya uso wake usawa wa mdomo kama vile anakohoa na kuinama kwa mbele kidogo akiengemea upande wa kushoto aliko mkewe, Pia unaweza kumuona mkewe akiwa anamkumbatia kwa kuzungusha mkono wake mabegani kwa Kennedy kumuuliza kama yuko 'OK'! (Mpaka muda huu hakujua kama mumewe amepigwa risasi).

Risasi hii hii ya pili iliyompiga Kennedy, ilipotoka kooni kwa Kennedy ilienda moja kwa moja ya kumpiga Gavana Connally!, Risasi hii ilimpiga Gavana Connally mgongoni chini kidogo ya kwapa upande wa kulia na kutengeneza tundu la umbo la duara na kuharibu kiasi cha inch 4 cha mbavu yake ya tano upande wa kulia na kisha kutokea kifuani katika chuchu, Risasi hii hii baada ya kutoka kifuani kwa Gavana Connally kupitia kwenye chuchu ilitua kwenye mkono wa kulia wa Gavana Connally, juu kidogo ya kiganja na kuvunja vunja sehemu hiyo katika vipande vinane, Risasi hii hii, hatimaye ikatua kwenye paja la kushoto la Gavana Connally.

(Nitaeleza huko mbeleni kuhusu utata wa risasi hii ya pili iliyompata Kennedy na Gavana Connally kwa pamoja na ile Risasi ya kwanza ambayo haikuleta madhara yoyote), Risasi ya pili kumpata rais (ambayo ilikuwa ni risasi ya tatu kupigwa) ilimpata kichwani upande wa juu kulia, Risasi hii ilifumua kabisa eneo hilo la kichwa na kusababisha sehemu ya ubongo wa mbele kumwagika.

Damu nyingine ikaruka nyuma ya gari kwenye 'trunk' na nyingine kutua mpaka kwenye mkono wa kushoto wa afisa wa Secret Services aliyekuwa anaendesha gari ya wanausalama waliokuwa gari ya nyuma ya Rais, Ndani ya sekunde mbili baada ya mumewe kufumuliwa na risasi kichwani, First Lady Jacqueline Kennedy akaruka kutoka kwenye siti yake na kuanza kuparamia nyuma ya gari kwenye trunk, Tofauti na wengi wanavyodhani kwamba alikuwa anajaribu kukimbia kuokoa maisha yake, ila ukweli ni kwamba alikuwa anaokota kipande cha mfupa wa fuvu la kichwa kilichodondoka kwenye nyuma ya gari kwenye trunk baada ya mumewe kufumuliwa kichwa na risasi. Baada ya kukichukua haraka haraka akarejea kwenye siti yake.

Sekunde hii hii ambayo First Lady alikuwa anaparamia gari kwenye trunk, katika gari ya nyuma (follow up car), Special Agent Clint Hill ambaye alikuwa ananing'inia kwenye mlango wa mbele kushoto akaruka na kuanza kuikimbilia gari iliyombeba rais na first lady, Dereva wa gari la rais alikuwa ameongeza mwendo baada ya mushkeli kutokea na dhahiri kuonekana kwamba rais yuko hatarini, Hivyo basi ilimbidi Clint Hill kujaribu kuparamia gari mara kadhaa mpaka alipofanikiwa kuidandia gari na mara moja kuwafunika rais na first lady akiwakinga kwa kutumia mwili wake kama ngao.

Baada ya Agent Clint Hill kuwakinga Rais na mkewe dhidi ya shambulio lingine lolote la risasi kuwafikia, gari ya rais liliendeshwa kwa kasi kubwa likifuatiwa na pikipiki za pembeni na ile follow up car ya maafisa usalama, Wakati haya yote yanatokea zilikuwa zimebaki takribani dakika tano pekee kufika walikokuwa wanaelekea, Trade Mart, Kwahiyo baada ya gari iliyombeba rais kuanza kuendeshwa kwa kasi, takribani saa 6 na dakika 35 walipita eneo la Trade Mart na kuelekea moja kwa moja hospitali ya Parkland Memorial Hospital ambako waliwasili majira ya saa 6 na dakika 38 na kupokelewa kisha Rais Kennedy alipelekwa moja kwa moja chumba cha dharura.

Licha ya watu wa usalama kujitahidi sana kuratibu taaarifa za kilichotokea zisivuje kabla ya taarifa rasmi ya serikali, lakini majira ya saa 6 na dakika 40 kituo cha televisheni cha CBS kikakatisha Igizo lililokuwa linaonyeshwa kwenye televisheni yao na kutoa "Breaking News" kuwa msafara wa Rais umeshambuliwa huko Dallas, Baadae kama muda wa saa 6 na dakika 45, Dan Rather mwandishi wa habari wa kituo cha CBS alifanya mawasiliano kwa siri sana na daktari anayemfahamu hapo hospitalini na kuvujishiwa taarifa kuwa kuna uwezekano mkubwa Rais Kennedy hayuko hai.

Ifahamike kwamba maafisa wa Secret Services waliwaleta hapa viongozi wengine wote wakuu waliopo kwenye msafara, yaani First Lady Jacqueline Kennedy, Makamu wa Rais Johnson, Mkewe Lady Bird na Gavana Connally ambaye alikuwa chumba cha wagonjwa mahututi, Ilipofika saa 7 kamili madaktari wakatoa taarifa yao kwa viongozi wa serikali na wanausalama waliokuwepo hapo kwamba, licha ya kutumia ujuzi wao wote na maarifa yao yote, wameshindwa kuokoa maisha ya Rais JF Kennedy, kwamba Rais Kennedy amefariki. Dunia tayari!! Huko mtaani habari zilikuwa zinaenea kwa kasi kama moto wa kifuu, kuwa Rais Kennedy amefariki, hivyo kwa busara watu wa usalama wakashauri kuwa itolewe taarifa rasmi kuhusu kifo cha Rais Kennedy ili kuepusha mkanganyiko na taharuki iliyopo mtaani.

Makamu wa Rais Johnson akakubali hilo lakini akaamuru taarifa hiyo itolewe kwa umma mara baada ya yeye kuondoka hapo hospitali kwa usababu ya usalama wake, kwamba hataki yeyote ajue kuwa yuko hapo hospitali kwa kuwa kwa vile Rais ameuwawa tayari yawezekana yeye kama Makamu wa Rais akawa ni "next target"! Saa 7 na dakika 26 Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson akaondolewa kwa siri kubwa kutoka Parkland Memorial Hospital na kupelekwa uwanja wa ndege wa Love Field ambako Airforce One ilikuwa imepaki.

Baada ya Makamu wa Rais kuondoka tu, dakika saba baadae yaani saa 7 na dakika 33 Katibu Msaidizi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Malcolm Kilduff ya Marekani akafanya mkutano na waandishi wa habari hapo hapo hospitali na kuutangazia rasmi ulimwengu kuwa Rais JF Kennedy amefariki baada ya kudunguliwa na risasi na mtu asiyejulikana, Bw. Kilduff hakujibu swali lolote la waandishi wala kutoa taarifa nyingine yoyote, Alipotoa taarifa hii tu akaumaliza mkutano na wanahabari, Baada ya waandishi wote kuondoka na kubakia watu wa serikali pekee na wanausalama ndani ya Hospitali kulitokea kisa ambacho naamini wengi hawajawahi kukisikia.

Ni kwamba, katika sheria za Marekani kipindi hicho zilikuwa zinaelekeza kwamba, endapo Rais atafariki akiwa jimbo Fulani.. Mwili wake unakuwa chini ya mamlaka ya jimbo na sio serikali kuu, Sasa, yule bwana swahiba wa Rais Kennedy na Katibu wake wa teuzi Kenneth O'Donnell, yule ambaye alimuamuru Afisa wa Secret Services, Agent Kellerman kuwa gari la Rais liondolewe paa na kubaki 'kibanda wazi', akatoa tena maelekezo kwa wanausalama wauondoe mwili wa Rais Kennedy kutoka hapo hospitalini na kuipeleka uwanja wa ndege wa Love Field na kuupakia katika Air Force One, Lakini madaktari walikataa mwili huo kuondolewa hospitalini bila kufanyiwa 'Autopsy' (uchunguzi wa kina wa kidaktari kuhusu chanzo cha kifo) ukizibgatia kuwa Rais Kennedy amekufa kwa mauaji ya kukusidiwa.

Bw. Kenneth O'Donnell akasisitiza kuwa hakuna muda wa kutosha kufanya Autopsy kwani Air Force One inatakiwa iondoke mara moja kuwarudisha Makamu wa Rais na First Lady Washington kwa sababu za kiusalama na First Lady amekataa kuondoka bila mwili wa mumewe, madaktari wakashilia msimamo wao kuwa hawawezi kuuachia mwili wa Rais bila kufanyiwa Autopsy. Na kusisitiza wanalolisema wakatumia kifungu cha sheria nilichokitaja hapo juu kuwaeleza kuwa wao (Kenneth na wanausalama) kama watumishi wa serikali kuu hawana mamlaka juu ya mwili wa Rais bali wao (madaktari) kama watumishi wa jimbo la Texas ndio wenye mamlaka juu ya mwili wa Rais.

Mzozo ukawa mkubwa sana mpaka kufikia hatua Kenneth O'Donnell na wanausalama wakataka kuutoa mwili wa Rais Kennedy kwa kutumia nguvu, Hii ikawalazimu madaktari kuita maafisa wa polisi (watumishi wa jimbo la Texas) kuwasaidia kuwadhibiti Kenneth na wanausalama wa Secret Services, Madaktari wakatanda mlangoni pamoja na Maafisa wa polisi wakiwa wameshikilia bastola kuwanyooshea Kenneth O'Donnell na wanausalama wa Secret services kuwaamuru waache mwili wa Rais.

Upande wa pili nao Kenneth na wanausalama walikuwa nao wamechomoa bastola kuwanyooshea madaktari na polisi wa jimbo la Texas kuwa wapishe mlangoni, Wakati mzozo huo unaendelea hospitali ya Parkland Memorial Hospital, huko uwanja wa ndege wa Love Field, ndani ya Air Force One Jaji wa mahakama Kuu, Sarah Hughes alikuwa anamuapisha Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson kuwa Rais wa Marekani.

Na huko mitaani wananchi walikuwa wako kwenye sintofahamu kubwa!! Ni nini kimetokea? Nani amemuua Rais? Amewezaje kutekeleza hilo? Sababu gani imemponza Kennedy kuuwawa??.....Maswali yalikuwa mengi na magumu pasipo majibu ya dhahiri!!..

Sasa turudi kwenye kufahamu zaidi kuhusu nani muhusika wa kifo cha JF. Kennedy?...

Baada ya kushambuliwa kwa msafara wa Rais Kennedy na hatimaye kupelekea kifo chake, mara moja ndani ya masaa mchache akakamatwa mtu anayejulikana kama Lee Harvey Oswald na kushutumiwa kuhusika na tukio hili, Hii ilikiwaje? Nitaeleza kile ambacho serikali ya Marekani wanajaribu ulimwengu wote waamini.

Marion Baker ni afisa polisi wa eneo la Dallas na siku ya tukio alikuwa amepangiwa kuwa moja ya wasindikiza msafara kwa pikipiki, piki piki yake ya polisi ilipangwa nyuma ya magari waliyopanda waandishi wa habari kama ambavyo nilielezea mpangilio wa msafara hapo nyuma, Baker anaeleza kwamba siku hiyo ya tukio, akiwa kwenye msafara sekunde chache baada ya kukata kona kutoka Huston Street na kuingia Elm Street msafara ulipotembea umbali wa kati ya futi 60 au 80 alisikia mlio mkubwa wa risasi. Baker anadai kwamba kwa uzoefu wake aligundua kuwa mlio huo ni wa 'Rifle' yenye nguvu kubwa na kuzingatia mlio uliotoka alihisi kwamba bunduki hiyo imefyatuliwa kutoka eidha Jengo la mbele yake (Texas School Book Depository) au jengo lililo mkabala na jengo hili kwa upande wa kulia, yaani jengo la Dallas Textile Building (DalTex).

Baker anaeleza kwamba, alipoangalia kwa umakini zaidi katika jengo la Texas School Books Depository akaona njiwa waliokuwa juu ya jengo wanaruka na kutawanyika kutoka kwenye paa, Baker anaeleza kwamba moja kwa moja akaendendesha pikipiki yake mpaka kwenye kona ya Huston Street na Elm Street ambako alipaki pikipiki yake na kisha kuelekea kwenye jengo la Texas School Books Depository na kuingia ndani ambako alikutana na msimamzi wa jengo hilo Bw. Roy Truly, Moja kwa moja baada ya kumueleza kwa haraka haraka kuhusu kilichokuwa kinaendelea huko barabarani alikotoka na kwanini yuko hapa, yeye na Roy wakapanda mpaka ghorofa ya kwanza na kuanza kupiga kelele mtu yeyeto aliyepo juu ashushe lifti kuja chini, Miaka hiyo lifti nyingi hazikuwa na mfumo kama huu wa sasa ambapo unabofya kitufe na lifti inakufuata ghorofa ulilopo. Kipindi hicho ilikuwa inabidi mtu aliyepo ghorofa ambalo ndipo lifti ilikuwepo kwa muda huo airuhusu kushuka chini au kwenda juu kulingana na uhitaji wa huo.

Baada ya Baker na Roy kuita kwa sekunde kadhaa bila majibu wakaamua watumie ngazi za kawaida za jengo kwenda juu, Wakapanda mpaka ghorofa ya pili ambako wakiwa wanaelekea kupanda ngazi kwenda ghorofa ya juu zaidi, Baker anadai kwamba alisikia mjongeo kwenye chumba kilichopo karibu yao. Chumba hiki kilikuwa kinatumika kama chumba cha chakula na wafanyakazi kwenye jengo hili, Baker akachomoa bastola yake kutoka kiunoni na kufungua chumba hiki. Ndani ya chumba hiki walimkuta Lee Oswald, Wanaeleza kuwa Oswald hakuonekana kuwa mtu mwenye mashaka au 'kupaniki' ila tu alishtuka kuona Polisi amemmnyooshea bastola.

Inaelezwa kuwa Oswald alikuwa anaonyesha dalili zote za mtu ambaye hakuwa anajua ni nini kilikuwa kinaendelea, Msimamizi wa jengo alimtambulisha Oswald kwa askari kuwa alikuwa ni mfanyakazi wa jengo hilo, hivyo ikambidi polisi amuache Oswald na kuendelea na upekuzi katika floor za juu, Purukushani yote hii kutoka muda ambao Baker alisikia mlio wa risasi akiwa kwenye msafara wa Rais mpaka kuja kukutana na Oswald ghorofa ya pili ya jengo la Texas School Books Depository, ilichukua kama sekunde 74 mpaka sekunde 90 tu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kamisheni maalumu iliyoundwa na serikali ili kuchunguza kifo cha Rais Kennedy, The Warren Commission wanaeleza kwamba inakisiwa kuwa Oswald aliondoka kwenye jengo la Texas School Books Depository muda wa saa 6 na dakika 33 kupitia mlango wa mbele huku akiwa ameshika soda mkononi kwa mujibu wa ushahidi wa mwanamama ambaye alikuwa anafanya kazi kama secretary kwenye jengo hili, Inaelezwa kwamba, baada ya upekuzi mnamo saa 6 na dakika 50, bunduki, Rifle aina ya Italian Carcano iligunduliwa ikiwa imefichwa kwenye lundo la vitabu katika ghorofa ya sita.

Baada ya kugundulikwa kwa bunduki hii mnamo majira ya saa 6 na dakika 50 jengo hili likawa 'sealed' kuzuia mtu yeyote asitoke au kuingia, Lakini ajabu ni kwamba kule barabarani ambapo Rais Kennedy alidunguliwa, kulikuwa hakujawekwa kizuizi chochote kuzuia watu wasipite ili kuepusha kuharibu 'crime scene', na kuna rekodi za video zikionesha magari yakiendelea kupita barabarani kama kawaida eneo lile ambalo dakika chache kumetokea mauaji ya Rais, Ripoti ya Warren Commission inaeleza kwamba mara baada ya Oswald kutoka kwenye jengo la Texas School Books Depository, Oswald alitembea kwa miguu umbali wa kupita majengo saba (seven blocks) na kisha kupanda bus, Bus lilitembea kwa muda mchache kabla ya kukwama kwenye foleni ya barabarani. Baada ya bus alilopanda kukwama kwenye foleni, Oswald alishuka na kutembea kwa mguu mpaka kwenye kituo cha mafuta. Hapo alichukua taxi ambayo ilimbeba mpaka mtaani kwake lakini hakushukia nje ya nyumba yake, taxi ilienda kumshusha majengo kadhaa kupita nyumba yake. Baada ya kushuka kwenye Taxi akatembea kurudi nyuma mpaka nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa mfanyakazi wa usafi kwenye jengo ambalo Oswald alikuwa amepanga, Earlene Roberts, anasema kwamba Oswald aliwasili nyumbani kwake 1026 North Beckley Avenue majira ya saa 7 kamili mchana na hakukaa sana ndani kwani aliondoka tena kama dakika tatu au nne baada ya kuwasili, Earlene anadai kuwa alimuona Oswald amesimama mbele ya nyumba akiwa anasubiri gari muda mchache baada ya kumuona amewasili hapo kabla.

Ilipofika majira ya saa 7 na dakika 15 mchana polisi walipokea taarifa juu ya kupigwa risasi kwa polisi mwenzao J.D Tippit katika makutano ya barabara za 10th St. na Patton Avenue. Sehemu hii ni takribani kilomita moja tu kutoka nyumbani kwa Oswald, Bado kuna utata na ubishani mkubwa kwanini polisi walimuhusisha Oswald na kupigwa risasi kwa polisi J.D Tippit, lakini inaelezwa kwamba Oswald alionekana akitembea kwa miguu kuelekea jumba la maonyesho ya sinema la Texas Theatre.

Kuna bwana mmoja anaitwa Johhny Calvin Brewer ambaye alikuwa anafanya kazi katika duka la viatu liitwalo Hardy's shoes Store ambalo liko ghorofa moja na ilipo Texas Theatre anadai kwamba alimuona Oswald akijificha sura mara baada ya magari ya polisi kupita karibu yake huku yakiliza king'ora, Bw. Brewer anadai kwamba akamfuatilia Oswald alikokuwa anaelekea na akamuona anaingia kimagendo bila kulipia mlangoni Texas Theatre muda ambao mkata tiketi Bi. Julie Postal alikuwa amejisahau na kuangalia pembeni.

Inaelezwa kwamba Brewer akamtaarifu bibie Julie kuhusu Oswald aliyeingia kimagendo ndani ya Theatre na baada ya hapo wakapiga simu polisi kuwafahamisha kuwa ndani ya Theatre kulikuwa na mtu ambaye walikuwa wana mashaka naye, Ndani ya dakika chache, kufumba na kufumbua zilifika zaidi ya gari za polisi 24, pamoja na ma-sheriff na wapelelezi.

Baada ya lundo hili la wanausalama kuwasili, mnamo majira ya saa 7 na dakika 50 mchana Lee Harvey Oswald akakamatwa kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha polisi J.D Tippit na muda mchache baada ya kufikishwa kituo cha polisi, Oswald aliongezewa mashtaka na kuhusishwa pia na kumdungua kwa risasi na kumuua Rais JF Kennedy.!!

Oswald Chini Ya Mikono Ya Polisi...

Baada ya Oswald kukamatwa kutoka jumba la kuonyesha sinema la Texas Theatre, moja kwa moja akapelekwa makao makuu ya polisi ya Dallas, Akiwa hapo kituoni Oswald alihojiwa na Asifa wa FBI, Special Agent James P. Hosty pamoja na Afisa mkuu wa Polisi kituo cha Dallas Captain Will Frizt, Oswald alikana kuhusika kabisa na mauaji yote mawili, yaani mauaji ya Rais Kennedy na mauaji ya polisi J. D Tippit, Akajieleza kwamba siku ya tukio ni kweli alikuwa kwenye jengo la Texas School Books Depository na hakukuwa na ajabu yeye kuwepo hapo kwa kuwa anafanya kazi kwenye jengo hilo.

Akaendelea kujieleza kuwa wakati tukio linatokea alikuwa anakula chakula cha mchana kwenye ghorofa ya kwanza na hakuwa anajua kinachoendelea huko mtaani na baada ya kumaliza kula chakula akapanda mpaka ghorlfa ya pili ili kwenda kuchukua soda aina ya coca cola kwenye 'vending machine'. (Ndio hii soda ambayo nilieleza kwenye sehemu iliyopita kwamba kuna mama secretary wa jengo hilo alimuona Oswald ameibeba akiwa anatoka nje ya jengo), Oswald akaeleza kuwa akiwa anarejea kutoka ghorofa ya pili kwenda ghorofa ya kwanza alikuta na wafanya kazi wengine wawili weusi ambao nao ni waajiriwa wa jengo hilo. Oswald aliwaeleza kumtambua mfanya kazi mmoja kwa jina la 'Junior' na mwingine hakuwa anamkumbuka kwa jina.

Polisi baadae waliwahoji wafanyakazi weusi wanaofanya kazi kwenye jengo hilo na walijitokeza wafanya kazi wawili Junior Jarman na Harold Norman ambao walikiri kwamba walimuona mtu akiwa kwenye chumba cha chakula au 'Domino Room' kama ambavyo walizoea kukiita lakini walikiri kuwa hawakuwa makini kumuangalia ni nani hivyo hawakumbuki, Oswald akaendelea kueleza kuwa aliporejea kwenye chumba cha chakula na kuketi ili ajiburudishe na soda yake ya coca cola, ndipo ghafla alishituka anaingia polisi ambaye baadae alikuja kumtambua kama Marion Baker na kumnyooshea bastola.

Licha ya maelezo yote haya lakini bado waliendelea kumbana na kumlazisha kukiri uhusika wake kwenye kumdungua Rais Kennedy, walimuonyesha Picha ambayo ilionyesha Oswald akiwa ameshikilia bunduki ambayo iliaminika kumdungua Rais Kennedy, Oswald alikanusha na kudai kuwa picha hiyo imetengenezwa.

Wakamuonyesha pia risiti za ununuzi wa bunduki hiyo kwa kutumia jina bandia la "A.J Hidell" lakini bunduki hiyo ilitumwa kwenye anuani ya nyumbani kwake, Oswald akakanusha kufanya manunuzi hayo na kusisitiza kuwa huo ni "mchoro" kuna watu wanajaribu kumsingizia yeye shutuma hizo ili kuficha wahusika halisi, Kitu pekee ambacho Oswald alikiri ni kumiliki bastola 0.38 revolver na alidai kuwa anaimilili kwa mujibu wa sheria na ulinzi binafsi, Pia ikumbukwe kuwa Oswald aliwahi kutumikia jeshi la Marekani kikosi cha Marine Corps.

Oswald pia alikataa kabisa kuwakilishwa na mawakili wa utetezi wa serikali au wale ambao serikali ilikiwa tayari kumlipia kama haki yake ya kiraia, Oswald alidai kuwa hakuwa na imani na watu hao au serikali kumtendea haki kwenye suala hili, Wakili pekee ambaye Oswald alikubali amuwakilishe kwenye mahojiano na kipindi cha kesi kusikilizwa alikuwa ni Bw. John Abt ambaye alikuwa anatokea American Civil Liberties Union, Lakini ajabu ni kwamba kwa siku zote mbili za mahojiano ya Oswald, John Abt alikuwa hapatikani kwenye simu yake ya nyumbani wala sehemu yake ya kazi.

Mahojiano ya polisi na Oswald yaliendelea kwa muda wa siku mbili mfululizo, Siku mbili zilipopita yaani siku ya Novemba 24, 1963 vyombo vya ulinzi viliazimia kumuhamisha Lee Oswald kutoka katika mahabusu ya polisi kituo cha Dallas na kumpeleka gerezani kwa ajili ya kushikiliwa kwa usalama zaidi akisubiria mahojiano zaidi na kesi yake kuanza kuunguruma, Muda wa saa 5 na dakika 15 asubuhi, Oswald alifunguliwa na kutolewa kwenye selo na baada ya kusainiwa kwa makaratasi yake ya kuhamishwa kutoka hapo kituoni ili apelekwe gerezani.

