baz kaiza
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 11,495
- 12,107
Bila kujali unatokea wapi una umri gani ni mda kupambana kuondoa vyombo vya dola mikononi mwa wahuni. Tafadhali sana nilikua sijawahi kupata mda wa kuangalia clips za Mauaji yaliyotokea wakati wa maadamano kutokana na majukumu ya hapa na pale bwana bwana hii hakubaliki kila mtu mwenye akili timamu haiwezekani. Jana kuna clips nimeona police wakiwinda wananchi utafikili wanawinda swala au Simba hiyo clip itafuteni naona na Trafic mtu wa usalama barabarani kapewa nae bunduki kama nae anawida swala au Simba porini au magaidi. Hii imeniumiza sana ni mta watu wote kupambana kuviondoa vyombo vya dola mikononi mwa wahuni Hii nchi yetu sote ndo ulithi wetu haiwezekani vyombo vya dola vimilikiwe na wahuni vitumike kukandamiza wananchi vijana waodai haki zao kupitia maandamano ambayo yanatambulika kikatiba na kisheria alafu waanze kuwindwa kama wanyama wa porini. Kwa clips nilizoziona alichokua anasema Polepole ni kweli 100% vyombo vya dola ambayo vinalipwa mishahara kupitia kodi za Wananchi wote visingeweza kufanya vitendo vya kinyama namna ile ni kweli vimetekwa na wahuni ndo maana Lissu yuko jela kwasababu ya wahuni tuwakatae tukomboe vyombo vya dola yale mauaji yanatisha.