Mkuu, kukopa sio tatizo na ni lazima tukope, Mimi mwenyewe nimekopa pesa nyingi Sana, tatizo ni "attitude".
Mama amesema Jana akibaki hapa nchini na kutembelea mikoani hakutokua na maendeleo, lazima asafiri nje ya nchi, huko ndiko kwenye pesa,
Magufuli alikua akisema hii nchi ni tajiri Sana, tukijipanga vizuri kwa kudhibiti na kukusanya mapato na kuziba mianya ya upotevu wa mapato tunaweza kufanya Mambo makubwa hata kuwa "donor country".
Nimemjibu Tony254 kwa kirefu hapo juu kwa kuelezea Mambo mbalimbali aliyotumia Magufuli ili kuongeza uwezo wa serikali katika kukusanya mapato, chukulia suala la kukamata dhahabu na madini mengine yaliyokua yanatoroshwa na kuyataifisha, ilikua haipiti miezi miwili bila kusikia kilo kadhaa za dhahabu zimekamatwa zikitoroshwa na zimetaifishwa.
Kama unakamatwa na dhahabu ya 1B, kwanza unatozwa hiyo 1B, kisha hiyo dhahabu inataifishwa, maana yake serikali imepata 2B.
Kuhusu TRA kufikia malengo yake waliojiwekea, Hilo nalo ni tatizo kubwa, TRA inajiwekea malengo kulingana na mapungufu yake, sio kutokana "standard" za kidunia.
Kawaida Serikali yoyote duniani inapaswa kukusanya 24% ya GDP Kama Kodi, lakini nchi nyingi hukusanya 18%, TRA hadi Leo wanakusanya 13%, Sasa mkuu hayo ni malengo gani yaliyofikiwa hata kustahili kupongezwa?, Wanajiwekea wenyewe malengo ya chini ili waonekane wanafanya kazi vizuri.
Sent from my itel L5007 using
JamiiForums mobile app