Kwani hata waislamu wangekuwa 99% ina implication gani kwa maendeleo ya taifa? Itasaidia kujenga shule zaidi, hospitali, maji safi, barabara umeme, n.k?
Mbona watanzania mnaacha kufuatilia na kushuguligikia mambo ya maana mnakeshea ujinga? Sasa hivi tulitakiwa tunaumiza kwa miaka 50 ya uhuru wetu mbona hali inazidi kuwa duni? Kwa rasilimali tulizo nazo madini, ardhi, watu, maji, bahari, milima mbuga za wanyama, amani, maziwa, mito hali nzuri ya hewa mbona umaskini unatumaliza! Mnakalia kutokwa mishipa ya shingo kutaka kujua waislamu na wakristu wepi wengi!! Au mnataka kutangaza taifa la kiislamu muwafukuze wakristu?
Mtanzania amka, umaskini, magonjwa, ujinga havichagui dini hata mnekuwa waislamu peke yenu isingewasaidia!!
Ukweli No. 1: Ni kwamba ni kutokana na KUJUANA, KUTAMBUANA NA KUHESHIMIANA DINI ZETU,ndio umoja na amani ya Tanzania na miongoni mwa waTanzania unapatikana. Mzee Athumani (muislamu mswalihina) na Mzee Raphaeli (mkristo wa kudumu kwenye misa) wamepanga pamoja pale Temeke Mikoroshini and Kigogo Mburahati kwa miaka nenda rudi tangu wakiwa mabachela mpaka wanajukuu. Wanatambuana (recognition), wanaheshimiana (respect), wanastahamiliana (tolerance) na wanapendana (neighbourly love) kwa miaka yote hiyo. Na hii yote ni mbali na ukweli kwamba Serikali kule juu (utawala) haina dini.
Ukweli No 2: Ni kwamba kama sikosei kile kipengele cha katiba na ibara zake kinachohusiana na jambo hili (sijui nambari zake) kinasema hivi "Serikali (nchi) ya Tanzania, haina dini, lakini waTanzania wanazo dini zao" Hii nadharia ya utambuzi wa hili katika yote, katiba pamoja na ufahamu wa waTanzania wenyewe(conscience) ikiwemo hata viongozi wa serikali (maana nao ni waTanzania vile vile), imekuwa ndio nguzo na mhimili ya umoja na amani ya Tanzania. Viongozi wetu (waTanzania wenzetu) wa kizazi hadi cha juzujuzi tu (mfano mpaka wakati wa Mwinyi) walilitambua hili na kulisimamia ipasavyo.
Yaani
1. Kila mTanzania anaaminika kuwa na imani yake (bila ya shaka imani ya uisilamu na ukristo in watu wengi zaidi)
2. Mbali na kuwa hizo imani zinatambulika na kuheshimika lakini vile vile na Kila Mtanzania (na imani yake) atatambulika, ataheshimika na kuthaminika.
Ukweli No 3: Ni kwamba ni imani zetu kwa mujibu ya fahamu zetu ndizo zitazotuundia maadili ambayo tumezoeana na kutambuana baina yetu (waTanzania), tunayajua tunayoyatarajia kutoka kwa kila mmoja wetu kutokana na kumjua imani yake, na inapjitokeza kivitendo hatushangaani kama kiroja, tunajua sote kwamba pombe kwa muislamu ni haramu na sote, wakristo, waislamu na mpaka mlevi mwenyewe (kama muislamu japo wa jina) anajulikana anakosea. Ama hakuna ushangao kwa mkristo kuona pombe ni kiburudisho, sote tunajua hivyo.
Lakini maadili yetu sote (imani zote)uzinifu hautarajiwi kuwa jambo la kawaida hata huu uzinifu wa kisasa uliopambwa (boy friend and girl friend)sote hatukubaliani nao. Kwa ufupi imani zetu na kutambuana kwetu kunatufanya kuwa na maadili yanayotarajiwa na mazuri kifamilia, kujamii, kitaifa na kimataifa.