Saa 5 na dakika 19 Oswald alikuwa anakaribia kufika kwenye mlango wa ghorofa ya chini kabisa (basement) ili kupelekwa kwenye gari maalumu lisilopenya risasi ambalo lilikuwa linasubiri ili kumbeba na kumpeleka gerezan, Tukio hili lilikuwa limeteka hisia za taifa zima na lilikuwa linafuatiliwa kila kona ya nchi ya Marekani na duniani kote kwa hiyo vituo vingi vya televisheni lilikuwa vinarusha tukio hili moja kwa moja, mubashara kabisa, Saa 5 na dakika 20 polisi wawili walitoka mlangoni ili kuhakikisha usalama na sekunde chache baadae Oswald akiwa amefungwa pingu na kuzungukwa na wanausalama kila kona alitoka kwenye mlango wa jengo kuingia basement ili aweze kupelekwa kwenye gari inayowasubiri.

Oswald na maaskari waliokuwa wamemzunguka walipiga kama hatua tano tu au sita na ghafla akajitokeza mtu aliyekuwa pembeni yao amekaa pamoja na wana Habari, na mkononi mwake alikuwa ameshika bastola akiielekeza moja kwa moja kwa Oswald, Hii lilikuwa ni saa 5 na dakika 21, Kabla wanausalama hawajafanya lolote, mtu huyu alimfyatulia risasi ya tumboni Oswald na moja kwa moja Oswald akadondoka chini, Wanausalama wakafanikiwa kumdhibiti mtu huyu na kumkamata na moja kwa moja wakamuingiza ndani kwenye kituo cha Polisi pamoja na Oswald.

Mtu huyu aliyempiga risasi Oswald anaitwa Jack Ruby na ni moja ya watu maarufu sana Dallas katika kipindi hicho kutokana na kumiliki Klabu kubwa ya usiku mjini hapo, Dakika chache baadae Oswald alichukuliwa na gari ya wagonjwa na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Parkland Memorial Hospital (hospitali ile ile aliyofia Kennedy siku mbili nyuma), Risasi aliyopigwa Oswald iliingia ubavu wa kushoto na ilikuwa imeenda kuharibu kabisa bandama, aorta, vena cava, figo, ini, diaphragm na mbavu ya kumi na moja ya kushoto na ikakwama katika ubavu wa kulia, Vile vile pia baada ya "juhudi kubwa" za madaktari kuokoa maisha ya Oswald kutozaa matunda hatimaye muda wa saa 7 na dakika 7 siku hiyo ya Novemba 24, Dallas Police Chief Bw. Jesse Curry aliutangazia uliwengu kuwa mtuhumiwa pekee wa mauaji ya Rais JF Kennedy, Bw. Lee Harvey Oswald amefariki dunia.

Mara moja baada ya habari hii kutangazwa iliwafanya watu wengi waanze kukuna vichwa, Siku mbili nyuma mara baada ya Rais Kennedy kupigwa risasi kulianza kuibuka minong'ono mitaani kwamba huo ulikiwa ni 'mchoro' wa watu wenye nguvu kwenye 'system', Baadae siku hiyo hiyo ilipotangazwa kuwa muuaji wa Kennedy amekamatwa, sintofahamu ikaongezeka zaidi kuwa imekuwaje mtu ambaye ametekeleza mauaji makubwa hivyo akamatwe 'kizembe' na kwa haraka namna hiyo, Lakini ilipotolewa taarifa ya Oswald kuuwawa, huko mtaani asilimia kubwa ya wananchi wazo moja kuu lilitawala vichwani mwao, kuwa "Oswald alikuwa amenyamazishwa"! Kuna uwezekano mkubwa wahusika halisi wa kifo cha Kennedy walikuwa wanahofia kesi ya Oswald kuanza kuunguruma kwani walihofia labda Oswald "angemwaga mchele!"

Pia kilichosgangaza zaidi ni mtu aliyempiga risasi Oswald. Jack Ruby ni mfanyabiashara mkubwa, mtu mwenye 'status' hapo Dallas, Inawezekaje mtu wa hadhi yake afanye kitu cha kipuuzi kiasi hicho kwa kumpiga mtu risasi hadharani mbele ya vyombo vya habari kwa suala ambalo alimuhusu moja kwa moja?? Ana maslahi gani kufanya hivyo??, Sasa ilikuwa dhahiri, kwamba, kuna jambo kubwa zaidi linafichwa nyuma ya pazia… kuna wahusika halisi wa kifo cha Kennedy!!

Ni kina nani, Na kwa nini walimuua Kennedy??....

Hakuna mwenye majibu kamili ya asilimia mia, lakini nitajitahidi kuleta kwenu vidhibiti kadhaa ambavyo vitasaidia kila mmoja kufikia conclusion yake binafsi!!

Japokuwa serikali ya Marekani wameendelea kushikilia msimamo kuwa Lee Harvey Oswald alihusika yeye kwa binafsi yake kudungua na kumuua Rais Kennedy kutokana na kudaiwa kuwa misimamo mikali wa sera za kijamaa, lakini kuna vidhibiti vingi vinavyoonyesha kuwa kuna kikundi au vikundi vya watu wenye nguvu kubwa walio nyuma ya mauaji haya, Kabla sijaweka vidhibiti vya kuonyesha labda ni watu gani wamehusika na kifo cha Kennedy, ningependa awali ya yote tujaribu kukiangalia kisa cha Oswald kuambiwa kuwa ndiye aliyemdungua rais na ukweli wake na maswali yayozunguka suala hili.

Dalili ya kuwepo ya wadunguaji zaidi ya mmoja...

Nikumbushe kuwa, wiki moja baada ya mauaji haya ya Rais Kennedy, Rais mpya Johnson aliunda tume maalumu kuchunguza ukweli juu ya tukio hili, Tume hii iliundwa kwa kutokana na Executive Order number 11130 na kutambuliwa na Congress kupitia Resolution number 137, Kamisheni hii ilikuwa chini ya Uenyekiti wa Chief Justice Earl Warren na ndio sababu ya kujulikana kamaa The Warren Commission, Kulikuwa na mabishano makali juu ya uundwaji wa kamisheni hii, huku baadhi ya viongozi waandamizi serikalini wakiamini kuwa kamisheni hii itaamsha hasira za wananchi badala ya kutatua utata uliopo.

Licha ya viongozi wengi wakuu serikalini kushauri kutoundwa kwa hii kisheni lakini kwa sababu ambazo Rais mpya Johnson yeye binafsi aliziona ni muhimu akaunda tume hii wiki moja tu baada ya tukio na ilifanya kazi kwa takribani miezi kumi na hatimaye kukabidhi ripoti yake kwa Rais tarehe 24 September, 1964 na kuwekwa hadharani kwa wananchi siku tatu baadae, Nitaizungumzi zaidi Ripoti hii na masuala kadhaa kuihusu huko sehemu za mbeleni za hii makala, Lakini jambo kuu zaidi hii Ripoti inachojaribu kuonyesha ni kwamba Lee Oswald alifanya tukio kwa utashi wake pekee na hakushirikiana na mtu yeyote!!

Siku moja tu baada ya ripoti hii kutoka ilikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa watu waliofuatilia tukio hili kwa makini pamoja na wachambuzi wa masuala ya intelijensia, Ripoti hii ilionekana kama vile ilikuwa ni jaribio la serikali kujisafisha na haikuwa na nia ya kuchimbwa ukweli juu ya nini hasa kilitokea siku ya November 22, 1963, Moja wapo ya vitu ambavyo Ripoti hii imepingwa vikali ni jaribio lake la kutaka kuaminisha umaa kuwa Oswald ndiye muhusika na alikiwa pekee kwenye tukio hili, Japokuwa ripoti yaa Warren Commission inabakia kuwa msimamo rasmi wa serikali mpaka leo hii juu ya kifo cha Rais Kennedy lakini vipo vidhibiti kadhaa vinavyoonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa tukio hilo (kumpiga risasi rais) siku ya Nov 22, lilitekelezwa na zaidi ya mtu mmoja.

Nitaeleza…

Kuna jambo moja la msingi sana ambalo nadhani wengi labda watakuwa hawajawahi kulisikia licha ya kusoma makala nyingi kuhusu kifo cha Kennedy, Wakati natafiti kuhusu makala hii nilijitahidi kuipitia ripoti ya Warren Commission na baada ya kuipitia kuna jambo lilijoficha sana ambalo nililiona na kufanya nichimbe zaidi kuhusu ni nini kilitokea polisi ambapo Oswald alishikiliwa.

Hiko hivi,

Bunduki iliyotumika kufyatua risasi iliyomuua Rais Kennedy inatajwa kwenye ripoti ya Warren Commission kuwa ni "Mannlicher-Carcano", Lakini ukifuatilia kwa undani utagundua kwamba bunduki hii ni aina ya 6.5x52mm Carcano (model 91/38 - Infantry Rifle), Bunduki hii ina uzito wa kilo 3.9 na urefu wa milimita 1285 (inch 50.6) ambapo urefu wa mdomo wa mbele pekee (barrel length) ni 780mm (inch 30.7), Risasi inayopigwa kutoka kwenye bunduki hii ina uwezo wa kusafiri mita 700 kwa sekunde na kwenda umbali mpaka kufikia mita 1000, Pia uzalishwaji wa bunduki hizi nyingi ulifanyika mwaka 1891 nchini Italia na kuna model chache zilitengenezwa miaka1940s huko huko Italia.

Bunduki nyingi zilizopo za Mannlicher-Carcano (hata kipindi hicho cha mwaka 1963) hazina Telescopic sight (darubini ya mdunguaji… yaani ile lenzi ambayo sniper anachungulia kupata muono mzuri wa target yake), Lakini bunduki inayodaiwa kutumiwa na Oswald ilikuwa na telescopic sight. Hii ina maana kwamba eidha aliifanyia modifications au alihangaika kupata model chache za Carcano zilizozalishwa miaka ya 1940s.

Sasa basi,

Kuna kitu ambacho naamini watumiaji wengi wa silaha watakuwa wanakifahamu, kinaitwa GSR au wengine wanaita CDR (Gunshot Residue au Cartridge Discharge Residue), Hili ni kama unga au vumbi fulani jembamba sana linatoka ukifyatua risasi na mara nyingi huwezi kuliona, Vumbi hili linatokana na propellant ya risasi ndani ya bunduki pale inapofyatuliwa, pia vipande vidogo vidogo sana (particles) za risasi na catridge ikifyatuka, Kitaalamu, GSR inaruka futi 3 mpaka 5 kutoka bunduki ilipofyatuliwa, kwa maana ya kwamba mtu anayefyatua bunduki hii ni lazima atarukiwa na 'vumbi' hili la GRS na vumbi hili huwa linakaa mwilini kwa mfyatuaji risasi kwa masaa matatu mpaka sita kitegemea na aina ya silaha iliyotumika.

Sasa,

Katika uchunguzi wa matukio ya uhalifu kwa kutumia silaha kuna kipimo kinaitwa Paraffin Test, Kipimo hiki huwa kinapima uwepo wa GRS katika nguo na mwili wa mtu ambaye anahisiwa kutumia hiyo silaha katika tukio hilo mahususi, Kipimo kikileta majibu positive - hii maana yake ni kwamba mtu huyo alifyatua hiyo risasi, au alikuwa karibu muda ambao risasi ilipofyatuliwa au aliigusa risasi silaha muda mfupi baada ya kufyatuliwa, Majibu ya kipimo yakija negative hii ina maana kwamba mtu huyo hakufyatua risasi, au hakuwa karibu muda ambao risasi ilifyatuliwa au hakuigusa silaha baada ya kifyatuliwa.

Turudi kwenye ninachojaribu kueleza… kwa mujibu wa taarifa ya makao makuu ya polisi Dallas ambapo Oswald alishikiliwa, alipokuwa hapo kituoni alifanyiwa Paraffin Test, Ajabu ni kwamba majibu yalikuja negative.!!, Maana yake ni kama nilivyoeleza hapo juu, majibu negative yanamaanisha kuwa mtu huyu hakufyatua risasi, na hakuwa karibu na silaha wakati inafyatuliwa na wala hakuigusa baada ya kufyatuliwa, Hii ina maana gani? Warren Commission na serikali hawakuiona hii ripoti ya Polisi??? Jibu ni kwamba waliiona na wakaja na "majibu" yao.

Kwamba,

Kwenye ripoti ya Warren Commission wanaeleza kwamba walimuhoji mama anayeitwa Earlene Roberts. Huyu ni yule mama wa usafi katika jengo ambalo kulikuwa na chumba cha Oswald anapoishi, Warren Commission wanadai kuwa mama huyu aliwaeleza kuwa alimuona Oswald akirudi kwake na kuondoka tena baada ya kama dakika tatu au nne na alipoondoka alikuwa amevaa nguo nyingine tofauti na zile za awali alizokuja nazo, Kwa hiyo Warren Commission wakatumia ushahidi huu kuhitimisha swali la kwanini majibu ya Parrafin Test ya Oswald yalikuja negative.

Ufafanuzi wao ni kwamba nguo alizozivaa wakati anapimwa hicho kipimo hazikuwa zile ambazo alizivaa wakati anafyatua risasi na hata baada ya kupekuliwa alipokuwa anaishi na nguo za awali kupatikana tayari muda ulikuwa umepita kuwezesha kipimo kubashiri uwepo wa GSR, Lakini huu ni ukweli nusu ambao unapotoshwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Nilieleza kwamba bunduki inayodaiwa kutumika na Oswald ina telescopic sight (darubini ya kudungulia). Maana yake kwamba mtumiaji lazima ainame juu ya bunduki ili aweze kuchungulia kutumia telescopic sight, Maafisa wote wa FBI ambao ni walengaji (Marksmen) ambao walitumiwa kwenye uchunguzi wa miaka ya hivi karibuni kutafiti juu ya GSR kwa kutumia bunduki ile ile inayodaiwa ilitumiwa na Oswald ikiwa na telescopic sight, katika vipimo vya Parrafin wote walikutwa na kiwango kikubwa cha GSR usoni na hasa hasa mashavuni, Kwa hiyo, maelezo ya kuwa Oswald alibadili nguo ndio maana majibu ya Parrafin Test yakaonyesha negative yanakuwa hayajitoshelezi sana.

Labda tuchukulie ndani ya dakika tatu hizo alizoingia chumbani, Oswald alioga kwa umakini wa hali ya juu na kujisugua haswa na kisha kubadili nguo (which is unlikely mtu kufanikisha yote hayo ndani ya dakika tatu)…. Bado kuna kiwango kikubwa cha sintofahamu kuhusu ufyatuaji wa risasi….

Utata Wa Risasi Iliyomuua Rais Kennedy...

Ni kwamba, katika teknolojia ya kurekodi video kuna kitu kinaitwa frames. Kwa lugha rahisi kabisa, frames ni picha mnato ambazo zinaunda video. Ndio kusema kwamba, kipande kifupi cha video kina Picha mnato mamia kadhaa. Au kwa lugha nyingine nyepesi zaidi ni kwamba video ni muunganiko wa maelfu ya picha mnato zilizorekodiwa katika mtiririko wa kufuatana, ukiangalia ile video ya tukio utaona upande wa juu kulia kuna namba zinatokea na zinaenda kama zinahesabu hivi. Namba zile zinakuonyesha muda huo husika unaangalia frame namba ngapi ya kipande hiki cha video.

Suala hili la kuelewa tukio gani limetokea frame namba ngapi kwenye kwenye video lina umuhimu wa kipekee sana kwenye kuelewa utata wa tukio hili la kuuwawa kwa Rais Kennedy kama ambavyo nitaeleza leo katika sehemu ya hii makala.

Sasa,

Nilieleza kuwa serikali kupitia Warren Commission wanashikilia msimamamo kuwa Oswald alitekeleza tukio peke yake kwa utashi wake pasipo kushirikiana na mtu yeyote yule. Serikali inashikilia msimamo huu ili kupinga msimamo wa wengi kuwa tukio hilo lilipangwa na watu na yawezekana kabisa ni watu wenye nguvu kwenye 'system', Pia nikumbushe nilipoandika kuhusu namna rais alivyopigwa risasi nilieleza kuhusu risasi ya kwanza kumpata ilitokea kooni/kifuani na kwenda kumpata Gavana Connally sehemu ya nyuma ya mgongo kulia chini kidogo ya kwapa na kumsababishaia majeraha makubwa tumboni, mkononi na kwenye paja.

Nadharia hii ya risasi moja kusababisha yote haya inaitwa "Single Bullet theory", kwamba risasi ya kwanza kumpata Kennedy ndio risasi hiyo hiyo ilimpata Gavana Connally, Lakini kuna mazingira yanayoashiria kwa uthibitisho mkubwa kwamba Connally hakujeruhiwa na risasi ambayo ilimpata Kennedy mara ya kwanza.

Tuangalie hivi,

Ukitazama video katika frame ya 224 ni dhahiri kwamba huu ndio muda ambao risasi ya kwanza ilimpata Kennedy, hapa ndipo ambapo Kennedy anashtuka kwa maumivu na kunyanyua mkono wake wa kulia na kuukunja ngumi na kuuinua usawa wa mdomo, Katika muda ambao frame 224 inaishia ndipo ambapo Connally anaonekana kushtuka pia kisha anageuka upande wa kulia na kujitahidi kugeuka nyuma kana kwamba anajaribu kumuangalia Rais Kennedy.

Katika frame hii Gavana Connally haonyeshi dalili yoyote ya kuwa katika maumivu (licha ya kushtuka), Pia kuna dalili kadhaa zinaonyesha kuwa si muda huu ambapo alipigwa risasi, Mfano ukimuangalia mkononi bado ameshikilia kofia yake ya 'pama'. Kama unakumbuka nilishaeleza huko mwanzoni kwamba moja ya sehemu ya mwili wa Gavana Connally ambayo risasi ilipenya ilikuwa ni sehemu ya juu ya kiganja chake cha mkono wa kulia na mfupa wake kupasuka katika vipande vinane, kwa hiyo haitegemewi mtu ambaye kiganja kimegawanyika katika vipande vinane aendelee kuwa na uwezo wa kushikilia kitu mkononi.

Lakini pia, kingine kinachothibitisha kuwa Connally hakupigwa risasi katika frame ya 224 ni kauli ambayo aliwahi kuitoa yeye mwenyewe. Namnukuu "..nilisikia mlio ambao mara moja nikang'amua kuwa ulikuwa ni mlio wa risasi. Nikashtuka na kugeula upande wa kulia kwa sababu nilihisi mlio bunduki ilikuwa imefyatuliwa kutoka upande huo. Lakini sikuona kitu chochote, niliona tu kundi la watu wanatupungia mikono. Nilipokata jicho kumuangalia rais nyuma yangu sikuweza kumuona bara bara…. nilikuwa nataka nimuone rais ili kujua usalama wake kwa kuwa niliposikia tu mlio wa risasi hisia zangu ziliniambia kuwa kulikuwa na jaribio la mauaji ya rais..."

Zaidi kuhusu utofauti ya frames niliouzungumza hapo juu kuonyesha kuwa Kennedy anaonekana alipigwa risasi frame ya 224 na Connally alipigwa risasi frame ya 275, Connally anaeleza kuwa baada ya hapo akawa anaanza kugeuka na ndipo ambapo alisikia maumivu kifuani na alihisi kuwa amepigwa risasi ambayo hata hakuisikia mlio wake, Maelezo yake yanathibitishwa na ukiangalia kipande cha video, Connally anaonekana akitunisha mashavu kama anapuliza hewa nje na kukunja uso kwa uchungu katika frame ya 275 kuonyesha kwamba risasi ilikuwa imempata muda huu.

Sasa, kwanini nasisitiza na kuonyesha vidhibiti kuwa risasi iliyopata Kennedy katika frame ya 224 haikumpata Connally??...

Iko hivi,

Ni kwamba, serikali kupitia Warren Commission wamekuwa wakieleza kuwa risasi iliyopata Kennedy ndiyi hiyo hiyo ilitokeza kifuani kwake na kwenda kumpiga Connally, ili hoja hii iwe sahihi maana yake ni kwamba kwa kuzingatia kasi ya mwendo wa risasi, tukio hili (risasi moja kumpiga Kennedy na Connally) lingetokea ndani ya 1/100 ya sekunde (sekunde moja gawanya kwa mia moja). Na tukio linalotokea ndani ya 1/100 ya sekunde haliwezi kurekodiwa kwenye frames tofauti ni lazima litatokea kwenye frame moja ya video.

Kutoka frame namba 224 ambayo Kennedy anapigwa risasi mpaka frame namba 275 ambayo Connally anaonyesha kuanza kuugulia maumivu ni takribani interval ya theluthi ya sekunde, Theluthi ya sekunde ni muda mwingi sana kwa risasi moja kusafiri kutoka kwa Kennedy kumpata Connally, Maelezo pekee ya kuelezea hili ni kwamba risasi ya kwanza kumpata Kennedy haikumpata Connally. Zilikuwa risasi mbili tofauti.

Lakini pia theluthi ya sekunde haitoshi kufyatua risasi mbili kutoka katika bunduki aina ya Mannlicher Carcona. Ukipiga risasi unahitaji kusubiri sekunde kadhaa ili 'kuikoki' tena bunduki na uweze kupiga tena, kwa kifupi ni kwamba kwa namna yoyote ile au muujiza wowote ule haiwezekani kufyatua risasi mbili ndani ya theluthi ya sekunde kutoka katika bunduki ya aina hii, Kwa hiyo hii inatueleza kwamba risasi iliyompiga Kennedy na iliyompiga Connally zilikuwa risasi mbili tofauti na zilipigwa kutoka kwa watu wawili tofauti.

Swali ni kina nani watu hawa??...

Kabla hatujafika mbali kuanza kujiuliza ni nani mwingine labda alifyatua risasi nyingine hebu tuangalie vidhibiti zaidi, Baraza la Senate liliwahi kuunda kamati ya kuchunguza mauaji mbali mbali ya kupangwa yaliyowahi kutokea nchi Marekani. Kamati hii iliitwa House Select Committee on Assassinations au kuwa kifupi kama HSCA, Moja wapo ya chunguzi walizofanya ni kuhusu mauaji ya Rais Kennedy.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alikuwa ni mtaalamu nguli wa patholojia, Dr. Cyril Wecht, Dr. Wecht aliandika andiko la maoni yake kwa kamati hii teule ya Senate na akawaeleza kuhusu nadharia aliyokuja nayo kuhusu tukio hilo ambayo nadharia hii ilikuja kujulikana kwa wengi kama "Right to Left trajectory ", Kama nilivyoeleza kwamba, serikali kupitia Warren Commission wanadai kuwa risasi zilipigwa na Oswald akiwa mkono wa kulia wa jengo la Texas School Books Depository, Katika andiko lake kwenda kwa HSCA, Dr. Wecht anaeleza kwamba kwa kuzingatia kuwa ripoti ya serikali inaeleza kuwa risasi ilifyatuliwa kutoka ghorofa ya sita kutoka kwenye jengo tajwa, na pia kuzingatia upande wa jengo ambao unaelezwa Oswald alikaa, kwa maoni yake haiwezekani kwa risasi hiyo iliyompata Kennedy upande wa kulia pia kumpata Connally upande wa kulia wa ubavu chini kidogo ya kwapa

Kwanini?

Ukipima pembe mlalo (horizontal angle) kutoka jengo la Texas School Books Depository kwenda kwenye gari aliyomo rais na mahali ilipokuwa katika frame 190 ya kipande cha video unapata nyuzi 13 (kutoka kushoto kwenda kulia), Papo hapo pia ukipima pembe wima (vertical angle) kutoka ghorofa ya sita kwenda kwenye gari ya Rais unapata nyuzi 21 kama utapima kwa kuchukulia kuwa barabara ilikuwa tambarare iliyo sawa (horizontal plane) lakini kama ukizingatia kuwa gari la rais lilikuwa linapita kwenye barabara yenye 'slope' ya nyuzi 3 maana yake kwamba pembe wima ya kutoka ghorofa ya sita mpaka kwenye gari ya Rais inakuwa ni nyuzi 18.

