KKKT Msikubali CCM iwageuze BAKWATA

KKKT Msikubali CCM iwageuze BAKWATA

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,748
Reaction score
50,170
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ni chombo kinachosimamia maslahi ya waislamu Tanzania lakini lisilokubalika na baadhi ya kizazi kipya cha waislamu.

Vijana wengi wa kiislamu hulishutumu Baraza hilo kutumiwa kisiasa kufanikisha maslahi ya CCM.

Miaka ya hivi Karibuni BAKWATA walibadili mfumo wao wa kupata masheikh wa mikoa kutoka masheikh wa kuchaguliwa na waislamu wa mkoa husika hadi masheikh wa kuteuliwa toka makao Mkuu ya BAKWATA.

Mfumo huo mpya ambao umelipa mamlaka Baraza la maulamaa kuteua masheikh wa mikoa, umeleta hofu na sintofahamu.

Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT) na lenyewe liko kwenye harakati za kubadili Katiba ya kanisa hilo kumpa mamlaka Mkuu wa kanisa mamlaka ya kuhamisha na kuteua Maaskofu.

Nasikitika kuwaambia KKKT mpango wa kubadili Katiba yao na kumpa mamlaka Mkuu wa kanisa kuteua na kuhamisha Maaskofu, umekaa kisiasa zaidi na utawagharimu.

Siku Katiba hiyo ikipitishwa, ndiyo KKKT itaanza kutumiwa kisiasa na CCM. Hivi Maaskofu wenye fikra huru kama Bagonza watasalimika kweli?
 
kwamba kkkt waskize porojo, mihemko, wivu, chuki binafsi na makasiriko yako nonsense, right?🐒
 
TENA ukimpa Malasusa Mamlaka kama hayo ambaye anasema hakulelewa kupingana na Serikali wakati Yesu alikua anapinga Serikali enzi zake sasa unashindwa kuelewa hizi dini !! iweje Yesu alikua anafanya harakati kufundisha watu na mitume hadi akahukumiwa kuuwawa leo hii hawa wetu wanasema harakati ni ugaidi kumbe Yesu angeibuka leo bado wangemnyonga vile vile mana alianza yeye harakati kupinga uonevu kupinga kila jambo baya....
 
Sisapoti hata kidogo wanachotaka kufanya kkkt, lkn kuhusu Yesu unaonekana hujui lolote, ila nitakusaidia mkuu.

Yesu hakuipinga serikali ya Roma iliyokuwa inatawala Israel kipindi chake Bali aliitambua kwa asilimia miamoja. Ndio mana aliwaambia wayahudi wanawajibika kulipa Kodi kwa Kaisari na vile vile kutoka sadaka kwa Mungu. (Ya Mungu mpeni Mungu na ya Kaisari mpeni Kaisari).

Waliomshitaki Yesu ni Wayahudi wenzie tena walimshtaki kwa maswala ya kiimani, ndio mana hata pilato(hakimu) hakuona kosa la Yesu kwa Sheria za kirumi akataka kumwachilia.

Pia hata askari wa kirumi Yesu aliwaasa wasiwachukulie watu Kodi Yao zaidi ya kiwango kilichowekwa (rushwa), hakuwaambia waondoke kurudi kwao ili Israel iwe huru.

Yesu hata aliwahi kuwaambia wayahudi kwamba vita vyake yeye ni vya kiroho (dhidi ya shetani) na sio vya kimwili (dhidi ya Dola ya Rumi).

Kwahiyo Yesu hakuipinga serikali, aliitambua japo ilikuwa haramu.
 
TENA ukimpa Malasusa Mamlaka kama hayo ambaye anasema hakulelewa kupingana na Serikali wakati Yesu alikua anapinga Serikali enzi zake sasa unashindwa kuelewa hizi dini !! iweje Yesu alikua anafanya harakati kufundisha watu na mitume hadi akahukumiwa kuuwawa leo hii hawa wetu wanasema harakati ni ugaidi kumbe Yesu angeibuka leo bado wangemnyonga vile vile mana alianza yeye harakati kupinga uonevu kupinga kila jambo baya....
Malasusa hamna kitu palee KKKT tumepigwa kitu kizito.
 
Back
Top Bottom