BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja Mkuu, Jun 13, 2012.

 1. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

  BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

  Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

  “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


  Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

  Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

  Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

  “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

  Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

  “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

  Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


  Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


  Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

  Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

  CHANZO: HabariLeo
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Jamani, mbona sensa za Kidini ni raisi mno kuzifanya, Kama kuna dini ama dhehebu inataka kujua ina waumini wangapi kuna shida gani ya kujihesabu kwenye masinagogi na mahekalu yao?

  Issue ya Dini na wala ukabila hauna umuhimu wowote kwenye sensa, tukishajua idadi ya dini fulani ndio wengi itasaidia nini?, maana tukisema wapewe upendeleo walio wengi (Kidini) na Wasukuma nao watataka upendeleo kwa sababu nao watasema wapo wengi na hawana uwakilishi wenye uwiano

  Kwa nini Bakwata wasitafute njia ya kuwekeza kwenye mambo ya Kijamii, (shule, Vyuo, Mahospital nk)?
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  kama hawataki tutawakadiria tu kama mafungu ya nyanya...
  wao kila siku ni negative ishues kwa kisingizio cha dini tu hawana chema???
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Thanks...nini tena kitasusiwa baada ya sensa?
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  suala la sensa lenyewe kwa ujumla wake halina tija sembuse kuweka kipengele cha dini
   
 6. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  baadae watasema kama rais,makamu na mawaziri wajao wasipokuwa waislamu watahama nchi
  na watataka nchi ifuate mfumo wa sharia
  wanadhani JK atawapigia magoti kuwaomba washiriki.
  tutawakadiria tunajua idadi yao haizidi 40% ya watanzania wote.
  HAKUNA KUWAENDEKEZA HAWA KAMA WANATAKA WAHAMIE SOMALIA AU UARABUNI
   
 7. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  sensa ni ya raia wa tanzania sio bakwata,kwani bakwata wako wangapi?tukijua bakwata ni wangapi itatusaidia nini kwa maendeleo?
   
 8. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kweli?:majani7: ...buffalo soldier... the hypocrites...
   
 9. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,174
  Likes Received: 10,515
  Trophy Points: 280
  Hiki kizazi cha Eshumaili kina tabu sana....... anyway tutafanyaje sasa inabidi tukaenao hivo hivo tuu labda kuna siku watabaadilika.
   
 10. B

  Bob G JF Bronze Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sensa ni kazi ya serikali Bakwata inahusikaje? Kama Bakwata wanataka kujua waumini wao kwanini wasiwahesabu? Mbona Wakristo wanajihesabu kila siku ya IBADA
   
 11. B

  Bob G JF Bronze Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sema wewe Kituko labda watakusikia hawa, maana kila kukicha ni malalamiko ova walikua wamezibwa mdomo na Super glew sa imebanduka. Tunalo!
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Hii Habari siwezi kuiamini haina ukweli wowote, Bakwata ni tawi la CCM sasa ni kitu ambacho hakiwezekani kupingana na Serikali yao wanayoitumikia, kama kuna kauli ya namna hii imetolewa basi itakuwa ni ya yule muhuni anayeitwa Shekh Ponda ambaye yuko kwenye jumuiya nyingine ambayo haina tofauti na UAMSHO.
   
 13. ha ha ha

  ha ha ha JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 641
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  i think ubwabwa..
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  An empty head is devil's workshop.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 15. D

  David webb Senior Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

  Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

  Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
   
 16. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ninatumaini kuwa maamuzi ya Waislamu yataheshimiwa katika nchi ya Kidemokrasia kama Tanzania.
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Maamuzi ya kupinga sensa? Itakuwa ni ujinga usiopingika kama unakuwa ni mnafiki wa mambo yenye maendelea bila sababu yeyote ya msingi ntashindwa hata kuwashangaa na hata wewe unaewasapot
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sensa ya mwaka 1957 haikuonyesha idadi ya Waislamu kuwa 65%. Pia kuna sensa iliyofuata 1967 pia ina takwim inayoonyesha idadi ya Waislamu na Wakristo. Kwa hiyo si sahihi unaposema kuwa baada ya 1957 sensa zote zilizofuata zilifuta kipengele kinachoonyesha dini za watu.
   
 19. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ni vizuri sana kwanini utoe kipengele cha dini?
   
 20. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  yeah Waislamu walikuwa wengi, Msisahau pia Wapagani au Wanaoamini Dini za kienyeji walikuwa wengi sana...
   
Loading...