Tazama kwa makini umbali na 'angle' kati ya jengo la Texas School Books Depository na mahali shots zilipotua (alama nyekundu kwenye Picha nilizoweka) Sasa, ifahamike kuwa namna ambavyo Rais Kennedy alikaa kwenye siti yake alikuwa amekaa kuegemea kabisa kwenye mlango wa gari na hata ukiangalia video kuanzia mwanzoni utaona akiwa ameweka mkono juu ya mlango wa gari. Lakini Gavana Connally alikuwa amekaa katikati ya siti yake mbali kidogo na mlango wa pembeni yake, hivyo basi kwa kuzingatia 'trajectory' ya risasi kutokana na nilivyoeleza position ya mdunguaji kule juu, Dr. Wecht anaweka hitimisho kwamba, kama risasi iliyompiga Kennedy ndiyo pia ilimpiga Connally basi ilitakiwa impate upande wa kushoto wa uti wa mgongo na sio kulia kama ambavyo ilitokea.

Kwa hiyo hii inatupa vidhibiti kingine kwamba kuna kila dalili kwamba kulikuwa na zaidi ya mdunguaji mmoja, ni nani huyo mdunguaji/wadunguaji mwingine???

Lakini pia, tuvute subira labla ya kujiuliza tena swali hili, tutazame kidhibiti kingine, Huko nyuma nilieleza juu ya mzozo uliotokea Parkland Memorial Hospital baada ya madaktari kugoma mwili wa Kennedy kuondolewa pasipo kufanyiwa autopsy lakini Kenneth O'Donnell na maafisa usalama wakatumia mabavu kuondoka nao mwili wa rais bila kufanyiwa autopsy, Kwanza hii inatia mashaka kuwa pengine kuna kitu ambacho madaktari wangekiona katika autopsy na kuvuruga kabisa kilichokuwa kimepangwa au maelezo ambayo tayari yalikuwa yameandaliwa na wauaji wa Kennedy kuaminisha ulimwengu.

Lakini hata hivyo bado kuna vitu kadhaa muhimu ambavyo vinaonekana katika cheti cha kifo kilichotolewa hospitali ya Parkland, Kwa mfano katika kwenye cheti inaonyesha kwamba Kennedy alipigwa risasi katika usawa pingili ya tatu ya shingo kwenda chini. Lakini katika ripoti ya Warren Commission wameongeza karibia inch tano au sita kwenda juu na kuripoti kuwa alipigwa risasi katika 'base of the neck', hii inatoa hisia kwamba walikuwa wanalazimisha kuweka usawa huu wa risasi kuingia ili waweze kuhalalisha wanachokilazimisha kwamba risasi hiyo hiyo ikaenda kumpiga Connally ubavuni chini kidogo ya kwapa la kulia.

Kama tukizingatia kilichoandikwa kwenye cheti cha kifo kwamba risasi ilipigwa katika 'third thoracic vertebrae' basi isingelimpata Connally ubavuni chini kidogo ya kwapa, pia daktari wa zamu ambaye alimpokea Kennedy siku hiyo hospitali, Dr. Robert N. McClelland anaeleza kuwa walipokuwa wanajitahidi kuokoa maisha ya rais, alipomuangalia nyuma ya kichwa kidonda alichokiona kwa utaalamu wake kilikuwa ni 'exit wound' (kidonda risasi ilipotokea), Kwa hiyo hii ina maanisha kwamba risasi iliingilia mbele na sio nyuma kama inavyodaiwa kwenye ripoti ya Warren Commission.

Hii pia inathibismtishwa hata ukiangalia video, rais Kennedy anapopigwa risasi ya pili anaonekana dhahiri kichwa kilisukumwa na risasi kurudi nyuma kwa kishindo. Na si hivyo tu hata kipande cha fuvu la kichwa kilichofumuliwa kinadondokea kwenye 'bodi' (trunk) ya nyuma ya gari, kiwango kikubwa cha ubongo kinarushwa nyuma ya gari na kudondokea kwenye follow up car ya wanausalama na kiwango kingine kinawadondokea hata mapolisi wa pikipiki waliopo nyuma.

Mojawapo wa mapolisi hawa wa piki piki Bobby Hargis, aliyekaa mkono wa kushoto nyuma ya gari ya Rais, anaeleza kuwa alidondokewa na kiwango kikubwa cha ubongo kilichoruka katika kasi kubwa na kutua kwa kishindo mwilini mwake kiasi kwamba alidhani labda naye amepatwa na moja ya risasi zilizokuwa zinapigwa, Hii yote inazidi kututhibitishia kuwa kulikuwa na waduanguaji zaidi ya mmoja katika tukio na mdunguaji aliyepiga risasi iliyomuua rais (fatal shot) alikuwa amekaa mbele ya msafara au mkabala nao lakini kamwe sio nyuma, tena juu ya ghorofa, na hii yote inathibitisha ukweli wa Cheti cha kifo cha Rais Kennedy ambacho kilitolewa na Parkland Memorial Hospital siku ya November 22, 1963

Ushahidi wa Abraham Zapruder...

ushahidi mwingine katika tukio la kifo cha JF. Kennedy ni video iliyorokodiwa na mtu anayeitwa Abraham Zapruder. Hii ndio sababu ya kipande hiki maarufu cha video kuitwa "Zapruder Film", Huyu alikuwa ni mwananchi wa kawaida tu ambaye alikuwa na mapenzi makubwa na shabiki wa Rais Kennedy, kutokana na napenzi yake makubwa kwa Rais Kennedy alipojitokeza barabarani kwenda kumlaki rais kama wananchi wenzake wengine, aliamua kwenda na kamera yake ya matumizi ya nyumbani aina ya Bell & Howell Zoomatic Director Series (model 414 PD) ambayo aliinunua mwaka 1962.

Baada ya kurekodi tukio la kuwasili kwa rais na kwa bahati kufanikiwa kurekodi namna rais alivyopigwa risasi na baadae mkanda wake wa video kuchukuliwa na maafisa usalama, kuna memo iliyoandikwa kwa mkono na afisa wa Secret Services ambayo iliwahi kupatikana na kufanya Zapruder kuitwa kutoa ushahidi pindi Warren Commission ilipoundwa, meno hii iliandikwa siku ya tukio November 22, 1963 kutoka kwa Agent Maxwell D. Phillips kwenda kwa Agent James Rowley, Katika hiyo memo Agent Phillips anamueleza Agent Rowley kuwa "..kwa mujibu wa Mr. Zapruder, mdunguaji alikuwa nyuma ya Mr. Zapruder.."

Ikumbukwe kwamba Zapruder alikuwa anarekodi msafara akiwa kwa mbele (mbele ya msafara pambeni barabarani) na kipindi rais anapigwa risasi alikuwa karibia mkabala na gari la Rais. Kwa hiyo kuamini kwake kuwa mdunguaji alikuwa mahali fulani nyuma yake ilikuwa inathibitisha tena kwamba aliyemdungua Rais hakuwa juu ya ghorofa la Texas School Books Depository, Zapruder alipoitwa mbele ya Warren Commission aeleze kwa nini alihisi kuwa mdunguaji alikuwa mahali fulani nyuma yake, alisema kwamba alipokuwa anarekodi alipata fursa ya kuona kwa uzuri zaidi nini kilikuwa kinatokea. Kwanza aliona fuvu la mbele la rais linafumuliwa na kisha kichwa cha Rais kutupwa nyuma kwa kishindo kikubwa kuashiria kwamba risasi ilimpata kwa mbele.

Pia Zapruder akaeleza jambo ambalo pengine watu wachache waliokuwepo kwenye tukio waliliona, akasema kwamba… sekunde chache baada ya risasi iliyomdungua Rais, aliona kundi la maaskari wanakimbia kuelekea mahali fulani nyuma yake na aliamini kuwa nao wameng'amua kuwa mdunguaji alikuwa huko, ushahidi wa Zapruder una nguvu kubwa sana katika suala hili, kwani licha ya watu wengi kuwepo sehemu ambapo Rais Kennedy alidunguliwa kwa risasi lakini pengine yeye ndiye alifauatilia kwa umakini zaidi tukio hilo sekunde kwa sekunde na hata kulirekodi na mpaka leo hii kuwa ndio rekodi pekee ya video iliyopo juu ya tukio lile, Huyu bwana nitamuongelea kwa upana zaidi huko mbeleni na namna ambavyo alifarikia kwa "utata" miaka michache baadae, na si yeye pekee bali pia wenzake kadhaa ambao walikuwa watu muhimu sana kwenye kutatua kitendawili cha kifo cha Kennedy, watu kama Jack Ruby (aliyemuua Oswald hadharani) na Clay Shaw (asset wa CIA aliyeropoka kuhusu njama ya kumuua rais) nao walifariki vifo vya kutia shaka sana miaka michache baadae.

Mfano Zapruder alifariki kwa "kansa ya tumbo", Jack Ruby alifariki kwa " kansa ya kibofu", na Clay Shaw alifariki kwa "kansa ya pafu" ambayo ilienea kwenye ubongo na ini, Wote walipata hizi "kansa" miaka michache baada ya tukio na ndio ulikuwa muda ambao wananchi wamechachamaa nchini Marekani kutaka kujua ukweli wa nini kilitokea, Lakini maneno yake Zapruder kupitia ushahidi alioutoa mbele ya Warren Commission, yanaturejesha tena katika dalili zinazoonyesha na kuthibitisha kuwa kulikuwa na wadunguaji zaidi ya mmoja siku ile tofauti na serikali wanavyotaka tuamini.!!

Uhusiano wa kifo cha JF. Kennedy na operation ya Bay Of Pigs Invasion nchini Cuba...

Mara tu baada ya Fidel Castro kuchukua madaraka mwaka 1959, mwaka uliofuata yaani mwaka 1960, CIA kwa ruhusa ya Rais Dwight Eisenhower ambaye alikuwa anakaribia kuondoka madarakani walianzisha mikakati ya namna gani watamuondoa madarakani Fidel Castro, Fursa kuuu waliyoiona ni kutumia wahamiaji walioingia Marekani kutoka Cuba kukimbia utawala wa Fidel Castro uliokuwa "unafanya usafi" dhidi ya raia waliokuwa wanamuunga mkono Fulgencio Batista, Kwa hiyo CIA wakakusanya mamia ya raia hawa kwa siri kubwa na kuwapandikizia hari na ushaiwshi wa kutaka kumpindua Fidel Castro.

Mwezi March mwaka 1960 rais Dwight Eisenhower alipitisha bajeti ya dola milioni 13.1 kwa ajili ya mpango huu wa mapinduzi, Raia hawa wa Cuba waliokimbilia uhamishoni nchini Marekani wakapelekwa nchini Guatemala kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi hili kujiandaa na mapinduzi, Kikosi hiki kiliitwa Brigade 2506.

Mafunzo haya ya kijeshi yakaendelea kwa mwaka mzima nchini Guatemala, Mpango huu wa kuivamia Cuba na kumpindua Fidel Castro ulipangwa ufanyike mapema mwaka 1961 na ulikuwa umekamilika kila kitu lakini raisi Eisenhower hakuupa 'approval' na aliacha jukumu hilo la kuidhinisha uvamizi huo ifanywe na atakaye kuja kumrithi yaani Rais JF Kennedy, Kwa hiyo mara baada ya uchaguzi mkuu mwezi November, 1960 na hatimaye JF Kennedy kuapishwa January 20 mwaka 1961, kitu cha kwanza ambacho alikabiliana nacho ni CIA kumkabidhi mkakati ulioandaliwa na wao CIA chini ya Rais Dwight Eisenhower kuhusu uvamizi wa Cuba na kumpindua Fidel Castro.

Hapa ndipo ambapo kulianza kutokea mfululizo wa matukio ambayo huko mbeleni yalikuja kutengeneza uhasama mkubwa kati ya Rais Kennedy na CIA, katika jamii ya intelijensia, taarifa zinazoaminika ni kwamba CIA walipowasilisha mkakati wao wa mapinduzi ya Fidel Castro kuna vitu vingi vya msingi walimficha Kennedy, Na hii inaonekana kwamba walichukua 'advantage' kwa sababu ya ugeni wa Kennedy katika wadhifa wake huu upya wa Urais na kwa hiyo kutofahamu uhalisia wa vitu vingi kwa hiyo CIA wakatumia hiyo fursa 'kum-mislead' katika vitu muhimu kuhusu mkakati huo.

Mkakati ulikuwa ni mpana sana, lakini kwa ufupi ni kwamba, wavamizi hawa wa Brigade 2506 ilikuwa imepangwa wavamie Cuba wakitokea Guatemala na Nicaragua wakiwa na askari wa miguu pekee, Kennedy hakutaka Marekani ionekane ikihusika moja kwa moja kwenye uvamizi huo ili kulinda taswira yake katika jamii ya kimataifa na pia kuepuka kuamsha hasira za Urusi ambao walikuwa ni mshirika mkubwa wa Cuba, kwahiyo kukabiliana na hili, CIA walipendekeza kuwatumia makomando wake wa SAD katika kuongoza wapiganaji wa Brigade 2506, pamoja na hayo yote, Rais Kennedy alisisitiza sana kwamba ili kulinda taswira ya nchi ya Marekani yeye kama Rais hatoruhusu Marekani kufanya mashambulizi ya anga kusaidia katika mapambani hayo ya kumuondoa madarakani Fidel Castro.

CIA huku wakijua fika kwamba hawawezi kushinda uvamizi huo pasipo mashambulizi ya anga wakakubaliana na sharti la Rais Kennedy kwamba hakutakuwa na mashambulizi ya anga. Walikubali hili huku wakiwa na dhamira iliyojificha kwamba mara tu vita hiyo itakapoanza watamshinikiza Rais Kennedy atoe ruhusa ya kufanyika mashambulizi ya anga. Walikuwa wanaamini kwamba lazima Rais Kennedy atakubaliana na shinikizo lao pindi atakapoonyeshwa umuhimu wa mashambulizi ya anga pindi vita ikiwa inaendelea, na lazima atafanya hivyo ili kuepusha Marekani kuaibika kushindwa vita wanayoiunga mkono ili kulinda heshima yai ya kijeshi ambayo ilikuwa inahitajika kuliko kitu chochote katika kipindi hiki cha vita baridi.

Rais Kennedy aliidhinisha rasmi uvamizi huu siku ya tarehe 4 April 1961, takribani miezi mitatu tu baada ya kuingia madarakani, Wapiganaji wapatao 1400 wa Brigade 2605 waliogawanywa katika infantry batalioni zipatazo tano na paratrooper battalion moja waliingia katika pwani ya Cuba iitwayo Playa Girón kwa kutumia boti kutokea Guatemala na Nicaragua siku ya tarehe 13 April 1961, Baada ya uvamizi tu kuanza CIA wakaanza kuweka shinikizo kwa rais Kennedy aruhusu japo shambulio moja la anga la ndege za kivita za Marekani kuharibu miundombinu ya viawanja vya ndege za kijeshi vya Cuba. Kennedy alikataa katakata lakini CIA walipozidisha shinikizo na kumpa angalizo kuwa wasipofanya hivyo kuna uwezekano wa wapiganaji hao kushindwa kutekeleza mapinduzi ya kumuondoa Fidel Castro, Kennedy alilazimika na kuruhusu mashambulio ya anga kwa awamu moja pekee.

Hivyo basi tarehe 15 April 1961 ndege za kijeshi zilizo chini ya CIA aina ya B-26, zilishambulia viwanja vya ndege za jeshi la Cuba na hatimaye tarehe 16 April wapiganaji wa Brigade 2506 walivamia rasmi Cuba, Mwanzoni mwa uvamizi huu wapiganaji wa Brigade 2506 wakiongozwa na makomando wa SAD katika CIA walionekana kulidhibiti jeshi la Cuba ambapo mwanzoni mwa mapambano haya upande wa Cuba vikosi vya kijeshi vilikuwa vinaongozwa na José Ramón Fernández, Baada kuonekana kuwa jeshi la Cuba linazidiwa ujanja na wavamizi hawa waliokuja kufanya mapinduzi, Fidel Castro mwenyewe akaingia katika uwanja wa vita na kumuondoa José Fernández kwenye jukumu la kuongoza jeshi kwenye mapambano haya na kujipa yeye binafsi hilo jukimu la kuongoza wanajeshi.

Baada ya Castro kushikilia usukani wa kuongoza mapambano kwa upande wa jeshi la Cuba, wavamizi wa Brigade 2506 wakiongozwa na makomando wa Marekani walizidiwa ujanja na mbinu zote na wakaanza kupigwa kwa aibu kubwa, mpaka kufika tarehe 19 April, ilikuwa dhahiri kwamba ushindi uko upande wa vikosi vya Cuba, kwani walikuwa wanawapiga wavamizi kwa urahisi kana kwamba wanamsukuma mlevi, Ndipo hapa ambapo CIA wakarudi tena kwa rais Kennedy kutaka aidhinishe mashambulizi mengine ya anga, Safari hii Kennedy alikataa katakata, akidai kuwa dunia nzima itaona uvamizi huu imefanywa na Marekani na sio raia wa Cuba wanaoishi uhamishoni.

Kennedy alihofia kuwa kama Marekani itaingilia mapigano hayo kwa kiwango hicho, kulikuwa na uwezekano wa Urusi nayo kuingilia vita hiyo kusaidia upande wa Cuba, kutokana na mvutano mkubwa uliokuwepo baina yao, Kennedy alihofia kuwa ingeweza kuchochea vita nyingine kati ya Marekani na Urusi, vita ambayo ingeigharimu pande zote mbili na Dunia nzima kwa ujumla na pengine hata kusababisha vita kuu ya Tatu ya Dunia, kwa hiyo Kennedy safari hii akakataa katakata kuidhinisha mashambulio ya anga kwa kutumia jeshi la Marekani.

Joint Chiefs Of Staffs wakaja na pendekezo kwamba litengenezwe shambulio la uongo kwenye pwani ya Marekani na kisha kutupa lawama kwa Cuba ili kuhalalisha mashambulizi ya anga nchini Cuba, lakini bado pia Kennedy alishikilia msimamo wake kwamba hawezi kuidhinisha shambulio lolote la anga kufanywa na jeshi la Marekani, Hapa ndipo ambapo CIA iliumbuka, mkakati wao tangu awali ulikuwa ni lazima mashambulizi ya anga yafanyike kama ili kuweza kushinda mapigano na kuvishinda vikosi vya Castro na kumuondoa Madarakani. Lakini walimficha kitu hiki Rais Kennedy baada ya kumuona kuwa hasingeli idhinisha uvamizi huo kama wangemuweka wazi kuwa hawawezi kushinda pasipo mashambulio ya anga, Tegemeo lao la kumshawishi tena kwa mara ya pili yafanyike mashambulio ya anga ndio yalikuwa yamegonga mwamba.

Tarehe 20 April 1961, siku tatu baada ya uvamizi, wapiganaji waliipatowa mafunzo na kuongozawa na makomando wa Marekani, waliovamia nchini Cuba ili kumpindua Fidel Castro waliweka silaha chini na kusarenda kwa vikosi vya jeshi la Cuba, Ilikuwa ni aibu kubwa ambayo haijawahi kutokea katika historia ya jeshi la Marekani. Mateka waliokamatwa na vikosi vya Fidel Castro walihojiwa mubashara kwenye televisheni nchini Cuba na kutoa siri zote namna ambavyo Marekani ilihuiska katika uvamizi huo ambapo Marekani walikuwa wanatafuta sehemu ya kuficha nyuso zao kwa aibu, nchini Cuba taifa zima lilikuwa linasheherekea kwa shamra shamra kushangilia ushindi huo mnono. Fidel Castro aligeuka kuwa shujaa mpya wa Taifa na kujipatia heshima kubwa kimataifa kwa kushinda vita dhidi ya jeshi hatari la 'Marekani'.

Huko Marekani bado bundi alikuwa ndio kwanza ametua. Kila upande ulikuwa unamsukumia lawama upande mwingine, CIA walimuona Rais Kennedy kama ndio kisababishi cha wao kushindwa kutekeleza kwa ufanisi uvamizi na hatimaye kufanikisha kumuondoa madarakani Fidel Castro, Na kwa upande wa Rais Kennedy aliwaona CIA kama wasaliti kwa 'kumdanganya' na kutompa mkakati kamili tangu mwanzoni kwamba wasingelieweza kushinda vita ile pasipo mashambulizi ya anga, CIA wakamuona Rais Kennedy kama kiongozi ambaye si imara na shupavu au jasiri, na kwa muono wao walihisi kuwa hatoshi kuwa Rais wa Marekani.

Kwa upande wake Kennedy aliwaona CIA kama taasisi iliyopewa nguvu kiasi kwamba imelewa madaraka na kujiona wako huu ya kila kitu na kila mtu. Na moyoni mwake aliamini kuwa hilo linatakiwa kubadilika, Ikumbukwe pia kwamba hapa ilikuwa imepita miezi mitatu pekee tangu CIA wamuue Patrice Lumumba siku ya Tarehe 17 January, 1961 jimboni Katanga, Congo-Kinshasa, Kennedy anafahamika kuwa hakupendezwa na hili tukio lakini kwa kuwa lilitokea kabla hajawa Rais (siku tatu kabla) basi alilimezea mate lakini bado alibaki na kinyongo Kwa hiyo kufeli kwa uvamizi wa Bay of Pigs kuliamsha hasira zake zote alizonazo dhidi ya CIA.

Japokuwa katika umma na hata alipoongea na wanahabari Kennedy alikubali kubeba lawama zote kwa kuwa yeye ndiye aliidhinisha uvamizi huo, lakini pembeni akiwa faragha na wakubwa wenzake alikuwa anaotupia lawama kubwa CIA kuwa ndio waliosbabisha aibu kubwa hii iliyoipata Marekani na jeshi lake, Baada ya hapa mwenendo wa Kennedy ukaanza kubadilika mno. Mwanzoni alipoingia madarakani alikuwa ni tegemezi mno kwa kupatiwa muhtasri wa hali ya usalama wa nchi (Daily Presidential Briefing) kutoka kwa vyombo vya Ujasusi hasa CIA, lakini baada ya tukio la kufeli kwa uvamizi wa Cuba hakutaka tena kupatiwa briefing na CIA badala yake briefings zake zote sasa alizipokea kutoka kwa washauri wa usalama wa taifa (National Security Advisors).

Lakini hakuishia hapo tu, Kennedy kuonesha ni namna gani alikasirishwa alienda mbali zaidi kufanya kitendo ambacho kilipingwa na maafisa wengi wa CIA na wanazi wao, Kennedy alimfuta kazi Mkurugenzi Mkuu wa CIA Bw. Allen Dulles, Katika ulimwengu wa Intelijensia unapomuongelea Allen Dulles hamuongelei tu jasusi, bali ni jasusi mkongwe na mzoefu na wa kiwango cha daraja la kwanza kabisa na mwenye heshima iliyotukuka, Allen Dulles ndiye Mkurugenzi wa CIA aliyetumikia kwa kipindi kirefu zaidi katika historia ya Taasisi hiyo mpaka leo hii (tangu 1953 mpaka 1961), Allen Dulles ndiye aliyesimami mapinduzi ya Waziri mkuu wa Iran miaka ya 1940s (Operation Ajax), Allen Dulles ndiye aliyesimamia mapinduzi ya Rais wa Guatemala mika 1950s, Allen Dulles ndiye aliyesimamia program ya ndege za kijeshi ya Lockheed U-2, Pia huyu ndie aliye simama operation Barracuda iliyo ratibu kifo cha Patrice Lumumba wa Kongo DRC.

