Dr. Slaa Vs Lowassa Urais 2015

Dr. Slaa Vs Lowassa Urais 2015

Nani unaona anafaa kuwa Rais kati ya Wawili hawa?

  • Edward Lowassa

    Votes: 103 13.0%
  • Dr. Willibrod Slaa

    Votes: 640 80.6%
  • Wote hawafai/sijaamua

    Votes: 51 6.4%

  • Total voters
    794
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Khaa!!! Urais upi? Tanganyika? Z'bar? Au muungano?? Katiba bado nyie mmeanza kura. Tujifunze kutumia resources zetu vizuri. Au kama labda mnataka kupunguza stresses hapo sawa

Popote pale ilimradi wawe hawa wawili!
 
CCM fanyeni sub... May be mtoeni Lowassa, muwekeni Magufuli tuone...
 
Wakati gazeti la Nipashe likianzisha kura ya maoni miongoni mwa wana-CCM wanaotajwa kuwania kuteuliwa na CCM kuwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao kwa lengo la kugombea nafasi ya uraisi kupitia chama hicho na huku bwana Lowassa akiongoza kwa kura,nafikiri ni busara na sisi kupitia mtando huu wa JF kumpambanisha bwana Lowassa na Dr. Slaa katika kinyang'aricho hicho cha uraisi kwa mwaka 2015.

Tupige kura kwa kuandika jina tu la mgombea unaedhani atafaa kuwa raisi endapo itatokea hao wawili wanateuliwa kuviwakilisha vyama vyao katika uchaguzi mkuu ujao.

NB😛iga kura bila kuendesha campaign yoyote.

------------------------------------------------------------------

*Kwa maoni zaidi ya washiriki wa JamiiForums kupitia ukurasa wa Facebook - Dr. Wilbrod Slaa Vs Edward Lowassa (JamiiForums facebook page)

dr.......slaa.....
 
WanaJF,

Kwa ufahamu wangu wa mambo ni kwamba siku zote ukitaka kulinganisha vitu, huwenda kwa kufananisha au kuvipambanisha, ni lazima angalau viwe ama wawe (kama ni watu), vyenye kukalibiana.

Nimeona uzi hapa JF na baadhi ya vyanzo vingine vya mawasiliano vikiweka mashindano ya aina hii, yani kati ya Lowassa na watu aina ya Dr Slaa. Haya ni matusi wanaJF.

Hapa Tanzania, Lowassa ana historia pana na ndefu sana katika siasa zetu, hili halihitaji mjadala. Lowassa amekuwapo enzi na enzi, Lowassa anayajua mawimbi ya kila aina ya mikiki mikiki ya siasa, Lowassa anajua kupwa na kujaa kwa siasa, Lowassa anaijua saikolojia ya Watanzania vizuri. Kweli mtu wa aina hii una mlinganisha na Dr Slaa?!!!

Dr Slaa ametumia asilimia 65 - 70 ya maisha yake yote kama padre (ingawa palimshinda), mbali na hilo, ametumia asilimia 40 - 50 ya maisha yake nje ya mipaka ya Tanzania, Dr Slaa hatujui Watanzania. Iweje leo mtu wa aina hii awe na uhalali wa kupambanishwa na gwiji?

Namaliza kwa kusema kwamba, kama kuna matusi ya kumtukana Lowassa yapo basi yatumike hayo mengine, ila naombeni msimtukane Lowassa kwa kumpambanisha na Dr Slaa. Chonde chonde wana JF.
 
HAMY-D Bora ugeendelea kuongea na uyo ndugu hapo jilani yako kuhusu kauli za mwenyekiti wenu jana uko Mbeya kuliko kuandika kitu kama hii.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom