BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

asaaalaam alequum.. Jaman tusigome sensa..! Tuweni na busara na hekima ili tuwe na aman kama mtume ..alivyo kuwa na busara na hekima mwenyez mungu akampa amani nae akawa rafiki wa aman na kuishi kwa aman.. Maisha yake yote!
 
MWISHO YA YOTE HAYA WAISLAM WATAPENDA WAJUE MTAA UPI KUNA NYUMBA NGAPI ZA WAKRISTO, NGAPI ZA WAISLAM WASHIKAO MSIMAMO MKALI, WAPI VUGUVUGU. PIA WATANZANIA WAJUE KWAMBA BAADA YA KUHESABU WANGAPI WAISLAM WANGAPI WAKRISTO KITAFUATA NINI TENA CHA KUHESABU KAMA SIO KKUSEMA TUNATAKA TANZANIA IFANYE KAZI UNDER SHARIAH LAW KWANI WAISLAM NI WENGI. PIA POINT IFUATAYO TUIANGALIE SANA ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” JAMANI NANI KASEMA WAISLAM HAWANA MAENDELEO? MBONA TUNA MIFANO MINGI TU YA WAISLAM WASOMI KABISA NA WENYE MADARAKA MAKUBWA TU HAPA NCHINI? ANZIA VYUO VIKUU VYOTE UTAONA WAHADHIRI NA WATUMISHI WAKE WENGI NI WAISLAM. ANGALIA IDARA MBALIMBALI. SASA LA KUGOMEA SENSA WAISLAM WANATAKA NCHI IJIPANGEJE KUWEKA VIPAUMBELE VYAKE? THINK TWICE WAPENDWA ZETU, RAFIKI ZANGU WENGI NI WAISLAM AKIWEMO NIMPENDAYE LAKINI KATIKA HILI NASEMA ASIKUBALIANE NAO
 
By
quote_icon.png
KALAMAZOO1

Kumbe sasa unapinga nini wakati unajua kuwa waislamu hawana elimu inabidi serikali ijue idadi yao ili ipange mipango ya kuwaptia elimu
Kwani sasa hivi wamenyimwa hiyo elimu?
 
asaaalaam alequum.. Jaman tusigome sensa..! Tuweni na busara na hekima ili tuwe na aman kama mtume ..alivyo kuwa na busara na hekima mwenyez mungu akampa amani nae akawa rafiki wa aman na kuishi kwa aman.. Maisha yake yote!

Waalekum..., Kwa waislamu kogomea tu hiyo sensa, na si kuchukua hatua nyengine yeyote zaidi ya hapo kwa sasa, ni sawa na ndio hatua afadhali (bora), yenye salama na amani kuliko zote ambazo wanaweza kuzifanya. Hekima yake ni kwamba ukamilifu wa hiyo sensa utapatikana inavyotakiwa, yaani:
1. Idadi ya waTanzania wote ni sensa iliyopita ni milioni 47
2. Wataoshiriki hii sensa ni wasio waislamu (yaani hasa wakristo) idadi yao itajulikana.
3. Waliobaki wasioshiriki itakuwa idadi ya waislamu(i. halisi ii. wasio halisi:- yaani wenye
kukubali kwa fikra zao wakiwemo wakristo wenye kupenda kulinda amani na utulivu wa nchi yetu
kwa kugundua umuhimu wa kuendelea kutambuana na kuheshimiana dini na imani zetu ambazo
zimetulindia maadili yetu.

Hapa ujanja uliopo ndugu yangu ni kuwa hiyo sensa inadhaminiwa na waMagharibi katika ile mbiu ya "Malengo ya Maendeleo ya karne" "Millenium Development Goals" na wanajificha katika mbiu hiyo lakini malengo yao hasa ni ili kutuacha uchi na dhaifu kimaadili ni lazima waondoshe "kwanza" hiki kipengele cha dini (imani zetu ambazo ndio chemchem za maadili yetu), yaani isiwe kama tulivyozowea kwamba ni "serikali (nchi)tu ndio isiyo na dini, lakini sisi wananchi tunazo dini zetu (tunatambuana na kuheshimiana na ndizo zinazotujengea maadili yetu kama tuliyo nayo)" lakini sasa watufanye na kututambua ya kwamba " Sio serikali tu ndio isiyo na dini bali hata sisi wananchi vile vile tutambulike ya kwamba "HATUNA DINI" kwa maana hatuna maadili yeyote.

Kitachofuata baada ya hapo ndio hiyo mipango ya experiment ilibandikwa jina na "Millenium Development Goals" iliyofungashwa na "demokrasia na haki za binadamu". Zigo hili lina mambo na mipango miiiiiingi isiyo ya kimaadili, yenye maadili maovu, yenye kupingana na maadili yetu adhimu, nk, nk. Au hujui wewe ndugu yangu kwamba waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ni mke wa mwanamme mweziwe? Au hujui wewe ndugu yangu kwamba waziri mkuu wa Ubelgiji au kama sikosei Luxemburg ni mume au sijui mke wa mwanamme mwenziwe. Kwa kifupi kuna lobby kubwa sana kwa nchi za Magharibi kutaka na sisi waArfika tufuate mkumbo huo huo, kwa hiari au lazima. Au hukusikia ndugu yangu jinsi Cameron (asiye na adabu) alivyoweza kuwaambia watu katika kadamnasi ya "Commonwealth" kuhusiana na hili kwa kupitia mgongo wa "haki za binadamu:???? Sasa kwa kuwa kwa hiari huwa tunajipapatuapapatua (na hii sio kutokana na ushupavu wa viongozi wetu wa serikali, la hasha!!!, hii ni kutokana na wao kujua maadili yetu wananchi (yaliyojengwa na imani na dini zetu) ndio maana wamegwaya kidogo, hawana njia kwa sasa ya kutu-convince, kinyume na hivyo hawa viongozi wetu wangeshatuuza kwa bei ya dezo zamaaaaaani, si unajua akili zao zilivyo kiufisadi?? Sasa hii ni moja ya mtego. Cameron (habithi) alituonya kwamba atazuia misaada na sasa watasema "hatutakadiriwa katika mipango ya maendeleo ya karne"

Haiwezekani kwamba mambo na mipango kabambe kama hii viongozi wa makanisa wasitambue au hata kushuku, isipokuwa labda ni ufuu wa akili, kutokuona mbali au ni kwa makusudi. Inasikitisha na ni bahati mbaya kwamba waumini wa kikristo pia wamepigwa changa la macho.
 
Hakuna kitu kimoja kinachoitwa waislamu,labda kama wanataka kujua idadi ya
1. madhehebu ya shia
a)hapa kuna karibu madhehebu madogo madogo zaidi ya kumi
2. Suni
3. Ismailia
4. Sufi
5 Salafi.
6. kurdishi
6. n.k

sasa wasitudanganye wanataka kujua kuna waislamu wangapi, hakuna kitu kimoja kinachoitwa waislamu, wangekuwa wamoja wasinge uana wao kwa wao.
 
Na maanisha, swala la dini lina matatizo na maswali mengi sana, hasa Tanzania. Ni swala ambalo limeshaleta machafuko na maafa duniani. In short, hili ni 'tatizo'. Hivi taifa likigawanyika how will you deal with that situation?

Kwa hiyo swala hapa ni kwamba either uwe mkristo au muislamu au dini yoyote, hilo halina uhusiano wowote na serikali, utajua wewe na Mungu wako. Ndo maana serikali inasema haina dini, very good point, inachojua ni haki za binadamu on contemporary basis, kwa mfano haki za watu kuabudu, kuishi, kunywa maji safi na salama, kulala mahali pazuri, kusoma, kupiga kura nk. Na katika hili zingatia kwamba huwezi leo kuanzisha dini inayokula watu halafu serikali ikakuruhusu eti kwa sababu tu 'unauhuru wa kuabudu'. Haya ni baadhi tu ya maswala ambayo serikali inadili nayo. Kama utakubaliana na mimi, haya maswala hayana uhusiona wa moja kwa moja na dini yako, na ndo maana hatuendi shule kusoma dini. Kwa hiyo tunapozungumzia maswala ya serikali , mambo ya dini hayana nafasi. Swala la haki za waislamu au wakristo wakadai misikitini au makanisani ambako tunaamini kuna maisha ya milele.

Kama waislamu wanataka kugoma ili serikali iwasikie vizuri basi wagome kwenda misikitini kusali mpaka serikali iwajengee misikiti au mbona hamgomi kusali kwa sababu serikali haijawaletea maji ya kunawa? au hivi siyo vya muhimu kwenu? au inabidi kuwa shirikisha wakristo kwenye vitu kama hivi?

Alafu sijawahi kusikia kwamba taasisi za kidini haziruhusiwi kuwa na idadi ya waumini wao, au nimeelewa tofauti?