Allen Dulles ni kaka wa John Dulles, waziri wa mambo ya nje wa Marekani (Secretary of State) wakati wa utawala wa Rais Dwight Eisenhower ambaye ndiye amerithiwa na Kennedy miezi mitatu iliyopita, kwa hiyo inahitaji kujitoa ufahamu kumgusa mtu kama Allen Dulles. Na Kennedy alijitoa ufahamu na kumfuta kazi Allen Dulles mtu ambaye anapendwa na kuhusudiwa na majasusi wa CIA pengine kushinda hata Kennedy mwenyewe, Karatasi ya juu ya ripoti rasmi ya CIA ambayo ndani yake kuna baadhi ya paragraph zikionyesha kuwa CIA hawakuridhishwa na namna ambavyo Kennedy alifanya maamuzi juu ya kukataa mashambulio ya anga

Kennedy hakuishia hapa tu… akiwa faragha na wakubwa wenzake alitamka kauli iliyokuja kuwa maarufu sana hapo baadae baada ya kuvuja, alisema hivi, namnukuu; "…i want to splinter CIA in a thousand pieces and scatter it to the wind.." (Nataka kuivunja vunja CIA kwenye vipande elfu na kuipeperusha kwenye upepo), Akiwa na maana kwamba, amedhamiria kuibomoa CIA taratibu sana kipande kimoja baada ya kingine mpaka taasisi hiyo ipotee yote na isiwepo, Kauli yake hii, ilikuwa ni kana kwamba alikuwa ametia sahini ya kifo chake mwenyewe.

Unaweza kuunganisha Dots kupata majawabu stahiki kuhusu tukio la kifo cha JF.Kennedy lilisababisha na akina nani! Pia unaweza kugundua kuwa kuna jmbo kubwa zaidi linafichwa nyuma ya pazia na unaweza kuelewa kuna wahusika halisi wa kifo cha Kennedy ni wapi na kwa nini waliamua kumuua Kennedy??...

Sasa turudi kwenye Warren commission...

Katika ripoti ya The Warren Commision, ile kamisheni iliyoundwa na Rais Lyndon B. Johnson kuna mahala inasema kwamba kuna mtu ambaye alijitambulisha kama "Clay Bertrand" alimpigia simu Dean Andrews Jr. ambaye alikuwa ni mwanasheria wa kujitegemea kwenye jimbo la New Orleans kumtaka apande ndege kwenda Dallas kumtetea Lee Harvey Oswald, lakini wajumbe wa Warren Commision wanadai kwamba walihangaika mno bila mafanikio na hawakujua huyu "Clay Bertrand" ni nani na wakafanya hitimisho kwamba hili halikuwa jina halisi bali ni 'alias' ambayo ilitumiwa tu na huyo mtu.

Ilipofika mwaka 1967 mwezi March… mwanasheria wa serikali wa New Orleans wa kipindi hicho aliyeitwa Jim Garrison alifanikiwa kung'amua huyu "Clay Bertrand" ni nani haswa, Bw. Garrison aligundua kwamba kuna mfanya biashara maarufu sana ambaye alikuwa anatumia "alias" hiyo kwenye jumuiya za watu wanaojihusisha na mambo ya ushoga, Mfanyabiashara huyu maarufu sana miaka hiyo alikuwa anaitwa Clay Shaw, Huyu alikuwa ni muanzilishi wa shirika la International Trade Mart, ambapo shirika hili lilikuwa na lengo kuu la kuchochea biashara ya kimataifa na makao makuu yao yalikuwa ni New Orleans, Vile vile nchini Italy Clay Shaw alikuwa ni mjumbe wa bodi ya kampuni ya CMC (Centro Mondiale Commerciale) ambayo ilikuwa ni 'subsidiary' ya kampuni mama inayoitwa Permindex (Permenent Industrial Expositions).

Sasa katika ulimwengu wa Espionage na hata mambo ya uhalifu kuna kitu kinaitwa 'front organisations'. Hizi ni kampuni ambazo zinaanzishwa kwa siri na idara ya kijasusi kwa lengo la kutekeleza maslahi yake pasipo idara husika ya kijasusi kujulikana, Hizi ndizo zilikuwa ofisi za International Trade Mart Organasation huko New Orleans.

Kwenye miaka ya hivi karibuni baada ya uchunguzi wa kina na nyaraka nyingi kuvuja imethibitika kwamba kwenye miaka ya 1960s na 1970s, CMC na Permindex zilikuwa zinatumiwa kama 'front organisation' za CIA kwenye nchi ya Italy. Kampuni hizi zilikiwa zinatumika kwa lengo kuu la kupitisha fedha kutoka CIA nchini Marekani na kwenda nchini Italia kugharamia mikakati ya kumuondoa madarakani Rais wa Italia kipindi hicho Bw. Charles de Gaulle ambaye alikuwa na sera za kufungamana mno na urusi na kupinga vikali siasa za kimagharibi, Katika bodi hiyo hiyo ya kampuni ya Permindex (na CMC) pia kulikuwa na mjumbe mwingine wa bodi aliyeitwa Loius Bloomfield.

Huyu alikuwa ni msomi wa hali ya juu na mfanyabiashara maarufu kutoka Canada ambaye kipindi cha uhai wake alionekana na wengi kama kiongozi wa jamii ya Wayahudi nchini Canada, Lakini ikumbukwe kwamba, Louis Bloomfield wakati wa vita kuu ya pili miaka ya 1940s aliitumikia idara ya kijasusi ya kimarekani iliyoitwa Office of Strategic Services. Idara hii ndio baadae (baada ya vita kuu ya pili) ilibadilishwa jina na kuitwa Central Intelligence Agency - CIA ambayo tunayo mpaka sasa, kwa maneno mengine mjumbe huyu wa bodi ya Permindex alikuwa ni jasusi nguli na hata kampuni yao hiyo (Permindex na CMC) kama ambavyo nimeeleza zilikuwa ni 'front organisation' za CIA.

Kwa hiyo basi kitendo cha mfanyabiashara maarufu Clay Shaw ambaye mwanasheria wa serikali Bw. Garrison aling'amua ndiye huwa anatumia a.k.a ya "clay bertrand"… kitendo chake cha kuwa pia mjumbe wa bodi ya CMC na Permindex inadhihirisha mafungamano yake na CIA na shughuli za kijasusi.

Hivyo basi….

Bila kuogopa mafungamano ya Clay Shaw na CIA, mwanasheria mkuu wa New Orleans Bw. Jim Garrison alimkamata Clay Shaw siku ya March 1, 1967 na kumfungulia mashtaka ya kupanga njama ya kumuua Rais Kennedy. Katika hati yake ya mashataka, Bw. Garrison alieleza pia kinaga ubaga kuwa CIA wamehusika pia kwenye tukio hilo, Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, Bw. Garrison alieleza mahakama sio tu kwamba Clay Shaw ndiye mwenye kutumia alias ya "Clay Bertrand" ambaye alikiwa anatafutwa miaka yote… bali pia alimleta shahidi wake aliyeitwa Perry Russo ambaye alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa masuala ya Bima.

Shahidi huyo alieleza mahakama kuwa alihudhuria tafrija nyumbani kwa bwana mmoja anaitwa David Ferrie ambaye anajulikana kuwa moja ya wapinzani wakubwa wa utawala wa Fidel Castro, shahidi akaeleza kuwa akiwa kwenye tafrija hiyo kwa bahati mbaya aliwasikia Clay Shaw, David Ferrie na watu wengine wachache ambao hakuwatambua walikuwa wamekaa chemba wakipeana maelekezo fulani kuhusu mpango huo.

Kesi hii iliunguruma kwa muda wa miaka miwili mfululizo. Lakini ajabu ni kwamba siku ya tarehe 1, March 1969…. Baraza la wazee wa mahakama (Jury) walikaa kwa muda wa chini ya nusu saa na kutoa uamuzi wa pamoja wa kumuachia Clay Shaw kuwa huru dhidi ya mashtaka yote hayo, Hii ilikuwa habari njema kwa CIA lakini umma ulijawa na hasira na hasira hizi walizielekeza moja kwa moja kwa Clay Shaw, Mwaka 1974 siku ya tarehe 15 August… Clay Shaw alifariki kwa "Kansa ya Mapafu", Kama ambavyo Jack Ruby (yule aliyempiga risasi Oswald) naye alifariki kwa "Kansa ya Mapafu" akiwa gerezani.

Na msururu mrefu wa kila ambaye alionekana kujua uhalisia wa mauaji ya Kennedy alifariki muda mchache tu katika mazingira ambayo yanazua maswali mengi.

Tukio hili la mauaji ya Rais JF Kennedy, CIA hawawezi kuruka ukweli kwamba mikono yao ilimwaga damu yake, na kwasababu hiyo hata kifo cha ndugu yake JFK aliyeitwa Robert Kennedy maarufu kama "Bobby" ambaye kipindi cha utawala wa kaka yake JFK… yeye (Robert) alikuwa mwanasheria mkuu wa Marekani na kipindi anauwawa alikuwa kwenye kampeni za Urais ambazo zilikuwa na kila dalili ya kushinda kiti hicho.

CREDIT/ACKNOWLEDGEMENT:
Chanzo kikubwa cha makala hii hasa simulizi za kifo cha JF. Kennedy inatoka kwa Mchambuzi na Mwandishi wa makala za Kijasusi ndugu Habib Anga "The Bold" inayokwenda kwa jina "UTATA JUU YA KIFO CHA JF.KENNEDY" aliyo ichapisha Jamii Forum kwa mara ya kwanza tarehe 07/05/2017.

Chanzo kingine ni kutoka taarifa za FBI zilizotolewa mwaka 1971 na 2016, na Declassified information za CIA za mwaka 1985, 1998, 2011 na 2017.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

images%20(2).jpeg
FB_IMG_1590666918880.jpeg
FB_IMG_1590666935112.jpeg
tapatalk_1590651827695.jpeg
tapatalk_1590651823530.jpeg
tapatalk_1590651831960.jpeg
tapatalk_1590667618940.jpeg
tapatalk_1590675312573.jpeg
Screenshot_20200528-210851.jpeg
Screenshot_20200528-210805.jpeg
Screenshot_20200528-210618.jpeg
 
Hii stori nimeanza kuisoma jana usiku sa 9 sikuimaliza, nimekuja kuendelea kuisoma saa 3:45 na kuimalizia saa 11:41

Kongole kwa makala safi yenye uchambuzi wa kina uliotulia, usichoke kutuletea vitu vipya vingine
 
Na Comred Mbwana Allyamtu
Thursday-28/05/2020
Marangu, Kilimanjaro- Tanzania.

John Fitzgerald "Jack" Kennedy ndiye rais wa kwanza wa marekani kuzaliwa karne ya 20, na ndiye rais pekee wa Marekani kuwa muumini wa dhehebu la katoliki, raisi Jonh Fitzgerald "Jack" Kennedy aliuwawa tarehe 22,11, 1963 huko Jimbo la Texas katika mji wa Dallas kwa kupigwa risasi na mtu aliyekuja kutambulika kwa jina la Lee Harvey Oswald, japo hakuna ushahidi wowote ulioonesha Oswald kuhusika, ntalieleza hili mbeleni.

Kennedy ndie rais wa pili Marekani kuchaguliwa akiwa na umri mdogo katika orodha ya marais walio wahi kuhudumu kwenye nafasi hiyo, Jonh Fitzgerald Kennedy alichaguliwa kuwa rais akiwa na umri wa miaka 43 na siku 236. Rais alieingia madarakani akiwa na umri mdogo zaidi ni rais wa 26 aliyeitwa Theodore Roosevelt ambae alikuwa raisi baada ya kuuwawa mtagulizi wake William McKinley.

Theodore Roosevelt alikalia kiti cha uraisi akiwa na umri wa miaka 42 na siku 322. Theodore Roosevelt ndie rais mdogo kukalia kiti cha uraisi huku Jonh Fitzgerald Kennedy ndie rais mdogo zaidi kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani....(The youngest person to assume the office was THEODORE ROOSEVELT, who became president following William McKinley's assassination, at the age of 42 years, 322 days. The youngest person elected president was JOHN F. KENNEDY, who was inaugurated into office at the age of 43 years, 236 days.)

John Fitzgerald Kennedy alizaliwa tarehe 29 Mei 1917 huko Brookline, Massachusetts, Marekani, kwenye familia ya kitajiri, ambapo baba yake mzazi aliitwa Joseph P. Kennedy ambae aliwahi kuwa Meya wa Boston na Mama yake Rose Fitzgerald Kennedy, JF. Kennedy mwenyewe alikuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 1961 hadi alipouawa tarehe 22,11, 1963 huko jijini Dallas Jimbo la Texas Marekani, John F. Kennedy alikuwa ni raisi wa 35 wa Marekani huku Makamu wake wa Rais alikuwa akiitwa Lyndon B. Johnson (ndie alie mrithi urais baada ya kifo chake, tutaona huko baadae) Jonh F. Kennedy aliapishwa kuwa raisi wa Marekani rasmi tarehe 20 januari 1961 kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Dwight D. Eisenhower ambae alikuwa ni raisi wa 34 wa Marekani.

Baada ya kifo chake mnamo tarehe 22 Novemba 1963 kwa kupigwa risasi, Kennedy alikuwa na umri wa miaka 46 na mwili wake ulizikiwa kwenye makaburi ya Arlington National Cemetery, huko Washington DC, John Fitzgerald Kennedy alifunga ndoa na mwanamke mrembo alieitwa Jacqueline Bouvier mwaka 1953 na kubahatika kupata watoto wanne ambao ni Arabella Kennedy, Caroline Kennedy, John F. Kennedy Jr. na Patrick Bouvier Kennedy.

J F. Kennedy alijiunga na Chuo Kikuu cha Harvard na kumaliza masomo mwaka 1940 akichukua Shahada ya mahusiano ya Kimataifa, pia aliwahi jiunga na Chuo Kikuu cha Stanford Lakini aliachia njiani na kujiunga na Jeshi la Marekani mwaka 1941. Jeshini alitumikia ngazi mbalimbali na mpaka anaondoka Jeshini alikuwa na cheo cha Luteni (Lieutenant) na pia alipokea tuzo nyingi hasa mara baada ya vita kuu ya pili ya dunia na hapo ndipo hapo alianza safari yake ya kisiasa.

Mnamo 03 Januari 1947 hadi 03 Januari 1953 alikuwa Mbunge/Mwakilishi wa Wilaya 11 zinazounda Jimbo la Massachusetts na kati ya 03 Januari 1953 hadi 22 Disemba 1960 alikuwa Seneta wa Jimbo la Massachusetts, mnamo 02 Januari 1960 JFK alitangaza rasmi nia yake kugombea Urais kupitia chama chake cha Democratics, pia katika mbio hizo, Lyord Johnson (ambaye alikuja kuwa Makamu wa Rais wake) alitangaza nia ya kugombea Urais.

JF.Kennedy alipingwa na baadhi ya wakongwe wa Chama chake wakidai kuwa hakuwa na uzoefu pia umri wake ulikuwa mdogo, mmoja wa waliompinga ni aliyekuwa rais Mstaafu kwa wakati huo Harry Truman (Rais wa 33 wa Marekani) na wengine wenye nguvu, baadhi yao walimpinga kwa kuwa sera zake zilipingana na Wamarekani wengi walimhusisha kuchanganya masuala ya dini/Kanisa lake la Katoliki na ya nchi na yeye alipinga vikali kwa kusema yeye hasimami kama mgombea urais wa Katoliki bali anasimama kama mgombea Urais wa Democratic na kamwe asingechanganya Kanisa na masuala ya Umma.

J F. Kennedy aliahidi kuleta haki sawa baina ya weupe na weusi (Hiki ndiyo kipindi watu weusi walipamba moto kudai haki zao) pia katika kuleta mahusiano mazuri na Umoja wa nchi za Kisovieti (USSR) pamoja na vita ya Vietnam, licha ya kuwekea vikwazo vingi, J F..Kennedy alimshinda mpinzani wake Richard Nixon wa Republican, huku yeye Kennedy akipata kura 49.7% na Richard Nixon alipata kura 49.5%, na kupata kura za wachaguzi wa majimbo (Electral College) 303 na huku mpinzani wake Richard Nixon akipata 219, matokeo hayo yalimuibua J F Kennedy kuwa mshindi kwenye uchaguzi huo.

JF. Kennedy Baada ya kuwa raisi wa Marekani hakuudumu kwa muda mrefu kwani aliuawa mapema tu mwaka 1963, utawala wake Kennedy ulihudumu kwa siku 1,306 tu , kati ya 20 Januari 1961 hadi 22 Novemba 1963 siku ambayo ni siku ya kifo chake alipokuwa Dallas huko Texas. Ukweli kuhusu kifo cha kennedy bado ulikuwa kitendawili juu ya nini haswa waliohusika katika kupanga na kutimiza lengo hilo, Oswald aliuawa siku chache tu baada ya kifo cha kennedy pia kulizima kabisa kupata ukweli juu ya waliohusika na kupanga mauaji hayo.

Miongoni mwa vitu vilivyoshangaza walimwengu ni kuwa kabla ya kutekelezwa kwa mauaji hayo Oswald alipiga simu kitengo cha upelelezi FBI na kuwaatarifu kuw yeye ni mmoja wa waliopanga kumuua rais Kennedy hata hivyo FBI hawakutilia mkazo taarifa hizo mpaka pale lilipotekelezwa shambulizi hilo baya kuwahi kutokea nchini Marekani karne ya 20, baadhi ya watu wanasema kuwa viongozi wa Cuba,Urusi na Vietnam ndio waliopanga mauaji hayo licha warusi walishakiri wao wenyewe kuwa walistushwa sana na kifo cha kiongozi huyo.

Makundi na magenge ya wahalifu wa Kimafia ni miongoni mwa watu walihusihswa na kifo cha rais JF kennedy, pia uhasama baina ya marekani na mataifa ya Cuba,Korea kaskazini, Urusi na Vietnam ulihusishwa kwa kiasi kikubwa kuwa ndio walipanga na kutekeleza mauaji hayo kwa JF Kennedy, taarifa za kichunguzi zaidi ya 3,100 juu ya mauaji ya JF Kennedy zimetolewa hadharani kwa wananchi tangu 2017 ili angalau kuwafungua akili zao juu ya kifo cha rais wao mpendwa, taarifa hizi zilifanywa kuwa siri kubwa za kitaifa kwa mda wote huo wa miiaka 56 mpaka sasa.

Sasa turudi kwenye tukio lenyewe lenye utata juu ya kifo cha JF. Kennedy......

Mwenzi June mwaka 1963 saa 9:45 asubuhi kulimalizika kikao maalum katika ikulu ya White house kikao hiki kiliwakutanisha raisi Kennedy, makamu wa Rais Lyndon B. Johnson na Gavana Connally kujadili mgogoro uliokuwepo baina ya Raph Yarborough na Don Yarborough dhidi ya Gavana wa jimbo la Texas wa Republican Bw. John Connall, hivyo Connall alialikwa ikulu kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wao, makubaliano yalifikiwa kuwa raisi Kennedy angepaswa kwenda Texas mwezi november kuwasuluhisha.

Mwenzi November mjini Dallas City......

Siku hii Rais Kennedy alikuwa amefika jimboni Texas hapa kwa ajili ya ziara fupi maalumu na mahsusi ili kwenda kusuluhisha mvutano uliokuwepo kati ya wanachama wa Democrat Bw. Raph Yarborough na Don Yarborough dhidi ya Gavana wa Republican Bw. John Connally (nitaeleza huu mgogoro ulihusu nini), Safari hii ya Rais Kennedy kutembelea jimbo la Texas ilikuwa imepangwa na kukubaliana tangu mwezi June ambapo Kennedy, makamu wa Rais Lyndon B. Johnson na Gavana Connally walipokutana kwenye kikao mwezi June mwaka huo 1963 kule Washington DC katika ikulu ya White house.

Safari hii ya Kennedy jimboni Texas ilikuwa na malengo makuu matatu.
Mosi, alikuwa anataka kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya kuongeza michango katika mfuko wa kampeni.
Pili, alikuwa anaweka mkakati kwa ajili ya uchaguzi uliokuwa unafuata mwaka mmoja baadae, yaani mwezi Novemba mwaka 1964.
Na tatu, Kennedy alikuwa anataka kujiimarisha zaidi katika jimbo la Texas kwa kuwa alipata ushindi mwembamba sana jimboni hapo na alikuwa na ushawishi Mdogo sana kwenye hili jimbo na hata kwenye eneo la Dallas alikuwa amegalagazwa kipindi cha uchaguzi.

Kwa hiyo licha ya nia yake ya kwenda kusuluhisha mgogoro ndani ya chama cha Democrat lakini pia alikuwa na malengo makuu hayo matatu.

Safari ya Kennedy kutembelea Texas ilitangazwa rasmi kwa umma mwezi September mwaka 1963, Mpangilio wa ruti ambayo msafara wake utapita ulikamilika kupangiliwa tarehe 18 Novemba na kutangazwa asububi ya Novemba 22 ili wananchi wajitokeze barabarani kumlaki, Taarifa ya Ikulu ambayo iliwasilishwa kwa Secret Services ilionyesha kwamba ndege ya Rais itaruka kutoka uwanja wa ndege wa kijeshi wa Carswell Airforce Base maeneo ya Fort Worth na kwenda kutua uwanja wa Dallas Love Field.

Baada ya hapo Rais Kennedy alikuwa anatakiwa kusafiri kwa msafara wa gari kutoka uwanja wa Dallas Love Field na kuelekea eneo la Dallas Trade Mart ambako Kennedy alitarajiwa kupata chakula cha mchana na wenyeji wake, Ruti hii ilipangwa na kupendekezwa na rafiki mkubwa wa Kennedy aliyeitwa Kenneth O'Donnell ambaye alikuwa pia ndiye katibu wake aliyehusika na masuala ya teuzi za watumishi wa ngazi za juu serikalini.

Ruti hii iliyokuwa inapendekezwa (kutoka uwanja wa ndege wa Dallas Love Field mpaka Dallas Trade Mart) ambayo ilikuwa na urefu wa kilomita 16 ilikuwa inategemewa kuchukua takribani dakika 45 kwa mwendo wa taratibu ili kumpa nafasi Kennedy kuwasabahi wananchi kwa kuwapungia mkono, Ratiba hii pamoja na ruti inayopendekezwa iliwasilishwa ofisi ya Secret Services ambapo maafisa walioehusika nayo kuipokea na kuiwekea mkakati wa kiusalama walikuwa ni Special Agent Winston G. Lawson ambaye alikuwa ni 'advance Secret Services agent' (afisa ambaye yuko kwenye Whitehouse Detail kwa ajili ya kumlinda Rais moja kwa moja) Pia alikuwa pamoja Agent Forrest V. Sorrels ambaye huyu ni Special Agent ambaye anahusika na ofisi ya Secret Services eneo la Dallas, Maafisa usalama hawa wawili walikutana mara kadhaa kuweka mkakati wa kiulinzi kwa ajili ya safari hii ya Rais ya Novemba 22.

Moja ya vikao vyao hivyo walikifanya tarehe 14 Novemba kwenye uwanja wa ndege wa Dallas Love Field ambapo baada ya kikao waliendesha gari pamoja kupita njia ile ambayo imependekezwa msafara wa Rais uje kupita wiki moja baadae, Siku hii ya tarehe 14, maafisa hawa walipokuwa wanaendesha gari kupita kwenye hii ruti inayopendekezwa kuna jambo waliliona, jambo ambalo liliwashitua kidogo na kuwafanya waingie wasiwasi juu ya hii ruti inayopendekezwa. Endapo jambo hili lingezingatiwa, basi Kennedy asingeuwawa wiki moja baadae!

Swali kwanini waliingiwa na wasiwasi baada ya kuona hicho walichokiona lakini bado msafara wa Kennedy ukapita ruti hii hii wiki moja baadae??....... Au swali la msingi zaidi waliona kitu gani?... (Tutaona kitu hicho ambacho maafisa usalama hao walicho kutilia shaka huko mbeleni.......

ALHAMISI YA NOVEMBA 21......

Rais John Kennedy na mkewe Jackie Kennedy wanawasili na Airforce One jimboni Texas katika uwanja wa ndege wa Carswell, katika viunga vya Fort Worth, Rais na mkewe walikuwa wanatokea Santo Antonio, Huston ambako mchana Kennedy alihutubia katika chuo cha matabibu ya Jeshi la Anga kwenye kituo cha Brooks Airforce Base na Jioni yake alitoa hotuba katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika Rice Hotel ambapo kulikuwa na kumbukumbu ya kifo cha Mbunge mashuhuri wa bunge la Congress aliyeitwa Albert Thomas.

