Umenena mkuu, mambo mengine ukitumia nguvu unaharibu zaidi,Uganda ilitakiwa ijiandae kwa kuwa independent kiuchumi,kísiasa,kijamii hata na kiuchumi pia.Itamuumiza sana kiuchumi na possibly ndo anaenda kuondoka softly au in a hard way.Hili jambo la ushoga na usagaji,lipo miaka na miaka na na haliwezi kumalizwa kiurahisirahisi kwa kasi yake ilivyotamalaki sasa.Mu7 angelikalia kimya huku wizara yake ya utamaduni ikilinda maadili kwa kutoa elimu kila uchwao kwa wananchi,ili maadili yaendelee kilindwa kama Zamani.Watakaopotoka wapotoke kivyao,na watakaofuata maadili wafuate kimyakimya kama ilivyokua kipindi cha nyuma.Inasikitisha sana mtu kuwa shoga,ila sasa kutunga sheria ngumu,sidhani kama ni suluhu,matokeo yake nchi yake huyu Mu7,itakosa madawa na misaada mingine,na suluhu itakua kufa au kuuawa na wazungu directly au indirectly.
Unamnyima Speaker wa Kiafrika Visa ya Marekani, umemkosesha nini, kuingia apple store ya Washington DC ????Naona spika wa Uganda kafutiwa Visa na Marekani. Museven kanyaga twende inabidi kuilinda human race isijimalize kama ambavyo mtu akitaka kujiua ni kosa.
Misingi ya Biblia inaruhusu kuua watu wasio na hatia kama Putin anavyofanya??Rais wa Marekani ni Mkatoriki nashangaa kwa kutofuata misingi ya Biblia. Nahisi hana washauri ktk kuabudu (Imani) ya Dini yake. Mara nyingi washauri wa Mme huwa ni Familia na Kiongozi wake wa Dini anakosari.
Yeye Kama Mkristo hata kama Sera ya Taifa lake ni Uenezaji Ushoga na labda kutoa Mimba, yeye ajarbu kuwa mtetezi kwa kukaa kimya. Hili awe kielelezo kwa Mataifa yenye kuabudu kwa Sheria za Mungu muhumba Mbingu na Nchi.
Naweza kutafsri demokrasia ya TAIFA hili Kama iliyopitiriza, na nimshauri Kiongozi wangu ambaye ni Rais hasimsikirize na wala hakuna haja ya kutunga Sheria maana sio utamaduni wa Mwafrica. Ila Tasisi za Dini zihamrishwe kuwa na sera ya kupinga Ushoga, ubahasha na usagaji na pia ktk Mitahara ya Elimu liwekwe hili.
Utamaduni wako ulikufa pale tu ulipoacha kuvaa ngozi na kaniki ukaanza kuvaa suti,Ushoga Sio utamaduni wetu waafrika mkuu
Hahahhahaha
Rais wa Marekani, Joe Biden ameilaani sheria mpya iliyotiwa saini na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni dhidi ya vitendo vya ushoga na kusema kuwa Marekani inaweza kuiwekea Uganda vikwazo huku akitoa wito wa sheria hiyo kufutwa mara moja.
Sheria hiyo mpya itawalazimu Watu wanaoshirki kwenye vitendo vya ushoga kutumikia hadi kifungo cha maisha jela.
Biden amesema ameliagiza Baraza la Usalama la Kitaifa la Ikulu ya Marekani kutathmini athari za sheria katika nyanja zote za ushirikiano wa Marekani na Uganda, ikiwa ni pamoja na uwezo wa Marekani kusitisha kutoa huduma za usalama chini ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kusaidia maambukizi ya UKIMWI (PEPFAR) na aina nyingine za msaada na uwekezaji.
Biden amesema Serikali yake itazingatia athari za sheria hiyo kama sehemu ya mapitio yake ya kustahiki kwa Uganda kwa Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika (AGOA), ambayo inatoa matibabu bila ushuru kwa bidhaa za nchi zilizoteuliwa za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Uganda inaenda kuwa kama Zimbabwe