Ukeli Tatizo No 1: Ni kwamba ulimwengu umebadilika na mitazamo ya viongozi wetu imebadilika na kuharibika. Viongozi wetu hawasimami tena kidete kutetea na kuhakikisha ustawi tulionao unaendelea. Wamekuwa wapumbavu wa kutoweza hata kunyanyua midomo na kupinga ufisadi unaotawanywa ulimwenguni hivi sasa na mafisadi wa magharibi. Wanaloliagiza wao basi viongozi wetu hufuata tu bila hata ya kuhoji. Hivyo kinachotokea sasa ni kwamba:
1. Kipengele cha katiba sasa kitasomeka "Serikali (Tanzania) haina dini, na waTanzania nao vile vile hawana dini"
2. Hivyo wasiulizwe, wasitambuliwe, na bila shaka baada ya hayo tena hapa haja ya kuheshimiwa.
Kwa mtazamo wangu mimi na kutokana na ukeli No. 1-2 hapo juu, basi kama tungekuwa kweli na viongozi waadilifu walitakiwa wafany "kinyume cha mwenendo wa sasa" na kuifanya katiba isomeke " Serikali (Tanzania) haina dini, bali waTanzania wana dini zao ambazo ndio chanzo cha vipimo vya maadili ya kila Mtanzania na nguzo ya maadili ya kiTanzaznia".
Kufanya hivi kutaifanya nchi yetu kuhimili hiki kipindi cha mpito cha maharibiko ya kimaadili ya kijamii ambayo waMagharibi wanatulazimisha na katika experiment zao.
3. Tatizo lililopo ni kwamba ndugu zetu wakristo (hasa viongozi wao kwa maslahi yao na kanisa lao) na baadhi ya waumini wakristo (kwa kujazwa kasumba za kiMagharibi kwamba uislamu na waislamu ni magaidi, nk) hawayani haya. Viongozi wa kikristo (lobby ya kikanisa)wamekaa kimya wakati nguzo na muhimili wa jamii zetu inatokomezwa.
Si hivyo tu wao kwa kushirikiana viongozi wetu wa kiserikali (lobby ya Western imperialism and capitalism)wanawaita waislamu wanaosimama kidete na kutaka mihimili hii isitokomezwe(yaani kujuana, kutambuana, kuheshimiana, kuvumiliana, kutarajiana kwa mujibu wa imani zetu)na kuwakebehi kwamba ni wakorofi, wajinga, hawaoni mbali, wamepitwa na wakati na maneno tele ya kebehi. Nini kitafuata...
4. Kwa kujua kwamba sensa hii inadhaminiwa na hao waliopanga hiyo mikakati ya "Millenium Development Goals" na viongozi wetu ni watekelezaji tu, wasiojali maslahi ya nchi bali ufisadi na kujaza matumbo yao na kiburi, isirafu na ufahari wa familia zao tu, basi pindi wakifanikiwa na kutokomeza mhimili wetu, nguzo ya umoja na amani yetu (imani na dini zetu)kimaadili watakuwa wamepata upenyo mzuri wa kuyaingiza mambo ambayo angalau huwa wakati mwengine tunajipapatua kuyakataa kutokana na maadili yetu yanayotokana na imani zetu.
Mfano: Swali: Kama sio hatuna imani na maadili yetu yatokanayo (hazitambuliki), nini kitakachowazuia kuya-push kutambulika ndoa za wanaume kwa wanaume au wanawake kwa wanawake (sodoma na gomora)katika kificho cha demokrasia na haki za binadamu? Wao hawawezi tena kuyazuia jamii zao zinanuka nayo, sasa wanataka watubambike na sisi na kipingamizi kikubwa kilichopo ni maadili yetu.
Wanajua kwa wakristo watapata greenlight lakini kikwazo kipo kutoka kwa waislamu na uislamu, na kufanya mashambulizi kwa kuchagua itakuwa ugomvi wa moja kwa moja (direct provocation) hivyo bora kutumia ujanja wa kuzifuta dini zote kwanza. Hicho ndicho wanachokifanya kwa kushirikiana na kanisa na viongozi wa serikali.
Bahati waislamu wanalitambua hili lakini ndugu zetu wakristo hawapo kabisaaaaa. Bora kwao wadanganywe na tawimu za uongo za viongozi wao kwamba wao ndio wengi nchini kuliko kupata ukweli kutoka chombo kinachohusika na mamlaka ya kufanya (serikali kama ikiweka dodoso hili)na kuendelea na amani na utulivu wa nchi yetu.
Ndugu zetu wakristo amkeni, wakati ndio huu. Kumbukeni kwamba mwisho wa yote haya haki itashinda tu na uongo utatoweka.