Siku hii ya alhamisi Rais Kennedy na mkewe waliwasili Texas majira ya saa 5 na dakika 7 usiku na kupokelewa uwanja wa ndege na Raymond Buck rais wa Fort Worth Chamber of Commerce, Pia katika ndege nyingine iliyombeba makamu wa Rais Lyndon B. Johnson walikuwa amefuatana na Gavana wa Jimbo la Texas, John Connally pamoja na hasimu wake mkubwa Seneta Ralph Yarborough.

Msafara wa Rais uliondoka uwanja wa ndege kupitia West Freeway ambapo licha ya kuwa ni muda wa usiku sana na mvua ilikuwa inanyesha, wananchi wengi walijitokeza na kujipanga barabarani kumpingia mikono, Walifika Hotel Texas majira ya saa 5 na dakika 34 usiku, ambako katika hoteli hii ndipo ambapo Rais Kennedy na mkewe walilala kwa usiku huo.

IJUMAA, NOVEMBA 22.......

Siku hii ya Ijumaa ilianza mapema sana kwa Rais Kennedy kwa shughuli muhimu asubuhi na mapema, Saa 2 na dakika 45 asubuhi, Rais Kennedy akiwa amefuatana na Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson, pamoja na Mbunge wa Congress Jim Wright pamoja na Seneta Yarborough alikuwa anaongea na wananchi eneo la Eighth Street na katika hotuba yake hiyo aliimwagia sifa sekta ya usafirishaji wa anga ya jimbo la Texas.

Baadae majira ya saa 3 na dakika 10 Rais Kennedy alikuwa amesharejea hotelini kwake na alikuwa anatoa hotuba kwa wageni maalumu waalikwa katika ukumbi wa Hoteli, Mkewe Jackie alichelewa na kuwasili dakika 15 baadae akipokelewa kwa makofi ya kishindo kutoka kwa wageni waalikwa, Baada ya Rais Kennedy kumaliza hotuba yake fupi, swahiba wake mkubwa Kenny O'Donnell ambaye pia alikuwa ni katibu wa teuzi za Rais, alimfuata Roy Kellerman Afisa kiongozi wa Secret Services juu ya Safari ya Rais (Secret Service In charge).

Maagizo haya ambayo O'Donnell alimpa Agen Kellerman, ni kwamba alikuwa anamtaka awasiliane na Maafisa wenzake walioko Dallas ambako Kennedy alikuwa anaelekea na kuwataarifu kuwa kama hakukuwa na mvua basi anataka gari itakayombeba Rais iondolewe paa juu (liwe wazi) ili kumpa rais fursa ya kuonekana vyema na wananchi na kupungiana mikono, Msafara wa Rais Kennedy uliondoka Hotel Texas majira ya kama saa 5 na dakika 10 asubuhi na majira ya saa 5 na dakika 23 Airforce One iliruka kutoka uwanja wa ndege wa Carswell kwenye viunga vya Fort Worth na kuelekea Dallas.

Airforce One ilitua Dallas kwenye uwanja wa Love Field majira ya saa 5 na dakika 38, Makamu wa Rais Johnson na Gavana Connally wao walikuwa wamewasili kabla ya Rais Kennedy, kwahiyo Airforce One ilipotua na kumshusha Rais na mkewe walilakiwa na Makamu wa Rais na Gavana wa Texas, Msafara wa Rais Kennedy, Mkewe Jackie Kennedy, Makamu wa Rais, Gavana Connally na Seneta Yarborough uliondoka uwanja wa ndege wa Love Field majira ya saa 5 na dakika 55 asubuhi.

Msafara ulikiwa unatarajiwa kupitia katikati ya mji wa Dallas na kuwasili Dallas Business and Trade Mart majira ya saa 6 na dakika 15 mchana, Msafara ulishika njia kuingia kati kati ya mji majira ya saa 5 na dakika 59…. Pasipo kujua, zilikuwa zimebaki dakika 31 tu za maisha ya Rais JF Kennedy.

DOWNTOWN DALLAS.......

Msafara wa Rais ulipokamata barabara kuingia katikati ya mji wa Dallas kuelekea Trade Mart ulikuwa kwenye mpangilio ufuatao;

- Gari ya Mbele

Gari ya mbele kabisa iliyokuwa inaongoza msafara ilikuwa ni gari aina ya Frord Mercury sedan, aliyekuwa anaendesha gari hii alikuwa ni mkuu wa Idara ya polisi katika mji wa Dallas ambaye aliitwa, Jesse Curry, Katika siti ya mbele ya mkono wa kulia alikuwa ameketi Afisa wa Secret Services, Special Agent Winston, Siti ya nyuma ya gari hii mkono wa kushoto alikuwa ameketi Bill Decker, Sheriff wa mji wa Dallas na siti ya mkono wake wa kulia alikuwa ameketi afisa mwingine wa Secret Services, SAIC Forrest Sorrels (SAIC - Special Agent In Charge).

- Gari ya Rais

Gari hii ambayo Rais Kennedy alipanda ilikuwa ni aina ya Lincoln Continental Convertible ya mwaka 1961, ambayo imeboreshwa ili kukidhi masuala ya kiusalama ilikuwa inaendeshwa na afisa wa Secret Services, Agent William Greer. Pembeni yake katika siti ya mbele alikuwa ameketi afisa mwingine wa Secret Services, ASAIC Roy Kellerman (ASAIC - Assistant Special Agent In Charge), huyu ndiyo yule afisa ambaye alipewa maagizo na O'Donnel swahiba wa Kennedy na katibu wake anayeshughulika na masuala ya Teuzi, kuwa kama hakutakuwa na mvua mjini Dallas basi ahakikishe kuwa gari atakayopanda Rais inakuwa wazi bila paa la juu ili kuwarahisishia wananchi kumuona Rais kwa uzuri na kupungiana mikono, Siti ya nyuma (kati za kati kati) mkono wa kulia alikuwa amekaa Gavana Connally huku mkono wake wa kushoto akiwa amekaa mkewe Nellie Connally, Siti za nyuma kabisa za gari hii ya wazi, mkono wa kulia alikuwa ameketi Rais Kennedy huku mkono wake wa kushoto akiwa ameketi mkewe Jacqueline Kennedy.

Pembezoni/ubavuni mwa gari ambalo alikuwa amepanda Rais Kennedy, kulikuwa na pikipiki mbili za Polisi kila upande, ambapo mkono wa kushoto kulikuwa na piki piki zilizoendeshwa na Polisi wa kituo cha mji wa Dallas, ofisa Billy Joe Martin na ofisa Bobby Hargis, Upande wa kulia kulikuwa na pikipiki zilizoendeshwa na ofisa James M. Cheney na ofisa Douglas L. Jackson.

- Gari ya nyuma ya Rais (follow up car)

Nyuma ya gari aliyopanda Rais Kennedy kulikuwa na gari aina ya Cadillac Touring Convertible ambayo iliwabeba maafisa wa Secret Services kwa ajili ya ulinzi wa Rais na First Lady, Dereva wa gari hili alikuwa ni Agen Sana Kinney. Pembeni yake siti ya mbele kulia aliketi ATSAIC Emory Roberts (Assistant To Special Agent In Charge), Katika mlango wa mbele mkono wa kushoto, kwenye mlango alikuwa ananing'inia Special Agent Clint Hill, ambaye anahusika na ulinzi wa First Lady, Kwenye mlango mwingine wa mbele kulia alikuwa ananing'inia Special Agent Jack Ready, Mlango wa nyuma kulia alikuwa ananing'inia Special Agent Paul Landis huku mlango wa mkono wa kushoto alikuwa ananing'inia Special Agent William T. McIntyre.

Ndani ya gari siti ya nyuma walikuwa wameketi watu wanne. Kulikuwa na Kenneth O'Donnell msaidi wa rais na katibu wake wa masuala ya teuzi, pia kulikuwa na David Powers ambaye naye ni msaidizi wa Rais na pambeni yao hawa mkono wa kulia aliketi Special Agent Glen Bennet na mkono wa kushoto aliketi Agent George Hickey.

- Gari ya makamu wa Rais

Nyuma ya gari iliyowabeba maafisa usalama wa ulinzi wa Rais ilifuata gari iliyombeba makamu wa Rais Lyndon B. Johnson, Gari hii aina ya Lincoln Convertible ilikuwa inaendeshwa na Hurchel Jacks, afisa wa Polisi wa kituo kikuu cha Dallas. Pembeni yake mkono wa kulia alikuwa ameketi ASAIC Rufus Youngblood (Assistant Special Agent In Charge), Siti ya nyuma walikuwa wamekaa Seneta Ralph Yarborough (kushoto), Lady Bird Johnson (kati kati) na kulia alikuwa ameketi Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson.

Gari iliyombeba makamu wa Rais kulikuwa na gari ya maafisa wa Secret Service maalumu kwa ajili ya ulinzi wa Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson (VP followup car), Nyuma ya VP followup Car kulikuwa na gari ya Mayor wa Dallas, iliyombeba Mayor Earle Cabell na mkewe Elizabeth Cabell.

Nyuma yao kulikuwa na gari iliyowabeba waandishi wa habari kutoka vituo vikuvwa vya kitaifa (National Press Pool), Nyuma ya gari hii zilifuata gari nyingine tatu za watu wa Picha (Camera Cars), ambazo zilibeba wapiga Picha za video, picha za mnato na waandishi wa habari wenyeji wanaofanyia kazi vyombo vya habari jimboni Texas, Nyuma ya gari hii tatu kulikuwa na gari nyingine tatu zilizowabeba wabunge wote wa Congress kutoka jimbo la Texas, Na mwishoni kabisa mwa msafari kulikuwa na magari makubwa mawili (Buses) ambazo zilibeba watumishi wengine wa Rais wa ngazi za chini, Mfano waandishi wa habari wa Ikulu, makatibu wa Idara za Ikulu, Daktari wa Rais na kadhalika.

Kisha nyuma ya mabasi haya mawili msafara ulimaliziwa na gari ya Polisi iliyofuatia nyuma, Hii ndio picha kamili ya msafara wa Rais Kennedy ulipotoka uwanja wa ndege wa Love Field kuelekea Trade Mart kati kati ya mji wa Dallas, Kama nilivyosema awali kwamba, umbali kati ya uwanja wa ndege wa Love Field na alikokuwa anaelekea Kennedy (Trade Mart) ni kilomita 16 tu, lakini zilipangwa msafara usafiri kwa mwendo wa taratibu na kutumia dakika 45 ili kumpa Rais muda wa kutosha kusalimiana na wananchi njiani.

Wananchi walikuwa wamejitokeza wengi haswa na kujipanga barabarani kumlaki Rais, Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu laki moja na nusu mpaka laki mbili walikuwa wamejitokeza, Msafara ulizidi kuchelewa zaidi baada ya Rais Kennedy kuamuru msafara kusimama mara mbili barabarani nje ya ratiba iligopangwa ili aweze kuwapa mikono wananchi, Mara ya kwanza aliamuru msafara usimame ili kuwapa mikono watawa wa kikatoliki waliokuwa wanampungia mikono barabarani. Mara ya pili walikuwa ni wanafunzi wa shule ambao nao walikuwa wamejipanga barabarani kumshangilia.

Majira ya saa 6 na dakika 29 msafara wa Rais uliingia katika eneo kubwa (mtaa) ujulikanao kama Dealey Plaza ambao zamani ulikuwa na bustani na maeneo ya watu kupumzika, mbele ya macho lilikuwa linaonekana "jengo lililobeba kifo" cha Rais Kennedy, Jengo la Texas School Books Depository, Wakiwa bado eneo hili hili la Dealey Plaza, msafara wa Rais ukakata tena kona ndogo kutoka mtaa mdogo wa Houston Street na kuingia mtaa wa Elm Street, Bado jengo la Texas School Book Depository, "jengo lililobeba kifo" cha Kennedy lilikuwa katika upeo wa macho yao japokuwa walikuwa wanaelekea kulipita.

Kennedy na Mkewe Jackie walikuwa wanapungia mikono mamia ya wananchi waliojipnga barabarani kumshangilia, Kwa kuzingatia kuwa Kennedy alipata kura kiduchu eneo hili la Dallas wakati wa uchaguzi mkuu, hivyo mkewe Jackie akamgeukia na kumtania,"…kwa hizi shamra shamra, huwezi kusema eti wananchi wa Dallas wanakuchukia…" Jackie akaongea huku anatabasamu kumuangalia mumewe, "…hakika! Siwezi kusema wananichukia.!!" Kennedy akamjibu kwa kifupi mkewe huku anatabasamu na kuwapungia mikono wananchi.

Na hii ndio ilikuwa kauli ya mwisho ya Rais JF Kennedy… tayari ilikuwa ni saa 6 na 30. Na mbele yake alikuwa amebakiza chini ya sekunde 15 za uhai wake.

Mlio wa kwanza wa risasi wengine wanadai kwamba hawakuusikia, na hata baadhi ya maafisa wa Secret Services baadhi yao nao wanadai kwamba hawakuusikia. Na hata wale waliosikia walidai kwamba walidhani labda ilikuwa ni pancha ya tairi la gari au kitu kingine, hii ndio sababu ukiangalia katika kipande cha video ya tukio lile baada ya kupigwa kwa risasi ya kwanza hakukuwa na taharuki yoyote kutoka kwa wanausalama wa kumlinda rais na msafara uliendelea kama kawaida.

Risasi hii ilipigwa katika muda ambao Rais Kennedy, mkewe Jackie na Gavana Connally wote walikuwa wameguukia mkono wa kushoto kupungia wananchi na ghafla wote wakageuka mkono wa kulia kupungia wananchi walio upande huo, Ni muhimu kukumbuka kwamba katika muda huu walikuwa wekwisha lipita Jengo la Texas School Book depository, na wamelipa mgongo kwa kuliacha umbali wa takribani mita 81.

Risasi ya pili kupigwa (risasi ya kwanza nitaiongelea baadae) ilifyatuliwa sekunde ambayo Kennedy ameinua mkono mmoja juu aliwapungia wananchi, risasi hii ilimpenya nyuma yake katikati kabisa ya shingo na nyama ya juu ya bega na kusababisha uharibu Mdogo kwenye uti wa mgongo, na kisha kupenya ndani na kuharibu sehemu ya juu kabisa ya pafu la kulia na kutokea kooni ikiharibu sehemu kubwa ya koromeo, baada ya kupigwa na risasi hii, katika kipande cha video unaweza kumuona Rais Kennedy akiwa amekunja ngumi na kuelekeza mkono mbele ya uso wake usawa wa mdomo kama vile anakohoa na kuinama kwa mbele kidogo akiengemea upande wa kushoto aliko mkewe, Pia unaweza kumuona mkewe akiwa anamkumbatia kwa kuzungusha mkono wake mabegani kwa Kennedy kumuuliza kama yuko 'OK'! (Mpaka muda huu hakujua kama mumewe amepigwa risasi).

Risasi hii hii ya pili iliyompiga Kennedy, ilipotoka kooni kwa Kennedy ilienda moja kwa moja ya kumpiga Gavana Connally!, Risasi hii ilimpiga Gavana Connally mgongoni chini kidogo ya kwapa upande wa kulia na kutengeneza tundu la umbo la duara na kuharibu kiasi cha inch 4 cha mbavu yake ya tano upande wa kulia na kisha kutokea kifuani katika chuchu, Risasi hii hii baada ya kutoka kifuani kwa Gavana Connally kupitia kwenye chuchu ilitua kwenye mkono wa kulia wa Gavana Connally, juu kidogo ya kiganja na kuvunja vunja sehemu hiyo katika vipande vinane, Risasi hii hii, hatimaye ikatua kwenye paja la kushoto la Gavana Connally.

(Nitaeleza huko mbeleni kuhusu utata wa risasi hii ya pili iliyompata Kennedy na Gavana Connally kwa pamoja na ile Risasi ya kwanza ambayo haikuleta madhara yoyote), Risasi ya pili kumpata rais (ambayo ilikuwa ni risasi ya tatu kupigwa) ilimpata kichwani upande wa juu kulia, Risasi hii ilifumua kabisa eneo hilo la kichwa na kusababisha sehemu ya ubongo wa mbele kumwagika.

Damu nyingine ikaruka nyuma ya gari kwenye 'trunk' na nyingine kutua mpaka kwenye mkono wa kushoto wa afisa wa Secret Services aliyekuwa anaendesha gari ya wanausalama waliokuwa gari ya nyuma ya Rais, Ndani ya sekunde mbili baada ya mumewe kufumuliwa na risasi kichwani, First Lady Jacqueline Kennedy akaruka kutoka kwenye siti yake na kuanza kuparamia nyuma ya gari kwenye trunk, Tofauti na wengi wanavyodhani kwamba alikuwa anajaribu kukimbia kuokoa maisha yake, ila ukweli ni kwamba alikuwa anaokota kipande cha mfupa wa fuvu la kichwa kilichodondoka kwenye nyuma ya gari kwenye trunk baada ya mumewe kufumuliwa kichwa na risasi. Baada ya kukichukua haraka haraka akarejea kwenye siti yake.

Sekunde hii hii ambayo First Lady alikuwa anaparamia gari kwenye trunk, katika gari ya nyuma (follow up car), Special Agent Clint Hill ambaye alikuwa ananing'inia kwenye mlango wa mbele kushoto akaruka na kuanza kuikimbilia gari iliyombeba rais na first lady, Dereva wa gari la rais alikuwa ameongeza mwendo baada ya mushkeli kutokea na dhahiri kuonekana kwamba rais yuko hatarini, Hivyo basi ilimbidi Clint Hill kujaribu kuparamia gari mara kadhaa mpaka alipofanikiwa kuidandia gari na mara moja kuwafunika rais na first lady akiwakinga kwa kutumia mwili wake kama ngao.

Baada ya Agent Clint Hill kuwakinga Rais na mkewe dhidi ya shambulio lingine lolote la risasi kuwafikia, gari ya rais liliendeshwa kwa kasi kubwa likifuatiwa na pikipiki za pembeni na ile follow up car ya maafisa usalama, Wakati haya yote yanatokea zilikuwa zimebaki takribani dakika tano pekee kufika walikokuwa wanaelekea, Trade Mart, Kwahiyo baada ya gari iliyombeba rais kuanza kuendeshwa kwa kasi, takribani saa 6 na dakika 35 walipita eneo la Trade Mart na kuelekea moja kwa moja hospitali ya Parkland Memorial Hospital ambako waliwasili majira ya saa 6 na dakika 38 na kupokelewa kisha Rais Kennedy alipelekwa moja kwa moja chumba cha dharura.

Licha ya watu wa usalama kujitahidi sana kuratibu taaarifa za kilichotokea zisivuje kabla ya taarifa rasmi ya serikali, lakini majira ya saa 6 na dakika 40 kituo cha televisheni cha CBS kikakatisha Igizo lililokuwa linaonyeshwa kwenye televisheni yao na kutoa "Breaking News" kuwa msafara wa Rais umeshambuliwa huko Dallas, Baadae kama muda wa saa 6 na dakika 45, Dan Rather mwandishi wa habari wa kituo cha CBS alifanya mawasiliano kwa siri sana na daktari anayemfahamu hapo hospitalini na kuvujishiwa taarifa kuwa kuna uwezekano mkubwa Rais Kennedy hayuko hai.

Ifahamike kwamba maafisa wa Secret Services waliwaleta hapa viongozi wengine wote wakuu waliopo kwenye msafara, yaani First Lady Jacqueline Kennedy, Makamu wa Rais Johnson, Mkewe Lady Bird na Gavana Connally ambaye alikuwa chumba cha wagonjwa mahututi, Ilipofika saa 7 kamili madaktari wakatoa taarifa yao kwa viongozi wa serikali na wanausalama waliokuwepo hapo kwamba, licha ya kutumia ujuzi wao wote na maarifa yao yote, wameshindwa kuokoa maisha ya Rais JF Kennedy, kwamba Rais Kennedy amefariki. Dunia tayari!! Huko mtaani habari zilikuwa zinaenea kwa kasi kama moto wa kifuu, kuwa Rais Kennedy amefariki, hivyo kwa busara watu wa usalama wakashauri kuwa itolewe taarifa rasmi kuhusu kifo cha Rais Kennedy ili kuepusha mkanganyiko na taharuki iliyopo mtaani.

Makamu wa Rais Johnson akakubali hilo lakini akaamuru taarifa hiyo itolewe kwa umma mara baada ya yeye kuondoka hapo hospitali kwa usababu ya usalama wake, kwamba hataki yeyote ajue kuwa yuko hapo hospitali kwa kuwa kwa vile Rais ameuwawa tayari yawezekana yeye kama Makamu wa Rais akawa ni "next target"! Saa 7 na dakika 26 Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson akaondolewa kwa siri kubwa kutoka Parkland Memorial Hospital na kupelekwa uwanja wa ndege wa Love Field ambako Airforce One ilikuwa imepaki.

Baada ya Makamu wa Rais kuondoka tu, dakika saba baadae yaani saa 7 na dakika 33 Katibu Msaidizi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Malcolm Kilduff ya Marekani akafanya mkutano na waandishi wa habari hapo hapo hospitali na kuutangazia rasmi ulimwengu kuwa Rais JF Kennedy amefariki baada ya kudunguliwa na risasi na mtu asiyejulikana, Bw. Kilduff hakujibu swali lolote la waandishi wala kutoa taarifa nyingine yoyote, Alipotoa taarifa hii tu akaumaliza mkutano na wanahabari, Baada ya waandishi wote kuondoka na kubakia watu wa serikali pekee na wanausalama ndani ya Hospitali kulitokea kisa ambacho naamini wengi hawajawahi kukisikia.

Ni kwamba, katika sheria za Marekani kipindi hicho zilikuwa zinaelekeza kwamba, endapo Rais atafariki akiwa jimbo Fulani.. Mwili wake unakuwa chini ya mamlaka ya jimbo na sio serikali kuu, Sasa, yule bwana swahiba wa Rais Kennedy na Katibu wake wa teuzi Kenneth O'Donnell, yule ambaye alimuamuru Afisa wa Secret Services, Agent Kellerman kuwa gari la Rais liondolewe paa na kubaki 'kibanda wazi', akatoa tena maelekezo kwa wanausalama wauondoe mwili wa Rais Kennedy kutoka hapo hospitalini na kuipeleka uwanja wa ndege wa Love Field na kuupakia katika Air Force One, Lakini madaktari walikataa mwili huo kuondolewa hospitalini bila kufanyiwa 'Autopsy' (uchunguzi wa kina wa kidaktari kuhusu chanzo cha kifo) ukizibgatia kuwa Rais Kennedy amekufa kwa mauaji ya kukusidiwa.

Bw. Kenneth O'Donnell akasisitiza kuwa hakuna muda wa kutosha kufanya Autopsy kwani Air Force One inatakiwa iondoke mara moja kuwarudisha Makamu wa Rais na First Lady Washington kwa sababu za kiusalama na First Lady amekataa kuondoka bila mwili wa mumewe, madaktari wakashilia msimamo wao kuwa hawawezi kuuachia mwili wa Rais bila kufanyiwa Autopsy. Na kusisitiza wanalolisema wakatumia kifungu cha sheria nilichokitaja hapo juu kuwaeleza kuwa wao (Kenneth na wanausalama) kama watumishi wa serikali kuu hawana mamlaka juu ya mwili wa Rais bali wao (madaktari) kama watumishi wa jimbo la Texas ndio wenye mamlaka juu ya mwili wa Rais.

Mzozo ukawa mkubwa sana mpaka kufikia hatua Kenneth O'Donnell na wanausalama wakataka kuutoa mwili wa Rais Kennedy kwa kutumia nguvu, Hii ikawalazimu madaktari kuita maafisa wa polisi (watumishi wa jimbo la Texas) kuwasaidia kuwadhibiti Kenneth na wanausalama wa Secret Services, Madaktari wakatanda mlangoni pamoja na Maafisa wa polisi wakiwa wameshikilia bastola kuwanyooshea Kenneth O'Donnell na wanausalama wa Secret services kuwaamuru waache mwili wa Rais.

