Hawa waropokaji wengine huwa nawakaushia tu, flyover inajulikana imeanza chini ya magu na kaimaliza mwenyewe, mtu anakuambia aliianzisha kikwete, hii yote ni kwasababu ya kutafuta nafasi ya kulamba teuzi tu au upigaji tu ndo maana unaona ukosoaji wa magu umeshika kasi namna hii.
Nimeona kuna sehem mtu anakuambia EACOP ni mpango wa TOTAL na kwamba bila jitihada za serikali hili bomba lingepita tu Tanzania, hivi hawa watu wanataka kutufanya sisi ni mazoba na kwamba hatujui miradi mingi iliyotakiwa kuwa hapa ilienda kenya? Ofisi nyingi za kimataifa zilipelekwa Kenya wakati Arusha ipo na ni sehem salama? Waache ujinga kwenye credit mpe mtu hata kama humpendi.