Mkuu wangu kwanza nakuomba usiniweke maneno ambayo mimi sijayasema. Hakuna mahala nimesema Marekani wanafanya sensa kwa kufuata Ukatoliki.. Sensa ni ukusanyaji wa takwimu wa wananchi wanaoishi ktk nchi hiyo iwe hata Saudia au China. Pengine mnachukulia swala la economics juu juu tu kwa fikra za kuwa watu wote sawa wakati hakuna usawa ktk fikra na hulka za kila mmoja wetu isipokuwa sheria ndio hutazama usawa huo na kuulinda baada ya kuhesabiwa.
Hivyo jibu langu kwako kuhusu Marekani, ni kwamba wao hawahesabu watu kwa sababu ya Ukristu au Ukatoliki wao. Siamini hivyo na wala hakunakitu hicho ila wanahesabu WATU kwa sababu mfumo mzima wa Ubepari unatofautiana na UJAMAA ktk kutambua MTU ni nani.. sisi ktk Ujamaa tunajificha nyuma ya pazia wakati wao wanakuwa open UWAZI kutambua na kumdefine MTU ktk kumhesabu maana Hata Mungu mwenyewe katuumba sisi tofauti kwa nini hakutuumba sote tuwe na sura moja, umbo moja, lugha moja na kadhalika.. Na kwa imani ya dini yangu imenambia ya kwamba Mungu alituumba kwa tofauti hizi ili TUTAMBUANE yaani hizi tofauti ndizo ID ya kila mmoja wetu. Unapowahesabu watu kwa nini uziache?.. Sasa Mnataka kusema Mungu mjinga kuweka alama zote hizi ili tutambueane? Na kama sii swala la Kutambuana nambieni UMUHIMU wa sensa?.. hamtaki hadi sasa hivi.
Nasisitiza tena ya kwamba ni muhimu tukubali kwanza tofauti zetu, kisha sheria itaweza kulinda na kutambuliwa haki za hao waliohesabiwa hata iwe ktk ibada zao. Upebari unakubali usawa wa binadamu kwa lengo la kulinda haki za watu wote na sii usawa wa mgao wa keki maana sisi sote hatuna ashiki sawa, matamanio sawa, matumbo sawa wala njaa sawa!.. ila inakuhakikishia kukaa mezani maana umehesabiwa ua utalindwa.
UJAMAA unalazimisha watu wote tuwe sawa wakati hakuna usawa huo kifikra. nchi zote za kijamaa zine fail kutokana na kutokubali ukweli huu na ndio maana kuna ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu China, Russia, na nchi zote za kijamaa kuliko nchi za Kibepari. This is the main reason Ujamaa ulishindwa kutambua tofauti za binadamu kwanza na hivyo kuwalazimisha watu kuamini usawa ambao haupo na hivyo tukashindwa kulinda haki za wanyonge baina yetu.
Tumepumbazwa na mchanganyiko wa siasa za Kijamaa na Kibepari, lakini binafsi nimeweza kuelewa matumizi mabaya ya fikra hizi ktk jumuiya zetu na mazngira yetu. Wenye nchi (CCM) wanaendelea kuogopewa, kuheshimika kiasi kwamba hadi kesho wana uhakika wa wataendelea kushika madaraka na wao tu ndio haki ya kugawanya na kugawana keki ya taifa kwa sababu sheria zipo kuwalinda wao.
Mnapinga kuweka kipengele cha dini lakini kila mmoja wetu dini yake (what U believe in) kuwa MUHIMU kuliko vitu vingine vyote, tena naweza sema yawezekana kuwa muhimu zaidi kuliko hata rangi, jinsia, kabila au Uraia wa kila mmoja wetu hapa - Kwa nini tusihesabiwe?..Swala la kufikiria hizi dini zimekuja kwa nini ni swala lile lile la kujiuliza mengi hata maendeleo yenyewe unaweza kuyakana kama utapenda kwenda deep intensio ya maendeleo. It's all about money, utajiri biashara na huwezi kuzungumzia maendeleo pasipo Utajiri au money - The end justifies the means..
Kifupi kuna tofauti ndogo sana kati ya Utawala wa Kifalme na ule wa KIJAMAA ambao unatambua kundi fulani la watu kama Royal families na wanaheshimika hadi kesho. Katika Ujamaa kuna wenye nchi ambao ndio wa kwanza kwenye mgawanyo wa keki ya Taifa,. utaona tunapeana madaraka, kupeana kazi kwa kigezo cha nasaba.. Utaulizwa wewe mtoto na nani? aaaah Mkandara yule wa Chuo kikuu? nikisema hapana basi nimeshindwa interview..Hii yote ni kutokubali ukweli kwamba vita ya Udini na Ukabila inawezeshwa na ukweli ktk kulinda haki za wale wanaopuuzwa.
Na labda nikukumbushe tu ya kwamba kinachonichefua mimi hapa JF ni pale kila swala huchukuliwa Udini, ni rahisi mtu kuuliza dini ina faida gani ktk maendeleo ya nchi lakini mtu huyo huyo amepinga wazo hili kwa sababu alosema ni Muislaam. Na nikasema kama angekuwa Pengo ungesikia wakristu wote wamejipanga nyuma yake na Waislaam kuanza kupinga hoja hiyo. Jiulize kwa nini kila kinachofanyika nchini kinatazamwa kwa jicho la Udini, why wamesema Waislaam imekuwa issue kubwa hapa JF wakati wanahesabiwa pia wakristu, wapagani na Hindu na Krishna!.. au hofu yenu kubwa ni pale ikijulikana Waislaam ni wengi itakuwa kero na shida nyingine kutokana na siasa za mafichoni? elezeni hofu yenu halafu tutaipima yenyewe na sio kutaka kujua faida ya kuwepo dini ikiwa lengo ni kuweka takwimu za WATU na sio NCHI.