Upande wa pili nao Kenneth na wanausalama walikuwa nao wamechomoa bastola kuwanyooshea madaktari na polisi wa jimbo la Texas kuwa wapishe mlangoni, Wakati mzozo huo unaendelea hospitali ya Parkland Memorial Hospital, huko uwanja wa ndege wa Love Field, ndani ya Air Force One Jaji wa mahakama Kuu, Sarah Hughes alikuwa anamuapisha Makamu wa Rais Lyndon B. Johnson kuwa Rais wa Marekani.

Na huko mitaani wananchi walikuwa wako kwenye sintofahamu kubwa!! Ni nini kimetokea? Nani amemuua Rais? Amewezaje kutekeleza hilo? Sababu gani imemponza Kennedy kuuwawa??.....Maswali yalikuwa mengi na magumu pasipo majibu ya dhahiri!!....

Sasa turudi kwenye kufahamu zaidi kuhusu nani muhusika wa kifo cha JF. Kennedy?.......

Baada ya kushambuliwa kwa msafara wa Rais Kennedy na hatimaye kupelekea kifo chake, mara moja ndani ya masaa mchache akakamatwa mtu anayejulikana kama Lee Harvey Oswald na kushutumiwa kuhusika na tukio hili, Hii ilikiwaje? Nitaeleza kile ambacho serikali ya Marekani wanajaribu ulimwengu wote waamini…

Marion Baker ni afisa polisi wa eneo la Dallas na siku ya tukio alikuwa amepangiwa kuwa moja ya wasindikiza msafara kwa pikipiki, piki piki yake ya polisi ilipangwa nyuma ya magari waliyopanda waandishi wa habari kama ambavyo nilielezea mpangilio wa msafara hapo nyuma, Baker anaeleza kwamba siku hiyo ya tukio, akiwa kwenye msafara sekunde chache baada ya kukata kona kutoka Huston Street na kuingia Elm Street msafara ulipotembea umbali wa kati ya futi 60 au 80 alisikia mlio mkubwa wa risasi. Baker anadai kwamba kwa uzoefu wake aligundua kuwa mlio huo ni wa 'Rifle' yenye nguvu kubwa na kuzingatia mlio uliotoka alihisi kwamba bunduki hiyo imefyatuliwa kutoka eidha Jengo la mbele yake (Texas School Book Depository) au jengo lililo mkabala na jengo hili kwa upande wa kulia, yaani jengo la Dallas Textile Building (DalTex).

Baker anaeleza kwamba, alipoangalia kwa umakini zaidi katika jengo la Texas School Books Depository akaona njiwa waliokuwa juu ya jengo wanaruka na kutawanyika kutoka kwenye paa, Baker anaeleza kwamba moja kwa moja akaendendesha pikipiki yake mpaka kwenye kona ya Huston Street na Elm Street ambako alipaki pikipiki yake na kisha kuelekea kwenye jengo la Texas School Books Depository na kuingia ndani ambako alikutana na msimamzi wa jengo hilo Bw. Roy Truly, Moja kwa moja baada ya kumueleza kwa haraka haraka kuhusu kilichokuwa kinaendelea huko barabarani alikotoka na kwanini yuko hapa, yeye na Roy wakapanda mpaka ghorofa ya kwanza na kuanza kupiga kelele mtu yeyeto aliyepo juu ashushe lifti kuja chini, Miaka hiyo lifti nyingi hazikuwa na mfumo kama huu wa sasa ambapo unabofya kitufe na lifti inakufuata ghorofa ulilopo. Kipindi hicho ilikuwa inabidi mtu aliyepo ghorofa ambalo ndipo lifti ilikuwepo kwa muda huo airuhusu kushuka chini au kwenda juu kulingana na uhitaji wa huo.

Baada ya Baker na Roy kuita kwa sekunde kadhaa bila majibu wakaamua watumie ngazi za kawaida za jengo kwenda juu, Wakapanda mpaka ghorofa ya pili ambako wakiwa wanaelekea kupanda ngazi kwenda ghorofa ya juu zaidi, Baker anadai kwamba alisikia mjongeo kwenye chumba kilichopo karibu yao. Chumba hiki kilikuwa kinatumika kama chumba cha chakula na wafanyakazi kwenye jengo hili, Baker akachomoa bastola yake kutoka kiunoni na kufungua chumba hiki. Ndani ya chumba hiki walimkuta Lee Oswald, Wanaeleza kuwa Oswald hakuonekana kuwa mtu mwenye mashaka au 'kupaniki' ila tu alishtuka kuona Polisi amemmnyooshea bastola.

Inaelezwa kuwa Oswald alikuwa anaonyesha dalili zote za mtu ambaye hakuwa anajua ni nini kilikuwa kinaendelea, Msimamizi wa jengo alimtambulisha Oswald kwa askari kuwa alikuwa ni mfanyakazi wa jengo hilo, hivyo ikambidi polisi amuache Oswald na kuendelea na upekuzi katika floor za juu, Purukushani yote hii kutoka muda ambao Baker alisikia mlio wa risasi akiwa kwenye msafara wa Rais mpaka kuja kukutana na Oswald ghorofa ya pili ya jengo la Texas School Books Depository, ilichukua kama sekunde 74 mpaka sekunde 90 tu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kamisheni maalumu iliyoundwa na serikali ili kuchunguza kifo cha Rais Kennedy, The Warren Commission wanaeleza kwamba inakisiwa kuwa Oswald aliondoka kwenye jengo la Texas School Books Depository muda wa saa 6 na dakika 33 kupitia mlango wa mbele huku akiwa ameshika soda mkononi kwa mujibu wa ushahidi wa mwanamama ambaye alikuwa anafanya kazi kama secretary kwenye jengo hili, Inaelezwa kwamba, baada ya upekuzi mnamo saa 6 na dakika 50, bunduki, Rifle aina ya Italian Carcano iligunduliwa ikiwa imefichwa kwenye lundo la vitabu katika ghorofa ya sita.

Baada ya kugundulikwa kwa bunduki hii mnamo majira ya saa 6 na dakika 50 jengo hili likawa 'sealed' kuzuia mtu yeyote asitoke au kuingia, Lakini ajabu ni kwamba kule barabarani ambapo Rais Kennedy alidunguliwa, kulikuwa hakujawekwa kizuizi chochote kuzuia watu wasipite ili kuepusha kuharibu 'crime scene', na kuna rekodi za video zikionesha magari yakiendelea kupita barabarani kama kawaida eneo lile ambalo dakika chache kumetokea mauaji ya Rais, Ripoti ya Warren Commission inaeleza kwamba mara baada ya Oswald kutoka kwenye jengo la Texas School Books Depository, Oswald alitembea kwa miguu umbali wa kupita majengo saba (seven blocks) na kisha kupanda bus, Bus lilitembea kwa muda mchache kabla ya kukwama kwenye foleni ya barabarani. Baada ya bus alilopanda kukwama kwenye foleni, Oswald alishuka na kutembea kwa mguu mpaka kwenye kituo cha mafuta. Hapo alichukua taxi ambayo ilimbeba mpaka mtaani kwake lakini hakushukia nje ya nyumba yake, taxi ilienda kumshusha majengo kadhaa kupita nyumba yake. Baada ya kushuka kwenye Taxi akatembea kurudi nyuma mpaka nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa mfanyakazi wa usafi kwenye jengo ambalo Oswald alikuwa amepanga, Earlene Roberts, anasema kwamba Oswald aliwasili nyumbani kwake 1026 North Beckley Avenue majira ya saa 7 kamili mchana na hakukaa sana ndani kwani aliondoka tena kama dakika tatu au nne baada ya kuwasili, Earlene anadai kuwa alimuona Oswald amesimama mbele ya nyumba akiwa anasubiri gari muda mchache baada ya kumuona amewasili hapo kabla.

Ilipofika majira ya saa 7 na dakika 15 mchana polisi walipokea taarifa juu ya kupigwa risasi kwa polisi mwenzao J.D Tippit katika makutano ya barabara za 10th St. na Patton Avenue. Sehemu hii ni takribani kilomita moja tu kutoka nyumbani kwa Oswald, Bado kuna utata na ubishani mkubwa kwanini polisi walimuhusisha Oswald na kupigwa risasi kwa polisi J.D Tippit, lakini inaelezwa kwamba Oswald alionekana akitembea kwa miguu kuelekea jumba la maonyesho ya sinema la Texas Theatre.

Kuna bwana mmoja anaitwa Johhny Calvin Brewer ambaye alikuwa anafanya kazi katika duka la viatu liitwalo Hardy's shoes Store ambalo liko ghorofa moja na ilipo Texas Theatre anadai kwamba alimuona Oswald akijificha sura mara baada ya magari ya polisi kupita karibu yake huku yakiliza king'ora, Bw. Brewer anadai kwamba akamfuatilia Oswald alikokuwa anaelekea na akamuona anaingia kimagendo bila kulipia mlangoni Texas Theatre muda ambao mkata tiketi Bi. Julie Postal alikuwa amejisahau na kuangalia pembeni.

Inaelezwa kwamba Brewer akamtaarifu bibie Julie kuhusu Oswald aliyeingia kimagendo ndani ya Theatre na baada ya hapo wakapiga simu polisi kuwafahamisha kuwa ndani ya Theatre kulikuwa na mtu ambaye walikuwa wana mashaka naye, Ndani ya dakika chache, kufumba na kufumbua zilifika zaidi ya gari za polisi 24, pamoja na ma-sheriff na wapelelezi.

Baada ya lundo hili la wanausalama kuwasili, mnamo majira ya saa 7 na dakika 50 mchana Lee Harvey Oswald akakamatwa kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha polisi J.D Tippit na muda mchache baada ya kufikishwa kituo cha polisi, Oswald aliongezewa mashtaka na kuhusishwa pia na kumdungua kwa risasi na kumuua Rais JF Kennedy.!!

OSWALD CHINI YA MIKONO YA POLISI.........

Baada ya Oswald kukamatwa kutoka jumba la kuonyesha sinema la Texas Theatre, moja kwa moja akapelekwa makao makuu ya polisi ya Dallas, Akiwa hapo kituoni Oswald alihojiwa na Asifa wa FBI, Special Agent James P. Hosty pamoja na Afisa mkuu wa Polisi kituo cha Dallas Captain Will Frizt, Oswald alikana kuhusika kabisa na mauaji yote mawili, yaani mauaji ya Rais Kennedy na mauaji ya polisi J. D Tippit, Akajieleza kwamba siku ya tukio ni kweli alikuwa kwenye jengo la Texas School Books Depository na hakukuwa na ajabu yeye kuwepo hapo kwa kuwa anafanya kazi kwenye jengo hilo.

Akaendelea kujieleza kuwa wakati tukio linatokea alikuwa anakula chakula cha mchana kwenye ghorofa ya kwanza na hakuwa anajua kinachoendelea huko mtaani na baada ya kumaliza kula chakula akapanda mpaka ghorlfa ya pili ili kwenda kuchukua soda aina ya coca cola kwenye 'vending machine'. (Ndio hii soda ambayo nilieleza kwenye sehemu iliyopita kwamba kuna mama secretary wa jengo hilo alimuona Oswald ameibeba akiwa anatoka nje ya jengo), Oswald akaeleza kuwa akiwa anarejea kutoka ghorofa ya pili kwenda ghorofa ya kwanza alikuta na wafanya kazi wengine wawili weusi ambao nao ni waajiriwa wa jengo hilo. Oswald aliwaeleza kumtambua mfanya kazi mmoja kwa jina la 'Junior' na mwingine hakuwa anamkumbuka kwa jina.

Polisi baadae waliwahoji wafanyakazi weusi wanaofanya kazi kwenye jengo hilo na walijitokeza wafanya kazi wawili Junior Jarman na Harold Norman ambao walikiri kwamba walimuona mtu akiwa kwenye chumba cha chakula au 'Domino Room' kama ambavyo walizoea kukiita lakini walikiri kuwa hawakuwa makini kumuangalia ni nani hivyo hawakumbuki, Oswald akaendelea kueleza kuwa aliporejea kwenye chumba cha chakula na kuketi ili ajiburudishe na soda yake ya coca cola, ndipo ghafla alishituka anaingia polisi ambaye baadae alikuja kumtambua kama Marion Baker na kumnyooshea bastola.

Licha ya maelezo yote haya lakini bado waliendelea kumbana na kumlazisha kukiri uhusika wake kwenye kumdungua Rais Kennedy, walimuonyesha Picha ambayo ilionyesha Oswald akiwa ameshikilia bunduki ambayo iliaminika kumdungua Rais Kennedy, Oswald alikanusha na kudai kuwa picha hiyo imetengenezwa.

Wakamuonyesha pia risiti za ununuzi wa bunduki hiyo kwa kutumia jina bandia la "A.J Hidell" lakini bunduki hiyo ilitumwa kwenye anuani ya nyumbani kwake, Oswald akakanusha kufanya manunuzi hayo na kusisitiza kuwa huo ni "mchoro" kuna watu wanajaribu kumsingizia yeye shutuma hizo ili kuficha wahusika halisi, Kitu pekee ambacho Oswald alikiri ni kumiliki bastola 0.38 revolver na alidai kuwa anaimilili kwa mujibu wa sheria na ulinzi binafsi, Pia ikumbukwe kuwa Oswald aliwahi kutumikia jeshi la Marekani kikosi cha Marine Corps.

Oswald pia alikataa kabisa kuwakilishwa na mawakili wa utetezi wa serikali au wale ambao serikali ilikiwa tayari kumlipia kama haki yake ya kiraia, Oswald alidai kuwa hakuwa na imani na watu hao au serikali kumtendea haki kwenye suala hili, Wakili pekee ambaye Oswald alikubali amuwakilishe kwenye mahojiano na kipindi cha kesi kusikilizwa alikuwa ni Bw. John Abt ambaye alikuwa anatokea American Civil Liberties Union, Lakini ajabu ni kwamba kwa siku zote mbili za mahojiano ya Oswald, John Abt alikuwa hapatikani kwenye simu yake ya nyumbani wala sehemu yake ya kazi.

Mahojiano ya polisi na Oswald yaliendelea kwa muda wa siku mbili mfululizo, Siku mbili zilipopita yaani siku ya Novemba 24, 1963 vyombo vya ulinzi viliazimia kumuhamisha Lee Oswald kutoka katika mahabusu ya polisi kituo cha Dallas na kumpeleka gerezani kwa ajili ya kushikiliwa kwa usalama zaidi akisubiria mahojiano zaidi na kesi yake kuanza kuunguruma, Muda wa saa 5 na dakika 15 asubuhi, Oswald alifunguliwa na kutolewa kwenye selo na baada ya kusainiwa kwa makaratasi yake ya kuhamishwa kutoka hapo kituoni ili apelekwe gerezani.

Saa 5 na dakika 19 Oswald alikuwa anakaribia kufika kwenye mlango wa ghorofa ya chini kabisa (basement) ili kupelekwa kwenye gari maalumu lisilopenya risasi ambalo lilikuwa linasubiri ili kumbeba na kumpeleka gerezan, Tukio hili lilikuwa limeteka hisia za taifa zima na lilikuwa linafuatiliwa kila kona ya nchi ya Marekani na duniani kote kwa hiyo vituo vingi vya televisheni lilikuwa vinarusha tukio hili moja kwa moja, mubashara kabisa, Saa 5 na dakika 20 polisi wawili walitoka mlangoni ili kuhakikisha usalama na sekunde chache baadae Oswald akiwa amefungwa pingu na kuzungukwa na wanausalama kila kona alitoka kwenye mlango wa jengo kuingia basement ili aweze kupelekwa kwenye gari inayowasubiri.

Oswald na maaskari waliokuwa wamemzunguka walipiga kama hatua tano tu au sita na ghafla akajitokeza mtu aliyekuwa pembeni yao amekaa pamoja na wana Habari, na mkononi mwake alikuwa ameshika bastola akiielekeza moja kwa moja kwa Oswald, Hii lilikuwa ni saa 5 na dakika 21, Kabla wanausalama hawajafanya lolote, mtu huyu alimfyatulia risasi ya tumboni Oswald na moja kwa moja Oswald akadondoka chini, Wanausalama wakafanikiwa kumdhibiti mtu huyu na kumkamata na moja kwa moja wakamuingiza ndani kwenye kituo cha Polisi pamoja na Oswald.

Mtu huyu aliyempiga risasi Oswald anaitwa Jack Ruby na ni moja ya watu maarufu sana Dallas katika kipindi hicho kutokana na kumiliki Klabu kubwa ya usiku mjini hapo, Dakika chache baadae Oswald alichukuliwa na gari ya wagonjwa na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Parkland Memorial Hospital (hospitali ile ile aliyofia Kennedy siku mbili nyuma), Risasi aliyopigwa Oswald iliingia ubavu wa kushoto na ilikuwa imeenda kuharibu kabisa bandama, aorta, vena cava, figo, ini, diaphragm na mbavu ya kumi na moja ya kushoto na ikakwama katika ubavu wa kulia, Vile vile pia baada ya "juhudi kubwa" za madaktari kuokoa maisha ya Oswald kutozaa matunda hatimaye muda wa saa 7 na dakika 7 siku hiyo ya Novemba 24, Dallas Police Chief Bw. Jesse Curry aliutangazia uliwengu kuwa mtuhumiwa pekee wa mauaji ya Rais JF Kennedy, Bw. Lee Harvey Oswald amefariki dunia.

Mara moja baada ya habari hii kutangazwa iliwafanya watu wengi waanze kukuna vichwa, Siku mbili nyuma mara baada ya Rais Kennedy kupigwa risasi kulianza kuibuka minong'ono mitaani kwamba huo ulikiwa ni 'mchoro' wa watu wenye nguvu kwenye 'system', Baadae siku hiyo hiyo ilipotangazwa kuwa muuaji wa Kennedy amekamatwa, sintofahamu ikaongezeka zaidi kuwa imekuwaje mtu ambaye ametekeleza mauaji makubwa hivyo akamatwe 'kizembe' na kwa haraka namna hiyo, Lakini ilipotolewa taarifa ya Oswald kuuwawa, huko mtaani asilimia kubwa ya wananchi wazo moja kuu lilitawala vichwani mwao, kuwa "Oswald alikuwa amenyamazishwa"! Kuna uwezekano mkubwa wahusika halisi wa kifo cha Kennedy walikuwa wanahofia kesi ya Oswald kuanza kuunguruma kwani walihofia labda Oswald "angemwaga mchele!"

Pia kilichosgangaza zaidi ni mtu aliyempiga risasi Oswald. Jack Ruby ni mfanyabiashara mkubwa, mtu mwenye 'status' hapo Dallas, Inawezekaje mtu wa hadhi yake afanye kitu cha kipuuzi kiasi hicho kwa kumpiga mtu risasi hadharani mbele ya vyombo vya habari kwa suala ambalo alimuhusu moja kwa moja?? Ana maslahi gani kufanya hivyo??, Sasa ilikuwa dhahiri, kwamba, kuna jambo kubwa zaidi linafichwa nyuma ya pazia… kuna wahusika halisi wa kifo cha Kennedy!!

Ni kina nani?? Na kwa nini walimuua Kennedy??.......

Hakuna mwenye majibu kamili ya asilimia mia, lakini nitajitahidi kuleta kwenu vidhibiti kadhaa ambavyo vitasaidia kila mmoja kufikia conclusion yake binafsi!!

Japokuwa serikali ya Marekani wameendelea kushikilia msimamo kuwa Lee Harvey Oswald alihusika yeye kwa binafsi yake kudungua na kumuua Rais Kennedy kutokana na kudaiwa kuwa misimamo mikali wa sera za kijamaa, lakini kuna vidhibiti vingi vinavyoonyesha kuwa kuna kikundi au vikundi vya watu wenye nguvu kubwa walio nyuma ya mauaji haya, Kabla sijaweka vidhibiti vya kuonyesha labda ni watu gani wamehusika na kifo cha Kennedy, ningependa awali ya yote tujaribu kukiangalia kisa cha Oswald kuambiwa kuwa ndiye aliyemdungua rais na ukweli wake na maswali yayozunguka suala hili.

Dalili ya kuwepo ya wadunguaji zaidi ya mmoja.......

Nikumbushe kuwa, wiki moja baada ya mauaji haya ya Rais Kennedy, Rais mpya Johnson aliunda tume maalumu kuchunguza ukweli juu ya tukio hili, Tume hii iliundwa kwa kutokana na Executive Order number 11130 na kutambuliwa na Congress kupitia Resolution number 137, Kamisheni hii ilikuwa chini ya Uenyekiti wa Chief Justice Earl Warren na ndio sababu ya kujulikana kamaa The Warren Commission, Kulikuwa na mabishano makali juu ya uundwaji wa kamisheni hii, huku baadhi ya viongozi waandamizi serikalini wakiamini kuwa kamisheni hii itaamsha hasira za wananchi badala ya kutatua utata uliopo.

Licha ya viongozi wengi wakuu serikalini kushauri kutoundwa kwa hii kisheni lakini kwa sababu ambazo Rais mpya Johnson yeye binafsi aliziona ni muhimu akaunda tume hii wiki moja tu baada ya tukio na ilifanya kazi kwa takribani miezi kumi na hatimaye kukabidhi ripoti yake kwa Rais tarehe 24 September, 1964 na kuwekwa hadharani kwa wananchi siku tatu baadae, Nitaizungumzi zaidi Ripoti hii na masuala kadhaa kuihusu huko sehemu za mbeleni za hii makala, Lakini jambo kuu zaidi hii Ripoti inachojaribu kuonyesha ni kwamba Lee Oswald alifanya tukio kwa utashi wake pekee na hakushirikiana na mtu yeyote!!

Siku moja tu baada ya ripoti hii kutoka ilikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa watu waliofuatilia tukio hili kwa makini pamoja na wachambuzi wa masuala ya intelijensia, Ripoti hii ilionekana kama vile ilikuwa ni jaribio la serikali kujisafisha na haikuwa na nia ya kuchimbwa ukweli juu ya nini hasa kilitokea siku ya November 22, 1963, Moja wapo ya vitu ambavyo Ripoti hii imepingwa vikali ni jaribio lake la kutaka kuaminisha umaa kuwa Oswald ndiye muhusika na alikiwa pekee kwenye tukio hili, Japokuwa ripoti yaa Warren Commission inabakia kuwa msimamo rasmi wa serikali mpaka leo hii juu ya kifo cha Rais Kennedy lakini vipo vidhibiti kadhaa vinavyoonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa tukio hilo (kumpiga risasi rais) siku ya Nov 22, lilitekelezwa na zaidi ya mtu mmoja.

Nitaeleza…

Kuna jambo moja la msingi sana ambalo nadhani wengi labda watakuwa hawajawahi kulisikia licha ya kusoma makala nyingi kuhusu kifo cha Kennedy, Wakati natafiti kuhusu makala hii nilijitahidi kuipitia ripoti ya Warren Commission na baada ya kuipitia kuna jambo lilijoficha sana ambalo nililiona na kufanya nichimbe zaidi kuhusu ni nini kilitokea polisi ambapo Oswald alishikiliwa.

Hiko hivi,

Bunduki iliyotumika kufyatua risasi iliyomuua Rais Kennedy inatajwa kwenye ripoti ya Warren Commission kuwa ni "Mannlicher-Carcano", Lakini ukifuatilia kwa undani utagundua kwamba bunduki hii ni aina ya 6.5x52mm Carcano (model 91/38 - Infantry Rifle), Bunduki hii ina uzito wa kilo 3.9 na urefu wa milimita 1285 (inch 50.6) ambapo urefu wa mdomo wa mbele pekee (barrel length) ni 780mm (inch 30.7), Risasi inayopigwa kutoka kwenye bunduki hii ina uwezo wa kusafiri mita 700 kwa sekunde na kwenda umbali mpaka kufikia mita 1000, Pia uzalishwaji wa bunduki hizi nyingi ulifanyika mwaka 1891 nchini Italia na kuna model chache zilitengenezwa miaka1940s huko huko Italia.

Bunduki nyingi zilizopo za Mannlicher-Carcano (hata kipindi hicho cha mwaka 1963) hazina Telescopic sight (darubini ya mdunguaji… yaani ile lenzi ambayo sniper anachungulia kupata muono mzuri wa target yake), Lakini bunduki inayodaiwa kutumiwa na Oswald ilikuwa na telescopic sight. Hii ina maana kwamba eidha aliifanyia modifications au alihangaika kupata model chache za Carcano zilizozalishwa miaka ya 1940s.

