Mkuu, duniani huwezi kufanya Kila kitu kwa wakati mmoja, nchi lazima iwe na vipaumbele vyake, hakuna nchi hata Moja duniani ambayo ipo mbele katika Kila kitu.
Tanzania na Africa kwa ujumla lazima tuanze na mambo "simple" ambayo hayahitaji Sana "HITECH", Ili kuwashirikisha watu wengi ambao Wana elimu ya kawawaida Sana.
Mkuu, bado nchi zetu hizi zinasumbuliwa na matatizo ya msingi kabisa, chakula, maradhi, upatikanaji wa maji safi, huduma za afya Bora, miundombinu ya usafirishaji, kilimo duni Cha kutegemea mvua, upungufu wa umeme wa kutosha, na ajira kwa vijana.
Anayofanya huyo Kijana wa Fernandez, sio kwamba sio muhimu, ila kwa Sasa hivi sio kipaumbele kwa Sasa, Wacha sector binafsi waingie kwa nguvu huko, serikali yetu sidhani Kama unapaswa kuilakamikia kwa Sasa.
Ngoja nikuulize swali, kwa kitendo Cha HQ ya NALA kuwa Kenya, Tanzania tumepungukiwa na lipi, hasa katika kutatua hayo niliyokutajia?