Hasa Tanzania !!! tangu lini, what a scare mongering slogan!!!!

Naona Mkuu unajichanganya au hukufahamu niliyoandika, baadhi ya point unarudia nilizoandika na ambavyo sote tunajua na wewe unazielezea hapa kama mimi nimezikataa. Mfano: Kusema serikali haina dini, nani asiyelijua hilo au nani analikataa?? Linalokataliwa na Waislamu ni kule kusema "Hata Wananchi vile vile hawana dini" Je hii kwa maoni yako ni sawa?? Kipengele cha dini kutokuwemo katika sensa maana yake ni kwamba "hatuulizwi, na kama hatuulizwi ni kwamba hatutatambulika, na kama hatutambulika, ni kwamba hatutaheshimka" Je hii kwako au viongozi wa kanisa lako ni sawa???

Mimi nilisema Wakristo wanaruhusiwa kuendesha na kuweka takwimu za idadi ya waumini wao, hata waislamu vile vile wanaruhusiwa, lakini nani wa kumuamini?, nani asiyejipendelea? Ndio maana inakuja kwamba ni serikali, utawala ndio uwe na mamlaka katika jambo hili KITAIFA, KITAIFA ndugu yangu, na sio taasisi za kibinafsi ikiwemo kanisa. Waislamu wanalijua hili na ukweli kwamba dini haitegemei saaaana idadi ya wanaodai wanaamini, bali hutegemea umadhubuti wa imani ya wale wenye kuamini, hivyo hawaendeshi sensa, na wanaliachia jukumu hilo SERIKALI na kuomba, kutaka, kutegemea na kuangalia kwamba inatenda haki, SASA KWANINI WAKWEPE WAJIBU WAO NA KUKIKWEPA KIPENGELE HICHO CHA DINI???? Sijui Mkuu unafahamu sijui.

Ndugu yangu hebu tafakari kisha eleza:
1. Ni nini kinachokupa hii idea na mentality kwamba waislamu wanapenda machafuko Tanzania inatokeo wapi kama sio u-kasumba? unaotokana na unayoyasikia bila ya kutafakari.
2. Nini waislamu watafaidika kwa machafuko??
3. Ukweli ni makanisa na viongozi wa makanisa, na baadhi ya waumini wa kikristo ndio wanauchukia utulivu uhuru wa maoni na kujadiliana, na ndio wao hushirikiana (wao kiroho na kijamii) na Imperialists (kisiasa, kiuchumi na kijeshi)kupenyeza fitna ili machafuko yatokee kwa faida ya "civilisation" au system ambayo wana-share kiutawala. Moja ya fitna hizo ni mambo yatakayokuwemo ndani ya hiyo "Millenium Development goals", ina mikono yao yote (Kanisa na Western impeliastic ideas) na ndio maana Viongozi wa makanisa Tanzania wamekaa kimya kwa kipengele hicho kutokuwekwa katika sensa inayoendeshwa KITAIFA. Je hawataki wao sensa halisi ifanywe na serikali?
 
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

“Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

“Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

“Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali

Mi nadhani ni ukosefu tu wa elimu ya kutosha kwa hii BAKWATA badala ya kufanya maswala ya msingi mnaishia tu kulalamika mambo yasiyo msingi si muhesabu waislamu nyie wenyewe huko msikitini kama wanavyofanya wengine kujua waumini wao...........na mnataka kipengele hicho kiwekwe ili mpate faida gani...........UJUMBE WANGU KWENI NI KWAMBA KADIRI NINYI MNAVYOFIKIRIA KULALAMIKA WENZENU WANAFIKIRIA NAMNA YA KUJIENDELEZA ZAIDI
 
Hasa Tanzania !!! tangu lini, what a scare mongering slogan!!!!

Naona Mkuu unajichanganya au hukufahamu niliyoandika, baadhi ya point unarudia nilizoandika na ambavyo sote tunajua na wewe unazielezea hapa kama mimi nimezikataa. Mfano: Kusema serikali haina dini, nani asiyelijua hilo au nani analikataa?? Linalokataliwa na Waislamu ni kule kusema "Hata Wananchi vile vile hawana dini" Je hii kwa maoni yako ni sawa?? Kipengele cha dini kutokuwemo katika sensa maana yake ni kwamba "hatuulizwi, na kama hatuulizwi ni kwamba hatutatambulika, na kama hatutambulika, ni kwamba hatutaheshimka" Je hii kwako au viongozi wa kanisa lako ni sawa???