Sasa basi,

Kuna kitu ambacho naamini watumiaji wengi wa silaha watakuwa wanakifahamu, kinaitwa GSR au wengine wanaita CDR (Gunshot Residue au Cartridge Discharge Residue), Hili ni kama unga au vumbi fulani jembamba sana linatoka ukifyatua risasi na mara nyingi huwezi kuliona, Vumbi hili linatokana na propellant ya risasi ndani ya bunduki pale inapofyatuliwa, pia vipande vidogo vidogo sana (particles) za risasi na catridge ikifyatuka, Kitaalamu, GSR inaruka futi 3 mpaka 5 kutoka bunduki ilipofyatuliwa, kwa maana ya kwamba mtu anayefyatua bunduki hii ni lazima atarukiwa na 'vumbi' hili la GRS na vumbi hili huwa linakaa mwilini kwa mfyatuaji risasi kwa masaa matatu mpaka sita kitegemea na aina ya silaha iliyotumika.

Sasa,

Katika uchunguzi wa matukio ya uhalifu kwa kutumia silaha kuna kipimo kinaitwa Paraffin Test, Kipimo hiki huwa kinapima uwepo wa GRS katika nguo na mwili wa mtu ambaye anahisiwa kutumia hiyo silaha katika tukio hilo mahususi, Kipimo kikileta majibu positive - hii maana yake ni kwamba mtu huyo alifyatua hiyo risasi, au alikuwa karibu muda ambao risasi ilipofyatuliwa au aliigusa risasi silaha muda mfupi baada ya kufyatuliwa, Majibu ya kipimo yakija negative hii ina maana kwamba mtu huyo hakufyatua risasi, au hakuwa karibu muda ambao risasi ilifyatuliwa au hakuigusa silaha baada ya kifyatuliwa.

Turudi kwenye ninachojaribu kueleza… kwa mujibu wa taarifa ya makao makuu ya polisi Dallas ambapo Oswald alishikiliwa, alipokuwa hapo kituoni alifanyiwa Paraffin Test, Ajabu ni kwamba majibu yalikuja negative.!!, Maana yake ni kama nilivyoeleza hapo juu, majibu negative yanamaanisha kuwa mtu huyu hakufyatua risasi, na hakuwa karibu na silaha wakati inafyatuliwa na wala hakuigusa baada ya kufyatuliwa, Hii ina maana gani? Warren Commission na serikali hawakuiona hii ripoti ya Polisi??? Jibu ni kwamba waliiona na wakaja na "majibu" yao.

Kwamba,

Kwenye ripoti ya Warren Commission wanaeleza kwamba walimuhoji mama anayeitwa Earlene Roberts. Huyu ni yule mama wa usafi katika jengo ambalo kulikuwa na chumba cha Oswald anapoishi, Warren Commission wanadai kuwa mama huyu aliwaeleza kuwa alimuona Oswald akirudi kwake na kuondoka tena baada ya kama dakika tatu au nne na alipoondoka alikuwa amevaa nguo nyingine tofauti na zile za awali alizokuja nazo, Kwa hiyo Warren Commission wakatumia ushahidi huu kuhitimisha swali la kwanini majibu ya Parrafin Test ya Oswald yalikuja negative.

Ufafanuzi wao ni kwamba nguo alizozivaa wakati anapimwa hicho kipimo hazikuwa zile ambazo alizivaa wakati anafyatua risasi na hata baada ya kupekuliwa alipokuwa anaishi na nguo za awali kupatikana tayari muda ulikuwa umepita kuwezesha kipimo kubashiri uwepo wa GSR, Lakini huu ni ukweli nusu ambao unapotoshwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Nilieleza kwamba bunduki inayodaiwa kutumika na Oswald ina telescopic sight (darubini ya kudungulia). Maana yake kwamba mtumiaji lazima ainame juu ya bunduki ili aweze kuchungulia kutumia telescopic sight, Maafisa wote wa FBI ambao ni walengaji (Marksmen) ambao walitumiwa kwenye uchunguzi wa miaka ya hivi karibuni kutafiti juu ya GSR kwa kutumia bunduki ile ile inayodaiwa ilitumiwa na Oswald ikiwa na telescopic sight, katika vipimo vya Parrafin wote walikutwa na kiwango kikubwa cha GSR usoni na hasa hasa mashavuni, Kwa hiyo, maelezo ya kuwa Oswald alibadili nguo ndio maana majibu ya Parrafin Test yakaonyesha negative yanakuwa hayajitoshelezi sana.

Labda tuchukulie ndani ya dakika tatu hizo alizoingia chumbani, Oswald alioga kwa umakini wa hali ya juu na kujisugua haswa na kisha kubadili nguo (which is unlikely mtu kufanikisha yote hayo ndani ya dakika tatu)…. Bado kuna kiwango kikubwa cha sintofahamu kuhusu ufyatuaji wa risasi….

UTATA WA RISASI ILIYOMUUA RAIS KENNEDY.........

Ni kwamba, katika teknolojia ya kurekodi video kuna kitu kinaitwa frames. Kwa lugha rahisi kabisa, frames ni picha mnato ambazo zinaunda video. Ndio kusema kwamba, kipande kifupi cha video kina Picha mnato mamia kadhaa. Au kwa lugha nyingine nyepesi zaidi ni kwamba video ni muunganiko wa maelfu ya picha mnato zilizorekodiwa katika mtiririko wa kufuatana, ukiangalia ile video ya tukio utaona upande wa juu kulia kuna namba zinatokea na zinaenda kama zinahesabu hivi. Namba zile zinakuonyesha muda huo husika unaangalia frame namba ngapi ya kipande hiki cha video.

Suala hili la kuelewa tukio gani limetokea frame namba ngapi kwenye kwenye video lina umuhimu wa kipekee sana kwenye kuelewa utata wa tukio hili la kuuwawa kwa Rais Kennedy kama ambavyo nitaeleza leo katika sehemu ya hii makala.

Sasa,

Nilieleza kuwa serikali kupitia Warren Commission wanashikilia msimamamo kuwa Oswald alitekeleza tukio peke yake kwa utashi wake pasipo kushirikiana na mtu yeyote yule. Serikali inashikilia msimamo huu ili kupinga msimamo wa wengi kuwa tukio hilo lilipangwa na watu na yawezekana kabisa ni watu wenye nguvu kwenye 'system', Pia nikumbushe nilipoandika kuhusu namna rais alivyopigwa risasi nilieleza kuhusu risasi ya kwanza kumpata ilitokea kooni/kifuani na kwenda kumpata Gavana Connally sehemu ya nyuma ya mgongo kulia chini kidogo ya kwapa na kumsababishaia majeraha makubwa tumboni, mkononi na kwenye paja.

Nadharia hii ya risasi moja kusababisha yote haya inaitwa "Single Bullet theory", kwamba risasi ya kwanza kumpata Kennedy ndio risasi hiyo hiyo ilimpata Gavana Connally, Lakini kuna mazingira yanayoashiria kwa uthibitisho mkubwa kwamba Connally hakujeruhiwa na risasi ambayo ilimpata Kennedy mara ya kwanza.

Tuangalie hivi,

Ukitazama video katika frame ya 224 ni dhahiri kwamba huu ndio muda ambao risasi ya kwanza ilimpata Kennedy, hapa ndipo ambapo Kennedy anashtuka kwa maumivu na kunyanyua mkono wake wa kulia na kuukunja ngumi na kuuinua usawa wa mdomo, Katika muda ambao frame 224 inaishia ndipo ambapo Connally anaonekana kushtuka pia kisha anageuka upande wa kulia na kujitahidi kugeuka nyuma kana kwamba anajaribu kumuangalia Rais Kennedy.

Katika frame hii Gavana Connally haonyeshi dalili yoyote ya kuwa katika maumivu (licha ya kushtuka), Pia kuna dalili kadhaa zinaonyesha kuwa si muda huu ambapo alipigwa risasi, Mfano ukimuangalia mkononi bado ameshikilia kofia yake ya 'pama'. Kama unakumbuka nilishaeleza huko mwanzoni kwamba moja ya sehemu ya mwili wa Gavana Connally ambayo risasi ilipenya ilikuwa ni sehemu ya juu ya kiganja chake cha mkono wa kulia na mfupa wake kupasuka katika vipande vinane, kwa hiyo haitegemewi mtu ambaye kiganja kimegawanyika katika vipande vinane aendelee kuwa na uwezo wa kushikilia kitu mkononi.

Lakini pia, kingine kinachothibitisha kuwa Connally hakupigwa risasi katika frame ya 224 ni kauli ambayo aliwahi kuitoa yeye mwenyewe. Namnukuu "..nilisikia mlio ambao mara moja nikang'amua kuwa ulikuwa ni mlio wa risasi. Nikashtuka na kugeula upande wa kulia kwa sababu nilihisi mlio bunduki ilikuwa imefyatuliwa kutoka upande huo. Lakini sikuona kitu chochote, niliona tu kundi la watu wanatupungia mikono. Nilipokata jicho kumuangalia rais nyuma yangu sikuweza kumuona bara bara…. nilikuwa nataka nimuone rais ili kujua usalama wake kwa kuwa niliposikia tu mlio wa risasi hisia zangu ziliniambia kuwa kulikuwa na jaribio la mauaji ya rais..."

Zaidi kuhusu utofauti ya frames niliouzungumza hapo juu kuonyesha kuwa Kennedy anaonekana alipigwa risasi frame ya 224 na Connally alipigwa risasi frame ya 275, Connally anaeleza kuwa baada ya hapo akawa anaanza kugeuka na ndipo ambapo alisikia maumivu kifuani na alihisi kuwa amepigwa risasi ambayo hata hakuisikia mlio wake, Maelezo yake yanathibitishwa na ukiangalia kipande cha video, Connally anaonekana akitunisha mashavu kama anapuliza hewa nje na kukunja uso kwa uchungu katika frame ya 275 kuonyesha kwamba risasi ilikuwa imempata muda huu.

Sasa, kwanini nasisitiza na kuonyesha vidhibiti kuwa risasi iliyopata Kennedy katika frame ya 224 haikumpata Connally??..........

Iko hivi,

Ni kwamba, serikali kupitia Warren Commission wamekuwa wakieleza kuwa risasi iliyopata Kennedy ndiyi hiyo hiyo ilitokeza kifuani kwake na kwenda kumpiga Connally, ili hoja hii iwe sahihi maana yake ni kwamba kwa kuzingatia kasi ya mwendo wa risasi, tukio hili (risasi moja kumpiga Kennedy na Connally) lingetokea ndani ya 1/100 ya sekunde (sekunde moja gawanya kwa mia moja). Na tukio linalotokea ndani ya 1/100 ya sekunde haliwezi kurekodiwa kwenye frames tofauti ni lazima litatokea kwenye frame moja ya video.

Kutoka frame namba 224 ambayo Kennedy anapigwa risasi mpaka frame namba 275 ambayo Connally anaonyesha kuanza kuugulia maumivu ni takribani interval ya theluthi ya sekunde, Theluthi ya sekunde ni muda mwingi sana kwa risasi moja kusafiri kutoka kwa Kennedy kumpata Connally, Maelezo pekee ya kuelezea hili ni kwamba risasi ya kwanza kumpata Kennedy haikumpata Connally. Zilikuwa risasi mbili tofauti.

Lakini pia theluthi ya sekunde haitoshi kufyatua risasi mbili kutoka katika bunduki aina ya Mannlicher Carcona. Ukipiga risasi unahitaji kusubiri sekunde kadhaa ili 'kuikoki' tena bunduki na uweze kupiga tena, kwa kifupi ni kwamba kwa namna yoyote ile au muujiza wowote ule haiwezekani kufyatua risasi mbili ndani ya theluthi ya sekunde kutoka katika bunduki ya aina hii, Kwa hiyo hii inatueleza kwamba risasi iliyompiga Kennedy na iliyompiga Connally zilikuwa risasi mbili tofauti na zilipigwa kutoka kwa watu wawili tofauti.

Swali ni kina nani watu hawa??.......

Kabla hatujafika mbali kuanza kujiuliza ni nani mwingine labda alifyatua risasi nyingine hebu tuangalie vidhibiti zaidi, Baraza la Senate liliwahi kuunda kamati ya kuchunguza mauaji mbali mbali ya kupangwa yaliyowahi kutokea nchi Marekani. Kamati hii iliitwa House Select Committee on Assassinations au kuwa kifupi kama HSCA, Moja wapo ya chunguzi walizofanya ni kuhusu mauaji ya Rais Kennedy.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alikuwa ni mtaalamu nguli wa patholojia, Dr. Cyril Wecht, Dr. Wecht aliandika andiko la maoni yake kwa kamati hii teule ya Senate na akawaeleza kuhusu nadharia aliyokuja nayo kuhusu tukio hilo ambayo nadharia hii ilikuja kujulikana kwa wengi kama "Right to Left trajectory ", Kama nilivyoeleza kwamba, serikali kupitia Warren Commission wanadai kuwa risasi zilipigwa na Oswald akiwa mkono wa kulia wa jengo la Texas School Books Depository, Katika andiko lake kwenda kwa HSCA, Dr. Wecht anaeleza kwamba kwa kuzingatia kuwa ripoti ya serikali inaeleza kuwa risasi ilifyatuliwa kutoka ghorofa ya sita kutoka kwenye jengo tajwa, na pia kuzingatia upande wa jengo ambao unaelezwa Oswald alikaa, kwa maoni yake haiwezekani kwa risasi hiyo iliyompata Kennedy upande wa kulia pia kumpata Connally upande wa kulia wa ubavu chini kidogo ya kwapa

Kwanini?

Ukipima pembe mlalo (horizontal angle) kutoka jengo la Texas School Books Depository kwenda kwenye gari aliyomo rais na mahali ilipokuwa katika frame 190 ya kipande cha video unapata nyuzi 13 (kutoka kushoto kwenda kulia), Papo hapo pia ukipima pembe wima (vertical angle) kutoka ghorofa ya sita kwenda kwenye gari ya Rais unapata nyuzi 21 kama utapima kwa kuchukulia kuwa barabara ilikuwa tambarare iliyo sawa (horizontal plane) lakini kama ukizingatia kuwa gari la rais lilikuwa linapita kwenye barabara yenye 'slope' ya nyuzi 3 maana yake kwamba pembe wima ya kutoka ghorofa ya sita mpaka kwenye gari ya Rais inakuwa ni nyuzi 18.

Tazama kwa makini umbali na 'angle' kati ya jengo la Texas School Books Depository na mahali shots zilipotua (alama nyekundu kwenye Picha nilizoweka) Sasa, ifahamike kuwa namna ambavyo Rais Kennedy alikaa kwenye siti yake alikuwa amekaa kuegemea kabisa kwenye mlango wa gari na hata ukiangalia video kuanzia mwanzoni utaona akiwa ameweka mkono juu ya mlango wa gari. Lakini Gavana Connally alikuwa amekaa katikati ya siti yake mbali kidogo na mlango wa pembeni yake, hivyo basi kwa kuzingatia 'trajectory' ya risasi kutokana na nilivyoeleza position ya mdunguaji kule juu, Dr. Wecht anaweka hitimisho kwamba, kama risasi iliyompiga Kennedy ndiyo pia ilimpiga Connally basi ilitakiwa impate upande wa kushoto wa uti wa mgongo na sio kulia kama ambavyo ilitokea.

Kwa hiyo hii inatupa vidhibiti kingine kwamba kuna kila dalili kwamba kulikuwa na zaidi ya mdunguaji mmoja, ni nani huyo mdunguaji/wadunguaji mwingine???

Lakini pia, tuvute subira labla ya kujiuliza tena swali hili, tutazame kidhibiti kingine, Huko nyuma nilieleza juu ya mzozo uliotokea Parkland Memorial Hospital baada ya madaktari kugoma mwili wa Kennedy kuondolewa pasipo kufanyiwa autopsy lakini Kenneth O'Donnell na maafisa usalama wakatumia mabavu kuondoka nao mwili wa rais bila kufanyiwa autopsy, Kwanza hii inatia mashaka kuwa pengine kuna kitu ambacho madaktari wangekiona katika autopsy na kuvuruga kabisa kilichokuwa kimepangwa au maelezo ambayo tayari yalikuwa yameandaliwa na wauaji wa Kennedy kuaminisha ulimwengu.

Lakini hata hivyo bado kuna vitu kadhaa muhimu ambavyo vinaonekana katika cheti cha kifo kilichotolewa hospitali ya Parkland, Kwa mfano katika kwenye cheti inaonyesha kwamba Kennedy alipigwa risasi katika usawa pingili ya tatu ya shingo kwenda chini. Lakini katika ripoti ya Warren Commission wameongeza karibia inch tano au sita kwenda juu na kuripoti kuwa alipigwa risasi katika 'base of the neck', hii inatoa hisia kwamba walikuwa wanalazimisha kuweka usawa huu wa risasi kuingia ili waweze kuhalalisha wanachokilazimisha kwamba risasi hiyo hiyo ikaenda kumpiga Connally ubavuni chini kidogo ya kwapa la kulia.

Kama tukizingatia kilichoandikwa kwenye cheti cha kifo kwamba risasi ilipigwa katika 'third thoracic vertebrae' basi isingelimpata Connally ubavuni chini kidogo ya kwapa, pia daktari wa zamu ambaye alimpokea Kennedy siku hiyo hospitali, Dr. Robert N. McClelland anaeleza kuwa walipokuwa wanajitahidi kuokoa maisha ya rais, alipomuangalia nyuma ya kichwa kidonda alichokiona kwa utaalamu wake kilikuwa ni 'exit wound' (kidonda risasi ilipotokea), Kwa hiyo hii ina maanisha kwamba risasi iliingilia mbele na sio nyuma kama inavyodaiwa kwenye ripoti ya Warren Commission.

Hii pia inathibismtishwa hata ukiangalia video, rais Kennedy anapopigwa risasi ya pili anaonekana dhahiri kichwa kilisukumwa na risasi kurudi nyuma kwa kishindo. Na si hivyo tu hata kipande cha fuvu la kichwa kilichofumuliwa kinadondokea kwenye 'bodi' (trunk) ya nyuma ya gari, kiwango kikubwa cha ubongo kinarushwa nyuma ya gari na kudondokea kwenye follow up car ya wanausalama na kiwango kingine kinawadondokea hata mapolisi wa pikipiki waliopo nyuma.

Mojawapo wa mapolisi hawa wa piki piki Bobby Hargis, aliyekaa mkono wa kushoto nyuma ya gari ya Rais, anaeleza kuwa alidondokewa na kiwango kikubwa cha ubongo kilichoruka katika kasi kubwa na kutua kwa kishindo mwilini mwake kiasi kwamba alidhani labda naye amepatwa na moja ya risasi zilizokuwa zinapigwa, Hii yote inazidi kututhibitishia kuwa kulikuwa na waduanguaji zaidi ya mmoja katika tukio na mdunguaji aliyepiga risasi iliyomuua rais (fatal shot) alikuwa amekaa mbele ya msafara au mkabala nao lakini kamwe sio nyuma, tena juu ya ghorofa, na hii yote inathibitisha ukweli wa Cheti cha kifo cha Rais Kennedy ambacho kilitolewa na Parkland Memorial Hospital siku ya November 22, 1963

Ushahidi wa Abraham Zapruder.........

ushahidi mwingine katika tukio la kifo cha JF. Kennedy ni video iliyorokodiwa na mtu anayeitwa Abraham Zapruder. Hii ndio sababu ya kipande hiki maarufu cha video kuitwa "Zapruder Film", Huyu alikuwa ni mwananchi wa kawaida tu ambaye alikuwa na mapenzi makubwa na shabiki wa Rais Kennedy, kutokana na napenzi yake makubwa kwa Rais Kennedy alipojitokeza barabarani kwenda kumlaki rais kama wananchi wenzake wengine, aliamua kwenda na kamera yake ya matumizi ya nyumbani aina ya Bell & Howell Zoomatic Director Series (model 414 PD) ambayo aliinunua mwaka 1962.

Baada ya kurekodi tukio la kuwasili kwa rais na kwa bahati kufanikiwa kurekodi namna rais alivyopigwa risasi na baadae mkanda wake wa video kuchukuliwa na maafisa usalama, kuna memo iliyoandikwa kwa mkono na afisa wa Secret Services ambayo iliwahi kupatikana na kufanya Zapruder kuitwa kutoa ushahidi pindi Warren Commission ilipoundwa, meno hii iliandikwa siku ya tukio November 22, 1963 kutoka kwa Agent Maxwell D. Phillips kwenda kwa Agent James Rowley, Katika hiyo memo Agent Phillips anamueleza Agent Rowley kuwa "..kwa mujibu wa Mr. Zapruder, mdunguaji alikuwa nyuma ya Mr. Zapruder.."

Ikumbukwe kwamba Zapruder alikuwa anarekodi msafara akiwa kwa mbele (mbele ya msafara pambeni barabarani) na kipindi rais anapigwa risasi alikuwa karibia mkabala na gari la Rais. Kwa hiyo kuamini kwake kuwa mdunguaji alikuwa mahali fulani nyuma yake ilikuwa inathibitisha tena kwamba aliyemdungua Rais hakuwa juu ya ghorofa la Texas School Books Depository, Zapruder alipoitwa mbele ya Warren Commission aeleze kwa nini alihisi kuwa mdunguaji alikuwa mahali fulani nyuma yake, alisema kwamba alipokuwa anarekodi alipata fursa ya kuona kwa uzuri zaidi nini kilikuwa kinatokea. Kwanza aliona fuvu la mbele la rais linafumuliwa na kisha kichwa cha Rais kutupwa nyuma kwa kishindo kikubwa kuashiria kwamba risasi ilimpata kwa mbele.

Pia Zapruder akaeleza jambo ambalo pengine watu wachache waliokuwepo kwenye tukio waliliona, akasema kwamba… sekunde chache baada ya risasi iliyomdungua Rais, aliona kundi la maaskari wanakimbia kuelekea mahali fulani nyuma yake na aliamini kuwa nao wameng'amua kuwa mdunguaji alikuwa huko, ushahidi wa Zapruder una nguvu kubwa sana katika suala hili, kwani licha ya watu wengi kuwepo sehemu ambapo Rais Kennedy alidunguliwa kwa risasi lakini pengine yeye ndiye alifauatilia kwa umakini zaidi tukio hilo sekunde kwa sekunde na hata kulirekodi na mpaka leo hii kuwa ndio rekodi pekee ya video iliyopo juu ya tukio lile, Huyu bwana nitamuongelea kwa upana zaidi huko mbeleni na namna ambavyo alifarikia kwa "utata" miaka michache baadae, na si yeye pekee bali pia wenzake kadhaa ambao walikuwa watu muhimu sana kwenye kutatua kitendawili cha kifo cha Kennedy, watu kama Jack Ruby (aliyemuua Oswald hadharani) na Clay Shaw (asset wa CIA aliyeropoka kuhusu njama ya kumuua rais) nao walifariki vifo vya kutia shaka sana miaka michache baadae.

Mfano Zapruder alifariki kwa "kansa ya tumbo", Jack Ruby alifariki kwa " kansa ya kibofu", na Clay Shaw alifariki kwa "kansa ya pafu" ambayo ilienea kwenye ubongo na ini, Wote walipata hizi "kansa" miaka michache baada ya tukio na ndio ulikuwa muda ambao wananchi wamechachamaa nchini Marekani kutaka kujua ukweli wa nini kilitokea, Lakini maneno yake Zapruder kupitia ushahidi alioutoa mbele ya Warren Commission, yanaturejesha tena katika dalili zinazoonyesha na kuthibitisha kuwa kulikuwa na wadunguaji zaidi ya mmoja siku ile tofauti na serikali wanavyotaka tuamini.!!

Uhusiano wa kifo cha JF. Kennedy na operation ya Bay Of Pigs Invasion nchini Cuba......

