Serikali yenyewe ina viongozi ambao hawaongei kwa sauti moja.

Wakati Waziri Biteko anasema tatizo linaisha kwa bwawa jipya kuanza kazi, RC wa Dar Chalamila alisema tatizo halitaisha kwa sababu kuna matatizo mengi katika distribution network, hivyo hata baada ya bwawa kuanza kazi kuna changamoto.

So far inaonekana Chalamila alikuwa muwazi zaidi na Biteko analeta siasa zaidi kuliko uhalisia.
 
Umepungua kwa siku ngapi sasa?

Bado nina mashaka….muda utatueleza!

Tutaona hali itakavyokuwa miezi mitatu ijayo, miezi sita ijayo, miezi tisa inayo, na miaka ijayo.

Siku mbili tatu za afueni haziwezi kunisahaulisha kauli zao za huko nyuma.
Mkuu kwa jinsi mgao ulivyokuwa mkali, sidhani hata kama wiki imepita tokea huo mgao umeanza kupungua.

Ni sawa na kuishi kwa njaa muda mrefu halafu ukipata chakula kwa siku tatu mfululizo unaweza ukahisi kwamba baa la njaa limekwisha. Ni saikolojia tu.

Hivyo nakubaliana na wewe kuhusu muda. Maana ni kweli ni siku mbili tatu umeme haujakatika. Na ukikata unarudi hapo hapo. Na hilo siyo jambo zuri bado.
 
Kwa hali nnayoiona kuanzia jumapili kwa hapa Mbeya ni mgao haupo. Umeme upo na umekuwa wa uhakika katika siku mbili tatu hizi

Kazi imefanyika✌
 
Juzi juzi hapa nilifika ofisi fulani ya Nida ili nipewe kitambulisho changu baada ya kusikia vitambulisho vya 2020 vipo tayari.

in charge wa nida akakiri kwamba ni kweli Id zipo tayari ofisin kwake ila wanasubiri uzinduzi kwanza ndio wavigawe.
 
Back
Top Bottom