Mimi nilisema Wakristo wanaruhusiwa kuendesha na kuweka takwimu za idadi ya waumini wao, hata waislamu vile vile wanaruhusiwa, lakini nani wa kumuamini?, nani asiyejipendelea? Ndio maana inakuja kwamba ni serikali, utawala ndio uwe na mamlaka katika jambo hili KITAIFA, KITAIFA ndugu yangu, na sio taasisi za kibinafsi ikiwemo kanisa. Waislamu wanalijua hili na ukweli kwamba dini haitegemei saaaana idadi ya wanaodai wanaamini, bali hutegemea umadhubuti wa imani ya wale wenye kuamini, hivyo hawaendeshi sensa, na wanaliachia jukumu hilo SERIKALI na kuomba, kutaka, kutegemea na kuangalia kwamba inatenda haki, SASA KWANINI WAKWEPE WAJIBU WAO NA KUKIKWEPA KIPENGELE HICHO CHA DINI???? Sijui Mkuu unafahamu sijui.

Ndugu yangu hebu tafakari kisha eleza:
1. Ni nini kinachokupa hii idea na mentality kwamba waislamu wanapenda machafuko Tanzania inatokeo wapi kama sio u-kasumba? unaotokana na unayoyasikia bila ya kutafakari.
2. Nini waislamu watafaidika kwa machafuko??
3. Ukweli ni makanisa na viongozi wa makanisa, na baadhi ya waumini wa kikristo ndio wanauchukia utulivu uhuru wa maoni na kujadiliana, na ndio wao hushirikiana (wao kiroho na kijamii) na Imperialists (kisiasa, kiuchumi na kijeshi)kupenyeza fitna ili machafuko yatokee kwa faida ya "civilisation" au system ambayo wana-share kiutawala. Moja ya fitna hizo ni mambo yatakayokuwemo ndani ya hiyo "Millenium Development goals", ina mikono yao yote (Kanisa na Western impeliastic ideas) na ndio maana Viongozi wa makanisa Tanzania wamekaa kimya kwa kipengele hicho kutokuwekwa katika sensa inayoendeshwa KITAIFA. Je hawataki wao sensa halisi ifanywe na serikali?

Mkuu Joka kunavitu viwili ambavyo inabidi tuvitofautishe, kuna wananchi kuwa na dini na kuna dini zao kutambulika na seriakali, sasa ni nani kasema hata wananchi vile vile hawana dini? Mimi kwa mtazamo wangu serikali kama serikali haitaji kutambua dini yako wewe kama wewe, ila dini zote zinatambulika kisheria kama jumuiya, kama zilivyo jumuiya nyingine au taasisi zozote.

Alafu labda nikucaution tu, dont be too delutional. Mi sijapoint fingers kwamba waislamu Tanzania wanafujo, I said swala la udini linaweza kuleta machafuko kama ambavyo imetokea sehemu nyingi duniani. Hilo halina ubishi, mifano tunayo. Alafu isitoshe watu wengi hawana elimu ya kutosha Tanzania kuelewa vitu kama hivi, kwa hiyo ni rahisi kupotoshwa. Hivi haoni kwamba this a 'vulnerable issue'?


Hivi unavyosema 'haki' ukimaanisha kwamba ni jukumu au wajibu wa serikali hauoni kwamba unapingana na mtazamo kwamba serikali haina dini? Kitu ambacho wewe mwenyewe umekubaliana nacho. Huku siyo kuwa delutional kweli?Unaweza kutofautisha mtazamo wako na hiki kipengele cha kutokuwa na dini?

Kwenye point ya tatu, unahofu na ufisadi, maadili kuporomoka au unahofu na ukristo au unahofu na mabepari? Yani sielewi yani? Kwa sababu hivi vitu havina uhusiano. Alafu sioni sababu ya kuhusisha ukristo na mabepari, ndo maana mi nasema you are kind of delutional, hauja fahamu vizuri what do you want, au labda unadhani sensa ya kidini itawaondoa mabepari wa uarabuni au magharibi!!? au anadhani kuporomoka kwa maadili kwenye uislamu kunatokana na idadi ya watu watu wadini za tofauti?

Swala hapa ndugu yangu ni jinsi gani serikali yetu itaendeshwa bila kuhusisha au kujihisisha na dini ya aina yoyote, hasa hizi zilizopitwa na wakati kutoka middle east.
 