Mara tu baada ya Fidel Castro kuchukua madaraka mwaka 1959, mwaka uliofuata yaani mwaka 1960, CIA kwa ruhusa ya Rais Dwight Eisenhower ambaye alikuwa anakaribia kuondoka madarakani walianzisha mikakati ya namna gani watamuondoa madarakani Fidel Castro, Fursa kuuu waliyoiona ni kutumia wahamiaji walioingia Marekani kutoka Cuba kukimbia utawala wa Fidel Castro uliokuwa "unafanya usafi" dhidi ya raia waliokuwa wanamuunga mkono Fulgencio Batista, Kwa hiyo CIA wakakusanya mamia ya raia hawa kwa siri kubwa na kuwapandikizia hari na ushaiwshi wa kutaka kumpindua Fidel Castro.

Mwezi March mwaka 1960 rais Dwight Eisenhower alipitisha bajeti ya dola milioni 13.1 kwa ajili ya mpango huu wa mapinduzi, Raia hawa wa Cuba waliokimbilia uhamishoni nchini Marekani wakapelekwa nchini Guatemala kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi hili kujiandaa na mapinduzi, Kikosi hiki kiliitwa Brigade 2506.

Mafunzo haya ya kijeshi yakaendelea kwa mwaka mzima nchini Guatemala, Mpango huu wa kuivamia Cuba na kumpindua Fidel Castro ulipangwa ufanyike mapema mwaka 1961 na ulikuwa umekamilika kila kitu lakini raisi Eisenhower hakuupa 'approval' na aliacha jukumu hilo la kuidhinisha uvamizi huo ifanywe na atakaye kuja kumrithi yaani Rais JF Kennedy, Kwa hiyo mara baada ya uchaguzi mkuu mwezi November, 1960 na hatimaye JF Kennedy kuapishwa January 20 mwaka 1961, kitu cha kwanza ambacho alikabiliana nacho ni CIA kumkabidhi mkakati ulioandaliwa na wao CIA chini ya Rais Dwight Eisenhower kuhusu uvamizi wa Cuba na kumpindua Fidel Castro.

Hapa ndipo ambapo kulianza kutokea mfululizo wa matukio ambayo huko mbeleni yalikuja kutengeneza uhasama mkubwa kati ya Rais Kennedy na CIA, katika jamii ya intelijensia, taarifa zinazoaminika ni kwamba CIA walipowasilisha mkakati wao wa mapinduzi ya Fidel Castro kuna vitu vingi vya msingi walimficha Kennedy, Na hii inaonekana kwamba walichukua 'advantage' kwa sababu ya ugeni wa Kennedy katika wadhifa wake huu upya wa Urais na kwa hiyo kutofahamu uhalisia wa vitu vingi kwa hiyo CIA wakatumia hiyo fursa 'kum-mislead' katika vitu muhimu kuhusu mkakati huo.

Mkakati ulikuwa ni mpana sana, lakini kwa ufupi ni kwamba, wavamizi hawa wa Brigade 2506 ilikuwa imepangwa wavamie Cuba wakitokea Guatemala na Nicaragua wakiwa na askari wa miguu pekee, Kennedy hakutaka Marekani ionekane ikihusika moja kwa moja kwenye uvamizi huo ili kulinda taswira yake katika jamii ya kimataifa na pia kuepuka kuamsha hasira za Urusi ambao walikuwa ni mshirika mkubwa wa Cuba, kwahiyo kukabiliana na hili, CIA walipendekeza kuwatumia makomando wake wa SAD katika kuongoza wapiganaji wa Brigade 2506, pamoja na hayo yote, Rais Kennedy alisisitiza sana kwamba ili kulinda taswira ya nchi ya Marekani yeye kama Rais hatoruhusu Marekani kufanya mashambulizi ya anga kusaidia katika mapambani hayo ya kumuondoa madarakani Fidel Castro.

CIA huku wakijua fika kwamba hawawezi kushinda uvamizi huo pasipo mashambulizi ya anga wakakubaliana na sharti la Rais Kennedy kwamba hakutakuwa na mashambulizi ya anga. Walikubali hili huku wakiwa na dhamira iliyojificha kwamba mara tu vita hiyo itakapoanza watamshinikiza Rais Kennedy atoe ruhusa ya kufanyika mashambulizi ya anga. Walikuwa wanaamini kwamba lazima Rais Kennedy atakubaliana na shinikizo lao pindi atakapoonyeshwa umuhimu wa mashambulizi ya anga pindi vita ikiwa inaendelea, na lazima atafanya hivyo ili kuepusha Marekani kuaibika kushindwa vita wanayoiunga mkono ili kulinda heshima yai ya kijeshi ambayo ilikuwa inahitajika kuliko kitu chochote katika kipindi hiki cha vita baridi.

Rais Kennedy aliidhinisha rasmi uvamizi huu siku ya tarehe 4 April 1961, takribani miezi mitatu tu baada ya kuingia madarakani, Wapiganaji wapatao 1400 wa Brigade 2605 waliogawanywa katika infantry batalioni zipatazo tano na paratrooper battalion moja waliingia katika pwani ya Cuba iitwayo Playa Girón kwa kutumia boti kutokea Guatemala na Nicaragua siku ya tarehe 13 April 1961, Baada ya uvamizi tu kuanza CIA wakaanza kuweka shinikizo kwa rais Kennedy aruhusu japo shambulio moja la anga la ndege za kivita za Marekani kuharibu miundombinu ya viawanja vya ndege za kijeshi vya Cuba. Kennedy alikataa katakata lakini CIA walipozidisha shinikizo na kumpa angalizo kuwa wasipofanya hivyo kuna uwezekano wa wapiganaji hao kushindwa kutekeleza mapinduzi ya kumuondoa Fidel Castro, Kennedy alilazimika na kuruhusu mashambulio ya anga kwa awamu moja pekee.

Hivyo basi tarehe 15 April 1961 ndege za kijeshi zilizo chini ya CIA aina ya B-26, zilishambulia viwanja vya ndege za jeshi la Cuba na hatimaye tarehe 16 April wapiganaji wa Brigade 2506 walivamia rasmi Cuba, Mwanzoni mwa uvamizi huu wapiganaji wa Brigade 2506 wakiongozwa na makomando wa SAD katika CIA walionekana kulidhibiti jeshi la Cuba ambapo mwanzoni mwa mapambano haya upande wa Cuba vikosi vya kijeshi vilikuwa vinaongozwa na José Ramón Fernández, Baada kuonekana kuwa jeshi la Cuba linazidiwa ujanja na wavamizi hawa waliokuja kufanya mapinduzi, Fidel Castro mwenyewe akaingia katika uwanja wa vita na kumuondoa José Fernández kwenye jukumu la kuongoza jeshi kwenye mapambano haya na kujipa yeye binafsi hilo jukimu la kuongoza wanajeshi.

Baada ya Castro kushikilia usukani wa kuongoza mapambano kwa upande wa jeshi la Cuba, wavamizi wa Brigade 2506 wakiongozwa na makomando wa Marekani walizidiwa ujanja na mbinu zote na wakaanza kupigwa kwa aibu kubwa, mpaka kufika tarehe 19 April, ilikuwa dhahiri kwamba ushindi uko upande wa vikosi vya Cuba, kwani walikuwa wanawapiga wavamizi kwa urahisi kana kwamba wanamsukuma mlevi, Ndipo hapa ambapo CIA wakarudi tena kwa rais Kennedy kutaka aidhinishe mashambulizi mengine ya anga, Safari hii Kennedy alikataa katakata, akidai kuwa dunia nzima itaona uvamizi huu imefanywa na Marekani na sio raia wa Cuba wanaoishi uhamishoni.

Kennedy alihofia kuwa kama Marekani itaingilia mapigano hayo kwa kiwango hicho, kulikuwa na uwezekano wa Urusi nayo kuingilia vita hiyo kusaidia upande wa Cuba, kutokana na mvutano mkubwa uliokuwepo baina yao, Kennedy alihofia kuwa ingeweza kuchochea vita nyingine kati ya Marekani na Urusi, vita ambayo ingeigharimu pande zote mbili na Dunia nzima kwa ujumla na pengine hata kusababisha vita kuu ya Tatu ya Dunia, kwa hiyo Kennedy safari hii akakataa katakata kuidhinisha mashambulio ya anga kwa kutumia jeshi la Marekani.

Joint Chiefs Of Staffs wakaja na pendekezo kwamba litengenezwe shambulio la uongo kwenye pwani ya Marekani na kisha kutupa lawama kwa Cuba ili kuhalalisha mashambulizi ya anga nchini Cuba, lakini bado pia Kennedy alishikilia msimamo wake kwamba hawezi kuidhinisha shambulio lolote la anga kufanywa na jeshi la Marekani, Hapa ndipo ambapo CIA iliumbuka, mkakati wao tangu awali ulikuwa ni lazima mashambulizi ya anga yafanyike kama ili kuweza kushinda mapigano na kuvishinda vikosi vya Castro na kumuondoa Madarakani. Lakini walimficha kitu hiki Rais Kennedy baada ya kumuona kuwa hasingeli idhinisha uvamizi huo kama wangemuweka wazi kuwa hawawezi kushinda pasipo mashambulio ya anga, Tegemeo lao la kumshawishi tena kwa mara ya pili yafanyike mashambulio ya anga ndio yalikuwa yamegonga mwamba.

Tarehe 20 April 1961, siku tatu baada ya uvamizi, wapiganaji waliipatowa mafunzo na kuongozawa na makomando wa Marekani, waliovamia nchini Cuba ili kumpindua Fidel Castro waliweka silaha chini na kusarenda kwa vikosi vya jeshi la Cuba, Ilikuwa ni aibu kubwa ambayo haijawahi kutokea katika historia ya jeshi la Marekani. Mateka waliokamatwa na vikosi vya Fidel Castro walihojiwa mubashara kwenye televisheni nchini Cuba na kutoa siri zote namna ambavyo Marekani ilihuiska katika uvamizi huo ambapo Marekani walikuwa wanatafuta sehemu ya kuficha nyuso zao kwa aibu, nchini Cuba taifa zima lilikuwa linasheherekea kwa shamra shamra kushangilia ushindi huo mnono. Fidel Castro aligeuka kuwa shujaa mpya wa Taifa na kujipatia heshima kubwa kimataifa kwa kushinda vita dhidi ya jeshi hatari la 'Marekani'.

Huko Marekani bado bundi alikuwa ndio kwanza ametua. Kila upande ulikuwa unamsukumia lawama upande mwingine, CIA walimuona Rais Kennedy kama ndio kisababishi cha wao kushindwa kutekeleza kwa ufanisi uvamizi na hatimaye kufanikisha kumuondoa madarakani Fidel Castro, Na kwa upande wa Rais Kennedy aliwaona CIA kama wasaliti kwa 'kumdanganya' na kutompa mkakati kamili tangu mwanzoni kwamba wasingelieweza kushinda vita ile pasipo mashambulizi ya anga, CIA wakamuona Rais Kennedy kama kiongozi ambaye si imara na shupavu au jasiri, na kwa muono wao walihisi kuwa hatoshi kuwa Rais wa Marekani.

Kwa upande wake Kennedy aliwaona CIA kama taasisi iliyopewa nguvu kiasi kwamba imelewa madaraka na kujiona wako huu ya kila kitu na kila mtu. Na moyoni mwake aliamini kuwa hilo linatakiwa kubadilika, Ikumbukwe pia kwamba hapa ilikuwa imepita miezi mitatu pekee tangu CIA wamuue Patrice Lumumba siku ya Tarehe 17 January, 1961 jimboni Katanga, Congo-Kinshasa, Kennedy anafahamika kuwa hakupendezwa na hili tukio lakini kwa kuwa lilitokea kabla hajawa Rais (siku tatu kabla) basi alilimezea mate lakini bado alibaki na kinyongo Kwa hiyo kufeli kwa uvamizi wa Bay of Pigs kuliamsha hasira zake zote alizonazo dhidi ya CIA.

Japokuwa katika umma na hata alipoongea na wanahabari Kennedy alikubali kubeba lawama zote kwa kuwa yeye ndiye aliidhinisha uvamizi huo, lakini pembeni akiwa faragha na wakubwa wenzake alikuwa anaotupia lawama kubwa CIA kuwa ndio waliosbabisha aibu kubwa hii iliyoipata Marekani na jeshi lake, Baada ya hapa mwenendo wa Kennedy ukaanza kubadilika mno. Mwanzoni alipoingia madarakani alikuwa ni tegemezi mno kwa kupatiwa muhtasri wa hali ya usalama wa nchi (Daily Presidential Briefing) kutoka kwa vyombo vya Ujasusi hasa CIA, lakini baada ya tukio la kufeli kwa uvamizi wa Cuba hakutaka tena kupatiwa briefing na CIA badala yake briefings zake zote sasa alizipokea kutoka kwa washauri wa usalama wa taifa (National Security Advisors).

Lakini hakuishia hapo tu, Kennedy kuonesha ni namna gani alikasirishwa alienda mbali zaidi kufanya kitendo ambacho kilipingwa na maafisa wengi wa CIA na wanazi wao, Kennedy alimfuta kazi Mkurugenzi Mkuu wa CIA Bw. Allen Dulles, Katika ulimwengu wa Intelijensia unapomuongelea Allen Dulles hamuongelei tu jasusi, bali ni jasusi mkongwe na mzoefu na wa kiwango cha daraja la kwanza kabisa na mwenye heshima iliyotukuka, Allen Dulles ndiye Mkurugenzi wa CIA aliyetumikia kwa kipindi kirefu zaidi katika historia ya Taasisi hiyo mpaka leo hii (tangu 1953 mpaka 1961), Allen Dulles ndiye aliyesimami mapinduzi ya Waziri mkuu wa Iran miaka ya 1940s (Operation Ajax), Allen Dulles ndiye aliyesimamia mapinduzi ya Rais wa Guatemala mika 1950s, Allen Dulles ndiye aliyesimamia program ya ndege za kijeshi ya Lockheed U-2, Pia huyu ndie aliye simama operation Barracuda iliyo ratibu kifo cha Patrice Lumumba wa Kongo DRC.

Allen Dulles ni kaka wa John Dulles, waziri wa mambo ya nje wa Marekani (Secretary of State) wakati wa utawala wa Rais Dwight Eisenhower ambaye ndiye amerithiwa na Kennedy miezi mitatu iliyopita, kwa hiyo inahitaji kujitoa ufahamu kumgusa mtu kama Allen Dulles. Na Kennedy alijitoa ufahamu na kumfuta kazi Allen Dulles mtu ambaye anapendwa na kuhusudiwa na majasusi wa CIA pengine kushinda hata Kennedy mwenyewe, Karatasi ya juu ya ripoti rasmi ya CIA ambayo ndani yake kuna baadhi ya paragraph zikionyesha kuwa CIA hawakuridhishwa na namna ambavyo Kennedy alifanya maamuzi juu ya kukataa mashambulio ya anga

Kennedy hakuishia hapa tu… akiwa faragha na wakubwa wenzake alitamka kauli iliyokuja kuwa maarufu sana hapo baadae baada ya kuvuja, alisema hivi, namnukuu; "…i want to splinter CIA in a thousand pieces and scatter it to the wind.." (Nataka kuivunja vunja CIA kwenye vipande elfu na kuipeperusha kwenye upepo), Akiwa na maana kwamba, amedhamiria kuibomoa CIA taratibu sana kipande kimoja baada ya kingine mpaka taasisi hiyo ipotee yote na isiwepo, Kauli yake hii, ilikuwa ni kana kwamba alikuwa ametia sahini ya kifo chake mwenyewe.

Unaweza kuunganisha Dots kupata majawabu stahiki kuhusu tukio la kifo cha JF.Kennedy lilisababisha na akina nani! Pia unaweza kugundua kuwa kuna jmbo kubwa zaidi linafichwa nyuma ya pazia na unaweza kuelewa kuna wahusika halisi wa kifo cha Kennedy ni wapi na kwa nini waliamua kumuua Kennedy??.......

Sasa turudi kwenye Warren commission.........

Katika ripoti ya The Warren Commision, ile kamisheni iliyoundwa na Rais Lyndon B. Johnson kuna mahala inasema kwamba kuna mtu ambaye alijitambulisha kama "Clay Bertrand" alimpigia simu Dean Andrews Jr. ambaye alikuwa ni mwanasheria wa kujitegemea kwenye jimbo la New Orleans kumtaka apande ndege kwenda Dallas kumtetea Lee Harvey Oswald, lakini wajumbe wa Warren Commision wanadai kwamba walihangaika mno bila mafanikio na hawakujua huyu "Clay Bertrand" ni nani na wakafanya hitimisho kwamba hili halikuwa jina halisi bali ni 'alias' ambayo ilitumiwa tu na huyo mtu.

Ilipofika mwaka 1967 mwezi March… mwanasheria wa serikali wa New Orleans wa kipindi hicho aliyeitwa Jim Garrison alifanikiwa kung'amua huyu "Clay Bertrand" ni nani haswa, Bw. Garrison aligundua kwamba kuna mfanya biashara maarufu sana ambaye alikuwa anatumia "alias" hiyo kwenye jumuiya za watu wanaojihusisha na mambo ya ushoga, Mfanyabiashara huyu maarufu sana miaka hiyo alikuwa anaitwa Clay Shaw, Huyu alikuwa ni muanzilishi wa shirika la International Trade Mart, ambapo shirika hili lilikuwa na lengo kuu la kuchochea biashara ya kimataifa na makao makuu yao yalikuwa ni New Orleans, Vile vile nchini Italy Clay Shaw alikuwa ni mjumbe wa bodi ya kampuni ya CMC (Centro Mondiale Commerciale) ambayo ilikuwa ni 'subsidiary' ya kampuni mama inayoitwa Permindex (Permenent Industrial Expositions).

Sasa katika ulimwengu wa Espionage na hata mambo ya uhalifu kuna kitu kinaitwa 'front organisations'. Hizi ni kampuni ambazo zinaanzishwa kwa siri na idara ya kijasusi kwa lengo la kutekeleza maslahi yake pasipo idara husika ya kijasusi kujulikana, Hizi ndizo zilikuwa ofisi za International Trade Mart Organasation huko New Orleans

Kwenye miaka ya hivi karibuni baada ya uchunguzi wa kina na nyaraka nyingi kuvuja imethibitika kwamba kwenye miaka ya 1960s na 1970s, CMC na Permindex zilikuwa zinatumiwa kama 'front organisation' za CIA kwenye nchi ya Italy. Kampuni hizi zilikiwa zinatumika kwa lengo kuu la kupitisha fedha kutoka CIA nchini Marekani na kwenda nchini Italia kugharamia mikakati ya kumuondoa madarakani Rais wa Italia kipindi hicho Bw. Charles de Gaulle ambaye alikuwa na sera za kufungamana mno na urusi na kupinga vikali siasa za kimagharibi, Katika bodi hiyo hiyo ya kampuni ya Permindex (na CMC) pia kulikuwa na mjumbe mwingine wa bodi aliyeitwa Loius Bloomfield.

Huyu alikuwa ni msomi wa hali ya juu na mfanyabiashara maarufu kutoka Canada ambaye kipindi cha uhai wake alionekana na wengi kama kiongozi wa jamii ya Wayahudi nchini Canada, Lakini ikumbukwe kwamba, Louis Bloomfield wakati wa vita kuu ya pili miaka ya 1940s aliitumikia idara ya kijasusi ya kimarekani iliyoitwa Office of Strategic Services. Idara hii ndio baadae (baada ya vita kuu ya pili) ilibadilishwa jina na kuitwa Central Intelligence Agency - CIA ambayo tunayo mpaka sasa, kwa maneno mengine mjumbe huyu wa bodi ya Permindex alikuwa ni jasusi nguli na hata kampuni yao hiyo (Permindex na CMC) kama ambavyo nimeeleza zilikuwa ni 'front organisation' za CIA.

Kwa hiyo basi kitendo cha mfanyabiashara maarufu Clay Shaw ambaye mwanasheria wa serikali Bw. Garrison aling'amua ndiye huwa anatumia a.k.a ya "clay bertrand"… kitendo chake cha kuwa pia mjumbe wa bodi ya CMC na Permindex inadhihirisha mafungamano yake na CIA na shughuli za kijasusi.

Hivyo basi….

Bila kuogopa mafungamano ya Clay Shaw na CIA, mwanasheria mkuu wa New Orleans Bw. Jim Garrison alimkamata Clay Shaw siku ya March 1, 1967 na kumfungulia mashtaka ya kupanga njama ya kumuua Rais Kennedy. Katika hati yake ya mashataka, Bw. Garrison alieleza pia kinaga ubaga kuwa CIA wamehusika pia kwenye tukio hilo, Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, Bw. Garrison alieleza mahakama sio tu kwamba Clay Shaw ndiye mwenye kutumia alias ya "Clay Bertrand" ambaye alikiwa anatafutwa miaka yote… bali pia alimleta shahidi wake aliyeitwa Perry Russo ambaye alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa masuala ya Bima.

Shahidi huyo alieleza mahakama kuwa alihudhuria tafrija nyumbani kwa bwana mmoja anaitwa David Ferrie ambaye anajulikana kuwa moja ya wapinzani wakubwa wa utawala wa Fidel Castro, shahidi akaeleza kuwa akiwa kwenye tafrija hiyo kwa bahati mbaya aliwasikia Clay Shaw, David Ferrie na watu wengine wachache ambao hakuwatambua walikuwa wamekaa chemba wakipeana maelekezo fulani kuhusu mpango huo.

Kesi hii iliunguruma kwa muda wa miaka miwili mfululizo. Lakini ajabu ni kwamba siku ya tarehe 1, March 1969…. Baraza la wazee wa mahakama (Jury) walikaa kwa muda wa chini ya nusu saa na kutoa uamuzi wa pamoja wa kumuachia Clay Shaw kuwa huru dhidi ya mashtaka yote hayo, Hii ilikuwa habari njema kwa CIA lakini umma ulijawa na hasira na hasira hizi walizielekeza moja kwa moja kwa Clay Shaw, Mwaka 1974 siku ya tarehe 15 August… Clay Shaw alifariki kwa "Kansa ya Mapafu", Kama ambavyo Jack Ruby (yule aliyempiga risasi Oswald) naye alifariki kwa "Kansa ya Mapafu" akiwa gerezani. Na msururu mrefu wa kila ambaye alionekana kujua uhalisia wa mauaji ya Kennedy alifariki muda mchache tu katika mazingira ambayo yanazua maswali mengi.

Tukio hili la mauaji ya Rais JF Kennedy, CIA hawawezi kuruka ukweli kwamba mikono yao ilimwaga damu yake, na kwasababu hiyo hata kifo cha ndugu yake JFK aliyeitwa Robert Kennedy maarufu kama "Bobby" ambaye kipindi cha utawala wa kaka yake JFK… yeye (Robert) alikuwa mwanasheria mkuu wa Marekani na kipindi anauwawa alikuwa kwenye kampeni za Urais ambazo zilikuwa na kila dalili ya kushinda kiti hicho.

CREDIT/ACKNOWLEDGEMENT:
Chanzo kikubwa cha makala hii hasa simulizi za kifo cha JF. Kennedy inatoka kwa Mchambuzi na Mwandishi wa makala za Kijasusi ndugu Habib Anga "The Bold" inayokwenda kwa jina "UTATA JUU YA KIFO CHA JF.KENNEDY" aliyo ichapisha Jamii Forum kwa mara ya kwanza tarehe 07/05/2017.

Chanzo kingine ni kutoka taarifa za FBI zilizotolewa mwaka 1971 na 2016, na CIA za mwaka 1985, 1998, 2011 na 2017.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

View attachment 1461883View attachment 1461884View attachment 1461885View attachment 1461887View attachment 1461888View attachment 1461889View attachment 1461890View attachment 1461891View attachment 1461892View attachment 1461893View attachment 1461894
...Makala Njema lakini kina mahali umeandika halo kuwa De Gaulle alikuwa in raisi wa Italy...Kumbukumbu zangu Mimi zinaniambia kuwa miaka hiyo ya mwanzo ya 60 De Gaulle alikuwa in raisi wa Ufaransa. Hebu cheki tena hili vizuri...
 
Ni ndefu mno ila haichoshi
Niliisoma nikalala nikaamka nikaendelea nikalala tena mpka imeisha
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom