tuusan
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 17,973
- 20,222
Nadhani wewe unashida fulani,Mkuu kuwa mkweli, unawezaje kumsifia mtu anayemalizia kitu ambacho tayari kilianzishwa na kumpuuza muanzilishi mwenyewe?. Kama sio unafiki, mbona unasema miradi yote iliyofanyika kipindi cha Magufuli ni zao la Kikwete na Mkapa lakini husifii JPM kwa kuimalizia?.
Flyovers zote za Dar ni wazo la Magufuli, alianzisha mwenyewe na kutekeleza mwenyewe. Bwawa la Umeme la Nyerere ni wazo la Nyerere lakini utekelezaji wake(Master minder) ni JPM na umaliziaji wake ni SSH.
Meli mpya na ukarabati wa meli zote ziwa Victoria ni mawazo ya JPM na utekelezaji wake ni JPM by 80%
Kufufua ATCL ni wazo la JPM na utekelezaji wake ni JPM by 90%. Upanuzi wa Barbara ya Kimara Kibaha na daraja la Wami na ujenzi wa miradi ya kimkakati yakiwemo masoko na viwanja vya ndege na stand za mabusi ni JPM huyo mkuu.
Bado tunasubiri mama naye abuni miradi mipya wakati akiendelea kuimalizia hiyo aliyoikuta, bado nchi yetu ni changa Sana, Kuna maeneo mengi Sana yanahitaji kufanyiwa ubunifu, anachopaswa ni kutulia nchini na kubuni miradi ya maendeleo
Ameanzisha ama hakuanzisha iyo sisi haituhusu,Kazi ya serikali ni nn so far?
Haiwezekani tuko apa jukwaani bado tunasifia Sijui JPM ama SSH, ni suala la serikali kama serikali na ni muendelezo wa mambo tu hapa haya mambo yote yapo kwenye makaratasi tayari ...
Mfano....
Alieanzisha Tanroads ni mkapa lakini hakuweza kujenga barabara madaraja na viwanja vyote nchini kutokana na sababu mbalimbali sasa tutoke uko tujadili mambo ya msingi



