tuusan, nchi lazima iwe na vipaumbele na kuvisimamia kwa nguvu zote. Enzi za Nyerere vipaumbele vilikua ni Elimu, Afya, kilimo na viwanda.
Kwa uwezo wa uchumi wetu wakati ule, hayo yalitosha Sana kukausha pesa ya taifa.
Nyerere alifanikiwa kujenga shule nyingi na kutoa Elimu na Afya Bure, wakulima walipewa pembejeo Bure au kwa malipo kidogo Sana, wakulima hawakukopwa mazao yao. Viwanda vilijengwa na kutapakaa nchi nzima.
Ktk kutimiza vipaumbele hivyo, baadhi ya maeneo yalidumaa kabisa, Barabara na reli vilidumaa, mishahara ya watumishi ilikua midogo Sana, bidhaa muhimu hazikupatikana madukani, zikiwemo nguo, sabuni, sukari na vinginevyo. Watumishi hawakulalamika Sana kwasababu Nyerere alikua alieleza nini anataka kuifanyia nchi.
Magufuli pia alikua na vipaumbele vyake, reli, Barabara, viwanda, Afya na Elimu na ujenzi wa meli na kufufua ATCL, nidhamu na uwajibikaji serikalini, kubana matumizi serikalini
Alikua akisema kwamba, hatoweza kuongeza mishahara hadi atakapokamilisha hiyo miradi, sote tuliona ni kiasi gani hii miradi ambayo watangulizi wake waliogopa hata kuigusa lakini yeye aliamua kuianza.
Kati ya Kikwete ambaye kila mwaka alikua akiongeza mishahara na kusafiri kila wiki lakini alishindwa hata kujenga daraja la Wami, na Magufuli ambaye alikua hasafiri Wala kuongeza mishahara lakini alifanikiwa kukusanya pesa ya kujenga
1)Bwawa la Nyerere $2.9B
2)Daraja la Kigongo busisi Tsh 700B
3)Ndege 11 za ATCL $700M
4)Upabuzi wa Barabara ya Kibaha $60M
5)Daraja la Wami
6)Mali ya MV Mwanza Tsh 90M
7)SGR Dar - Moro $1.9B
Hivi kweli unasahau haya yote eti kwasababu watumishi wa serikali wasiozidi 2M hawajaongezewa mishajara?.
Sasa ukiacha kuongeza mishahara, tena kwa asilimia ndogo ambayo bado haiwatoshi ninyi watumishi hebu tupe vipaumbele vya SSH, ukiacha hiyo miradi aliyoikuta.