Wana JF.
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania zimetangaza rasmi mgogoro na Serikali baada ya kueleza kuwa haitashiriki Sensa ya Watu na Makazi kutokana na muhimili huo wa Dola kukataa kuingiza kipengele cha dini kwenye dodoso la Sensa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Issa Ponda alisema, Jumuiya za Kiislamu ziliwasilisha serikalini mapendekezo matatu kabla ya Waislamu kushiriki zoezi hilo.

Mapendekezo hayo kushauriana na wawakilishi wa dini iunde tume huru ya Sensa na kuitangaza kabla ya Agosti 20 mwaka huu iwe na wawakilishi wa dini za Waislamu, Wakiristo, na madhehebu mengine katika hatua za mchakato wa Sensa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira alikataa mapendekezo hayo, Sheikh Ponda alisema kuanzia sasa wataendelea kuzitaarifu balozi zote zilizopo nchini, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Nchi wafadhili na mamlaka zingine kwamba kitachofanywa Tanzania ni utafiti na wala siyo Sensa kwa kuwa zaidi ya nusu ya raia wake hawajahesabiwa.

Waislamu tumepanga kufanya maandamano makubwa ya amani nchi nzima kupinga dhulma dhidi ya Waislamu.

CHANZO: MWANANCHI JUNI 22 2012
 
Serikali legelege itashindwa kukusanya data za wananchi wake.
 
Wana JF.
J
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira alikataa mapendekezo hayo, Sheikh Ponda alisema kuanzia sasa wataendelea kuzitaarifu balozi zote zilizopo nchini, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Nchi wafadhili na mamlaka zingine kwamba kitachofanywa Tanzania ni utafiti na wala siyo Sensa kwa kuwa zaidi ya nusu ya raia wake hawajahesabiwa.

Assuming hiyo "zaidi ya nusu ya raia" ambayo hawatahesabiwa ni waislamu (kwa kugoma kuhesabiwa kwa kutokuwa na kipengele cha dini kwenye fomu za taarifa ya sensa) ina maana idadi yao inajulikana, kwa hiyo "bifu" la nini??????
 
Zoezi hilo la Sensa limeonyesha litajumuisha idadi ya Makanisa na Misikiti, sasa iweje wanaongia ndani ya Misikiti na Makanisa hawataki wahesabiwe.
 
Sensa inajumuisha vipengele vingi zaidi 200 ambazo ni muhimu kwa taifa na watu wake..

Kama kipengele kimoja hakipo (say dini) ina umuhimu wa vipengele vingine unabaki uleule..

Kwa kuzingatia muktaba huu...SIWAUNGI MKONO..
 
Napendekeza wasusie hata kupita barabarani
 
Hivi kuna tatizo gani serikali wakiweka dodoso za dini kwenye Sensa?
 
Wana JF.
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania zimetangaza rasmi mgogoro na Serikali baada ya kueleza kuwa haitashiriki Sensa ya Watu na Makazi kutokana na muhimili huo wa Dola kukataa kuingiza kipengele cha dini kwenye dodoso la Sensa.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Issa Ponda alisema, Jumuiya za Kiislamu ziliwasilisha serikalini mapendekezo matatu kabla ya Waislamu kushiriki zoezi hilo.

Mapendekezo hayo kushauriana na wawakilishi wa dini iunde tume huru ya Sensa na kuitangaza kabla ya Agosti 20 mwaka huu iwe na wawakilishi wa dini za Waislamu, Wakiristo, na madhehebu mengine katika hatua za mchakato wa Sensa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira alikataa mapendekezo hayo, Sheikh Ponda alisema kuanzia sasa wataendelea kuzitaarifu balozi zote zilizopo nchini, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Nchi wafadhili na mamlaka zingine kwamba kitachofanywa Tanzania ni utafiti na wala siyo Sensa kwa kuwa zaidi ya nusu ya raia wake hawajahesabiwa.

Waislamu tumepanga kufanya maandamano makubwa ya amani nchi nzima kupinga dhulma dhidi ya Waislamu.

CHANZO: MWANANCHI JUNI 22 2012

Udini mtupu
Mods please ondoeni huu udini humu JF
 
Mhesabiwe au msihesabiwe, hamna athari yoyote ile hapa nchini ya kimaendeleo zaidi ya Uamsho.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Mods mnakera kwa kulea udini humu JF. Hii ni siasa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom