Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,884
NEC isipomuegua Tundu Lissu, ni go-ahead ya kuipoteza CCM Zanzibar. Je, muungano utasalimika?
Na, Robert Heriel
Jambo kubwa linaloendelea katika vichwa vya wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa ni pamoja na Tundu Lisu kupenya NEC. Hofu kubwa ipo miongoni mwa wafuasi wa Mgombea huyo wa CHADEMA wapo katika fukuto la wasiwasi kwa mgombea wao kuenguliwa. Pengine ni hofu ya uzushi kuwa Tundu Lisu ataenguliwa, lakini pengine sio uzushi bali ni jambo halisi kutoka kwa vyanzo walivyonavyo CHADEMA.
Tundu Lisu naye siku ya jana tarehe 23/08/2020 alielezea hofu yake ya kuenguliwa na NEC kugombea Nafasi ya Urais kupitia CHADEMA. Je hii ni njama na hila za CCM kuhakikisha Tundu Lisu hatoboi? Je, ni kwa nini njama hii itumike? Je, CCM wanaogopa kushindwa na Tundu Lisu? Lakini Maswali haya yanaweza yakamezwa na swali moja; kwani NEC ni CCM? Jibu, ni hapana. Kama NEC sio CCM Kwa nini Tundu Lisu aogope kukatwa? Labda tuseme kuwa Huenda CCM inamkono wake Huko NEC, Lakini nani ataweza kuthibitisha hayo? Je matendo ya NEC ni kiashiria cha hofu kwa Lissu?
Binafsi naamini kuwa Tundu Lisu hata apewe nafasi ya kugombea Urais kamwe hataweza kushinda, ingawaje anaweza kufurukuta na kujipatia kura nyingi tuu. Niliwahi kusema siku 60 ni nyingi sana kwa mtu mwenye uwezo wa kushawishi watu kama Tundu Lissu. Naufahamu uwezo wa Lisu katika kujenga hoja.
Kwa muono wangu, CCM hawana hofu na Tundu Lissu kushindwa, bali wanahofu ya kushindwa huko visiwani Zanzibar. Jicho langu linaniambia kuwa Tundu Lisu atapata 40% za kura huku Mhe Rais aliyemadarakani John Magufuli akipata kura 50%. Hata hivyo hilo ni jicho langu na linategemea na usawa katika mchakato wa uchaguzi. Jicho langu linaniambia kuwa hofu ya CCM ipo Zanzibar zaidi kuliko Bara.
Ili CCM iendelee kuwepo Zanzibar itabidi Tundu Lissu aenguliwe hivi Leo 25/08/2020. Kwa muono wangu, ACT- WAZALENDO itachukua Zanzibar licha ya kuwepo kwa Figisu Figisu. Maalimu Seif ananafasi kubwa ya kushinda huko Zanzibar, atakachohitaji na Backup kutoka bara ambayo ataipata kwa Tundu Lissu na Zito Kabwe.
Kutokana na Tabia ya Msimamo wa Tundu Lissu, kama hataenguliwa, najua atakubali kushindwa hiyo october 28 kama atakuwa ameshindwa halali na atashindwa halali. Lakini atampa nguvu Maalimu Seifu ambaye ataibuka kidedea huko Zanzibar.
Na ikiwa CCM itakuwa imepoteza Zanzibar ni wazi kuwa yatakuwa maandalizi ya 2025 kutolewa huku bara. Njia rahisi wanayoweza kuitumia Wapinzani ni kuiondoa CCM Zanzibar kwani kule ndio rahisi kutokana na udogo wa eneo na uchache wa watu. Kisha waje waiondoe huku bara.
Swali kubwa linalopiga kichwa changu ni je, usalama wa Muungano upo kwa kiasi gani mara tuu CCM itakapofungasha virago huko Zanzibar? Kwa jicho langu, naona muungano hautabaki salama. kulingana na viongozi wa Upinzani wanaogombea mwaka huu kote bara na visiwani. Tundu Lissu niliwahi kumsikia akizungumzia suala la Muungano alipokuwa akihutubia huko Zanzibar. Maneno yake nayakumbuka kiasi, ni kama alikuwa akiwaambia Wanzanzibar wanatawaliwa na Wabara, hivyo wanatakiwa wajikomboe. Lakini Pia ukimuangalia Maalimu Seif yeye naye anamsimamo wa namna hiyo ingawaje hapendi kuuonyesha.
Seif anachoshindwa mara nyingi kwenye uchaguzi huko Zanzibar ni Backup kutoka Bara. Mwaka 2015 hakupata Backup nzuri kutoka kwa Edward Lowasa, hii ni kutokana na tabia ya upole wa Lowasa wa kumuachia Mungu. Lakini mwaka huu, Tundu Lissu na Zito Kabwe watampa Backup ya kutosha endapo atashinda.
Nina uhakika CCM hawana Hofu kubwa na Tundu Lissu kushinda bara kwani wanajua hatashinda, lakini hofu ipo visiwani.
Muhimu: NEC izingatie haki kwa kila mgombea, asiwepo wa kuonewa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300